SEASON 1: TOBO LA PANYA (01)

SEHEMU YA KWANZA

Naaaaaaam!, hadithi yetu inaanzia ndani ya chumba kimoja kipana, chenye kuta ngumu, zisizo pitisha sauti toka nje, na utulivu wa kutosha, ungesema ni chumba cha upasuwaji, kwa utulivu wake.

Ndani ya chumba iki, wanaonekana watu watatu, walio kalia viti vya chuma, vilivyo zunguka meza ya chuma, kwa mpango wa watu wawili, yani mschana mrembo mwenye mwonekano wa kiafisa, na makadilio wa umri wa miaka 25.

Pamoja na mwanaume mtu mzima, mwenye mkadilio wa umri wa miaka zaidi 40, nae mwenye mwonekano wa kiafisa, wakiwa upande mmoja wa meza, huku mbele yao kukiwa na vijitabu vidogo vya kunakili, yani note book, na karamu za wino.

Watu hao wawili waliovalia mashati mepesi ya vishikizo, na suruali nadifu za vitambaa, zilizowapendeza na kuwakaa vizuri, walikuwa wanamtazama kwa macho ya mshangao na kuto kuamini, kijana mdogo, mwenye mkadilio wa umri wa miaka 19 hadi 21, alie valia tishert jeupe, lenye nakshi ya rangi nyekundu iliyokosa mpangilio, mfano wa mfanyakazi wabuchani.

Maafisa awa wawili wanamtazama kijana huyu, ambae licha ya kuonekana ametapakaa damu kwenye nguo na mikono yake, iliyofungwa pingu, ikiungwanishwa na myororo, ulio unganishwa kwenye meza nzito ya chuma, lakini alionekana kuwa katika hali ya utulivu, usio na hofu ata kidogo.

Maafisa wawili, wanatazamana kidogo, kwa mshangao, nikama walikuwa wanajiuliza jambo mioyoni mwao, kisha wanamtazama yule kijana mdogo, huku nyuso zao akionekana wazi kukosa majibu.

“kijana unaitwa nani na una unamiaka mingapi?” anauliza yule mwanaume mtu mzima, huku wote wawili wakimtazama kijana, huyu mwenye sura tulivu, ambae uso wake ameutazaisha chini, anatazama mikono iliyofungwa pingu.

“mna uhakika mtasadiki nitakacho waambia?” anauliza kijana yule mdogo, kwa sauti tulivu, huku bado uso wake ameekeza kwemikono, na mkono wake wa kushoto ukiupapasa mkono wakulia.

Maafisa wawili wanatazamana kama vile wanakubariana jambo, kisha wanamgeukia kijana mpole, na kuitikia kwa vichwa kwamba watasadiki kile watakacho ambiwa, “ndiyo tutasadiki” wanasema kwapamoja.

Yule kijana mtulivu anainua usowake taratibu, na kuwa tazama maafisa awa awawili, akianza na huyu wakiume, ambae ni mtu mzima, aliekuwa anachukuwa karamu na kijitabu chake, tayari kuandika atakacho tamka kijana huyu.

Kijana anaamisha macho yake kwa afisa wakike, ambae tayari alikuwa na karamu na kijitabu chake mkononi, akimtazama kijana huyu, kwa macho yake mazuri yaliyo pamba uso wake mzuri wenye mapambo yakike, pamoja na rangi nyekundu ya mdomo.

“naitwa Panya, namiaka 20” alisema kijana yule, kwa sauti ya taratibu sana, kiuharisia ungetarajia kusikia kicheko toka kwa watu wanao msikiliza, lakini baada yake, chumba kilikuwa tulivu, huku maafisa hawa wawili wakitazamana kwa mshangao.

Ni wazi hawakulizika na jibu na jibu la kijana huyu, alie jitambulisha kwa jina la Panya, ambae ukimtazama hali yake, usinge itaji kuambiwa na mtu kuwa, alikuwa ametoka katika tukio kubwa la umwagaji damu.

Lakini maafisa awa wanakosa namna ya kukataa jina, sababu makubaliano, waliyo yaweka muda mfupi uliopita, yalikuwa ni kwamba, wataamini kile atakachosema.

“ok!, Panya, unaweza kutuambia umepata wapi, umafunzo ya kutumia silaha za aina nyingi, na umewezaje kuuwa watu wengi kiasi hiki, katika umri mdogo kama huo?” aliuliza yule afisa wakike, huku anamtazama kijana huyu mdogo, mwenye jina linalofanana na yule mdudu mdogo mwalibifu.

Lakini kabla kijana huyu ajaongea neno lolote, mala ghafla mlango mzito wa chuma unafunguliwa, kwa pupa, kwa mshtuko mkubwa, maafisa wawili wanageuza nyuso zao na kutazama mlangoni, kwa macho yaliyojaa hofu, wakiamini tayari wamesha vamiwa, na watu ambao wanakuja kumwokoa kijana huyu mdogo, aliejitambulisha kwa jina la Panya.

Hapo wanaonekana watu wanne, huku wawili wakiwa wamevalia suit nyeusi, mmoja sale za jeshi la polisi, zilizo pambwa na ngao za jeshi la polisi kwenye mabega yake sambamba na nyota mbili, ikimaanisha ni cheo cha ACP, Asistant Camissioner Polisi, na mwingine akiwa amevalia nguo nadhifu za za kiraia. Hivi huyu Panya ni nani aswa, na kwanini amekamatwa, Naaaaaaam!, huo ndio mwanzo wa mkasa huu, wa TOBO LA PANYA

 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata