TOBO LA PANYA (02)

SEHEMU YA PILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: Hapo wanaonekana watu wanne, huku wawili wakiwa wamevalia suit nyeusi, mmoja sale za jeshi la polisi, zilizo pambwa na na ngao za jeshi la polisi kwenye mabega yake sambamba na nyota mbili, ikimaanisha ni cheo cha ACP, Asistant Camission Polisi, na mwingine akiwa amevalia nguo nadhifu za za kiraia… ENDELEA…..

“sitisha mahojiano, anaitajika kwa mkulugenzi TSA” alisema yule mwenye sale za jeshi la polisi, ambae alikuwa ni mtu mzima, kama yule alie valia nguo za kiraia, wale wamausalama wawili ambao ni wapelelezi toka Crime Intergence Dipatment cha jeshi la polisi wanatazamana kwa mshangao, “huyu ni nani?” kila mmoja alimwuliza mwenzie.****

Naaam, miezi miwili nyuma, ulikuwa ni mwaka 2000, mwezi wa kwanza, miezi mitatu toka Tanzania, itoke katika msiba mzito wa rais wa kwanza wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mida ya saa kumi na moja za jioni, huku Songea mkoani Ruvuma.

Tunaliona gari dogo aina ya mercedise benz E501, likikatiza maeneo ya ofisi za mkoa, kwa speed kali sana, likitokea upande wa mashariki, huku ndai akiwepo dereva peke yake.

Na gari linapo karibia kwenye makutano ya barabara ya iringa na Tunduru, linapunguza mwendo na kuingia upande wakushoto, likikamata barabara ya iringa, na kuongeza mwendo.

Mercedes benz, ili lenye rangi nyeusi linapunguza mwendo mita kama mia nne mbele, linapo ikuta njia panda ya Songea club, na linakata kona ya ghafla, kuingia kushoto, na kuikamata barabara afifu ya vumbi.

Gari linapita pembezoni majengo ya Songea club, na makumbusho ya sehemu ambayo, lilitumika kunyongea mashujaa sabini, walio ongoza vita kubwa ya maji maji, mwishoni mwa miaka ya 1800, tukiwazungunzia wakina Chief Songea Mbano.

Bado gari linaenda kwa speed kali, likivuka nyumba kadhaa, zenye mwonekano wa majengo ya ofisi mbali mbali, baada ya mita kama mia sita hivi, toka barabara kuu, lina chepuka kushoto tena, nakwenda kusimama kwenye viunga vya nyumba moja kubwa sana, ambayo ukiitazama vyema unaweza kuhisi kuwa mmiliki alitumia fedha vibaya.

Maana licha ya ukubwa na uzuri wa jengo ili, ambalo linamwonekano wa makazi binafsi ya watu, lakini bado mwonekano wake ulionekana kama vile wakazi wa jengo ili, hawa kuwa makini na utunzaji wa mazingira ya nyumba hii.

Pia ukimya na ukosefu wa pilika za kibinadamu katika maeneo ya nyumba hii, ambayo ungetabiri kuwa wanaishi watu wachache sana, ambao pia siyo wakaaji wazuri wa nyumbani.

Zaidi kwa nje tunaona nguo chache zilizo anikwa kwenye kamba, magari manne yaliyo egeshwa ubavu wa kulia wa nyumba ile, ambayo imezungukwa na midizi mingi iliyostawi vyema, huku ikikosa uangalizi wa karibu, na kufanya kichaka kikubwa.

Lakini pia kwenye kibaradha cha mbele cha nyumba hii, walionekana wanawake wawili wenye umri tofauti, yani mmoja mama mtu mzima, akiwa na maschana wa umri wakati, wakiongea ili nalile na kucheka kwa pamoja wakiwa kawaida kabisa, kwa mavazi ya kushindia nyumbani.

Wanawake hawa wanalitazama gari ili dogo jeusi aina ya mercedis benz, ambalo linaonekana mlango wa kulia wa dereva ukifunguliwa, anashuka kijana mmoja mtanashati, akiwa na bahasha kubwa ya kaki.

Mschana mdogo, anainuka haraka na kumfwata dereva, ambae pia anatembea kuelekea kibaradhani, wanakutana kati kati, bila kuuliza, dereva anamkabidhi yule dada ile bahasha, nae anaipokea nakugeuka alikotoka, wakati dereva pia anarudi kwenye gari.

Mwanadada anafika pale kibaradhani, ambako anamkuta yule mama mtu mzima, akiwa amesha simama, nikama alikuwa alikuwa anamsubiri huyu mschana mdogo mwenye bahasha.

Ni kweli alikuwa anamsubiri yeye, maana yule mwanamke mwenye bahasha, alipo fika kibaradhani, yule mama mtu mzima, aliipokea ile bahasha na kuingia nayo ndani, ya ile nyumba kubwa.

Mama mtu mzima anaibukia kwenye sebue kubwa, ambapo pana watu sita, wote ni vijana wadogo, wanawake wawili na wanaume wanne, waliokuwa wanatazama pambano la mpira kupitia kituo flani cha television.

Mwanamke mmoja anainuka haraka, na kupokea ile bahasha toka kwa mama mtu mzima, kisha anaanza kutembea kulifwata kolido moja fupi, linalo ibukia jikoni, ambako kuna wanawake wawili wanaendelea na mapishi.

Mmoja wao anachukuwa ile bahasha, na kufungua mlango, mmoja uliopo kwenye ukuta wa upande wa kulia wa pale jikoni, ambako unaweza kuona kuwa ni store ndogo yenye kabati la vyombo.

Yule mwanamke anatoa kikombe kimoja kati ya vyombo vingi, vilivyowekwa kwenye ifadhio la mstari wa kati kati, kati ya minne, iliyojaa vyombo, ambapo pana onekana kitufe flani, mfano wa kiwashio cha taa za umeme, yani switch.

Mwanamke mpishi anabofya ile switch iliyo shikizwa kwenye kuta za kabati, kisha anakuma lile kabari ambalo linazunguka upande na kuacha nafasi kubwa ya mlango, na yule dada anapita kwenye ule uwazi.

Naaaaaaam!, dada mpishi anaibukia kwenye chumba kipana sana, ambacho ndani kilikuwa na mwonekano wawazi kuwa, ni ofisi kubwa yenye hadhi ya mkulugenzi, ambayo licha kuwa na meza kubwa ya wastani yenye makolokolo mengi menzani, sambamba na simu ya mezani, majarida na computer.

Pia mbele ya meza hiyo, kulikuwa na meza nyingine kubwa ya duara, yenye viti kumi na mbili, ambavyo sasa vilikuwa vimekaliwa na watu wanne, walio valia mavazi nadhifu, ambao niwanaume watatu, moja akiwa ni mtu mzima na mwanamke mmoja mtu mzima, walio onekana kuwa katika mjadara mkubwa sana.

Mwanamke mpishi anaenda moja kwa moja mpaka mwa mwanaume mmoja mtu zima kuliko wote mle ndani, na kumpatia ile bahasha, “yeeees, mzigo huu hapa, humu kuna maelezo juu ya Secret Agent namba 26” alisema yule mwanaume mtu mzima, wakati huo yule mwanamke mpishi, anatoka katika njia aliyo ingilia.

Watu wote wanamtazama mwanaume mtu mzima, ambae anaifungua ile bahasha na kutoa karatasi kadhaa, zilizo ungwa pamoja kwa pin, “afadhari nazani sasa tutaweza kupata majibu sahihi” alisema yule mwanamke mtu mzima alikuwepo mle ndani.

Mwanaume mtu mzima anaweka sawa zile karatasi, na kusoma kurasa mbili tatu, kimya kimya, kisha anaonekana kutoa macho kwa mshangao, na kuto kuamini, “mh!, inawezekanaje?” anauliza mwanaume mtu mzima, kwa sauti yenye mshangao wa ajabu, huku anakodolea macho yale makaratasi mkononi mwake…… mwanaume mtu mzima ameona nini, na huyu SA -26 ni nani, anaweza kuwa ni tofauti na Panya, basi endelea kufwatilia mkasa huu wa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata