TOBO LA PANYA (45)

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NNE: Insp Aisha nikama anagutuka toka kwenye wenge, anamtazama huyu A-Insp, kwa macho ya mshtuko na kumbu kumbu, “afande Ayoub Mzee” anasema Aisha, huku anaanza kukimbilia upande wa gari la ASP Ayoub Mzee. . . . ..Endelea…….

“afande tumesha mpakiza kwenye gari, bado amepoteza fahamu, ila wengine wote wamesha uwawa, je unaweza kunieleza kilitokea” alisema yule A-Insp na hapo Insp Aisha ambae alikuwa amesha fikia gari, anaingia ndani ya gari na kuanza kukagua, ambapo anaibuka na bastora mbili, yani ya kwake na ile ya ASP Ayoub Mzee.

A-Insp anamfwata Insp Aisha, pale kwenye gari, “afande mbona uongei, nini kimetokea hapa, maana watu wanne wameuwawa?” aliuliza tena yule A-Insp, safari hii, kwa msisitizo, ni wazi aliona kuwa mkuu wake wakazi hayupo sawa, “sikia afisa, huu siyo muda wa maswali ambayo majibu yake yapo wazi, tuondoke eneo ili, nazani RCO anaitaji kupata taarifa hii mapema” alisema Aisha, ambae ni wazi akuitaji maswali.

“lakini afande hapa kuna watu walio uwawa, na magari mawili zaidi, tunayafanyaje?” aliuliza A-Insp, “ilo gari dogo ni gari la afande Ayoub Mzee, na ilo jingine ni gari la vijana wa Tino Nyondo, pelekeni kituo cha polisi, na hiyo miili pelekeni mutual, mimi naenda hospital kumsimamia afande Ayoub Mzee apate matibabu” alisema Insp Aisha, huku anatembea kulifwata gari ambalo aliambiwa kuwa ASP Ayoub Mzee alikwua amepakizwa.

Naaaaaaam! jibu la Insp Aisha linamshtua sana, A-Insp huyu, ambae anasimama huku ameshika kichwa chake kwa mikono, “mama yangu, hii sasa ni vita, jioni hii nimesikia mdogo wake ameuwawa, na sasa naona vijana wake wameuwawa, nani huyu anaeweza kumchezea Tino Nyondo” anajiuliza yule A-Insp, huku amesimama.

Anasimama kwa sekunde kadhaa, kisha anamfwata askari polisi mwenye cheo cha koplo, “angalia kama miongoni mwetu kuna madereva, waondoke na hayo magari mawili” alisema hivyo kisha nae akaingia kwenye landi rover jingine.

Dakika chache baadae mipango ilikuwa imesha kaa sawa, na safari ya kuelekea mjini ikaanza, huku Insp Amary akiwa kwenye gari la mbele kabisa, kichwani mwake anawaza kile alicho kiona kwa macho yake.

Kitu ambacho unatakiwa kuelewa ni kwamba, Insp Aisha amesha wai kushuhudia miili ya watu walio uwawa, kwa mitindo ya aina mbali mbali, ikiwa ni pamoja na mwili wa kijana Aloyce, alio ushuhudia siku iliyopita.

Pia alisha wai kuona mauwaji kadhaa yakitokea, mbele ya macho yake, ikiwa ni vifo vya majambazi walio uliwa na polisi, au polisi walio shambuliwa na majambazi, na kuuwawa mbele yake.

Lakini hii ya leo, ilikuwa ni zaidi ya kile ambacho, Insp Aisha alisha wai kuona siku za nyuma, hakika kichwani mwake ilikuwa inamjia picha, ya yule kijana ambae mpole, ambae masaa machache yaliyopita alimwona kama vile kijana nyonge, namna alivyo kuwa zamisha kisu kwenye miili ya waadamu wenzake, ambao licha ya kuwa walikuwa ni waalifu hatari, lakini ilitisha kutazama.****

Naaaaaaam! sasa tupo mtaa wa mahenge, nyuma ya makazi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma, hapa tunazungumzia hotel moja tulivu ya kipekee na hadhi ya nyota tatu, yani nyumbani lodge.

Liacha ya eneo la mbele la hotel, kuwa na wateja wengi, walio kuwa wanapata vinywaji vyao, wengi wakinywa pombe, lakini chakuvutia ni kwamba, eneo ili lilikuwa tulivu sana.

Moja kati ya meza nyingi zilizopo eneo ili la mbele, ya jengo ili lenye ghorofa mbili, iliyojaa vyakula na vinywaji vya aina mbali mbali, ilikuwa imekaliwa na watu watano, nao ni familia ya bwana Haule, au James Bond, kama wengine wanavyo penda kumwita, akiwa katika majukumu yake.

Utulivu ndio unaoileta familia hii, maali hapa, ambapo wali patumia pia kukutana na mama yake Eva, kwa mala ya kwanza, “Eric nini unazani kitatokea wewe na Eva mkienda dar kwaajili ya manunuzi ya maandalizi ya kwenda shule?” ana uliza mzee Haule, mkulugenzi wa mambo ya usalama na majukumu ya siri ya taifa, kwa ngazi ya mkoa.

Swali lina washtua watu wote, kasoro binti yao Vestina pekee, ambae akuwa ameelewa chochote, “baba Eric, swali gani una mwuliza mtoto, tena mbele ya mwenzake?” anauliza mama Eric, yani mke wa mzee Haule, kwa sauti ya kunong’ona.

“kwani mimi nimeuliza kitu kibaya, au we unahisi kitatokea nini?” anauliza mzee Haule kwa sauti ya juu kidogo, “hapo Eric na Eva wanatazamana kisha wanaziba midomo yao, kwa viganja vya mikono yao, wakizuwia vicheko.

“na nyie mnacheka mnazani ni mambo mazuri aya?” anauliza mama Eric, huku anawatazama Eric na Eva, na wakati huo huo, mzee Haule analiona gari aina aina ya mercides benz rangi nyeusi, likiingia kwenye maegesho ya hotel na kusimama.

“tayari kazini kumepatikana kazi” anasema Haule, huku anainuka toka kwenye kiti chake, “vipi tena mwenzetu, kiti cha moto?” anauliza mama Eric, huku anamtazama mume wake, huku wakina Eric, wakiendelea kula pasipo kufwatilia kinachoendelea.

“nakuja” alisema mzee Haule, huku anaanza kutembea kuelekea kwenye maegesho ya magari, huku analitazama mercides benz, ambalo sasa mlango wake wa dereva ulifunguliwa akatokea kijana mmoja mtanashati, alie valia mavazi mazuri yenye kumletea heshima mbele za watu.

Kijana anafunga mlango wa gari, na kuanza kutazama kule ambako, watu wamekaa wanapata vyakula na vinywaji, ni kama kuna mtu alikuwa anamtafuta, lakini macho yake yanaishia kwa mze Haule aliekuwa anakuja usawa wake.

“mh!, huyu mzee noma, yani amesha niona na amejuwa namfwata yeye” alijisema kijana yule, huku anaachia tabasamu, “nikweli unajambo la kufurahisha kiasi cha kutabasamu, wakati umesha nijaza wasi wasi?” anauliza mzee Haule, akiwa anamfikia kijana huyu. . . . . ..
MWISHO SEASON TWO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!