TOBO LA PANYA (30)

SEHEMU YA THELATHINI


ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA: Bila kuongea neno lolote, ASP Ayoub Mzee, anakanyaga blakena kusimamisha gari, karibu na wale watu wawili, Insp Aisha anamwona yuple mschana mrembo akiwa mwenye uso wa uoga na wasi wasi, huku kijana mwenye sura ya upole akiwa pembeni yake. ……..Endelea ….

“shikamoo” alisalimia kijana mpole, mara baada ya ASP Ayoub Mzee kushusha kioo cha gari, huku gari la polisi likisimama nyuma ya ili gari dogo, “marahaba kijana, eti kuna mtu mme mwona amepita hapa, amelowa damu, au ameshika panga au silaha yoyote?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, huku anamtazama yule mwanamke mrembo.

Anastansia ambae sasa alijuwa kuwa wanakamatwa na polisi kwa mauwaji ya yule kijana mkorofi, anamtaazama kijana mpole, ambae masaa machache alikuwa anamwita dogo, “hapana” alijibu kijana mpole, kwa sauti ile tulivu.

“nyie ni wanafunzi hapa chuo?” aliuliza ASP Ayoub Mzee huku macho yake yamemlenga mwanamke mrembo, “ndiyo niwanafunzi” safari hii anajibu Nancy, kwa sauti ya pupa na haraka sana.

“kuna sehemu ya kupiga simu hapa chuoni?” anauliza ASP Ayoub Mzee, “ndiyo, kuna call box pale bwaloni, au ofisini kwa mkuu wachuo, alisema Nancy ambae sasa alikuwa amesha ondokewa na uoga wote, baada ya kuona kuwa, hawa polisi hawa kuwa wanamjuwa wanae mtafuta.

Hapo bila kuongea kitu, ASP Ayoub Mzee anaondoa gari kuelekea upande wa chuo, likifwatia gari lenye askari, ambao pia walikuwa anamtazama Anastansia kwa macho ya matamanio.

“hivi ni kweli kulikuwa na aja ya kusimama pale?” anauliza Insp Aisha, huku anaachia kicheko cha sanifu, “mh!, we ungepita bila ata kumsemesha yule mtoto, yani mzuri kinyama, alafu yupo kichochoroni na kijana mshambaaaa” anasema ASP Ayoub Mzee, huku anaendesha gari kuyavuka majengo ya mabweni ya wanafunzi.

“atakama mshamba, lakini mwenzio ndie keshapenda” alisema Insp Aisha, huku anatazama upande wake wakulia, kumtazama mwanamke mmoja alie kuwa amesimama mita chache toka kweye banda lenye mwonekano wa choo, alie valia tauro, huku ndoo ikiwa pembeni yake.

“kuna wakati huwa najilahumu kuzeeka mapema” anajisemea ASP Mzee, “lakini siyo mbaya, maana kuna wakati vijana wenyewe wanakuwa wa ovyo, kama huyu ambae ameuwawa leo” alisema Aisha, “siyo jambo zuri Aisha, amini nakuambia, patachafuka hapa mjini, ata ule mpango wa kwenda kupumzika, achana nao” alisisitiza

Dakika chache gari lao linasimama mbele ya jengo la bwalo la chakula, ambalo upande wa mbele palikuwa na wanafunzi wengi wenye vyombo vya chakula, ikiashulia kuwa mida hii ya saa kumi na mbili, ndiyo mida ya chakula.

ASP Mzee anapekuwa mkebe wa kwenye dash board ya gari lake, na kutoa card ndogo yenye ndembo ya kampuni ya simu ya serikali, “wacha nimjulishe afande RCO, ajuwe atakavyo mjulisha mtu wake” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anashuka toka kwenye gari, akiacha Insp Aisha ndani yagari.

ASP Ayoub Mzee anatembea kufwata sehemu ya jumuhiya yakupigia simu, iliyoitwa call box, akiwa na card yake mkononi, bahati nzuri lilikuwa wazi hapakuwa na mtu menye kulitumia, hivyo anachomeka card yake na kunyakuwa mkonga wasimu, kisha anabofya namba flani za simu, na kuweka mkonga sikioni.

Sekunde cha baadae simu inapokelewa, “nyumbani kwa Zamoyoni Mpeta, nani mwenzangu” ilisikika sauti ya mwanamke mtu mzima, toka upande wapili wa simu.

“samahamani shemeji, naomba kuongea na afande Zamoyoni, kuna zarula” alisema ASP Ayoub Mzee, hapo ikafwata sauti ya mama mtu mzima, iliyokuwa inaitwa kwa mbali toka upande wapili wa simu, “baba Cathe!, baba Cathe!, kuna simu toka kazini” alisikika mke mwanamke mtu mzima upande wapili wa simu.

Hapo kimya kimya, vinasikika vishindo vikisogelea simu, “hallow Zamoyoni hapa, nani mwenzangu” alisikika SP Zamoyoni toka upande wapili wa simu, “ni ASP Mzee hapa, samahani afande, kuna taarifa ya tukio la mauwaji, huku madizini matogoro” alisema ASP Mzee.

“mauji gani tena mapema hii?” aliuliza RCO Zamoyoni, “afande kulitokea tukio la kurushiana risasi, lina wausisha vijana wa bwana Tino Nyondo, ambapo mtu mmoja ameuwawa na wengine wanne wamejeruiwa” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti tulivu, huku akisikilizia mapokeo ya mkuu wake wakitengo.

“nazani unajuwa la kufanya, kwa matukio anayo yafanya Nyondo, au vijana wake” alisema Zamoyoni toka upande wapili wasimu, “samahani afande, kwaili sina uwezo wa kufanya chochote, ndio maana nime lileta kwako” alisema Ayoub Mzee.

Hapo nikama anamshtua kidogo, SP Zamoyoni, “kivipi Ayoub Mzee, toka lini umeshindwa kushughulikia jambo dogo kama ilo?” anauliza SP Zamoyoni, kwa sauti ya ukali kidogo, “afande sidhani kama ni jambo dogo, vyema ukapata maoni, ya Tino Nyondo Nyondo, kabla atuja fanya lolote” alishauri ASP Ayoub Mzee mzee ambae bado alikuwa amesimama mbele ya call box, amaeshikilia mkonga wasimu.

“kwanini ishindikane, wakati siku zote uwa tunafanya hivyo, au unataka nionekane mpuuzi, mbele ya yule mjinga alie jawa nwa dharau?” anauliza RCO Zamoyoni, “sababu walio shambuliwa ni vijana wa Tino Nyondo, na alie uwawa ni mdogo wa Tino Nyondo…” kabla Ayoub Mzee ajamaliza kuongea, akakatishwa na SP Zamoyoni.

“hapana Ayoub Mzee, itakuwa ujatazama vizuri” ilikuwa ni sauti ya mshtuko mkubwa, toka kwa SP Zamoyoni, na kabla ASP Ayoub Mzee ajaongea neno lolote, akasikika tena RCO zamoyo, “vipi kuhusu wauwaji mme wapata, au kuwatambua?” anauliza Zamoyoni, kwa sauti yenya tahamani na mshtuko wa hali ya juu.

“tumefika kwenye eneo la tukio, na kukuta nuuwaji ambae alikuiwa peke yake, akiwa amesha kimbia” alijibu ASP Ayoub Mzee, “inamaana muuwaji ni moja tu, auliza Zamoyoni, kwa namna ya kushangaa.

Ndiyo afande, kwa maelezo ya wale wengine wanne, ni kwamba, mtu alie washambulia, ni mwanaume mmoja tu” anajibu ASP Ayoub Mzee, na upande wapili wa inasikika pumzi ndefu ya uchovu.

Kinapita kimya kifupi, kabla RCO ajavunja ukimya, “dah!, hii sasa ni vita, damu itamwagika sana hapa, mjini, sizani kama Tino Nyondo, atamwacha” alisikika Zamoyoni akiongea kwa sauti iliyopoa na kunyongea.

“ok!, nyie endeleeni kuchunguza juu ya muuwaji, hakikisheni mna mpata, mimi nampigia Tino Nyondo kumpatia taarifa, pia nijuwe anachukuwa uamuzi gani, nyie pia mkiwa na shida yoyote nijulisheni kwa haraka” alisema Zamoyoni kabla simu aija katika.****

Naaaaam!, eneo la chuo wanafunzi wanaonekana wakiwa wamesimama kwa makundi, wanajadiri juu ya ujio wa magari mawili, yenye polisi wenye silaha, ikiwa ni muda mfupi toka iskike milipuko ambayo mwanzo walizania ni mpasuko wa gurudumu la baskeri.

Wakati huo huo, upande wa mabweni ya wanawake, mwanadada Farida, alikuwa bado amesimama mita kadhaa, toka lilipo bafu, anatazama upande wa makazi ya walimu na wafanyakazi wa chuo, ambako sasa anamwona mwadada mrembo kuliko yoyote pale chuoni, yani Anastansia Anthony, akiwa na kijana mmoja mpole masikini, ambae mala nyiongi uja pale chuo kutazama mpira wa kikapu.

Farida anawatazama wawili wale ambao walionekana kuwa katika mjadara, mkali sana, nikama Anastansia, alikuwa na wasi wasi wa jambo flani juu ya kijana yule mpole, “sijuwi itakuwa wanausika na mlipiko wa risasi” anajiuliza Farida, ambae bado anawatazama wawili wale.

Farida anatamani kusikia maongeazi yake, lakini awezi, kusikia chochote, kutokana na umbali, lakini anaona itakuwa vyema kama ataendelea kusimama pale pale, ili kuweza kuona nini kitaendelea baada ya pale.

Lakini sisi tunaweza kusogea pale waliposimama wawili wale, na kusikia maongeazi yao, “kweli autakamatwa na polisi, mbona mimi naogopa sana” anasema Anastansia, mwanamke ambae kiukweli uwezi kumwona na ukaacha kumpa sifa ya uzuri alionao.

“usiwe na hofu dada, wewe nenda kapumzike, lakini kumbuka kuwa, ujaona kitu, wala ujuwi kitu chochote kuhusu mimi” alisema kijana mpole, kwa sauti tulivu, kama ilivyo kawaida yake, na kumfanya Nancy amtazame kwa macho ya mshangao.

Nancy anagandisha macho yake usoni kwa kijana huyu, ambae alikuwa amesimama mbele yake anamtazama, “sawa mimi naenda, lakini kesho naomba tuonane, siutakuja kunichukuwa hapa chuo?” analiuliza Anastansia, huku anamtazama kijana huyu mpole, ambae katika maisha yake, alimwona aklitabasamu mara moja tu, tena ni sekunde chache kabla ajaanza kutembeza kipigo cha maana.

“ndiyo” anaitikia kijana mpole, kwa sauti yake ya upole, sambamba na kichwa, na baada ya hapo Nancy anaanza kutembea kuelekea upande wa bwenini, huku mala kwa mala anageuka kumtazama yule kijana, ambae alikuwa bado amesimama anamtazama yeye.

Nancy anatembea hatua kadhaa, kisha anatazama tena nyuma, anamwona bado kijana mpole, anamtazama kwamacho tulivu kabisa, katika hali tata aliyo kuwa nayo Nancy, anashindwa kuelekwa kwanini kijana mpole anamtazama, je ni kwaajili ya kuhakikisha usalama wake, au anamtazama makalio yake, kama wanaume wengine wanavyofanyaga. …….Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!