TOBO LA PANYA (10)

SEHEMU YA KUMI

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: “shikamoo afande Mzee” alisalimia Insp Aisha kwa sauti iliyo changaka, huku anamtazama mwanaume huyu, ambae alikuwa anatazama kwenye meza yake, “Insp vipi, mbona unafwatilia taarifa za Tino Nyondo?” aliuliza mwanaume huyu, alie itwa Mzee, kwa maana ya jina lake ukoo. Endelea….

Aisha anarudisha macho mezani, na kutazama jarida la matukio ya kila siku, lililopo mezani kwake, “yah!, nimejaribu kufwatilia matukio ya huyu mtu, naona kama yanajirudia sana, inashangaza kuona achukuliwi hatua zozote za kisheria” alisema Aisha, kwa namna ya kushangaa, ungesema alisahau alichokutana nacho siku iliyopita.

“Aisha bwana, kila mji una wenyewe, tena hapo kuna mengine ayajaandikwa kabisa” alisema mwanaume mtu mzima, “kwanini iwe hivyo sasa, na itakuwaje akileta mazara makubwa, au mtu akimlipizia kisasi kwa unyama anao ufanya?” aliuliza Insp Aisha, ambae alionekana wazi kupingana na kile anacho amini Mzee.

“hapo ndipo tuta amrishwa tumpatie ulinzi, na kumsaidia kupambana, zidi ya maadui zake” alisema Mzee na kabla Aisha ajauliza tena, mwanaume mtu mzima akamuwai, “ebu achana na hayo, kisha nieleze kuhusu tukio ambalo jana ulienda kuliangalia huko msamala” alisema Mzee, huku anavuta kitiu toka kwenye meza ya pembeni, na kukaa karibu na Insp Aisha.

Wakati Aisha anaeleza kile alicho kiona kule msamala, sisi tumfahamu huyu mwanaume mtu mzima, ambae kwa majina anaitwa Ayoub Mzee Ayoub, ambae ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga.

Yeye ni askari wa jeshi la polisi, mwewenye cheo cha Asistance Super lutendant wa polisi, ambae kwa madaraka katika majukumu yake ya jeshi la polisi hapa mkoa wa Ruvuma, alikuwa ni mkuu msaidizi wa idara ya upelelezi.

Ukaribu na Insp Aisha, siyo wa kazi pekee, ila pia ni watu walio tokea mkoa mmoja kiasiri, yani mkoa wa Tanga, na walikuwa wanafahamiana kabla ya kukutana mkoani Ruvuma, ambako mwenyeji alikuwa ni ASP Ayoub Mzee, alie mpokea Insp Aisha Amary.****

Saa tatu nne za asubuhi, maeneo ya ofisi za kampuni ya zamani ya uchukuzi, maarufu kama mtaa wa KAURU, ambapo kwa sasa palikuwa na bango kubwa la Tino Nyondo Trans, lilisimaishwa kwenye nguzo imara mbele ya majengo ya kisasa ya ofisi ya kampuni hii ya uchukuzi.

Ukiachilia upande wa nyuma wa ofisi hizo, yani ndani ya uzio mkubwa waukuta, ambako kulikuwa na magari mengi ya mizigo, pia upande wambele wa ofisi hizo, palikuwa na watu wengi, waliokuwa katika pilika zao, yani wafanyakazi wa kampuni, pamoja na wateja waliokuwa wamekuja, kwa maitajio ya kusafirisha mizigo yao.

Lakini wakati huo huo, tuna mwona mwanadada Rose, akiwa anaingia kwenye viunga vya ofisini za Tino Nyondo, akionekana kuwa, katika hali ya unyonge ulio pitiliza, ungesema ni mgonjwa au amefiwa na mtu muhimu sana, maana ni wazi alikesha usiku kucha akiwa analia.

Rose akiwa mwenye tahadhari kubwa anatazama kwenye maegesho ya magari ya VIP ambayo utumika kwa gari ya familia ya Nyondo mwenyewe, pamoja na mdogo wake Lukas, pia na gari la meneja wa kampuni, ambapo mpaka sasa linaonekana gari la meneja peke yake.

Rose akiwa na uhakika wa kuwa, Lukas na kaka yake awajafika pale ofisini, anaingia kwenye jengo la utawara la kampuni, ambapo anapita sehemu ya mapokezi ya wateja, yenye watu wengi waliokuwa wana endelea kuandika kumbukumu za oda za wateja wao.

Yeye anatembea kwa haraka, uso ameuinamisha chini, anaitikia salamu za wenzake, ambao wanamsalimia kwa uchangamfu, lakini unyobgewake unawashangaza baadhi yao, ila wengine wanafahamu kuhusu kutoweka kwa mpenzi wa mwanamke huyu, yani bwana Aloyce.

“Rose mbona umechelewa sana kufika kazini, kwani umeshamwona Aloyce?” ilikuwa ni sauti ya kike, ambayo safari hii ilimfanya Rose asimame, tofauti na mwanzo aliposalimia na kutembea.

Rose anamgeukia mlie msalimia, ni mwanamke mwenye kimo na mwonekano kama yeye, inaonesha ni mala fiki, “bado sijamwona, sijuwi wakina Luka wamemfanya nini” anaongea Rose kwa sauti ya kulalamika, iliyo jawa na unyonge wa hali ya juu.

“he!, kwani jana ulikutana na Lukas, maana jioni alipiga simu hapa ofisini, alikuwa anakuulizia” alisema yule mwanamke, Rose anatazama chini, anafuta machozi usoni mwake, “Lukas alikuja nyumbani, akanilazimisha kufanya, akaniambia simwoni tena Aloyce” alisema Rose kwa sauti ya chini yenye kilio cha kwikwi.

“jamaniiiii, hivi kwanini anakuwa hivi huyu shetani, sasa ataendelea kufanya uonevu mpaka lini” anaongea kwa sauti ya chini, yenye kulalamika huyu mwanamke, huku anaonyesha udhuni ya wazi kabisa.

“eti anasema atakuwa anakuja kila anavyo jisikia” alisema Rose kwasauti ya chini yenye masikitiko, “kha!, hivi huyu anakichaa” anaongea yule mwanamke kwa sauti iliyojaa jazba, “sikufichi Hidaya, mimi naenda kuacha kazi, nitaenda kutafuta sehemu nyingine” alisema Rose, akionyesha nia ya wazi ya kuacha kazi kwenye ile kampuni ya Tino Nyondo.

“lakini Rose …….” Huyu mwanamke anaitwa Hidaya nikama alitaka kumhsuri kitu Rose, lakini akupewa nafasi, “tutaongea baadae wacha nikaongee na meneja” alisema Rose huku anaanza kutembe, kuelekea upande wa vyumba vya ofisi.

Hidaya anamtazama rafiki ya Rose, akitamani kwenda kumshauri atumie busara kutatua tatizo ili, maana akikikurupuka anaweza kupoteza maisha yake, au akawa mtumwa wangono wa kudumu.

Hidaya anamwo Rose akiwa anapotelea kwenye kolido la kuelekea kwenye ofisi ya meneja, Hidaya anapotaka kupiga hatua kumfwata mala anasikia sauti za watu wanasaliia, upande wa mapokezi, “shikamoo boss” zilikuwa ni shikamoo nyingi toka kwa kila mtu, ambazo zinaitikiwa mala moja tu, “marahaba, endeleani nakazi” ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume mtu mzima.

Hidaya akuitaji King’amua sauti, ili kuibaini hii sauti kuwa ni ya mzee Augustino Nyondo, hivyo anaingiwa na wasi wasi mkubwa, akiofia kuwa, endapo ata mkuta Rose ofisini anaacha kazi, anaweza kitu kibaya mle mle ofisini.**

Yaaaaaap!, mida hii ya saa nne na nusu za asubuhi, wanafunzi wa chuo cha uongozi wajamii na ualimu pale matogoro, wanaonekana wakiwa wanamaliza kunywa chai, ili waende kupumzika na kuianza week end, na waumini wa islam, waende msikitini, kwamaana leo siku ya ijumaa ilichukuwa kama nusu ziku ya masomo.

Lakini siku kama hii ya ijumaa, ndio siku ambayo mwanadada Anastansia uitumia kutembea maeneo ya jilani, akinyoosha miguu, kwamaana akutumia gari au usafiri wa aina yoyote, ni sehemu ya mpango wake wa mazoezi.

Ukiachilia siku hii ya ijumaa, ambayo uitumia kutembea kwa miguu maeneo ya kijirani na chuo, pia utumia siku ya juma mosi kutulia chuoni akijisomea na kufanya usafi wa nguo zake, huku siku ya jumapili, akitumia kutembelea nyumbani kwa mama yake na kufanya manunuzi mjini.

Hivyo Anastansia, ambae alikuwa miongoni mwa wanafunzi walio toka mapema, sasa alikuwa anatoka kwenye lango chuo, huku akiwa ajanywa chai, akipanga kwenda kutafuta chai nzuri, huko mitaani, kama ilivyo kawaida yake kwenye upande wa vyakula, akupenda kula vyakula vya chuo.

Anastansia alitembea taratibu akitoka kwenye lango la chuo, kama kawaida yake alikuwa peke yake, huku akiwa amevalia truck suit ya chini, yenye rangi ya kijivu na fito nyeusi, tishert la njano lenye picha ya uwa jekundu kifuani, na raba nyeupe nzuri.

Anastansia ambae akujuwa uelekeo sahihi wa kuelekea siku ile, kwamaana uwa anabadiri uelekeo kila siku, ili kuyafahamu mazungura ya jirani na chuo, alitembea taratibu huku amejifunga koti la truck suit kiunoni, kwa madai ya kuzuwia makalio yake makubwa kiasi yasionekane kwenye macho ya midume yenye uchu.

Japo wenye macho walisema inazidisha utamu wa umbo lake, nikutokana na jinsi nguo hii, ilivyo kuwa ime mkaa vyema, na kusadifu umbo lake zuri lenye kutamanisha na kuvutia kila mwanaume mwenye afya njema ya macho na uzazi.

Anatastansia anakamata uelekeao wa mtaa mpya wa seed farm, akitamani kama angempata mtu ambae angemwongoza kwenye mtaa huo ambao unanyumba chache, zilizo tenga nishwa na vichaka vikubwa vya nyasi ndefu, na mashamba makubwa ya maindi.

Anastansia anapanga kwenda umbari mfupi, anatembea huku kichwani mwake anawaza na kutafakari, kuhusu maisha yake ambayo licha ya kuwa ya kifahari, lakini alikuwa anapitia usumbufu mkubwa toka kwa wanaume, ambao kiukweli alisha aamua kuto kujiusisha nao toka akiwa kidato cha tatu, alipoachana na mwanaume wake wakwanza.

Bila shaka, katika vipande vya mbele, tuta angazia kwa kifupi kuhusu mausiano yake ya kwanza, ngoja kwanza turudi kwenye ofisi za Tino Nyondo Trans.****

Rose anatembea kwa haraka, akikatiza kwenye kolido la jengo ili kubwa, anapitiliza moja kwa moja, mpaka kwenye ofisi iliyo andikwa manager, ambapo anagonga kidogo na kuluhusiwa kuingia.

Rose anafungua mlango na kuingia ndani ya ile ofisini, ambako anamkuta mama mmoja mtu mzima, alie tulia kwenye kiti chake kalamu ikiwa mkononi mwake, na kijitabu kidogo kikiwa mezani, “afadhari Rose umefika, nazani utanieleza imekuwaje kuhusu Aloyce, maana boss ameagiza afutwe kazi” alisema yule mama mtu mzima, huku anaweka kalamu mezani. . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata