
TOBO LA PANYA (39)

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA NANE: “Mahundi hapa, kuna jambo unatakiwa kulisikia” ilisikika sauti ya kiume, toka upande wa pili wa simu, “nakusikiliza Mahundi” alisema mzee Haule, ambae alionekana kuwa katika umakini mkubwa. ……Endelea ….
“kuna tukio la mauwaji huko midizini matogoro, karibu na chuo cha ualimu, lime usisha kijana mmoja anae fahamika kwa jina la Lukas Nyondo, huku wenzake wanne wakijeluhiwa vibaya sana na muuwaji, ambae kwa maelezo ya moja ya vyanzo vyetu vya habari, pale hospital ya mkoa, kama alivyo nasa maongezi ya Tino Nyondo, inawezekana kabisa, akawa ni SA-26” alieleza Mahundi upande wapili wa simu.
Haule anaonekana kushtuka kidogo, “achana na huyu kijana mpuuzi, alie uwawa, nyie mmefanya juhudi gani, kumpata huyo mnae mhisi ni SA-26” anauliza mzee Haule kwasauti ya chini yenye shahuku.
“njia ya kumpata huyo jamaa, ni kumpata huyo mwanamke, ambae ni mwanafunzi wa chuo cha ualimu, lakini hapo kuna tatizo, sababu mpaka sasa, tayari vijana wa Tino Nyondo Nyondo, wapo njiani wanaenda kumchukuwa huyo mwanamke hapo chuoni” alisema Mahundi.
“sikia Mahundi, kama huyo mwanamke ni muhimu kwa SA-26, lazima atamfwatilia, mara tu Nyondo atakapo mteka, na pengine, akaitaji kuzuwia utekaji wake, hivyo basi, weka mtu afwatilie kwa ukaribu matukio na mienendo ya hao wakina Nyondo” alisema mzee Haule, kwa sauti ya chini, kama alivyo fanya muda wote wa maongezi.
Baada ya hapo mzee Haule akakata simu na kumgeukia mke wake, “sasa mnasubiri nini, mimi nilizania mmesha fika kwenye gari” anasema mzee Haule, huku anapiga hatua kuufwata mlango wa kutokea nje, ambako mke wake na Eva, walikuwa wamesimama karibu yake.
“mh! we mwenyewe ulishajuwa mtoko umesha vurugika hapo, maana hizi simu za usiku, zina balaa lake hizi” alisema mama Eric, huku anafungua mlango na wote wakaanza kutoka.****
ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, wanatembea kwa tahadhari wakilifwata gari aina ya land rover mia na kumi, rangi nyeupe, namba za kiraia, linalo milikiwa na jeshi la polisi na kutumiwa na mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai, mkoa wa Ruvuma.
“sijuwi anataka kutuambia nini huyu” anasema Ayoub Mzee, kwa sauti ya chini, huku Insp Aisha akiishia kuguna kwa kukata tamaa, ikifwatia na ukimya mkubwa mpaka walipolifikia gari, “mnaenda wapi?” anauliza RCO Mpeta, aliekuwa ndani yagari, huku anawatazama wote wawili kwa hawamu.
“afande tulikuwa tunaelekea….” Alisema ASP Ayoub Mzee, ambaer alisita kidogo na kumtazama Insp Aisha, “msiangaike kutafuta jibu, najuwa mnataka kufwatilia kikundi cha Nyondo” alisema RCO Mpeta, huku anawatazama kwa zamu wawili awa.
ASP Ayoub Mzee, anatabasamu kwa aibu ya kufumaniwa, huku anamtazama Insp Aisha, nikama alikuwa anamtaka asema chochote, lakini anakuta nae akiwa anamtazama uso wake ukiwa ume tawaliwa na tabasamu la aibu kama yeye, maana wote wawili walisha juwa kuwa, wamekiuka amri ya mkuu wao wakufwatilia habari za mtu huyu.
ASP Ayoub Mzee anapiga moyo konde na kukubari jibu la mkuu wake wakazi, “ni kweli afande, ila lengo letu, ni kupata taarifa za kile kinachoendelea” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti yenye tahadhari kubwa, maana alijuwa tayari yupo kwenye makosa, ya kufwatilia habari za bwana Tino Nyondo.
“lakini nilisha waonya juu ya kufwatilia habari za mtu huyu” alisema RCO Mpeta, huku anatatazama kwa awamu wote wawili, ambao sasa walikuwa wameinamisha vichwa vyao chini, kwamaana ya kukosa jibu.
“ok! sasa nawapa luksa, ya kufwatilia lakini hakikisheni, amfikishi kwa taarifa hizi kwa mtu yoyote zaidi yangu” alisema Mpeta kwa sauti yenye msisitizo, huku akiwatazama kwa hawamu wote wawili, yani kama alivyo fanya tokea mwanzo.
Hapo Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee, wanainua nyuso zao zikiwa zenye tabasamu, na kumtazama mkuu wao wakazi, kabla awaja tazamana wenyewe, kama ambao awakuamini walicho sikia.
“afande na kuhakikishia, kuwa wewe ndiyo utakuwa wakwanza kupata habari kabla ya mtu yoyote” alisema ASP Ayoub Mzee mzee, kwa sauti yenye uhakika wa kiwango cha juu, “aya fanyeni haraka, muwai huko wanakoelekea” alisisitiza Mpeta, na hapo askari wawili awa wangazi ya gazeted afisa, wakaaga kijeshi na kuondoka zao, kuelekea kwenye gari lao na safari ikaanza mala moja.****
Naaaaaaam!, eneo la chuo cha matogoro, lililofunikwa kwa giza kwa asilimia kubwa, kasoro kwenye madarasa na bweni, hii ni kutokana na ukongwe ulio sababisha miundo mbinu mingi kufa, mfano taa za kwenye njia, na barabara za ndani ya chuo, yalionekana kuwa tulivu kwa kiasi flani.
Mida hii, wanaonekana wanafunzi wa chuo cha ualimu na uongozi wa jamii, kwa uchache, wakipita kwenye njia za kuelekea madarasani, ambako kwa ratiba za chuo, mida hii kuna kuwa na vipindi vya maandalizi na kujisomea wao wenyewe, ni baada ya kupita kwa vpindi vya dini mbali mbali.
Lakini kwenye bweni moja la wanawake, anaonekana mschana mrembo Anastansia, akitokea kwenye chumba chake, alie valia tauro kubwa na refu, juu ya kitenge, alicho jifunga kwa ndani, mkononi akiwa na ndoo tupu, pamoja na kibeseni ya kuwekea sabuni, maji, yani sop dish.
Anastania akiwa mwenye mawazo mengi kichwani, mwake, hofu a mshaka juu ya kile alicho kishuhudia, kinafwanywa na yule kijana mpole, ambae mpaka sasa akuwa anamjuwa kwa jina, kijana ambae sikuzote alikuwa anamwona kuwa ni kijana mnyonge, mwenye kukosa matumaini.
Ukiachilia kumwona kijana yule akichomoa roho ya mtu, huku akilishuhuia tabasamu lake la kwanza, pia Anastansia kwake, ilikuwa ndiyo mala ya kwanza kumwona mtu akiuwawa, tena sababu ikiwa ni kulinda usalama wake yeye mwenyewe.
Anastansia anashuka kwenye ngazi taratibu, huku mawazo yanamsokota kichwani mwake, “sijuwi ni mpigie mama nimweleze, au nitamtisha” anawaza anastania, huku anamaliza kushuka ngazi, na kuelekea upande wa mabafuni, ambako kulikuwa na bomba la maji, ulio tawaliwa na giza nene.
“wacha nimwambie, maana polisi wanaweza kumkamata kijana mpole, na akashindwa kupata utetezi, pengine ni kimwambia mama mapema, atamwambia baba ajuwe la kufanya kusaidia yule kijana” anawaza Anastansia, ambae alipolifikia bomba anakinga ndoo yake, na kufungulia maji.
Naaaam! hali ya utulivu wa eneo lile, unafanya sauti pekee inayosikika kuwa ni ile ya maji kuingia kwenye ndoo, Nancy anawaza ingekuwa endapo vijana wale wange mchukuwa na kuondoka nae, siyo kwamba akujuwa kitu ambacho kinge mtokea usiku waleo.
Hakika Nancy, alijuwa fika kuwa angebakwa na kufanyiwa vitendo vya aibu, “afadhari yule kaka alinisaidia, ningeweka wapi sura yangu” anawaza Anastansia, huku anatazama maji, ambayo ayakuwa yamefika ata nusu ya nusu.
Wakati Anastansia anawaza hayo, maa akaona gari magari mawili yana yanakuja upande wa chuo kwa mwendo wa kasi ya ajabu, mapigo ya moyo yaanza kwenda mbio, “he! polisi wanakuja tena” anawaza Anastansia, ambae kutokana na giza lililotanda akuweza kuyatambua yamagari.
Mwana dada mrembo Anastansia Anthony au Nancy, anatazama kwa umakini gari lile, mpaka yanapo enda kugota kwenye geti dogo, ambako anawaona watu wanne, wanashuka toka kwenye gari na kumsogolea mlinzi, huku hali zao zikionyesha wazi kuwa, hapakuwa na amani katika ujio wao.
Anastansia anatazama kwa umakini, huku wasi wasi, ukianza kumtawala mrembo huyu, ambae anamwona mlinzi akiwasogelea watu wale, bila shaka kwa lengo la kuwahoji, shida yao usiku ule.
Lakini kabla Nancy ajaona nini kinatokea baada ya watu wale kumfikia mlinzi, mara ghafla anashtuka akiwa ameshikwa mkono, na mtu toka nyuma yake, kitendo ambacho kilimshtua vibaya sana, halimanusla aanguke kwa kihoro, anageuka kumtazama alie mshika mkono……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

