JOGGING MASTER (14)

JOGGING MASTER πŸ’žπŸ’ž14
(Master of Love πŸ’—)
πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—

Nilijilaza pale chumbani nisijue kama Niko ndotoni au ni uhalisia wa mambo umekuwa …….imekuwa ghafla sana mpaka nikaogopa

hivi hizi ndo zile nyakati sahihi za Mungu?πŸ€”

“Huyu ni malaika au ni Jini amenitokea kunisaidia ? niliwaza sana
Nitamlipa Nini Bwana kwa matendo yake makuu aliyonitendea maishani mwangu 😒😒

Sikupata usingizi kabisa nilikesha kufikiria maisha yangu yatakuwaje , ndo kwanza nimekutana na Jarred, Jarred ninani na ametokea wapi …….? 😒😒
maswali mengi kichwani bila majibu


Usiku sana nikapitiwa na usingizi nilikuja kushtuka ni saa tatu asbh…..

Dah nimechelewa mno kuamka Leo ,hata ungekuwa wewe ungechelewa kuamka kutoka kulalamika masalfeti mpaka kulala juu ya godoro la spring πŸ™ŒπŸ™Œ….

nilijiandaa na kuvaa gauni langu moja wapo bayabaya nikakaa standby kumsubiri Jarred 😌😌

Mara simu iliita…..ni zile simu za mezani nikapokea ….

“Hallo ” niliota

“Hope umeamka salama” alikuwa Jarred

“Yeah am okay Jarred 😌

“Okay Niko chini hapa nakusubiri ….alisema na kukata simu

Muda huohuo mlango wa chumbani uligongwa ….
“Atakuwa Jarred huyu nilienda kufungua haraka ….. but hakuwa yeye

Alikuwa ni mhudumu wa pale Lodge

” samahani kwa usumbufu dada ,Nina mzigo wako …..alinipatia mfuko mmoja mzuri huo hatari 😌😌😌

“Kutoka wapi. ? nilimuuliza

“Mr Jarred ,alitoa order uletewe ….alijibu

“Okay , nashkuru sana …nilimwambia na kufunga mlango….

Niliingia ndani na kuufungua ule mfuko

Kulikuwa na gauni moja Kali sana ndefu nzurii ya Mpira rangi ya pink 😌😌😌

Niliivaa na kwakweli iliingia ile mbaya πŸ˜‚πŸ˜‚

Vile nina kishepu cha kichokozi hahaha nilipendeza sana

Basi kulikuwa pia na sleepers nzuri hizo nikazivaa za ZaraπŸ”₯πŸ”₯

Huyu jamaa sijui kajuaje size yangu ila kapatia mnooooooo πŸ”₯

Nilitoka na kumkuta Jarred Yuko pale restaurant pa Jana usiku

“U look so beautiful Fenny”alisema mara yu aliponiona 😌

“Thankyou somuch Jarred ubarikiwe sana nilimwambia

Alitabasam na kunivutia kiti nikakaa

Hapohapo ililetwa chai nzito ya Nazi chapati mayai na matunda kibao πŸ˜‹πŸ˜‹
Napenda kula nilishawaambia πŸ˜‚πŸ˜‚

Tulianza kula slowly bila kupiga kelele
yaan imekuwa ghafla bin vuu maisha yangu yamebadilishwa na jogging master aisee πŸ™ŒπŸ™Œ

Hata Mimi siamin kabisa kama ndo Mimi najikataa kabisaaa πŸ˜‚πŸ˜‚

“Baada ya kula sasa ……tunaanzia wapi kupay fees au shopping ?
Aliniuliza

“Popote tu utakapopenda am ready 😊
Nilimwambia

Okay let’s go

Nilimfuata tukaingia kwenye Gari na kwenda huko mjini kabisa kwa matajiri wenzetuπŸ˜‚πŸ˜‚

Tuliingia duka moja la electronics akanichukulia PC na simu Kali jamani uwiiii nilimshukuru karibu nimmeze kwa shukrani 🀣🀣🀣

Tukatoka na kwenda bank

Namba ya account ya chuo Sina ikabidi tumpigie Maombi akanitumia namba faster

Aisee Jarred alilipia ada ya miaka mitatu mfululizo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nyie hivi ni kweli ???

Akanipatia pay slept na kunambia akitoka kazini ataniletea mahitaji yangu mengine ila kwa sasa niende chuoni nikasajili coz ….

Aliniitia tax na kunipatia elfu 50 kwaajili ya matumizi yangu oya πŸ™ŒπŸ™Œ

Kabla sijaondoka

“Usiguse wanaume” ndo kauli aliyonambia na kutabasam 😁 huyooo akaondoka zake

Sikuamin macho yangu aiseee

Tax ilinifikisha mpaka chuo ambapo nilikutana na Maombi… kwanza yeye mwenyewe hakuamin kama ndo Mimi

“Fanikiwa 😱nilikwambia Mungu yupo umeamin sasa ?

“Hakika yupo na anajua kutenda nilimjibu

“Jarred is the best kwako sasa vijana wa hapa chuoni wasije kukudanganya ukasahau
ulikotoka alisema Maombi na kunikumbatia

Siwezi kuwa mjinga Maombi nina akili ingawa zako ni nyingi kuliko Mimi siwezi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚…….
Nilimwambia tukilia zetu kama kawaida πŸ™Œ

Basi tulitafuta kijisehemu tukakaa na nikampigia baba simu ……imekuwa siku ya tatu sasa hakupatikani …. safari hii alipatikana

“Hallo baba ….

“Fanikiwa mwanangu nilipoteza simu mama nilikuwa na hofu sana juu yako mwanangu nimepata kale kahela sasa nakutumia kwa namba ipi mama uendelee na masomo yako?

Nilitokwa na machozi mengi mnoooo …..
Baba msijali na msowaze kuhusu Mimi Tena ……Mungu ametenda nimepata mkopo na hakika Mungu ni mkuu sana naomba hiyo pesa ongezea kwenye mahitaji yako na nitakuwa nikikutumia kadri nitakavyobarikiwa 😒
itaendelea dears

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

KIBOKO YANGU FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL