
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI: Gari linatimua vumbi, mpaka linapo fika kwenye eneo la vwanja wa michezo, vya wazi, huku ndani kukiwa na Insp Aisha Amary na ASP Ayoub Mzee, “afande, ni vyema kama ukipunguza mwendo, ili tujuwe kinachiendelea, maana awa jamaa tayari wapo hapa” alisema Insp Aisha, akimweleza afande wake Ayoub Mzee.ENDELEA…….
“hupo sahihi Aisha, tena ingefaa kama tungetafuta njia tofauti ya kuingilia ndani ya chuo” alisema ASP Mzee, huku anaondoa mguu wake, kwenye kibati cha mafuta, nakukanyaga brake kidogo, gari linapunguza mwendo.
ASP Ayoub Mzee anakanya klachi na kutoa gia namba nne, akiipachika namba tatu, akarudia tena kufanya hivyo akiweka gia namba mbili, na kufanya gari lienda taratibu sana.
“punguza mwanga wataa, wasije kutuona, maana ni watu hatari sana awa” alisema Aisha, ambae anaonekana kuwa mwenye tahadhari kubwa, “hupo sahihi Aisha, awa jamaa ni zaidi ya hatari, wanaweza kutuondoa duniani dakika moja tu, na wasi fanywe chochote” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anapunguza mwanga wa taa zambele za gari, akibakiza mwanga aififu.
kumbe basi muda mfupi uliopita, pale ambapo Farida na Nancy wakiwa wanazidi kutembea kusogelea uzio, huku Anastansia anajiuliza maswali bila majibu, anawaza labda Farida ni pandikizi la ulinzi wa siri aliouweka baba yake, kuhakikisha usalama wake, lakini mbona hakuwa na ukaribu nae kwa namna yoyote.
“sasa Farida unanipeleka wapi, na wewe umeyajuwaje aya yote?” anauliza Anastansia kwa sauti iliyojaa uoga, na wakati huo huo, unaonekana mwanga afifu wa taa za gari, ukija upande wao, toka upande wa mabatini, sambamba na ngurumo nyepesi.
“nakupeleka kwa mtu anaweza kukulinda” alisema Farida huku anaongoza kupenya kwenye mpenyo wa kati ya mti na mti, sehemu ambayo ni wazi baadhi ya wanafunzi utumia kutorokea.
Lakini basi, wakati huo huo, Insp Aisha Amary na ASP Ayoub Mzee, wanawaona wanafunzi wawili, wakiwa wanatembea kwa tahadhari ndani ya udhio wa miti wa chuo, wakija upande wa barabarani, “wanafunzi bwana, sikute wanatoroka usiku huu” alisema ASP Ayoub Mzee, “tena wote ni wakike, inashangaza sana” alisema Aisha, huku wanawatazama wanafunzi wale waliokuwa wanazidi kusogelea uzio wa chuo.
“Afande, mimi nimepata wazo” alisema Insp Aisha, huku anamtazama afande wake, “wazo gani Aisha, maana mpaka sasa umesha toa mawazo matatu na nimeyatekeleza” alijibu ASP Ayoub Mzee, lakini kwa sauti yenye utani kidogo.
“unaonaje kiwatumia awa watoro, kumfahamu huyo mwanamke wanaekuja kumfwata awa vijana wa Tino Nyondo” alisema Insp Aisha, “umengionea point Aisha, tena tunaanza kwa kuwa chimba mkwala kidogo” alisema ASP Mzee, akiunga mkono wazo la Insp Aisha.
Naaaaaaam! wakati huo huo pia, bwana Mbwilo, akiwa na wakina Nzala, Lisanga na Malibuka, walikuwa wanatembea kwa haraka kuelekea upande wa bweni walilo onyeshwa, mara ghafla Hamad Lisanga, akaona kitu, “Mbwilo, tazama kulembona kama kuna mademu wanatoroka” alisema Lisanga, akitazama mia kama mia nne, mbele yao, upande viwanja vya michezo ya wazi, wa karibu na barabara, ndani ya uzio.
Na wenzake wanatazama, huku wakisaidiwa na mwanga wa bweni la jilani, kuwaiona wanawake wawili waliokuwa wanatembea kwa tahadhari kuufwata uzio wa, “hoya ndio wenyewe, hakuna kuluhusu wafike, ambali, haraka sana” alisema Mbwilo, huku anamtazama Daud Nzala.
“Nzala na Lisanga, zungukieni upande wa wanjani, haraka, mimi na Malibuka tuna enda kuchukuwa gari” alisema Mbwilo, huku anaanza kutembea kuelekea ukumbi wa mahakuli, waliko mwacha Sixmund Haule, ambae ndie dereva wa gari lao.
“sawa mkuu, mtatukuta tumesha mkamata” alisema Nzala, huku mkono wake unazama kiunoni na kutoa bunduki ndogo, aina 5FG pistor, na kuikoki, kisha kuikamata mkononi madhubuti, kama ambavyo Lisanga pia alifanya.
“hakikisheni, anatapatikana akiwa mzima, siunajuwa anamaswali ya kujibu huyo mwanamke” alisisitiza Mbwilo, wakati kila kundi likitokomea upande wake, wakionekana kuwa na haraka, kwamaana awakutaka kumwangusha boss wao, Tino Nyondo.
Wakati wakina Mbwilo wanawazunguka wanafunzi wawili wakike, huku wanafunzi wenyewe ambao ni wakina Farida na Anastansia, walikuwa wanakaribia kabisa uzio wa miti, pasipo kujuwa hatari iliyopo mbele yao.
“Farida hivi unataka nikuamini, mbona unanipeleka kwa mtu ambae simjuwi, na wala simwoni” alisema Nancy, kwa sauti yenye mashaka makubwa na wasi wasi, “jamani Nancy, kwani ulioni gari hapo barabarani?” anauliza Farida, kwa sauti yenye kukata tamaa.
“una uhakika gani, pengine ndio hao majambazi wanakuja kunifwata” analisema Anastansia kwa sauti yenye wasi wasi, akijaribu kumzuwia Farida sivuke ule uzio wa miti ya kupandwa, “acha uoga Nancy, nifwate mimi” alisema Farida, huku namaliza kuvuka uzio.
Anastansia kwakuona amebakia peke yake mle ndani, akiwa mevalia tauro lake, kandambili na kitenge kwa ndani, huku soap dish ikiwa mkononi, akapenya kwenye lile tundu alilopenya mwenzie, ambako sasa waliona mwanga wagari umetoweka ghafla, na kubakia ngurumo ya gari, iliyokuwa inawasogelea kwa ukaribu.
Wote wanatazama upande unakotokea ngurumo ya gari, wanaliona gari dogo rangi ya maziwa, aina ya Toyota crester, lililokuja karibu yao na kusimama karibu yao, “aya Nancy, ingia ndani ya gari, sasa hupo salama” anasema Farida huku anafungua mlango wa gari upande wa seat za nyuma. Endelea kufwatilia hadithi hii, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU