TOBO LA PANYA (27)

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
 
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA: Lakini anashangaa kuona kijana huyu, anaachia tabasamu laini, ikiwa ni mala ya kwanza kuona tabasamu usoni mwa kijana huyu, siyo kwamba ilimshangaza Anastansia peke yake, ila pia iliwashangaza ata wakina Lukas, “unaleta mzaa dogo, acha ujinga bastora yakweli hii, nitakupasua kichwa…”……..Endelea ….
 
Kabla Lukas ajakaa sawa Lukas, akashtuka mkono wake ukipapaswa kwa kasi ya umeme, ile kufumba na kufumbua, tayari bastora yake ilikuwa aipo mkononi, na ile kutazama mbele, tayari mtutu wa bastora yake ulikuwa unamtazama usoni.
 
“umekosea sana kaka, maana nilikuambia ukusikia” aliongea alisema kijana mpole kwa sauti ya taratibu, safari hii sura yake, ikionyesha kutokuwa na utani ata kidogo, huku anatoa kimkebe cha risasi, na kukitupa pembeni, kisha akakikoki ile bastora na kuhakikisha hakuna risasi kwenye chemba yake, kisha anaitupa pembeni.
 
Ilimshangaza Anastansia, ambae anashindwa kuelewa kijana mpole amewezaje kufanya alivyo fanya, mbona kama ametumia ujuzi mkubwa sana kupokonya ile bastora mikononi mwa huyu kijana mkorofi, anawezaje kufanya vile.
 
Naaaaam!, lakini sasa, hapo nikama kijana mdogo, alikuwa amechokoza nyuki, maana Nancy anawaona wale vijana wanne toka kwenye ubavu wagari wakimkimfwata kijana mpole mbio mbio, huku Lukas akirudi nyuma kwa hatua kadhaa, ni kama alikuwa ameshangazwa na tukio la kupolwa bastora.
 
“dada, fumba macho” alisema kijana mpole, akimweleza Anastansia, ambae ni kama akuwa ameambiwa yeye, maana akujiangaisha kufumba macho kama alivyo ambiwa, zaidi alikodoa macho kuwatazama wale vijana waliokuwa wanakuja mbio mbio.
 
Ile wakanza anamfikia kijana mpole na kuvulumisha mkono ulioshika chupa, kuelekea kwa kijana huyu mpole, kijana mpole anaudaka mkono wa yule jamaa, wenye chupa, nakumvuta kuja kwake, huku anampisha kidogo, na kuruka teka lamaana lillotuwa kwa kubaga, ambae akutarajia kitendo kile, hivyo akuwa na ujanja wakupisha teke la kijana huyu, lililotuwa usoni kwake, usawa wa pua.
 
Wakati Kubaga anajipapasa na kuona damu nyingi puani kwake, huyu alie shikwa mkono, sasa alikuwa anapokea ngumi nzito ya mdomo, ambayo ilipasua mdomo wa juu, kiasi cha meno ya juu kuonakana wazi wazi.
 
Siyo Anastansia peke yake, ata Lukas nae alishangaa uwezo wa kijana huyu, ambae alikuwa anawatwanga wakina Tibasana mmoja baada ya mwingine, tena kipigo kikali, maana ukimwacha tiba sana ambae alikuwa amechanika mdomo wa juu, sasa Kubaga, ambae alikuwa amejaa damu usoni, alimfwata tena kijana mpole, ambae alikuwa ana ukita mguu wake, juu ya goti la Migendi.
 
Inasikika sauti “khaaa!” mfano wa sauti ya kuni kavu, huku mguu wa migendi ukigeuka nyuma mbele nyuma, Kubaga ambae alijuwa kuwa, ile ndiyo nafasi ya kumtandika kijana mpole, anarusha ngumi nzito kuekelea kwa kijana, lakini bahati mbaya kwake.
 
Maana kijana mpole anamdaka mkono wa kubaga, na kuuzungusha kwa ghafla, kisha anaukita kwenye goti lake, inasikika sauti kama ile ya mwanzo, “khaaa!” ikifwatia na kilio kikali toka kwa kubaga, kama ilivyokuwa kwa Migendi, iliashiria kuwa, tayari mfupa wa mkono huo, ulikuwa umesha gawika mala mbili.
 
Kuona hivyo Lukas akakimbilia pale kwenye bastora, na kuiokota, kisha anaielekeza kwa kijana mpole ambae sasa alikuwa anatupa ngumi mfululizo usoni kwa Mwakaleja, uso ukivuja damu kama vile fuko lenye maji mekundu.
 
Lukas anaminya kifyetulio cha bastora yake, “kacha!, Kacha!” unasikika mlio ambao, uliashiria kuwa, hapa kuwa na risasi ndani ya bastora hiyo, Lukas anakumbuka kuwa kijana mpole alitoa mkebe wa risasi kwenye ile bastora.
 
 
Haraka sana anatazama sehemu ambayo, ule mkebe ulitupwa, na bahati ilivyokuwa upande wake, mala moja akauona mkebe, na kuufwata kwa haraka, akauokota na kuupachika kwenye bastora, kwa haraka, kisha akaikoki mala moja.
 
Lakini basi, alivyokuwa na bahati mbaya sasa, ile Lukas anaelekeza bastora kwa kijana mpole, akashtuka mkono umedakwa na kuinuliwa juu, huku yeye pia anaminya kivyetulio cha bastora yake, “paaah” unasikika mlipuko wa risasi, na risasi moja inaenda juu, huku mlipuko huo ukisikika hewani.
 
Hapo akashtuka ngumi nzito inatuwa usoni kwake, na kupasua mgongo wapua, wakati anasikilizia mchuzi wenye joto kwenye eneo la juu la mdomo, akashtuka mkono wake wenye bastora una zungushwa na kuishia kwenye goti la kijana huyu ambae anaroho ngumu, tofauti na sura yake.
 
Wakati huo huo kidole cha Lukas kinaminya kifyetulio, inayo fyrtua mtego wa nyundo, ambayo inagonga pini, inayo enda kugonga kitako cha risasi, ambacho kinakandamiza baruti ndani ya kasha la risasi, na kusababisha mlipuko, “phaaaa!” hapo gas kubwa ndani ya risasi inasukuma kichwa cha risasi, ambacho kinatoka kwenye ganda lake, nakupenya kwenye mtutu wa mm 4.0.
 
Risasi inaenda kugota kwenye paji la uso la Lukas, ambae tunafahamu kuwa ni ndugu wa damu wa bwana Tino Nyondo, mmiliki w kampuni ya usafirishaji, mtu ambae ajiulizi mala mbili juu ya utoaji wa adhabu kwa mtu alie mkosea.
 
Kila mmoja pale anatoa macho ya mshangao na mshtuko, ukiachilia kijana mdogo, ambae akuonyesha kushangaa wala kushtuka, Anastansia yeye alikuwa anamtazama kijana huyu, ambae sikuzote anamwona kama kijana ambae awezi kufukuza ata mbwa anae iba kuku, kutokana unyonge alionao.
 
Wakina kubaga nao walisahau maumivu yao kwa muda, na kutamtazama Lukas ambae alikuwa anajibwaga chini kama furushi, “tuondoke haraka, hapa siyo salama” alisema kijana mpole, huku anaanza kutembea, kuelekea upande wa chuo cha ualimu.
 
Anastansia anamfwata kijana mpole, kwa mwendo haraka, huku anageuka kuwatazama wale vijana wanne, ambao licha yakuwa nao walikuwa katika hali mbaya, lakini sasa walikuwa wanamtazama mwenzao aliekuwa amelala chini, damu zinavuja kwenye paji la uso.****
 
Naaaaaam!, sasa turudi makao makuu ya jeshi la polisi, mkoani Ruvuma, ambako bado, Insp Aisha na ASP Zamoyoni wapo kwenye benchi wanaongea ili na lile kabla ASP Zamoyoni ajachek saa yake ya mkononi.
 
“Aisha naona muda ndiyo huu, inabidi tuondoke zetu” anasema Zamoyoni huku anasimama na kujinyoosha kidogo, “kweli mwaya, ila tukitoka kwako, naenda nyumbani kulala” alisema Aisha huku nayeye anasimama na kujinyoosha kidogo.
 
“wala usiwe na wasi wasi, tukitoka nyumbani nakupeleka kwako moja kwa moja” alisema Zamoyoni, huku anasogelea gari, nafunguo mkononi, lakini kabla awaja fungua ata mmlango mmoja wa gari, mala wakasikia vishindo vya mtu anakuja mbio mbio, nao wakahgeuka na kumtazama.
 
Alikuwa ni askari wa mapokezi, “afande samahani, kuna taarifa imekuja sasa hivi, kuna tukio la kutupiana risasi, huko madizini matogoro, karibu na chuo cha ualimu” Aisha na Zamoyoni, wanatazamana kidogo.
 
Zamoyoni anamtazama yule askari wa kike mwenye cheo cha contable, “mh! taarifa imeletwa na nani?” anauliza ASP Zamoyoni, “tumepigiwa simu toka chuo cha ualimu, karibu na eneo la tukio” alijibu yule askari wa mapokezi, ambae alilazimika kuacha mapokezi, kuja kumweleza mkuu wake juu ya tukio ilo.
 
“ok!, mjulishe mkuu wa doria, mwambie askari waingie kwenye gari mala moja” alisema ASP Zamoyoni, huku yeye na Insp Aisha wanatembea kwa haraka kuelekea kwenye ghara la silaha.****
 
Naaaaaaaaaam!, nyumbani kwa mkurugenzi Haule, linaonekana Toyota land cruiser likiwa linaondoka, huku mzee Haule akipokelewa na mke wake, mama Eric, “vipi leo kunajipya lolote” aliuliza mzee Haule, huku anaongozana na mke wake kuingia ndani.
 
“unataka jipya gani wakati yazamani yamekushindwa kuyatekeleza” anasema mama Eric, akionekana kuwa amechukizwa na jambo flani, “mh!, mbona kama kunaaa…” awaza mzee Haule huku amesimama, anamtazama mke wake, nakujaribu kuwaza alicho kosea kwa mke wake. ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata