
TOBO LA PANYA (29)

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE: Wanatulia kwa sekunde kadhaa, wakiwatazama askari waliokuwa wanakagua eneo lile kuhakikisha usalama, na wanapo lizika na usalama, ndipo na wapo wanapo jitokeza na kuwasogelea wale vijana. ……..Endelea ….
“mh!, afande, mbona kama ni lile gari la wale vijana wapumbavu?” aliuliza Insp Aisha Amary, ASP Ayoub Mzee, ajibu kitu, zaidi ya kulitazama lile gari kwa macho yenye mashaka na bumbuwazi, huku wote wawili wanaendelea kutembea, kuwasogelea wale vijana, ambao walionekana kuchakazwa nakitu ambacho, kama siyo ajari basi kipigo kikali sana, toka kwa kundi la watu.
Nikama vile ASP Ayoub Mzee ajaamini anacho kiona, anatazama pale walipokuwepo wale vijana, kujilizisha kama ni wao ai siyo wao, lakini anawaona vijana wanne, ambao kila mmoja alikuwa anaugulia maumivu yake, hku askari wakijaribu kuwa kagua na kuwapa huduma ya kwanza.
“mmoja ameuwawa” anasema askari mmoja mwenye cheo cha koplo, na wote wawili yani Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee, wanatazama kule alipokuwepo mtoa taarifa, yani yule koplo, ambako wanamwona mtu mmoja akiwa amelala chini, na damu nyingi zilizoganda, zikionekana kwenye uso wake, kuanzia kwenye paji la uso.
“wapakizeni kwenye gari, tuwawaishe hospital” alisema ASP Mzee, huku akiongozana na Insp Aisha kusogelea pale alipokuwepo koplo, ambae sasa alikuwa amesimama kwa mwonekano wa kukata tamaa, maana mkono mmoja ulikuwa kiunoni na mkono mwingine kichwani, huku bunduki yake akiwa ameinung’iniza begani kwa kutumia mkanda wake.
Nao wanafika na kumtazama yule mtu alie lala chini, ambae akuitaji maelezo ya Doctor, kutambua kuwa alikuwa amesha poteza maisha, “mungu wangu, tayari yametimia” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti yenye mstuko wawazi kabisa, na kumfanya Insp Aisha amtazame marehemu kwa umakini, kama anaweza kukiona kilicho mshtuwa ASP Ayoub Mzee.
Lakini Insp Aisha aoni kitu zaidi, anao mwili wa mtu ambae anakila dalili ya kuwa alikuwa amepigwa risasi kichwani, “vipi koplo mbona kama umeshtuka sana, unamfahamu huyu marehemu?” aliuliza Insp Aisha, huku anasogelea pembeni na kuokota bastora, iliyokuwa mita chache toka alipo lala mwanaume kijana.
“anaitwa Lukas Nyondo, ni mdogo wa Tino Nyondo” anasema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti yenye kuanza kuchanganyikiwa, huku anatembea kuelekea kwa wale vijana, ambao sasa walikuwa wanabebwa na kupelekwa kwenye gari la polisi ili wapelekwe hospital.
ASP Mzee anamchagua mwenye uafadhari kidogo, ambae alikuwa amevunjwa mkono na kupasuliwa mdomo wa juu, “muuwaji amelekea wapi?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, mala baada ya kumfikia mmoja wao, “ameelekea chuo ni” alisema kijana huyu, ambae ni kubaga, huku anasaidiwa kupanda kwenye land rover defender.
“koplo waambie askari waliokuwepo kwenye gari lile, wapande kwenye gari wanifwate, wewe hakikisha unafikisha wagonjwa na marehemu hospital ya mkoa, na ili gari lao lifike kituoni” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anaelekea kwenye gari lake, yani Toyota crester, Insp Aisha akifwata nyuma.
Sekunde chache baadae, tayari magari yalisha chomoka pale migombani, kuelekea upande wa chuo, huku wakimwacha koplo na wale askari wengine, wanawapikiza wale vijana, pamoja na mwili wa marehemu, kwenye defender, tayari kwa safari ya hospital.***
Naaaaaaam!, wakati huo huo, kilomita kama tatu hivi toka migombani, upande wa chuo cha ualimu na uongozi wa jamii, wanaonekana watu wakiwa wanaondoka eneo la viwanja vya michezo, vya chuo, na kuelekea majumbani mwao.
Huku wanachuo, kwa maana ya wanafunzi, wakielekea kwenye mabweni yao, wengi walikuwa wanaongelea tukio la milipuko miwili ya risasi iliyosikika muda mfupi uliopita, katika hali ya ubishani, wapo walio sema ni tairi la gari lime pasuka, wapo walio sema itakuwa risasi, imelia kwenye kambi la polisi la jilani.
Upande wa mabweni ya waschana nako, mwanadada Farida nae anaonekana upande vyooni, akiwa na ndoo yake ya maji, amejifunga tauro kubwa kiunoni, juu ya vitenge viwili, mkononi ana kikombe chenye sabuni, atayembea uelekea bafuni.
Farida anapiga hatua kadhaa, huku anatafakari juu ya milipuko ya risasi aliyo isikia muda mfupi uliyopita, “ile milipuko ni ya bastora, ile ya kwanza ilienda hewani, ila yapili ili gota kwa mtu, je ni nani huyo?” anajiuliza Farida, ambae anaonekana wazi kuwa anauzoefu na silaha za aina mbali mbali.
Farida anatembea kidogo, na kuweka ndoo chini, kwamaana ya kupumzika kidogo, kisha anatazama mbele yake, upande wa kulia, kwenye barabara inayoelekea kwenye makazi ya walimu, ndio uelekeo wa mlipuko wa risasi uliko sikika.
Farida anajikuta anatoamacho kwa mshangao, ni baada ya kuwaona watu wawili, “mh!, huyu nae vipi tena?” anajiuliza Farida, ambae anamwona mwanadada Anastansia, ambae anakaa nae bweni moja, japo vyumba tofauti, lakini vilikuwa karibu.
Licha ya kumfahamu Nancy na tabia zake, uwezo na sifa zake, lakini akuwai kufikilia kama anaweza kuwa karibu na kijana huyu mpole, ambae kila siku jioni ua anakuja kwenye viwanja vya michezo, kutazama mpira wa kikapu.
Farida anawaona wawili wale wanatembea kuja upande wa mabweni, wakitokea upande wa nyumba za walimu, ambako kunauelekeo wa midizini, “sijuwi kama ausiki huyu” alijisemea Farida, huku anawenzake wanampita na kuelekea bafuni.***
Lakini wakati huo huo upande wa kaskazini wa chuo, yani upande wenye majengo ya walimu na wafanya kazi wa chuo, yaliyopakana na viwanja vikubwa ya michezo, ikiwa riadha na mpira wa miguu.
Tuna waona mwanadada Anastansia na kijana mpole, wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kawaida, kwa mwendo wa haraka, huku Anastansia akiwa mwenye uoga mwingi na hofu kubwa sana.
Anastansia anamtazama yule kijana mpole, kwa macho ya kumtafakari, lakini anakosa jibu, la kuwa huyu kijana ambae siku zote umwita dogo, ni mtu wa aina gani aswa.
Anashindwa kujielezea kwa kijana mpole, hivyo anaacha mpaka wanapo karibia sehemu ya kuingilia kutokea upande wa makzi ya walimu na wafanyakazi, “aya sasa nenda” alisema kijana mpole kwa sauti tulivu.
Lakini Anastansia aonyeshi dalili ya kuondoka, “tumeshafika dada, unaweza kwenda bwenini” alisisitiza kijana mdogo, ambae mpaka sasa atulijuwi jina lake, “kaka mwenzio mi naogopa” alisema Anastansia kwa sauti ambayo ilimaanisha anacho kisema, maana alionekana wazi kuto kuitaji kwenda bwenini.
“sikia dada, we nenda bwenini, hakuna mtu atakaye kufwata” alisema kijana mdogo, na wakati huo huo wakasikia ngurumo ya gari likija kwa speed kutokea upande wa waliotokea wao, yani kule midizini.
Ile wanageuza shingo zao kutazama upande ule, mita kama hamsini toka walipo, wanaona magari mawili, moja la kiraia na jingine la polisi, yakija kwamwendo wa kasi ya ajabu, huku lile la polisi, likiwa na askari kadhaa, wenye silaha.
Ndani ya gari la mbele, aina ya Toyota crester, unasikika mguno wa mshangao, toka kwa Insp Aisha, “afande, ebu mtazame huyo mwanamke alivyo mzuri” alisema Insp Aisha, huku wakiwatazama watu wawili waliokuwa wamesimama pembeni ya barabara, mita kama ishirini mbele yao, wakilitazama gari lao.
Bila kuongea neno lolote, ASP Ayoub Mzee, anakanyaga blakena kusimamisha gari, karibu na wale watu wawili, Insp Aisha anamwona yuple mschana mrembo akiwa mwenye uso wa uoga na wasi wasi, huku kijana mwenye sura ya upole akiwa pembeni yake. ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

