
TOBO LA PANYA (56)

SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO: Mwenzie anageuka kutazama kilikotokea kisu, anamwona mtu akiwa hewani anakuja usawawake, atokea usawa waukuta, wa uzio, visu viwili katika mikono yake, aliyo itanua kama mbawa za mwewe, anaeshuka kuchukuwa windo lake. . …..Endelea…….
Fumba na kufumbua, tayari ali kifuti, yani goti la kijana yule, wa ajabu, lilisha tuwa kifuwani kwake, huku akishindilia visu kwenye shingo yake, na kuchomoa kwa haraka, akimwacha anaenda chini, na kwa wepesi wa haraka, anamuwai yule mwingine ambae nae alikuwa anaenda chini taratibu, na kumchomoa kisu kifuani, na kumwacha nae akienda chini, na wote wanaanguka kwa pamoja.***
Naaaaaaam!, kituo kuu cha polisi mkoa wa Ruvuma, ndani ya jengo kubwa lenye ghorofa nne, sehemu ya mapokezi, wanaonekana askari wawili, mmoja akiwa wakike mmoja akiwa wakiume.
Yule wakiume alikuwa ameshikilia mkonga wasimu ya ofisi, anaongea na mtu upande wapili, huku yule wakike akiwa ametulia kiti chake nyuma ya meza kubwa, anasoma gazeti moja maarufu la udaku.
“ndiyo afande, nitapiga simu nyumbani kwake, kisha nimpatie ujumbe, maana bado ajapita” alisikika akisema yule askari wakiume aliekuwa anaongea kwa simu, na wakati huo wakamwona ASP Ayoub Mzee, akiingia ofisini mbio mbio, miguu ikiwa peku peku.
“kata simu haraka, niongee na RCO, ni dharula” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anamsogelea yule askari aliekuwa anaongea na simu, “RCO huyu hapa yupo kwenye simu” alisema yule askari huku anampatia mkonga wasimu, wote wawili wakimshangaa afande wao huyu, kwa jinsi alivyoonekana.
ASP Ayoub Mzee anachukuwa mkonga wasimu, na kuweka sikioni, “hallow afande Insp Aisha ametekwa na Nyondo, sijuwi wanampeleka wapi” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti ye haraka yenye pupa, “ebu subiri Mzee, wewe siulikuwa umelazwa hospital, na imekuwaje wamemteka” aliuliza RCO Mpeta, toka upande wapili wasimu.
“walivamia pale hospital na kumchukuwa Aisha, Nyondo mwenye akiongoza” alisema ASP Ayoub Mzee, inamshtua RCO, “eti!, unasema wamemteka Insp Aisha?” anauliza RCO kwa sauti yenye mshangao.
“ndiyo afande, wamemchukuwa na kuondoka nae haraka, sikuweza kuwafukuzia” alisema ASP Ayoub Mzee, ambae alionekana kuchanganyikiwa, kutokana na lile tukio la kutekwa kwa Insp Aisha Amary.
“huyu mshenzi amezidi sasa, hakika hili alivumiliki” alisema SP Mpeta Zamoyoni, kwa sauti yenye kukelekwa na jambo ilo, “sikia Ayoub, naimani sasa imekaa sawa, andaa askari kumi, kisha subirini maelekezo” alisema RCO kabla ya kukata simu.
Hapo ASP Ayoub Mzee, anampatia mkonga wasimu yule askari, “vipi afande, imekuwaje ilo tukio?” anauliza yule askari, huku anapokea mkonga wasimu na kuuweka sehemu yake.
“nimakosa yetu kumwendekeza Nyondo, sasa anaturudia sisiwenyewe” alisema ASP Ayoub Mzee, ambae alikuwa anaitaji kwenda nyumbani kwake, kubadiri nguo ili asubiri majukumu, toka kwa RCO.***
Naaaaaaam!, twendeni chuo cha ualimu na uongozi wa jamii, kilichopo matogoro, ambako sasa wanafunzi walikuwa wameshaingia kwenye vyumba vyao, japo bado awajalala, lakini walikuwa wanaongea ili na lile, kuhusu tukio lililotpkea muda mfupi uliopita, ni lile tukio la kusikika milipuko ya risasi, japo awakujuwa kama kuna mauwaji yametokea, mita chache toka pale walipo.
Nje ya majengo aya ya mabweni ya chuo, walionekana watu wachache sana, tena kwa uchache sana, wakienda au kutoka chooni, na sivinginevyo, japo kwa siri sana, kuna wale wenye kutumia uzio wa chuo kama sehemu ya kupeana dudu, nao wangekuwa katika hali ya mashaka sana.
Mwana dada Farida aliekuwa anatoka kuoga, ikiwa ni baada ya kumaliza jikumu lake, la kumtorosha, Anastansia, “hivi hukuoga wakati tumetoka uwanjani?” anauliza Joyce, ambae alikuwa amejilaza kitandani, huku anamtazama Farida aliekuwa anaingia chumbani, akiwa amevalia kitenge kilicho lowa maji, mkono wake wa kushoto, ameshilia nguo ya ndani aliyoifua, na mkono wa kulia ameshikilia ndoo yenye kopo yenye sabuni ndani yake.
“nilighairi, watu walikuwa wengi bafuni” alisema Farida, huku anaweka ndoo chini, anaanika nguo yake ya ndani, kisha anaanza kujifuta maji mwilini mwake, akihakikisha afunuwi mwili wote.
“yani awa majambazi leo wamearibu mipango ya watu mpaka basi, sijuwi kama watu wamesimamisha minazi huko nje” alisema Joyce, kwa sauti yenye masikitiko, na kulaani hali ile.
“kwahiyo umesha tamani kukutana na mtu wako, sijana tu mlienda kule kwenye uwanja wa riadha?” anauliza Farida kwa sauti ya mshangao, huku anaanza kujipaka mafuta mwilini.
Joyce anacheka kidogo, kicheko cha aibu, “dada Farida jamani, kwahiyo unazani kila tukikutana lazima tufanye” anauliza Joyce, kwa sauti yenye kujitetea, “kwahiyo aitoshi, mnakutana bwaloni, mnakuta prepo, mnakutana uwanjani, bado tu mkatazamane vichakani” anaongea Farida kwa sauti yenye mashaka na kuto kukubariana na Joyce.
Joyce anacheka kidogo, “dada Farida heee!, we niache tu, ujuwi huko nyumbani watu tunabanwa kiasi gani huko nyumbani” kinapita kimya kifupi, Farida anamaliza kupaka mafuta, kisha anachukuwa nguo nyingine ya ndani na kuivaa, akifwatia na gauni fupi.
“kwahiyo unataka kuniambia wazazi wako wanakubana sana, kiasi cha kukosa kuwa na mpenzi?” anauliza Farida, huku anapanda kwenye kitanda chake, “tatizo siyo kuwa mpenzi, tatizo huyo mpenzi unakutana nae vipi” anajibu Joyce, akionyesha msisitizo kwenye jibu lake.
“mh!, kwahiyo wewe kufanya aya mambo ni mpaka uje chuoni?” aliuliza Farida, huku anavuta shuka lake na kujifunika mpaka kifuani, “ndio maana nakuambia we niache tu nifaidi huku chuo, vinginevyo mpaka niolewe, au nipate kazi yang…..” kabla Joyce ajamaliza kuongea, wote wawili, wakasikia mlango wa chumba chao unagongwa, toka nje.
Wote wanatazamana, kila mmoja kichwani mwake akiwa anajiuliza lengo la mgongaji wamlango, wakati Joyce anatamani awe mjumbe toka kwa mpenzi wake, huku Farida anajipatia mashaka ya haraka.
Kwamaana kama aliweza kufanya kosa la kumkabidhi Anastansia kwa polisi, bila yeye kujuwa, je ni wangapi walimwona, inamaana wale polisi awaja mtambua, na kama wamemtambua ato tumika kama ambavyo Anastansia anatumika kumtafuta SA-26, vipi kama mgongaji amemfwata yeye. TOBO LA Panya….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

