
JOGGING MASTER (11)

JOGGING MASTERππ11
(Master of Love π)
ππππππππ
“Nilimkumbatia Maombi na kumshukuru kwa moyo wake wa dhahabu , she is the best ,sijawah kuona mtu mwenye upendo kama huyu …..
“Nimebakiwa na laki mbili na nusu tufanye maarifa ni kitu gan tufanye Ili kujiokoa kwenye huu mtihani alisema ….
“But siko sawa nahisi naumwa naomba tujadili hili kesho rafk angu ,nilimuomba
Sawa au twende hospital. ?
Hapana nitakuwa sawa nikipumzika
Basi nililala zangu kupunguza mawazo …..
Asbh na mapema niliamka nikiwa fiti kalikitu ,Maombi aliwahi darasani na mm niliwahi kule kule kwa Jana π
Nikiwa njian hata kabla sijafika pale barabarani kwenye lile duka
Kuna gari ilipita nyuma yangu na kunipigia honi , haikuwa ile gari ya Jana hii ni nyingine …..
Piiip,nilisogea pembeni kidogo
who is this guy? nilijiuliza
nikiwa kwenye kujiuliza
Kioo kilishushwa na dereva alikuwa ni Jarred ππ
“Uko sawa ?
“Ndiyo shkamoo” nilimsalimia
“Marahaba”
Alikuwa na kikombe Cha kahawa zile za takeaway
“Ingia nikusogeze” alisema
“Hapana nitafika” siyo mbali hata
“please alisisitiza”
“Nitafika tu nashkuru” Cha ubishi Mimi kama kawaida yangu π
“Please hakuna kibaya nitakufanya trust me”π aliongeza msisitizo
“Sawa ila uache milango wazi …. nilimwambia
Alicheka kwanza π€£ ,
“how can I drive milango ikiwa wazi π aliuliza akicheka
“Basi acha vioo wazi ππ”
“Sawa nitaacha …alinifungulia mlango wa pembeni yake nikaingia π€£π€£
Akashusha vioo vyooote mpaka vya nyuma π€£π€£π€£ nifungue na buti pia ? akaniuliza ππ niliishia kucheka sana
“Umeniamin sasa ? akaniuliza
“Ndiyo , kidogo tu”
Alicheka akiangalia mbele , safari hii hakuvaa nguo za mazoezi alikuwa full suit ,amewakaa kavaa official kabisa Yan hatarious π π
“Can I know u’re name ? aliniuliza
“Naitwa Fanikiwa
“okay nice name na utafanikiwa kweli ,alisema π
“Hutaki kujua jina langu ? Aliniuliza
“Nalijua unaitwa Jarred”π
“Yeah u’re right”
“unaelekea wapi ?
“Kazini
“Okay” alisema
Aliendesha gari mpaka karibia na ule mgahawa …ni palee nilimuonesha nikimpa ishara asimamishe gari mbali kidogo na pale π
“Hutaki nikufikishe ? Aliuliza
“Hapana wataanza kusema nimepata mchumba πmi
staki mambo ya wachumba wachumba nimekuja kusoma huku π
Jarred alicheka mno
“Unasoma ?
“Ndio ila nakaribia kuacha chuo na kurudi nyumbani Namtumbo
“Ooh una graduate right”
“Nilimtizama na kutikisa kichwa ishara ya kukataa”π’
“It’s okay go then after here
utanitafuta kwa ile namba for more stories alisema …..
Nilimshukuru na kushuka kwenda kazini ….
Alinipungia na kuondoka zake ,
Kazi kazi mtoto wa maskini nilipiga kazi balaaa…. piga kazi mnooo mpaka jion Niko hoiii πkama kawaida nikalipwa ujira wangu na kuanza kuondoka nilitembea kama dakika mbili tu
Mara paaaap ile gari hii hapa ikapack pembeni yangu π mtego huu jamani π
Kioo kikafunguliwa
“How was u’re day ?
“It was fine” nilimjibu
“Okay twende nikusogeze” alisema
Rule no 1 ?nilimwambia
“To open all the shadows “πππ alijibu
nilishindwa akujizuia nilicheka mno nae akiwa anacheka slowly tu π kicheko Cha kitajiri ππ
Niliingia kwenye gari na kweli akafungua madirisha yooote πππutoto Raha Sana π….
“Unadhan naweza kukufanyia nn ? aliniuliza
“Hamna mi staki kuguswa na wanaume π
“What? ,But kuguswa tu au Kuna one thing more ? akauliza
“I don’t know but mama alisema marufuku
kugusana na wanaume π
“I like u’re childhood(nimependa utoto wako)π€£alisema Jarred
“Unaelekea wapi?
Nilimwambia chuo ninachosoma
Ooh kumbe pale okay napajua vzr aliendesha mpaka pale tukafika
Kama kawaida nilimuomba asimame mbali kidogo na pale Ili kuepusha wambea wasinione wakajua nimepata mchumba π€£
“How can u work and studying at once ?u awezaje kufanya kazi na kusoma kwa pamoja ? akauliza
“Ni story ndefu sana Jarred ipo siku nitakusimulia kama nikiendelea kuwepo hapa mjini …nilimjibu
“What do mean .? Aliniuliza
Kabla sijamjibu
“Fanikiwaaa ,sauti ya Maombi ilisikika masikion mwangu π€£π€£amenionaaaaaaaaπ hahahaha
“Bye Jarred see u tomorrow” nikatomua mbio π
Nilienda kwa Maombi na kumkumbatia
“Yule ninani ? aliuliza hakutaka ngonjera kabisa π
” Ni Jarred”
“Yupi ? Aliuliza kama mzazi wangu Yan ππ
Nilikaa kimya kidogo
itaendelea dears

