TOBO LA PANYA (47)

SEHEMU YA AROBAINI NA SABA

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SITA: “miongoni mwa wafu, inamaana kuna vifo zaidi vitaendelea kutokea?” anajiuliza kijana mtanashati, ambae anatamani alipate jibu toka kwa mzee Haule, lakini tayari alisha fika mbali, na angeuliza kwa umbali ule, lazima usiri ungekosekana. . . . . . ..Endelea…….

Baada yake kijana mtanashati anaingia kwenye gari na kuondoka zake, huku kichwani mwake akiwa amevurugwa wka taarifa hii, maana na yeye ni mmoja wa watu walio teuliwa katika operation ya kumsaka SA-26, “Ee mwenye Mungu, wape busara wakuu wetu, waachane na huyu mtu, kunusuru shingo zetu” alijisemea kijana huyu, huku anakanyaga mafuta kuondoka eneo la nyumbani Logde.***

Naaaaaaam!, SA-54 mwanadada Farida, ambae alikuwa anajilahumu kwa kuosa alilotaka kulifanya, la kumkabidhi Anastansia kwa polisi, alitembea kwa haraka akivuka mabweni ya wanafunzi, ambako sasa wanafunzi walikuwa wengi sana, kwamaana walisha kimbia kutoka madarasani, na kuja upande wamabweni, wamesimama kwa makundi wakijadiri kuhusu tukio kubwa la kuogopesha lililotokea usiku huu.

Yani tukio la uvamizi wa vijana wanne, ambao walikuwa wanamwulizia Anastansia, pia milipuko ya risasi, iliyo sikika muda mfupi baadae, baada ya wale jamaa kuelekea bweni la wanawake, wakimfwata Anastansia.

Farida anakatiza na kuingia chumbani kwake, ambako anamkuta Joyce, akiwa anatoka chumbani, “dada Farida ulikuwa wapi, hivi umesikia mi bunduki ilivyo pigwa, jamaa wamevamia wamempiga mlinzi, wame wapiga wakina Adelah, alafu wamemkamata Anastansia na kuondoka nae” alisema Joyce ambae ni rafiki wa karibu wa Farida, alie kutana nae hapa hapa chuoni.

“ni wakina ninani hao jamaa ni wakina nani?” anauliza Farida kama vile ajuwi kinachoendelea, “nasikia ni wafanyakazi wa Tino Nyondo, yule mzee makatili mwenye gari kule mjini, yani sijuwi itakuwaje, maana nasikia wale jamaa wakikukamata wanakubaka kwanza ndio wanakuuwa” alisema Joyce, kwa sauti yenye taharuki, huku anarudi chumbani kumfwata Farida.

“mh!, kwanini wamfanyie hivyo, kwani kunakitu amewakosea?” aliuliza Farida kwa sauti ya mfano wa mtu asie juwa kitu, “yani hapa kila mtu anasema lake, wengine wanasema eti, alimkataa mdogo wake Nyondo” alisema Joyce huku anaa kwenye kitanda.

“kwahiyo polisi wanamuacha tu, huyo Nyondo afanye anacho taka?” aliuliza Farida, ambae sasa alikuwa anachukuwa card ya kupigia simu, toka kwenye mfuko wa pembeni wa begi lake dogo.

“weeeeeh!, tena usitegemee polisi kabisa, anaweza kuja kukuchukuwa pale pale, wenzio kuna polisi waliwai kuleta unoko, na mpaka sasa hawajulikani walipo, yani walitoweka ghafla tu” alisema Joyce, huku anamtazama Farida, ambae ni wazi alionekana anataka kutoka.

“duh!, ni hatari, kama ata polisi wanamwacha, basi Anastansia yupo hatarini” alisema Farida kabla ajaaga kwa Joyce kwamba anaenda kupiga simu nyumbani kwao.***

Giza lilikuwa limezidi kutanda, Anastansia akiwa amejifunga tauro kiunoni, ndani akitanguliza kitenge, anatembea kwa ukaribu kabisa pembeni ya kijana mpole, mwenye roho ngumu, hapa kuwa na maongezi yoyote, ni kama kila mmoja alikuwa anatafakari jambo lake, kichwani mwake.

Wakati kijana Hance anawaza namna ya kumfanya Anastansia awe msiri wake, ili aweze kuwa hepuka TSA, ambao wanamsaka, kwa hudi na uvumba, ili kumwangamiza, sababu ikiwa ni kujitoa shirikani.

Huku mwanadada Nancy akiwaza mambo tatu kwa wakati mmoja, moja ukubwa wa tatizo linalo mkabiri mbele yake, tatizo ambalo ilikuwa lazima litokee, kutokana na upuuzi wa wale vijana, kule midizini, tatizo ambalo hajuwi litagharimu mnaisha ya watu wangapi.

Pili Nancy aliwaza kuhusu usalama wake, aliwaza atafute mawasiliano ya wazazi wake, ili waweze kuwajulisha polisi, lakini anakumbuka kuwa polisi hawana sauti kwa watu hao, ameshuhudia kwa macho yake polisi wakiwakimbia watu hao.

Hivyo atawaingiza wazazi wake kwenye vita ambayo, inaweza kusababisha hatari kwa mama yake, ambae angechelewa kupata msaada toka kwa baba yake ambae anaishi nchi jilani.

Kamaana hiyo sehemu salama ni kukaa na kijana huyu, ukizingatia wale vijana wa Tino Nyondo, pale chuoni wanaingia kama nyumbani kwao, swala la tatu lililompa mawazo ni uvaaji wake.

“sasa nikaaje na mwanaume nikiwa nimevaa hivi” anawaza Anastansia, ambae kiukweli ni mwanamke ambae ni mzuri kweli kweli, na mwenye kutamanisha, “kama mchana nilivaa vile akanitamani, itakuwa hivi nilivyovaa” aliwaza Nancy, huku anaendelea kutembea ubavuni mwa Hance, wakikatiza pembeni ya uwanja, mkubwa wa mbio ndefu.

Wakati huo wawili awa, tayari walisha yaona magari ya polisi, yakiondoka kuelekea mjini, Anastansia anawaza umbali anao takiwa kutembea akiwa amevaa tauro pekee, “watu watanifikiliaje wakiona nime vaa hivi?” anawaza Nancy, huku anatembea pembeni ya kijana huyu mpole, ambae ni mkombozi wake kwa sasa.

Kabla Anastansia ajapata jibu la swali lake, mala anashuhudia safari yao iki ishia pembeni ya gari dogo, aina ya BMW rangi nyeusi, ambalo lilikuwa linaunguruma.

Kabla ajauliza kama lile gari lina wahusu au wanapita na safari yao, maana kwa haraka Anastansia akuweza kuamini kuwa, kijana huyu mpole na fukara, anaweza kumiliki gari kama ili, endapo pale kwenye kibanda cha udongo akiuweza kuona ata baskeri mbovu.

Anastansia anamwona kijana, Hance akifungua mlango wanyuma wa mbele wa abiria wagari lile, niishala ya kuwa anamtaka Anastansia aingie ndani ya gari, nae kwa kulijuwa ilo anaingia ndani ya gari na kukaa vizuri akijitaidi kufunika vyema mapaja yake mazuri, yenye kutamanisha na kifua chake, kilichobeba maziwa manono.

Hance nae anaingia kwenye gari na safari inaanza, wakielekea upande wa seed farm, Anastansia anajiuliza juu ya kijana huyu, ambae ni vigumu kumtafasiri, au kumfafanua, ni mtu wa aina gani.

Maana ukiachilia kuwa mwenye sura na mwonekano wa upole, kupita kiasi, lakini kijana huyu, anamatendo ya kikatili ambayo ayajapata kuyaona ata kwenye filamu, kijana ambae amekuwa akimchukulia kama kijana mnyonge, ata alipomtuma akamletee chakula, alimtuma kama kijana mnyonge, alie mshuhudia akinyanyasika na mlinzi wa geti la pale chuoni. . . . . . . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!