
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Mwanaume mtu mzima anaweka sawa zile karatasi, na kusoma kurasa mbili tatu, kimya kimya, kisha anaonekana kutoa macho kwa mshangao, na kuto kuamini, “mh!, inawezekanaje?” anauliza mwanaume mtu mzima, kwa sauti yenye mshangao wa ajabu, huku anakodolea macho yale makaratasi mkononi mwake……ENDELEA…..
Mwanamke mtu mzima, anachukuwa zile karatasi toka mkononi mwa mwanaume mtu mzima, na kuanza kuzisoma kwa sauti ya wazi, “anaitwa SA 26, anae fahamika na idara ya TSA, jina harisi hajulikani, alizaliwa mwaka 1980 feb 26” alisikika mama mtu mzima, ambae aliendelea kusoma.
“SA-26 alijiunga na kuwa wakara wa siri wa usalama, mwaka 1994, akiwa darasa la saba na umri wa miaka 14, hii ni baada ya kumwokoa mkulugenzi wa idara ya usalama wakati huo, bwana Sospeter Kingumwile, toka kwenye mtego wa kifo” alisoma mama mtu mzima, ambae akuacha kusoma.
“Security Agent-26, alihudumu katika idara, huku anaendelea kusoma, mpaka alipomaliza kidato cha nne mwaka 1998, wakati wote wa masomo, akiwa anapewa majukumu ya siri, ma wakara mkuu toka dar es salaam, ambako Kingumwile alikuwa ameamia, na kuyatekeleza vyema.
“Imeandikwa kuwa, licha kufanikisha majukumu yote aliyopewa TSA, ikiwa ni kuwafwatilia na kuuwa baadhi ya watu, walio onyesha dalili yakuwa tishio au kuleta machafuko nchini, asa wadau wakisiasa, lakini bado utekelezaji wake majukumu, ulikuwa na utata mwingi, ambao ulipelekea kwenda kupimwa akili mala kadhaa, na kubainika kuwa, hakuwa na atizo lolote la akili” alieleza mama mtu mzima, huku wenzake wakiendelea kumsikiliza.
“baadhi ya matukio ya SA-26, yaliyo tafsiliwa kuwa ni ualibifu, ni tukio la kwanza kabisa, baada ya kujiunga na idara ya usalama wa siri wa nchi” alisema mama mtu mzima na kuweka kituo.
“inaelezwa kuwa, ilikuwa mwaka 1994, mwezi wa kumi, akiwa na miaka 14, tayari amesha maliza mitihani ya darasa la saba, SA-26 alipewa jukumu la kufwatilia mwenendo wa binti wa mkuu wa mkoa, ambae ilisemekana kuwa, kuna mwanaume alikuwa anamlubuni”
“kwa mujibu wa shuhuda, anasema kuwa, SA-26 alifanikiwa kumpata mlengwa, ila mlengwa nae alibaini ushushushu wa , na kuamua kutuma watu wa wili, ili wamuuwe kijana huyu mdogo, lakini kilicho watokea watu hao, awakuweza tena kutembea kwa miguu yao, maana alihakikisha ameitenganisha miguu yako, vipande kadhaa, ndipo akatoa taarifa idarani, kuomba msaada wa kuwapeleka hospital”
Mpaka hapo wanaume watatu wanatazamana kwa mshangao, “ukiachilia pia tukio la kumwokoa mkulugenzi kingumwile, kwa kuuwa mtu mmoja alie mkata shingo yake bila huruma, kijana huyu akiwa na umri wa miaka kumi na nne, pia katika kipindi cha miaka sita, aliyokuwa kwenye idara ya usalama, inakadiliwa kuwa SA-26 ameuwa watu zaidi ya mia moja hamsini, akiwa katika majukumu ya usalama wa nchi”
Safari hii wanaume watatu, pamoja na mama mtu mzima, wanatoa macho ya mshangao na uoga, “mh!, hii ni taarifa ya mtu tunae mtafuta, au ni moja ya hadithi za Edgar Mbogo” anauliza mwanaume mtu mzima, kwa sauti ya mshangao.
“mkulugenzi, kiukweli ata mimi nashindwa kuamini, ebu ona hapa walivyo eleza” anasema mama mtu mzima, na kuwafanya wale wanaume wote kutega sikio, ilikusikia habari za kijana huyo.
“agent huyu wa siri, mweye namba 26, aliepata mafunzo yake kwenye chuo cha kijasusi cha fuvu la simba, yani Lion Skull Base au LS BASE, mashariki mwa Stone Town City, kama ambavyo vijana walipaita Trench Town au TT City, huko nchini #Mbogo_Land”
“inasemekana kuwa idadi kubwa ya watu kuwauwa pamoja, ni kundi la watu arobaini na mbili, alilo pambana nalo katika operation ya siri, katika kambi moja la wahasi, huko nchini Angora, alikoenda kufanya kazi ya kijasusi, kwa ushurikino na wanausalama kutoka nchi za kusini mwa africa”
“akiwa peke yake katika jukumu ilo, ndani ya kambi la siri la wahasi, SA-26 gunduliwa na adui, nakujikuta akilazimika kujitoa kwa adui kwa mapigano, yaliyo mlazimu kuuwa watu zaidi ya arobaini, wakati huo akiwa na umri wa miaka 17” alisimulia yule mama mtu mzima.
“ebu tafuta kisa cha huyu dogo kuacha kazi ghafla” alisema mwanaume mtu mzima, na yule mama anafungua kurasa kadhaa, na kuanza kusoma, “usiku wa mwaka mpya wa kuingia mwaka 2000, SA-26 akiwa katika matembezi yake ya kawaida, huko jijini dar es salaam, alikokuwa anafanyia kazi, mala akawaona vijana wanane, wanamvamia mwanamke mmoja kwa lengo la kumbaka na kumwibia vya vyake”
“SA-26 ambae mala zote utembea na kisu kidogo chenye ukali wa kiwembe, alipambana na wale vijana, huku akikata shingo zao, mmoja baada ya mwingine, mwisho akajikuta mikononi mwa polisi, na kuja kutolewa na mkulugenzi wa idara, wa hapo dar es salaam, ambae alikuwa ni bwana kingumwile”
“mala alipo achiwa toka polisi, akaomba kuacha kazi, kwa sababu zisizo julikana, lakini idara aikumpa kibari, kwa kuofia kuwa atavujisha siri za kiutendaji, lakini yeye SA-26, aliendelea kuwa na msimamo wake, ambao ulipeleka idara kuandaa mpango wa kifo chake”
“bado aijajulikana nani alimweleza kijana huyu, ila kiukweli SA-26 alitoweka ghafl, na serikali inaamini kuwa SA-26 atakuwa mkoani Ruvuma, sababu ndio mji alio zaliwa na alipo kulia, japo anauwezo wakuishi mkoa wowote, nchi au sehemu yoyote”
“japo mpaka aijulikani anaishi wapi, wazazi wake hawajulikani, jina lake harisi halijulikani, mji wa mama yake wala baba yake aujulikani, hakuna kabira wala dini yake, hakuwa na rafiki wakike, wala wakiume, ila inakadiliwa atakuwa anaishi maisha ya kifahari, na utajiri mkubwa, kutokana na fedha nyingi aliyolipwa katika majukumu yake ya nje ya nchi” alisema mama mtu mzima.
Hapo mwanaume mtu mzima, anashusha pumzi kwa nguvu, “kazi hipo, mimi ni James bond, lazima nitamfahamu tu” alisema mwanaume mtu mzima, ambae akuishia hapo.
“sikilizeni maajent, kuanzia sasa kinacho takiwa ni kwamba, kila mmoja idarani atege sikio mitaani, ukisikia mtu wa aina hii, taarifa zije mala moja, tumkamate, ila kumbukeni kuwa mtu huyo ni hatari sana, anaweza kujiuliza mala mbili kuhusu kunywa au kula, lakini siyo kwenye swala la kuuwa adui yake, uwa ajiulizi mala mbili” alisema mwanaume mtu mzima.
Huyo ni mkulugenzi wa idara ya uchunguzi na usalama wa siri wa nchi, mkoa wa Ruvuma, ambae kwa wanao mfahamu, huyu ndie mzee Haule, mala nyingi ujiita James bond, (soma kiapo cha damu, mrembo kipofu na mwalimu anataka)… bado tunaitaji kumtambua SA-26, je wataweza kumpata, lakini ninani huyu mtu, basi endelea kusoma hadithi ya #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU