
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA SABA: “saa mbili kasoro tano, siyo kawaida yak…..” kabla mzee Johnson ajamaliza kusema alichokuwa anasema, mala wakasikia sauti ya mschana wakazi, upande wa mlango wa jikoni, uwa tunaita uwani. ……Endelea ….
“karibu kaka Hance” sauti ambayo ili leta ujumbe ambao, ulifungua furaha nioyoni mwa wazazi hawa wawili, ambao nyuso zao zilikunjuka, “asante” ilikuwa nisauti ya chini yenye utulivu wa hali ya juu, sambamba na vishindo vyepesi vilivyo sikika vikija upande wa sebuleni.
“atajwi huyu mtoto” anasema mama Hance, huku uso wake ukionyesha furaha ya wazi kabisa, “huyu ni kama mvua za majanga, uwa azitajwi hovyo” alisema mzee Johnson, huku yeye na mke wake wanatazama upande wa kolido la kutokea jikoni.
Wote wawili wanamwona Hance akiwa anaibukia toka kwenye kolido, mwenye uso ulipoa, japo ni kawaida kumwona Hance akiwa hivi, ila kwa mtu ambae anamfahamu vyema Hance, lazima angejuwa kuwa, leo Hance alikuwa tofauti kidogo.
“shikamoo baba, shikamoo mama” alisalimia Hance, huku anafwata moja kati ya makoch mzuri ya kisasa, yaliyokuwepo pale sebuleni, “marahaba Hance” waliitikia wote wawili kwa pamoja, lakini mzee Johnson akaendelea.
“vipi Hance, mbona hivyo kuna tatizo, alafu hapo mkononi mbona kama kuna…?” aliuliza mzee Johnson, ambae anashindwa kuweka sawa swali lake, maana wakati huo huo, dada wakazi nae alikuwa anaingia.
Lakini ni wazi kabisa, Hance alisha elewa swali la baba yake, maana alijitazama kwenye mkono wa kulia, akaona kuna alama ndogo ya damu, kisha kinapita kimya kifupi, mpaka dada wakazi alipomaliza kuweka sahani mezani, na kuelekea upande wajikoni.
“wamenirudisha katika maisha ambayo ninayachukia” alisema Hance, kwa sauti iliyopoa, “kivipi Hance, inamaana umepigana?” aliuliza mke wa mzee Johnson, kwa sauti ya chini yenye mshangao na tahadhari, “aikuwa kusudio langu, walinichokoza, walinitishia bastora” alisema Hance kwa sauti yenye masikitiko makubwa.
“naimaini italeta shida kwako, auna haja ya kuuzunika” alisema mzee Johnson, kwasauti yenye kumwondoa wasi wasi Johnson, “lakini sipendi kuendlea kuwa hivi, naitaji niishi maisha ya kawaida kama watu wengine, niwe na familia yangu, nao waishi katika amani na usalama” alisema Hance akionyesha msisitizo.
Hakika maneno hayo yaligusa mioyo ya wazazi wa Hance, ambao walitazamana, na kabla awaja jibu lolote, mara ukasikika mlio wa simu, toka upande wa kushoto wa sebule, ambakp kuna meza ndogo yenye simu juu yake.
Bila kujiuliza mala mbili, Hance akainuka na kwenda kupokea simu, nikawaida mtu yoyote kupokea simu, kisha kumwita anae itajika kuongea na ile simu, ndiomaana Hance alipo pokea simu akasikika akisema, “hallow! nyumbani kwa mzee Johnson hapa” ilikuwa sauti ile ile tulivu.
“Hance sikiliza toka kwangu” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima,, iliyosikika kwa usikivu wa mnong’ono, toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo ilimfanya Hance ashtuke kidogo.
“nakusikiliza mzee Kingu, vipi kuna shinda” aliongea Hance kwa sauti tulivu ya chini, “rudi chuo cha uharimu, ukamchukue mschana Anastansia Anthony, yupo hatarini kwa sasa” alisikika mwanaume mtu mzima, wa upande wapili wa simu.
“ni haraka sana mzee, kwa wewe kusikia jambo ili” alisema Hance akionyesha maska ya wazi juu ya usambaaji wa habari za tukio lililotokea masaa mawili yaliyopita.
“sababu mtu ambae me muuwa ni ndugu wa mtu hatari sana, asie fikilia mara mbili anapooamua kutoa roho ya mtu mwingine” alisema mwanaume mtu mzima upande wapili wa simu.
“unazani natakiwa kumwogopa, au kuna hatari kubwa, iliyopo mbele ya Anastansia” alisema Hance kwa sauti tulivu ya chini, huku anawatazama wazazi wake, ambao japo walikuwa katika hali ya utulivu, pasipo kumtazama Hance, wakijaribu kufwatilia maongezi yake.
“Anastansia ni mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa #Mbogo_Land, bwana Anthony Mchopa, alie mzaa ma mpenzi wake wa zujana, wa hapa nchini kwetu, na huyo Anastansia, kwa sasa ndie mtu pekee anae kufahamu kama muuwaji wa mdogo wa tajiri na jambazi hatari, bwana Tino Nyondo, ambae kwa namna yoyote, lazima wataenda kumchukuwa huyo binti kwa lengo la kukupata wewe” alisema bwana Kingu, ambae ni mkurugenzi wa mawakara wasiri wa usalama wa nchi.
“kitu ambacho unapaswa kukizingatia ni kwamba, Nyondo ajawai kumwacha mtu akiwa mzima, lazima ata sababisha kifo cha mwanamke huyo baada ya kumbaka, na hapo atasababisha msako mkubwa sana” alisema mwanaume mtu mzima, toka upande wapili wa simu.
“maana #Mbogo_Land awato kubari, kuliacha swala ili, na hapo ndipo utakapo anza uchunguzi, utakao kubainisha, na kama nilivyo kudokeza ni kwamba, utakiwi kuingia mikononi mwa TSA” alisema mwanaume mtu mzima, toka upande wapili wa simu.
Hapo zilitumika sekunde chache sana, kwa tafakari ya na uvutaji wa kumbu kumbu, maana Hance alikumbuka uzuri na ukalimu wa Anastansia mschana alie shinda nae kutwa nzima ya leo, pia akakumbuka dalili ya kile ambacho wale vijana walitaka kumfanyia mschana huyo, akajuwa kuwa akichelewa kuna jambo litamkuta Anastansia.
“sina namna inabidi ni rudi kazini, nitumie maelezo zaidi ya Tino Nyondo” alisema Hance kisha akarudisha mkonga wa simu juu ya simu yake, kisha akaanza kutembea kuelekea pale walipokaa wazazi wake, yani seating room.
Baba na mama Hance wanamtazama Hance, kwa umakini mkubwa sana, wakijaribu kupima uzito maongezi aliyotoka kuyafanya, “mama na baba natakiwa kuondoka, kunamtu ananiitaji” alisema Hance, huku anaendelea kutembea akikatiza sebuleni, yani pale seat room, akilifwata kabati la vyombo.
“lakini chakula tayari mwanangu, kwanini usisubiri” anasema mama Hance, huku yeye na mume wake wakimtazama Hance, ambae alikuwa anachukuwa funguo ya gari ju ya kabati la vyombo pale sebuleni.
“sina muda wa kusubiri nienda kupika nyumbani” alisema Hance, huku analifwata kolido la mlango wa jikoni, kule ambako ingilia, huku mama na baba yake wanamsindikiza kwa macho, mpaka kijana wao alipotokomea nje.
“sijuwi kuna nini huko” anasema mzee Johnson, yani baba yake Hance, huku anamtazama mke wake, “lakini alisema ameshaacha kazi, sasa hii inamaana gani?” anauliza mama Hance.
Dakika chache baadae wanasikia ngurumo ya gari upande wa mbele wa nyumba yao, ambalo lina unguruma kwa sekunde chache, kabla ya kuanza kuondoka, huku ngurumo kitokomea upande wa mashariki.****
Naaaaaaam!, turudi seed farm B, nyumbani kwa mkurugenzi Haule, wanaonekana Eric, Eva na Vestina, watoto na na rafiki wa kike wa mkurugenzi Haule, wakiwa sebuleni, wamevalia mavazi nadhifu, yaliyo ashiria kuwa, walikuwa wanaenda matembezi usiku huu.
Sekunde chache baadae, mzee Haule na mke wake, wanaibuka wakitokea upande wa chumbani kwao, “mnasubiri nini kwenda kwenye gari, tumechelewa sana, Eric chukuwa funguo” alisema mzee Haule, akimaanisha kuwa Eric ndie dereva wao usiku wa leo.
“baba, namini nifundishe kuendesha gari” alisema Vestina, kwa sauti ya kudeka, “nitakufundisha mwanangu, ondoa shaka” alisema mzee Haule, wakati huo Eric alikuwa anachukuwa funguo ya gari kwenye drow ya kabati dogo, la vitabu pale sebuleni.
“hakuna kumfundisha kuendesha gari mpaka afike form two” anasema mama Eric, huku anatembea kuelekea kwenye mlango wa kutokea nje, na wakati huo huo simu ya mezani pale sebuleni inaanza kuita, “bora iwe simu ya maana” anasema mzee Haule, huku anaisigelea simu juu ya sturi ndogo, pembezoni mwa kochi dogo la mtu mmoja.
Mama Eric anasimama karibu na mlango huku Eva akiwa pembeni yake, wote wanamtazama mzee Haule, ambae anainua mkonga wasimu toka kwenye kikalio chake, na kuweka sikioni, “Haule hapa, nani mwenzangu” aliongea Haule kwa sauti yenye tahadhari.
“Mahundi hapa, kuna jambo unatakiwa kulisikia” ilisikika sauti ya kiume, toka upande wa pili wa simu, “nakusikiliza Mahundi” alisema mzee Haule, ambae alionekana kuwa katika umakini mkubwa. ……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU