
TOBO LA PANYA (43)

SEHEMU YA AROBAINI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI: “kwahiyo we fala, unazani unaweza kutukimbia sisi?” aliuliza Mbwilo, kwa sauti yenye jadhba, huku anainua mkono ulioshika bastora na kuushusha usoni kwa ASP Ayoub Mzee, akitanguliza kitako cha bastora hiyo, iliyoenda kukita kwenye paji la uso kwanguvu, na kumfanya ASP Ayoub Mzee, aanguke chini kama furushi. . ..Endelea…….
Farida anamwona ASP Ayoub Mzee akiwa ametulia pale chini, ni wazi alisha poteza fahamu, sasa anasikia kilio cha uoga, toka kwa Anastansia, ambae bado alikuwa amevalia tauro na vitenge, sijuwi kama ndani alikuwa amevaa ile nguo ndogo kabasa.
“Nzala, ebu mchukue huyu mwanamke, mwingize kwenye gari tusepe zetu” alisema Mbwilo, huku anageuka na kuanza kulifwata gari, “vipi kuhusu huyu?” aliuliza Malibuka, huku anamwonyesha Insp Aisha, aliekuwa amesimama akisali kimoyo moyo, wasi mfanye kitu chochote.
“usiulize majibu, huyo mzime asije kutuletea kimavi” alisema Mbwilo huku anaendelea kutembea kuelekea kwenye gari, akimwacha Malibuka akimsogelea Insp Aisha kwa mwendo wa kifaru, lengo likiwa ni kwenda kumzowa mtama.
Insp Aisha anafumba macho kwa uoga na ukativu wa tamaa, akisubiri kushuhudia akishushiwa kipigo kizito, toka kwa mmoja kati ya vijana awa wenye miili iliyojengeka kimazoezi.
Lakini gafla, Insp Aisha akasikia vishindo vina koma mbele yake, wakati vitu kama manyunyu ya mvua vyenye joto ridi nyuzi 36, vina mmwagikia usoni, huku masikio yake yakisikia sauti ya mkoromo wa ajabu, toka kwa mtu aliepo mitachache mbele yake, sambamba na miguno ya mshangao, toka kwa watu wengine, “mama yangu, nini iki?” hapo Insp Aisha anafumbua macho.
Insp Aisha anakutana na picha la kutisha, asa anapomwona yule jamaa aliekuwa anakuja kumshambulia, akiwa amesimama kama sanamu, huku ameshikilia shingo yake akiziba koo, lililokuwa linavuja damu kama bomba bovu, kama ilivyokuwa puani na mdomoni.
Kijana huyu ambae achukuwi dakika ata moja, anaanguka chini kama mzigo, wakati huo huo, Aisha anamwona mtu ambae hapo mwanzo akuwepo eneo lile, akimsogelea yule mwanaume ambae alikuwa amemshika Anastansia, kwa kasi ya ajabu, huku mkononi ameshikilia kisu kidogo, chenye kung’aa kwa makali yake mfanano wa kiwembe cha upasuaji wa hospital.
Kuona vile yule Nzala, anamwachia haraka Anastansia, na kuinua bastora yake, kuielekeza kule ambako mwanaume huyu, ambae Insp Aisha alimwona masaa machache yaliyopita akiwa na Anastansia, alikokuwa anakuja kwa kasi.
Lakini Nzala, alikuwa amesha chelewa, maana Aisha, Farida na Anastansia, wanashuhudia kijana huyu, ambae Anastansia, anamtazama kwa macho ya mshangao, kutokana na kile ambacho anachoendelea kukishuhudia kwa kijana huyu.
Kijana mpole anaonekana akimfikia nzala, kwa uharaka wa ajabu, akipishana na mkono wenye bastora, ulio elekezwa kwake, kwakushumba upande wa kushoto, huku mkono wake wakulia, ukiudaka mkono wa Nzala, ambao wakati huo kidole chake kilikuwa kina minya, kifyetulio na kuluhusu risasi ichomoke toka kwenye bastora, na kuelekea hewani.
Lakini sasa, wakati huo huo, mfano wa mashine ya kushonea nguo, kijana huyu, ambae siku zote uonekana mpole na mtulivu, alichezesha mkono wake kwenye eneo la mbavu za Nzala, kwa idadi ambazo ni vigumu kuzitaja, kutokana na kasi ya mkono huo, ambao ulikuwa una zamisha kisu na kuchomoa.
Michomo, nane ya visu vya mbavu, vilitosha kumlegeza Nzala ambae alianguka chini akiwa amekosa nguvu ata ya kutoa sauti ya kuugulia maumivu aliyokuwa anayasikia wakati hule, kiu kali ya maji inakausha koo lake, huku pumzi inakatika taratibu, na kumpa wakati mgumu katika upumuwaji.
Siyo tu wakina Insp Aisha, Farida na Anastansia, au wakina Sixmund Haule ambae ni dereva wagari la wakina Mbwilo, pamoja na Kubaga, ambae alikuwa anaielewa kazi ya kijana huyu hatari.
Pia mita kama hamsini toka eneo la tukio, alikuwepo yule mwanayme mtu mzima, aliekuwa amekamata baskeli yake, yenye furushi kubwa kitakoni, alikuwa anashuhudia Mbwilo akighairi kuingia kwenye gari, kisha baada yake anapeleka mkono, kwenye vungu ya seat ya abiria wambele, inakuwa lahisi kwake, kuchukuwa bastora, sababu mlango wa gari tayari ulikuwa wazi.
Lakini aikusaidia kitu, maana kijana huyu hatari, alikuwa amesha iokota bastora na kuielekezea kwa Mbwilo, na kitendo bila kuchelewa, kidole kilisha minya kifyetulio, nakuluhusu risasi ichomoke.
Kwa kasi ya ajabu, risasi inaenda moja kwa moja, na kukita kwenye bega la la kulia la Mbwilo, ambae pia kwa mshtuko, anainua bastora usawa gari, huku kidole chake kinakandamiza trigger na kuluhusu risasi moja ichomoke, na kwenda usawa wakichwa cha Sixmund Haule.
Risasi inapenya kwenye paji la uso na kuzama kabisa, ikusababisha damu kuanza kutililika toka kwenye pachi la uso la dereva huyu, ambae anaonekana akiwa ameganda kama sanamu, ametoa macho kama amefumania.
Mbwilo anajaribu kuimiliki vyema bastora yake, lakini maumivu ya mkono yanamzidia, kutokana na risasi ya bega, anajaribu kuamisha mkono na kuishika bastora kwa mkono wa kushoto.
Lakini wakati huo anagundua kuwa alisha chelewa, maana tayari kijana huyu alikuwa mbele yake, kwa haraka Mbwilo anarusha mkono wake wa kushoto, akitanguliza kitako, cha bastora, kuelekeza kwenye kichwa cha kijana huyu, ambae ukimtazama usoni, unaweza kusema ni kijana myonge, alie fika hapa kuomba msamaha.
Lakini wakati mkono ukiwa hewani unaenda kichwani kwa kijana huyu, Mbwilo anashangaa mkono wake ukiwa umedakwa, huku kitu chenye ncha kali kikipenya ubavuni mwake chini kidogo ya mbavu zake, ile anajiuliza ni kitu gani kimemchoma, tayari michomo mitano, ilipenya kwenye mbavu zake, ungesema kuna mashineinatumika kumchoma.
Mbwilo akaona kuwa, akizubaa, anapoteza maisha kama Nzala, hivyo akaona itakuwa vyema akitumia bastora kujiokoa, japo alikuwa ameishika kwa mkono wa kushoto.
Bahati nzuri kwake, wakati huo huo, Lisanga alikuwa anamsogelea kijana huyu, kwa uharaka sana, akitokea nyuma yake, na alikuwa amesha mfikia, na kumfanya Mbwilo aamini kuwa, wanaweza kumdhibiti kijana huyu mdogo, endapo wata mshambulia kwa pamoja. . . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

