
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TATU: Hapo ukafwatia mlio “tuff!,” sambamba na kilio toka kwa kijana yule, “mamaaaa ananiumiza macho” kusikia hivyo yule mwingine akamvamia Hance ambae kwa wepesi wa hali ya juu, alijiinua toka chini na kumdaka, kisha akambwaga chini. ……Endelea ….
Ile kijana anafika chini, akauona mguu wa Hance ukimfwaya usoni, akishinwa kuuzuwia na ukakita usoni kwake, na bomoa tena uso pamoja na pua, akishindwa kupiga kelele kama ilivyokuwa kwa huyu mwenzie alie tobolewa macho.
“jamani siwaoni, naomba mnisaidie siwaoni” alilalamika yule alie tobolewa macho, ambae licha ya kujuwa hatari iliyopo mbele yao, lakini alishindwa kuona njia ya kukimbilia.
Kijana alie kanyagwa usoni, aliona akizubaa anaweza kupoteza maisha, hivyo akiwa pale chini, anatupa mguu wake wakulia na kupiga Hance kifuani, nakumfanya Hance aanguke pembeni.
Hapo kijana ambae sasa alikuwa amelowa damu uso mzima, aliinuka haraka, huku anatema damu iliyo changanyika na vipande vya meno, hapo Hance ambae ni kama alipandwa na mapepo, akumpa nafasi kijana huyu, ambae amemzidi umri, ili ajiandae.
Alimfyetua mtama wa nguvu, na kumfanya kijana yule arudi chini kama furushi la pamba au tumbaku, akifikia kiuno, na kumsababishia maumivu makali sana.
“nisamehe kaka, siyo mimi ni huyo Beka, ndiyo mwenye demu wake, siyo mimi” ombeleza yule kijana, ambae alimwona huyu kijana mdogo, ambae muda mfupi uliopita, alikusudia kumwingilia kimwili, akimsogelea bila kuongea neno.
Hance ambae alikuwa tofauti na yule tunae mfahamu yani mcheshi na mchangamfu, anamsogelea yule kijana na kuanza kumkanyaga usoni, kama alikuwa anauwa mdudu mwalibifu, kijana akishindwa kujitetea, na kuacha miguu ishuke usoni kwake, na wakati mwingine kwenye shingo, kiasi kwamba ikafikia wakati akalegea na kutulia kabisa.
Hance anasimama kwa sekunde kadhaa, ameganda kama sanamu, akimtazama yule alie mkanyaga kanyaga, anagundua kuwa amefanya kosa kubwa sana, maana licha ya kupiga mara kadhaa, lakini hakuwai kumuumiza mtu namna hii.
Hance anamtazama Beka, ambae alikuwa amelala ka tulia, kama huu mwingine, dimwi la damu likionekana pembeni yake, huku kipande cha kijiti, kikiwa kina ning’inia kwenye koo lake.
Hapo Hance analiona balaha mbele yake, ni wazi anatakiwa kuondoka mala moja asikamtwe kabla ajaonwa na watu wengine, maana alijuwa fika kuwa kitendo alicho kifanya ni kosa kubwa kisheria.
Lakini kabla ajainua mguu wake, akamwona yule alie mtoboa macho, akamtazama kwa sekunde kadhaa, akifikilia amuuwe au amwache, lakini roho ya huruma inamwingia na kuamua kumwacha.
Hance anapiga hatua kadhaa, kuelekea barabarani, lakini akasikia sauti ya yule mwingine, “we mshenzi umenipasua macho, alafu unaniacha hapa, nakwambia lazima ufungwe, nitawaeleza polisi kila kitu” alisema yule mmoja alie bakia, na kumgutua Hance, ambae alimtazama yule jamaa ambae alikuwa amesimama, pasipo kujuwa pakuelekea.
Hance akuongea kitu chochote, zaidi anatazama anautazama mwili wa Beka, na kuusogelea, kisha anachukuwa kile kipande cha mti, ambacho kilikuwa kina ning’inia shingoni kwa Beka.
Anamsogelea huyu kijana ambae aoni chochote, huku ameshikilia kipande cha mtui kwa mkono wa kulia, “unataka kunifanya nini, niache usino sogelee” anasema yule kijana huku anatupa ngumi hewani, akikusudia kumpiga Hance.
Dah!, inaitaji roho ngumu kidogo kuelezea kilicho tokea, ila ka kifupi ni kwamba, sekunde chache baadae, tayari yule kijana alikuwa amealala chini, huku kipande cha kijiti kikiwa kina ning’inia kooni mwake, damu zina mtoka kwa fujo, kijana anakoroma kama mbuzi anae chinjwa.
Bila kuchelewa wala kusubiri, Hance ambae alikuwa amejwa na hofu na bumbuwazi, anaingia zaidi kichani, akiacha ile njia ya kwenda kutokea barabara kuu.
Hance anaibukia kwenye bonde la mto, nakuvukia ng’ambo, ambako ni makambi, kisha anatembea huku akiwa mwenye hofu kubwa na wasi wasi, akikatiza kwenye majumba na chochoro za mitaa ya makambi, mpaka anapo ibukia barabara kuu.
Hance anatembea kwa haraka, akipandisha kueleka mtaani kwao, ambako ni makambi juu, ata alipofika usawa wanyumba ya wakina Lulu, ambapo ilimlazimu kupita kabla ya kufika kwao, anamwona Lulu amekaa kibaradhani na baadhi ya ndugu zake.
“Hance!, we Hance njoo kwanza” alipaza sauti Lulu, lakini kiukweli Hance akutaka ata kumtazama mara mbili mschana huyu, ambae kwa mara ya kwanza amemfanya awe muuwaji.
Hance anatembea kwa haraka kueleka nyumbani kwao, ambako alifika saa mbili na dakika alobaini na tano, akiwakuta wazazi wake wapo sebuleni wanapata chakula cha jioni.
Hance anapita kimya kimya mpaka chumbani kwake, ambako anasimama katikati ya chumba akiitazama mikono yake iliyo lowa damu zilizoganda, huku nguo zake, zikiwa zimelowa damu kama alitoka machinjioni.
Ni wazi wazazi wake walisha iona hali na mwonekano wa mtoto wao, ambae licha kuzowea na kupokea kesi, na taarifa na mapigano ya kila siku, lakini akuwai kufikia hali kama hii.
Baba na mama wote wanavamia chumba cha Hance, wakizania mtoto wao alikuwa ameumia, “mwangu umepatwa na nini, mbona umelowa damu namna hii?” aliuliza mama Hance kwa sauti ya kuchchwa, iliyo jawa hofu na kukalibia kuangua kilio, huku wote wawili wanamkagua mtoto wao wapekee.
“hapana ajaumia, sijuwi ni damu za nani” anasema mzee Johnson, huku anamaliza kumkagua Hance, ambae alikuwa kimya, pasipo kuongea chochote, “Hance imekuwaje lakini we mtoto, mbona unataka kusababisha matatizo jamani?” anasema mama Hance, lakini Hance akuongea lolote.
“sikia mama Hance, tunapaswa kukaa kimya, tusubiri kesi, maana huyu ni wazi awezi kuongea chochote” alisema mzee Johnson, “sawa baba Johnson, lakini kunasiku watamuumiza huyu mtoto, sijuwi tunaliaje, maana mtoto mwenyewe ni mmoja tu” alisema mama Johnson akimlalamikia mume wake.
“kuna wakati lazima tujuwe kuwa, kama siyo mpinzani wake kutoka damu, basi izi damu zingetoka kwake, lazima ajipambanie” alisema mzee Johnson, uku anamtazama Hance, “ni kweli lakini, basi ngoja nikamwekee maji ya moto bafuni” alisema mama Hance, huku anatoka chumbani kwa Hance na kuelekea jiko la nje, ambalo utumia kuni.
Mzee Johnson anabakia na kijana wake, anajaribu kumdodosa, kuhusu kilichotokea, lakini Hance aongei kiti chochote, “aya komandoo, vua nguo ukaogoe, hizo nguo peleka jikoni zikachomwe moto” alisema mzee Johnson, huku anatoka chumbani kwa Hance.
Siku iliyofwata, Hance aliendelea kuwa mtulivu na mkimya, kiasi cha kuonekana kama mnyonge, siku ya pili zikianza kuzagaa taarifa ya kutoweka kwa vijana watatu, ambao ni watoto wa askari wa jeshi la polisi, waliokuwa wanasoma kiadato cha nne, Ruvuma sekondari.
Watoto ambao miili yao ilipatikana siku ya tatu, kwenye vichaka vya mto Makambi, ikiwa imeshaanza kuaribika, kwa kuoza na kuliwa na mbwa, habari ambayo kwa bahati nzuri, Lulu akuunganisha na tukio la kufukuzwa siku ile usiku, ni tukio ambalo lilizidi kumduwaza Hance, ambae alizidi kuwa mtulivu kama zezeta. ……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU