
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA NNE: Watoto ambao miili yao ilipatikana siku ya tatu, kwenye vichaka vya mto Makambi, ikiwa imeshaanza kuaribika, kwa kuoza na kuliwa na mbwa, habari ambayo kwa bahati nzuri, Lulu akuunganisha na tukio la kufukuzwa siku ile usiku, ni tukio ambalo lilizidi kumduwaza Hance, ambae alizidi kuwa mtulivu kama zezeta. ……Endelea ….
Taharifa hiii ilizuwa taharuki kubwa sana, katika mji wasongea, na kusababisha watu waishi kwa tadhari, wakiamini kuwa kuna kikundi cha wauwaji, wanatekeleza mauwaji hayo, sababu kile alie hadithiwa ualibifu wa miili ya vijana wale, aliogopa sana.
Siku zilienda, huku polisi wakiaidi kuwakamata wausika, kupitia uchunguz uliokuwa unaendelea, huku kijanahance akianza kubadirika taratibu, kutoka kwenye utulivu wa kupitiliza na kuwa katika hali ya utulivu wa upole, akiacha kupigana akiacha uchokozi, akiacha kujichanganya watu, kwa kuofia kulazimishwa kuingia kwenye ugomvi, ambao ameshaona madhara yake kuwa ni mabaya.
Lakini licha kuamua hivyo, kuna mambo mawili mabaya zaidi yakaanza kujitokeza kwake, moja ikiwa ni kuanza kunyanyasika, kwa kupigwa na wenzake mara kwa mara.
Kibao kiligeuka, na kuwashangaza wazazi wake, ambao sasa walikuwa wanapokea kesi za kupigwa kwa mtoto wao, na siyo mtoto wao kupiga watu wengine, kilicho mchukiza zaidi mzee Johnson na mke wake ni kitendo cha wazazi wengine, ambao walionekana kufurahishwa na kitendo cha watoto wao kumwonea Hance.
Mzee Johnson alijaribu kuongea mala kadhaa na Hance, akimwuliza kwanini anakubari kuonewa kiasi kile, lakini Hance akujibu chochote, au angetoa jibu moja tu, “sitaki ugomvi na watoto wawatu” tena kwa sauti tulivu ya upole.
Ilimshangaza sana mzee Johnson, ambae alijaribu kuunganisha tabia mpya ya Hance na tukio la lowa damu, lakini hakupata jibu, ni kilitkea mpaka mtoto wake amekuwa na tabia kama hii.
Kitu ambacho hakuna alie juwa kuhusu tabia mpya ya Hance, ni kwamba, alikuwa anashikwa na hasira ya hali ya juu sana, pale anapoona mtu anamletea dharau, au kujaribu kumtishia amani, au kumwonea mtu mwingine.
Na mbaya zaidi nikwamba hasira zake ambazo alitumia nguvu kubwa kuzizuwia, mara zote zilimpa ushauri wa kuuwa au kumvunja vunja mtu alie sababisha hasira hizo.
Mtu wa kwanza kujuwa hasira za kijana huyu, alikuwa ni bwana Kingumwile, ambae wakati huo alikuwa mkulugenzi wa mawakara wa siri wa usalama wa taifa na majukumu ya siri ya nchi, ilikuwa siku ile ambayo alivamiwa na kutaka kuuwawa, na Hance akaja kumsaidia.
Tukio ambalo lili sababisha Kingumwile, kuamua kumwajili kwa siri kijana huyu, akimpatia namba ya uwakara 26, sawa na tarehe yake ya kuzaliwa, huku mkataba wa mwanzo, ukiacha kuto kuwa usisha wazazi Hance, na mkataba ukisema hakuna kujuwana familia wala kazi.
Hance anafanya majukumu makubwa ya siri, yenye hatari na ukatili mkubwa, katika umri mdogo, huku akichukuliwa kama SA mwenye maamuzi ya ghafla yenye kuitaji roho ngumu sana, asa linapo kuja swala la kutoa roho ya mtu.
Mkataba wa pili uliandikwa mwaka 1998, baada ya Hance kumaliza shule, huo uliwausisha wazazi wa kijana Hance, ambae aliamishiwa makao makuu ya shirika ilo la siri, huko dar es salaam, wakati bwana kingumwile akiwa mlugenzi wa idara iyo mkoa wa dar es salaam.
Kijana Hance, kutokana na ujasiri wake na matukio aliyo shiriki, anapata nafasi ya kwenda #Mbogo_Land, kupata mafunzo ya kijeshi, na matumizi silaha, mbali mbali za kivita, ikiwa ni pamoja bunduki ndogo ndogo, kiwango cha kati, na zile za juu.
Pia visu vya aina mbali mbali, ikiwa ni vidogo, visu vikubwa, pamoja na mafunzo ya mapigano ya kutumia mikon mitupu, nambinu mbali mbali za kujilinda, au kujitoa kwenye mikono ya adui, na kubadiri kitu chochote kuwa silaha.
Miezi kumi na mbili, aliyokuwa na wakufunzi wenye uwezo wa hali ya juu, wa ARU, ndani ya LS Base, huko nchini Mbogo #Mbogo_Land, akiuzulia mafunzo ya Amour Racce Spacial Force.
Ata baada ya kurudi Tanzania, na kufanya majukumu yake kwa ufanisi wakiwango chajuu, katika kitengo cha KMT, kwa urefu unaweza kuita killing Machine Team, ambako ndani ya miaka miwili alitekeleza mauwaji mengi sana, ya watu ambao kwa namna moja au nyingine, ni hatari kwa taifa au ni chanzo cha kuhatarisha amani ya raia wenzake.
Akiwa kama wakara wa daraja la juu la usiri, SA-26, alifikia kiwango cha juu cha utekelezaji wa mauwaji, kiasi cha mawakara wenzake, kuanza kumwogopa, kwakumwona siyo binadamu wa kawaida, au ni mtu alie changanyikiwa kwa damu alizo mwaga.
Kuna wakati, alitekwa na kundi flani la majajusi, linalo milikiwa na tajiri mmoja toka nchini urusi, mashuhuda walisema alitekwa na watu watatu, walio kuwa gari aina ya land rover mia na kumi, taarifa ambayo ilimshangaza kila mmoja, maana ilikuwa idadi ndogo ya watu, ukilinganisha na uwezo aliokuwa nao SA-26.
Baada ya kupata taarifa za uhakika juu ya sehemu aifadhiwa, kuanzia ulinzi na idadi ya watu 30 walio kuwepo na silaha wazo kuwa nazo, pamoja na mbwa zaidi ya kumi wenye mafunzo na uzowefu wa kuuwa na kula nyama ya binadamu, SA wakakata tamaa ya kwamwokoa SA-26.
Lakini basi, wakiwa wamesha kubari kumpoteza wakala huyu muhimu, kwenye kitengo cha KMT, wakashangaa jioni ya siku ile ile, wanapata taarifa ya kwamba, wakala huyu wa siri, anaendelea na majuku yake kama kawaida.
Ata walipo fwatilia, SA-26, amewezaje kutoka katika mikono ya wateka, ndipo walipo shangazwa, kwa kugundua kuwa, SA-26, alifanikiwa kuuwa kundi zima, pamoja mbwa wao, huku akiteketeza mahabara ya kuzalishia dawa za kulevya, pamoja na tani kadhaa za dawa hizo.
Hapo siyo tu mawakala wenzake, ila pia kitengo cha TSA nzima ilizidi kumwogopa SA-26, kutokana na mauwaji ya kikatili aliyo yafanya, maana hakuna jasusi ata mmoja alie tazamika mara mbili, kwa kifupi kijana Hance alikuwa amewaponda vibaya sana majusi wale, pamoja na mbwa wao.
Lakini miezi minne baadae, SA-26, anaingia kwenye tukio kijingine, la kuuwa vijana nane ambao walikuwa wanajaribu kumbaka mschana mmoja, kwenye mkesha wa mwaka mpya, wa kuingia mwaka 2000.
Na ndio tukio ambalo, SA-26, alipokamtwa na polisi, na kuwapanamba ya mkulugenzi kingumwile, ambae wakati huo alikuwa ndie mkulugenzi wa kitengo cha SA jiji la dar es salaam.
Tukio ambalo lilikuwa la mwisho akiwa SA, kwamna week moja baadae, alipeleka ombi la kuacha kazi, licha ya kupokelewa na kukubaliwa kwa ombi lake, lakini hakuna alie ajuwa sababu ya SA-26 kuacha kazi ghafla namna ile, kitu ambacho, kilileta maswali mengi kwa wakuu wa idara ya TSA, huku majibu yakiwa mengi.
Wapo walio hisi kuwa, SA 26 ameajiliwa na shirika flani la kijasusi, wapo walio hisi kuwa, SA 26 amelipwa fedha kwaajili ya kazi flani ya kuhujumu serikali, pia kuna agent mmoja, alisema kuwa, bado ajajiunga au kulipwa na kundi lolote, ila yeye mwenywe, anaweza kuwa hatari kwa taifa, naikawa vigumu, kwa tahasisi nyingine za usalama kumthibiti.
Hivyo wote kwa pamoja wakakubariana kuwa, SA-26 atafutwe na auwawe, haraka iwezekanavyo, kwa usalama wa taifa, na bila kuchelewa wakachaguliwa watu sita, kwaajili ya kuanza msako mara moja.
Lakini katika hali isyo ya kawaida, kumbu kumbu zote za SA-26, zikatoweka, kuanzia taarifa zake, mpaka picha na maelezo binafsi ya kijana huyu, ambazo zilitunzwa kwenye computer za makao makuu ya TSA, haikujulikana ninani alie futa kumbu kumbu izo. ……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU