
TOBO LA PANYA (05)

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: Kazi aikusimama mpaka mguu ulipo tenganishwa, na kuamia mguu mwingine, kisha mkono, yani mpaka walipo hakikisha wamemtenganisha sehemu zote za mwili, na huyu jamaa kukata roho, katika maumivu makali…ENDELEA…..
Baada ya kumaliza zoezi la kumcharanga huyu mwanaume, kwa kosa la kutongoza mwanamke asie juwa anapendezeshwa na nani, watu awa kwa ushirikiano walikusanya viungo vya mwanaume huyo, na kuvitupia mtoni, kisha wote kwa pamoja wanaingia kwenye gari na kuondoka zao, kuelekea mjini.
Huyu mwanaume mtu mzima anaitwa Augustino Nyondo, ni mfanya biashara na mmiliki wa kampuni kubwa ya TINO TRANS CO LITD, usafirishaji ukanda wakusini mwa Tanzania, na nchi jirani za Msumbiji na #Mbogo_Land.
Lakini licha hayo yote, pia kulikuwa na tetesi za kwamba, bwana Augustino, ay Tino kama wenzake wanavyo mwita, alikuwa anajiusisha na bashara haramu, za dawa za kulevya na nyara za serikali, kama vile pembe za ndovu na ngozi za chui.
Kiukweli bwana Tino, ni mtu ambae afikilii mala mbili kutoa roho ya mtu alie mchukia, au kumchukiza, kwamaana yeye adhabu ndogo kwake ni kifo kwa njia ya risasi, vinginevyo angekuuwa katika maumivu makali.
Pia bwana Tino Nyondo, ambae anaga kosa dogo, uwa anachukizwa sana na kitendo cha mtu mwingine kuisumbulia familia yake kwa namna yoyote, iwe mke au watoto wake wawili, au mdogo wake Lukas Nyondo, ambae ni mdogo wake wamwisho, mwenye miaka 27.***
Masaa 16 baadae, Maeneo ya chuo cha ualimu, na uongozi wa jamii, cha Matogoro, huko Songea mkoani Ruvuma, kusini mashariki mwa mji huu wa kihistoria, chuo ambacho kina historia ya kusomewa na viongozi wakubwa, akiwemo King Eric Mbogo wa ishirini na tano, mfalme wa hamsini na mbili wa #Mbogo_Land.
Tunazungumzia saa kumi na moja za jioni, eneo la viwanja vya michezo ya mpira wa mikono, yani net ball, volley ball na basket ball, katika chuo iki kikubwa katika ukanda wakusini, wanaonekana watu wengi sana, wakike kwa wakiume, idadi kubwa ikiwa ni vijana, huku wengi wao wakiwa wamevalia nguo za kimichezo, katika mwonekano wa kisasa, na umaridadi.
Hakika katika mchanganyiko huu wa wanafunzi wa chuo na vijana toka mtaani, ungeweza kuona waschana warembo walio pendeza katika mavazi yao pamoja na vijana walio valia kimaridadi, walio zunguka viwanja vidogo vidogo, vya michezo mbali mbali.
Wapo walio simama wawili wawili, kwamaana ya mwanamke na mwanamke, kwamaana ya urafiki wa kawaida, au wapenzi, na wapo walio simama kwa vikundi kwamaana ya ushangiliaji.
Sasa basi, licha ya uwingi wa watu wote hao, na shamla zilizo kuwepo hapo uwanjani, lakini basi, mita kama ishirini hivi toka kilipo kiwanja cha mpira wakikapu, ungeweza kumwona mschana mmoja mrembo na mwenye kuvutia, alie valia gauni refu lililofunika mpaka nyayo za miguu yake.
Maana ukiachilia kuwa na rangi nzuri ya ngozi yake, ambayo siyo mweupe sana, na wala siyo mweusi, pia mschana huyu mrembo kama miss Tanzania wa zamani, alikuwa mwembemba wa kaiwaida, alie balikiwa sura nzuri ya kuvutia, kifua kilicho beba matiti yenye kubwa wastani, na makalio makubwa kiasi, yaliyo shndwa kujificha kwenye gauni lake refu, na kujichora vizuri na kuleta picha flani ya kusisimua.
Licha ya watu kushangilia mpira, na kuongea na watu waliokua nao karibu, lakini kila mmoja kwa wakati wake, akuweza kupisha dakika mbili mpaka tatu, kabla ya kutazama kule alikosimama mwanamke huyu, ambae alikuwa amesimama peke yake.
Mschana mrembo, mwemye sura ya upole, alie funga nywelezake ndefu na kuzilaza mgongoni kama mkia wa farasi, anaonekana akiendelea kutazama mchuano mkali wa mpira wakikapu, ulio kuwa undelea, huku mala chache akionekana kutabasamu, katika midomo yake mizuri, na kuruhusu vijisima mashavuni mwake, nakumfanya azidi kuwa mzuri mala dufu.
Wamaume wenye uchu wanamtazama mwana dada huyu, huku wananong’onezana, na wengine wakionyesha dalili za wazi za kumtamani mrembo huyu, mwenye mkadilio wa umri wa miaka ishirini na tatu, ambae akinaishi kumtazama.
Naaaaa!, huyu mchana mrembo anaitwa Anastansia Antony, ni mwanafunzi wa mwaka wapili hapa chuoni, akiwa amebakiza miezi miwili tu, kumaliza chuo, katika mkondo wa uongozi na ushirikiano wa jamii, aijulikani ni mtoto wa tajiri gani, ila mala kadhaa mama yake mzazi alisha mtembelea hapa chuoni, akiwa anaendesha gari zuri aina Mitsubish Pajero.
Ukiachilia kwa ufahari wa mama yake, pia mschana huyu, aliishi maisha ya pekee hapa chuoni, achana na mavazi yake na vito vya thamani alivyo kuwa anavaa mwanadada Anastansia au Nansi kama wenzake wanavyo mwita, pia mschana huyu, alikuwa ana kula vyakula vya kipekee, kwa gharama zake binafsi, tofauti na vile vilivyokuwa vinapatikana hapa chuoni.
Anastansia Antony, ambae fedha kwake aikuwa tatizo, hakuwa na ukaribu na mtu yoyote pale chuoni, iwe wakike au wakiume, japo akuacha kusalimia na wenzake bila kujari jinsia, sana sana ungekosa salamu yake, pale tu ambapo ungeingiza swala la kumtongoza, au kujifanya kuwadi zidi yake, kwakifupi hapakuwa na mtu wa kumshawishi kwa fedha wala maneno.
Mschana huyu ambae kiukweli akikutazama, japo kwa sekune tano, ungesema anakuambia kitu flani kitamu sana, ni kutokana na kujaliwa kuwa na macho mazuri kupita kiasi, ambayo muda wote ungesema anakutazama kwa mahaba.
Tatibu kubwa ni pale anapo tabasamu, kitu pekee ambacho watu ushuhudia kwa uchache sana, maana usiusingweza kumwona anacheka ata kwabahati mbaya, yeye mala zote uishia kutabasamu, na anapo tabasamu, ufanya watu waache kucheka na kuduwazwa na uzuri wake ambao uongezeka mala dufu, pengine Anastansia alisha gundua swala ilo, maana pia utabasamu mala chache sana, tena kwa muda mfupi sana.
Kitu ambacho wengi walikuwa awakujuwi ni kwamba, Anastansia Anthony, ni mtoto wa nje wa bwana Anthony Chikawe, waziri mkuu wa zamani wa #Mbogo_Land, ambae pia alikuwa msaidizi na mshauri wakaribu wa mfalme Eugen wa pili, alie zaa mzee na mwana mama Stellah, wakati wanasoma katika chuo hiki cha matogoro, japo aikuwai kusimuliwa, ila unaweza kusoma kwenye mkasa wa zamani wa (#UMEKOSEA_LAKINI_TAMU) iliyo wausisha wakina Tausi na mfalme Eric Mbogo wa 25.
Kwakifupi ni kwamba, waziri mstaafu Anthony, ambae ni mmoja kati ya watu wenye fedha na utajiri mkubwa katika ukanda huu wa Africa, alikuwa anatoa huduma zoto na kuwapa kila kitu, Anastansia na mama yake, ambae tunaweza kusema kuwa, bado wapo kwenye mausiano, maana mala kwa mala, mzee Anthony, alikuwa anaingia Songea kwa siri na kukutana na familia yake, huku akilala mpenzi wake huyu wa siri.
Anatastania akiwa amesimama mita kadhaa toka kwenye kundi la wanafunzi wenzake, pamoja na watu toka mitaani, walio kuja kutazama au kushiriki michezo, anainua mkono wake na kutazama saa yake ya mkononi, “saa kumi na mbili kasoro” ananong’ona Nancy, huku anageuza usowake kutazama kushoto na kulia, ni kama alikuwa anatafuta mtu au kitu.
Lakini macho yake yanakutana na macho ya watu wengine yaliyokuwa yanamtazama kwa mshangao na mastaajabiko, “ina chosha kwakweli” anajisemea Nancy, ambae licha kuzowea kutazamwa kwa mshangao namna ile, lakini pia wakati mwingine uchukizwa na kitendo kile, maana inasababisha watu wamfwatilie kwa ukaribu sana, na kujuwa kila anachofanya, ata akikoowa wanajuwa, akipiga chafya wanajuwa, akijikwaa nao wanakuwa wanajuwa, leo Anastansia amejikwaa mala ngapi.
Anastansia anaendelea kutazama watu waliokuwa pale uwanja, mpaka macho yake yanapo kutana na kijana mmoja wakiume, aliekuwa amesimama mita kama kumi, hivi toka pale alipokuwa amesimama yeye.
Alikuwa ni kijana mtulivu na mpole, mwenye makadilio wa umri wa mioaka ishilini, alievalia suruali ya jinsi la blue, iliyo pauka, tishert jeusi lililochakaa kidogo, na raba nyeusi miguuni mwake, ambayo pia ilikuwa imeshaanza kuchakaa, aliekuwa amesimama peke yake, anatazama mchezo wa mpira wakikapu. Leo siongei chochote, nasikia toka kwako msomaji….. endelea kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

