
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: “kwa mama mdogo hapakufai Rose, ni bora ukajifiche bombambili, pale napoishi, kwa mama yako mdogo lazima wataenda kukuangalia” alisema Hidaya, huku wanaendelea kuweka baadhi ya vitu kwenye begi. . . . . Endelea….
“jamani nimewakosea nini lakini” analalamika Rose huku anasaidiana na Rose kuweka vitu kwenye begi, “yani boss amekasirika, anasema eti umemletea dharau, amesema wanakuteka unaenda kubakwa, kisha wanakuuwa” alisema Hidaya na kuzidi kumchanganya Rose.****
Gari dogo aina ya Toyota crester linaonekana lina tembea taratibu, kwenye barabara ya kutoka iringa, likitokea makao makuu ya jeshi la polisi, kuelekea katikati ya mji, ndani likiwa na maafisa wawili wa jeshi la polisi.
Hao ni ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, “Aisha uliishia wapi ule mpango wako wa kuchumbiwa?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, ambae alikuwa anaendesha gari, “usinikumbushe afande, Hassan ni mpuuzi sana, anatamaa ya wanwake kama fisi” alijibu Aisha, huku safari inaendelea, wakikaribia siko kuu.
“mpuuzi kivipi, ulimfunia au?” anauliza ASP Mzee, huku anapunguza mwendo, akiwa amewasha taa elekezi, kuashilia kuwa, mita chache mbele anakata kona kulia, kuingia soko kuu la Songea mjini, ikiwa ni tahadhari kwa magari manne yaliyokuwepo nyuma yake.
“wala sijamfumania, ila kunawakati alipunguza mawasiliano, hakuna cha barua wala nini” alisimulia Aisha, “mh! sasa tamaha yake ipo wapi hapo, labda arua zilikuwa zina kwama sehemu?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, ambae wakati huo alikuwa anakata kona kulia kuingia soko kuu.
Wakati huo awakujuwa kuwa, kuna gari aina ya Toyota Hiace, lina kuja kwa mwendo mkali, toka nyuma yao liki yapita magari mengine, kinyume na alama za barabarani.
“kuna siku nilitumia simu ya ofisini, kupiga simu nyumbani, nikaambiwa kuwa Hassan alikuwa amesha owa, nilipoenda nyumbani na kukutana nae, akasema nikweli ameowa, lakini anataka aniowe mke wapil….,” Kabla Aisha ajamaliza kusimulia, ASP Ayoub Mzee akakanyaga brake za ghafla.
Kama siyo mkanda wa wasalama wa kwenye kiti, alio jifunga Aisha, basi angejibamiza kwenye koo cha mbele, maana brake zilikuwa za ghafla kweli kweli, kiasi cha kusotesha magurudumu ya gari lile.
Wakati Aisha anashangaa nini kimetokea, mala analiona gari aina ya Toyota hiace alikipita kwa wendo wa mkali pembeni yao, upande ule ule wa kulia kwao, “acha ujinga wewe, kuwa makini barabarani” ilisikika sauti ya juu toka kwenye lile Toyota hiace.
Aisha anamtazama ASP Ayoub Mzee anamwona akiwa analitazama lile Toyota hiace ambalo hapo mwanzo, akuliona kabisa miongoni mwa magari manne yaliyo kuwa nyuma yao, hivyo akujuwa kama lilianza kuyaover take, magari yote manne pamoja na lile la kwao, kiasi cha kutaka kuwa sababishia hajari.
“afande unasubiri nini, twende tuwakimbize wale washenzi” anasema Insp Aisha, kwa sauti yenye jadhba na hasira, “achana nao” anasema ASP Ayoub Mzee, huku anaondoa gari, kuingia barabara ya soko kuu, na kumfanya Aisha amshangae afande wake.
“afande, hivi unajisikia unacho sema, yani watuhatarishie maisha yetu alafu tuwaache bila kuwaadabisha?” anauliza Aisha kwa mshangao, lakini ASP Mzee, ajibu kitu, zaidi ya kuendesha gari na kwenda kuegesha gari kwenye maegesho ya soko kuu.
Inamshangaza sana Aisha, ambae anashindwa kumwelewa afande wake, kwamba amepatwa na nini, “unajuwa sikuelewi afande, yani tunamwacha mtu ambae, anaonekana wazi akivunja sheria za barabara?” aliuliza Insp Aisha, wakiwa bado wapo ndani ya gari.
Hapo ASP Ayoub Mzee anamtazama Insp Aisha, kwa macho tulivu, ni kama anatafuta lugha nzuri ya kumweleza Aisha, “sikia Aisha, muda mfupi uliopita, ulimsikia afande Zamoyoni” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti tulivu, kisha akafungua mlango wagari na kutoka nje ya gari, akimwacha Aisha ametoa macho kwa mshangao.
“afande lakini yule siyo Tino Nyondo” alisema Aisha, huku na yeye anashuka toka kwenye gari, “yule anaitwa Lukas Nyondo, mdogo wa Augustino Nyondo, ni mala mia umkosee Tino Nyondo, kuliko mdogo wake” alisema ASP Mzee, huku anafunga milango ya gari kwa funguo yake, kisha anaanza kutembea kuingia ndani ya soko.
“hakika ni zaidi ya nilivyokuwa nafikilia, inamaana tunatakiwa kufumbia macho tabia za kishenzi kama hizi” alisema Insp Aisha, huku anamfwata afande wake, wakiingia sokoni.
“ulicho kiona leo siyo kitu, kwa tabia na matukio ya Lukas, anamatukio ya kuchikiza sana” alisema ASP Ayoub Mzee, huku wanaendelea kutembea, “kwa iyo tunatakiwa kuwa wavumilivu, inakuwaje anapo tufanyia sisi matukio ya kijinga?” anauliza Insp Aisha, ambae anaonekana kushangazwa na utaratibu wa jeshi ili ukanda huu wakusini.
“tena kaa nae mbali sana, maana ukimgusa tu, umetengeneza vita kubwa sana na bwana Tino Nyondo” alisisitiza ASP Ayoub Mzee, na hapo Aisha akaamua akae kimya kabisa, maana aikuwa na maana yoyote kutafuta habari za mtu kama huyu.***
Naaaaam!, huko mfaranyaki nako, kwenye nyumba ambayo tunafahamu kuwa anaishi mwanadada Rose, tuna waona wakina dada wakiwa wamejaa kolidoni, wanaendelea na mapishi na maongezi yao, kama ilivyo kawaida yao.
Lakini dakika chache baadae, tunawaona Rose na Hidaya wakiwa wanatoka ndani ya chumba cha Rose, huku wamebeba begi dogo la Rose, na mikoba yao, wakionekana kuwa, Rose asinge rudi kwa siku ile au siku inayofuata.
Rose anafunga mlango kwa funguo, kisha anaweka funguo kwenye mkoba wake wa mkononi, alafu anamsogelea mwanamke alikuwepo karibu yake, ambae kimwonekano alikuwa ni mdada wakamamo kidogo anae kimbilia kuwa mmama.
“dada Maimuna, mimi natoka kidogo, naenda kwa mama mdogo matogoro” anasema Rose ambae alikuwa amebeba mkoba wake wa mkononi, huku begi lake dogo likiwa limebebwa na Hidaya, ambae sasa alikuwa anakaribia kuufikia mlango wa kutokea nje.
“unarudi lini?” aliuliza yule yule dada Maimuna, ambae ata utazamaji wake ni kama alikuwa anamownea huruma sana Rose, “sidhani kama nitarudi hivi karibuni, kama nita hama, basi nitamtuma mtu, aje kuchukuwa vitu vyangu” alisema Rose, kisha akaanza kutembea kuelekea kwenye mlango wa kutokea nje.
Rose anatumia dakika nne mpaka kufika nje, huku akiwaaga majirani na wapangaji wenzake, “Rose tuondoke haraka, wanaweza kutukuta hapa” alisisitiza Hidaya, huku anatembea akiongoza barabara ya soko la mkulima, akiacha barabara mbili, yani ile inayoelekea upande misufini na ile inayoelekea matarawe.
Huku wale wapangaji wenzake, wakiwasindikiza kwa macho, na kuwaona wakitokomea upande huo, wa soko la wakulima, maarufu kama manzese, “masikini Rose, sijuwi amewakosea nini awale mashetan…..” alisema mmoja kati wa pangaji wale, kwa sauti iliyo jaa huruma.
Lakini kabla ajamaliza ata kuongea, wakaliona gari dogo aina ya Toyota Hiace, wakati huo likitambuliwa kwa jina moja tu, la dara dara, linasimama nje ya nyumba yao, tena karibu kabisa na mlango.
Ni gari ambalo siyo geni machoni pao, maana ukiachilia kuliona hapa nyumbani kwa mala ya tatu, yani juzi jioni jana jioni na leo, lakini pia walikuwa wanafahamu fika kuwa, ni gari linalo tumiwa na kijana maharufu, na mdogo wa tajiri mwenye sifa ogopeshi hapa mjini. . . . . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU