TOBO LA PANYA (17)

SEHEMU YA KUMI NA SABA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA: Ni gari ambalo siyo geni machoni pao, maana ukiachilia kuliona hapa nyumbani kwa mala ya tatu, yani juzi jioni jana jioni na leo, lakini pia walikuwa wanafahamu fika kuwa, ni gari linalo tumiwa na kijana maharufu, na mdogo wa tajiri mwenye sifa ogopeshi hapa mjini. . . . . . Endelea….

Leo ilikuwa tofauti kidogo, maana aikuwa kama ilivyokuwa jana na juzi, kwamba wanashuka wote, kisha Lukas peke yake ndie anaingia ndani, ila leo walishuka wote wakiwa na chupa zao za pombe, na wakaingia wote ndani.

“ebu pisha, mnashangaa nini nyie” alisema Lukas, ambae alikuwa ametangulia, huku wenzake wakimfwata nyuma, “ondoa takataka zako” anasema mwingine anae fahamika kwa jina la Mgendi Ngurai” huku anasukuma kwamguu, sufuria lenye maharage, lililokuwepo sakafuni, linasubiri kuendelea kufanyiwa utaratibu mwingine.

Bahati nzuri kina mwagika kiasi kidogo cha maharage toka kwenye sufuria, mmiliki wa mboga hii anaiwai na kusogeza pembeni zaidi, wengine pia wanafanya hivyo kwa haraka.

Moja kwa moja wakina Luka wanaenda kusimama mbele ya mlango wa chumba cha Rose, Lukas anashika kitasa cha mlango na kujaribu kukinyonga kwa kufungua.

Lakini mlango aufunguki, Lukas anarudia mala kadhaa kunyonga kitasa cha mlango, lakini bado mlango ni mgumu kufunguka, hapo Lukas anaugonga mlango kwa nguvu, “fungua mlango we Malaya, kabla sijauvunja” anasema Lukas sauti kali sana, iliyojaa hasira.

“hoya Luka, mbona kama ndani hakuna mtu” alisema mmoja wao, na hapo Lukas anamgeukia mwanamke aliekuwa jilani, ambae ni dada mtumzima kidogo, “yupo wapi huyu” aliuliza Lukas kwa sauti ya ukali.

Ni kweli maimuna aliagwa na Rose, lakini hakuona kama itakuwa vyema kumweleza kijana huyu, ambae jana tu, ametoka kumbaka mwanamke huyo, hapa hapa nyumbani kwake, “wewe siunaulizwa, sasa unashangaa nini?” aliuliza Mgendi, huku anarusha kofi lililotuwa kishwani kwa Maimuna.

“mamaaaaa nakufa, jamani Rose ameenda Matogoro, kwa mama yake mdogo” alisema Maimuna huku anaachia kilio cha maumivu, “pumbavu sasa kwanini unaacha sisi tunaangaika hapa” alisema Lukas huku anaanza kutembea kuelekea nje.

Watu wote kimya wanawatazama vijana wababe, wakitoka nje “awezi kutukimbia huyu Malaya” alisema Lukas, wakiwa wanatoka nje kabisa ya jengo, na kuingia kwenye gari lao, kisha wakaondoka zao.****

Naaaaaam!, kule seed farm bado tuna mwona mwanadada mrembo mwenye vuto wanguvu, akiwa amekaa kwenye kiti, anamalizia kula muindi, huku akipepesa macho kushoto na kulia, ni kama anakagua mazingira, sauti ya music laini inamburudisha.

“hivi hapa kichakani kwenye ikikijumba cha udongo, anaishi na nani?” anajiuliza Anastansia, ambae bado tumbo lake linahisi kuwa linaitaji kuendelea kula, “anawezaje kupata maitaji yake, au anafanya kazi ndogo ndogo” anajiuliza Nancy huku anatazama jikoni, anaiona miindi mitatu iliyobakia.

Anastansia anatamani kula muhindi mwingine, lakini anaona kuwa bado alikuwa anaitaji chakula chepesi cha moto zaidi, lakini naona wazi hapakuw ana uwezekano wa kijana huyu, kumpatia chakula anacho itaji, au kinachoweza kumfaha.

Anastansia anawaza kidogo kama ni sahihi kuchukuwa muindi mwingine, “au nimsubiri aje anipe mwenyewe” anajiuliza Nancy ambae anakosa jibu, maana njaa ilikuwa imemshika vyema.

Nancy anaamua kuchukuwa uamuzi mwenyewe, hivyo anajiinua toka kwenye kiti, na kulifwata jiko, lakini ile anainama kuchukuwa muhindi, akasikia sauti toka upande wa mlango wakibanda cha udongo, “ungesubiri kwanza upate japo chai au uji” ilikuwa ni sauti ya upole, ya kijana mdogo na mpole.

Anastansia anashtuka na kutazama kule mlangoni, ambako anamwona kijana mdogo, akiwa na sinia kubwa chakavu, lenye vitu vingi juu yake, ikiwa ni pamoja kikaango kidogo plyer pan, mafuta na mayai vitunguu, na chupa ya chai, pamoja na kikombe cha plastic.

Inamshtua kidogo Anastansia, ambae anatazama sinia lililobebwa na kijana mdogo, akitamani kujuwa anaandaliwa nini, “umeongea jambo zuri, ni vyema nipata chai ya moto” anasema Anastansia huku anarudi alipokuwa amekaa mwanzo, yani kwenye kiti cha uvivu.

Kijana mdogo aongei kitu, anaweka sinia juu ya kichanja cha miti pembeni ya kidogo ya jiko, kisha anaelekea kwenye banda la kuku, akimwacha Anastansia anatazama lile sinia, akikagua vyombo na vifaa, kuona kama vinaubora au adhi ya kumfanya yeye aweze kula.

Kiukweli ni vyombo vya hali ya chini sana, japo usafi wake na upya wake ulilidhisha kidogo, “mh!, nitaweza kweli?” anajiwazia Anastansia, huku anamtazama kijana mdogo na mpole, aliekuwa anarudi toka bandani, akiwa amebeba mayai manne ya kuku mkononi mwake, kumbuka wakati huo Songea hapakuwa na mayai ya kukuwa kisasa.****

Naaaaaaaam!, maeneo ya soko kuu la Songea mjini, tuna waona ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, wakiwa wanatoka ndani ya soko, huku bwana bwana Ayoub Mzee, akiwa amebeba mfuko mdogo wa Rambo mkononi mwake.

“kwahiyo afande, baada ya hapa tunaelekea wapi?” aliuliza Insp Aisha, huku wanaelekea kwenye maegesho, nikama vile ASP Ayoub Mzee akutarajia lile swali, maana alisimama kidogo, na kutafakari kwa sekunde chache.

“ni vyema tukaenda kituoni, tukatazame mpango wa majukumu, maana toka juzi sijaingia jioni” alisema ASP Mzee, kisha akaanza kutembea kulifwata gari, “kwani hukusoma ubao ile asubuhi, mbona leo unaingia saa kumi na mbili, mimwenzako, nataka niende nyumbani nikapumzike kabisa” alisema Insp Aisha.

“kumbe nipo jioni, sasa kwanini hukuniambia mapema, sasa hivi ningekuwa nimesha fika home” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anafungua mlango wagari kwa funguo, kisha akamfungulia na Insp Aisha, “nilizania ulisha soma” alisema Aisha, huku anaingia kwenye gari.

“basi wacha nikupeleke nyumbani kwako, kisha na mimi nikapumzike” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anawasha gari na kuliondoa taratibu, kuingia barabara kuu, huku akiwasha taa za upande wa kushoto, kuonyesha anaelekea upande huo.

ASP Mzee anapo ukaribia barabara, anasimamisha gari na kutazama upande wake wakulia, kuona kama kuna gari au pikipiki inakuja, akaona kuwa gari linalokuja lilikuwa mbali hivyo angeweza kuingiza gari barabarani, akatazama kushoto, akaona magari yapo upande wakushoro wa barabara, hivyo nae akaona ni salama kuingiza gari.

Lakini lakini basi, kabla matairi ya gari la ASP Mzee ayagusa barabara, akajikuta anakanyaga blake za ghafla, na kusimamisha gari, kisha wakatazama upande wakushoto, ambako ulisikika mvumo wa gari, lililokuwa linakuja kwa speed kali sana . . . . . . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata