TOBO LA PANYA (58)

SEHEMU YA HAMSINI NA NANE

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA:. Duh!, kaaazi kweli kweli, hakika mwanaume mtu mzima, akipewa nafasi ya kumalizia kuongea, maana haraka kama umeme, alishtuka Farida akifunua kitabu chake na kupeleka mkono mbele, haraka kama umeme….ENDELEA………

Fumba na kufumbua, tayari kisu kidogo, kilikuwa kimesimama kwenye kwenye koo la mwanaume mtu mzima, ambae alikumbatia koo lake, huku akishindwa kuhemwa wala kuvuta pumzi.

Ilekutahamaki, mwaume kijana anashangaa mdomo wa bastora umemtazama, “mwambie mkulugenzi aijawai kuwa lahisi kumpata SA-26, vyema mkajiuliza tena, kama mpo sahihi au la” alisema Farida huku anamtazama kijana huyu, ambae alikuwa anatetemeka.

Farida akiwa ameelekeza mtutu wa bastora, kwa mwanaume kijana, anachukuwa begi dogo, analivaa mgongoni kwamkono mmoja, kisha anachukuwa viatu vya raba, aina ya DH, anavishika mkononi, “lala chini, kabla sijakupasua ubongo” anasema Farida, kwa sauti kavu ya chini.

Mwanaume kijana anatii amri mala moja, analala chini haraka, pasipo kujali damu ya mwanaume mzee, ambae sasa alikuwa anatupa mikono na miguu, katimka nyakati zake za mwisho, Farida anachomoa kisu kwenye koo la mwanaume mtu mzima, na kufanya damu izidi kutoka kwa wingi, kisha anaanashindilia mguu wake kwanguvu, kwenye kichwa cha mwanaume kijana.

Hapo bila kuchelewa, mwanaume kijana anakata moto, na kupoteza fahamu zake, Farida anatoka nje haraka, akiwa ameificha bastora, viatu mkononi, begi mgongoni.

Farida anatembea haraka akishuka ngazi, na wakati anakaribia kufika chini, akasikia vishindo vya mtu akija kwenye ngazi, akitokea upande wa bwaroni, Farida akaruka mpaka chini na kujificha chini ya ngazi.

Akatulia kidogo, akisikilizia vishindo, ambavyo viliongezeka, mpaka alipomwona mwanamke alie kuwa anakuja wka mwendo wa haraka, akianza kupanda ngazi, “mshenzi sana yule mwanamke, yani utazani mchawi, sasa kwanini anidanyanye mwenzie” Farida alimsikia mwanamke akiongea mwenyewe, kwa sauti yenye hasira na malalamiko.

Farida anamtazama yule mwanamke ambae alimtambua kuwa ni Joyce, mpaka alipo vuka ngazi mbili tatu, nae akachomoka na kukimbilia ubavuni mwa jengo la bweni lao, nyuma ya jengo la bweni lao.

Farida anaweka viatu vyake chini, na kuanza kuvaa, lakini wakatii huo huo akasikia sauti toka kwenye bweni lao, “mamaaaaaa, nakufaaaaaa, nisaidieni, jamani kuna watu wamekufa hukuuuuu” ilikuwa ni sauti ya Joyce, ikitokea ghrofa ya pili.

Watu wanatimka mbio kuelekea kwenye bweni lile, lakini Farida kuangaika nao, yeye anamaliza kuvaa viatu, anabeba vyema begi lake, na kutokomea upande wa uwanja mkubwa riadha, akisogelea uzio wa miti wa chuo, ni mita chache toka pale alipo mpitishia Anastansia wakati ule.***

Pele MAKIMAKULUGA MOTEL, RPC na staff officer wake walikuwa bado kwenye ukumbi wa VIP, wakipata vinywaji, japo kulikuwa na burudani ya macho, wakiwashuhudia wadada kadhaa, waliovalia kama wapo chumbani, wakicheza music karibu kabisa na meza yao, lakini kiukweli akili zao kwa sasa, nikama zilisha ama na kwenda sehemu nyingine kabisa.

“hivi dawa ya huyu jamaa ni nini, ujuwe amesha sababisha vifo vingi sana, asa wakati ule ambao tulikaamata dawa zake za kulevya” alisema staff officer, kwa sauti yenye kuonyesha kuchoshwa na matukio ya bwana Tino Nyondo.

“achana na tukio lile, mimi nilipofika hapa nilikuta habari moja mbaya sana, kuhusu yeye” alisema RPC, ambae aliweka kituo kidogo, akinywa pombe yake kwenye grass, kabla ajaendelea kutoa maelezo yake, juu ya bwana Tino Nyondo.

“ilikuwa ni baada ya askari sita wa doria, kumkamata Tino Nyondo, akiwa anamshambulia raia mwema, baada ya kumkamata na kumleta kituoni, baadae RPC aliekuwepo, alimwachia kutokana na heshima ya bwana Nyondo, hapa mkoani, lakini kumbe RPC alifanya kosa kubwa sana” alieleza RPC.

“siku mbili tu, baada ya kuachiwa kwa bwana Nyondo, wale askari walitoweka ghafla, bila taarifa yoyote, na wakaja kuonekana siku moja baadae, wakiwa wameuwawa kikatili, miili yao ikiwa na majelaha mengi sana” alieleza RPC, huku staff officer, akiendelea kumsikiliza, kwa umakini mkubwa sana.

“ukweli tuhuma hizo, zilienda moja kwa moja kwa Tino Nyondo, huku wakishindwa kumtia hatiani, kwa kukosa ushaidi, makao makuu wakaagiza RPC aamishwe, nikaja mimi, na nikapewa maelekezo, niwe nae makini sana mtu huyu, endapo nitamkamata kwa makosa yoyote, basi niwe na uhakika kuwa atoki, wala shindig kesi hiyo” alimaliza RPC kusimulia mkasa wake.

Wakati wanaongea ili na lile mala akaingia RCO Mpeta, huku sura yake imesawajika kwa fadhaha, “vipi tena Mpeta, mbona kam…?” aliuliza RPC kwa mshangao na tahadhari yenye mashaka, “afande hali ni mbaya, Tino Nyondo amemteka Insp Aisha, ameenda nae kusiko julikana” alisema RCO Mpeta, huku akiwa amesimama.

RPC anamtazama staff officer, ambae pia anamtazama RPC, kwamaana walitazamana, “hii sasa imezidi, hatuna na namna, lazima tufanye jambo” alisema RPC, huku anasimama, na staff officer nae akasimama, “Mpeta, piga simu kituoni, kikundi kiandaliwe haraka” alisema staff officer, huku wanaanza kutembea kutoka nje ya ukumbi,.

“tayari nimesha toa maagizo, zoezi litasimamiwa na ASP Ayoub Mzee, ambae ameshatoka hospital” alisema RCO Zamoyoni Mpeta, huku akiongozana na wakuu wake wakazi, kuzifwata ngazi za kushikia chini, wakati huo lift ilikuwa bado aijawekwa.

“ok!, waambie tukutane msibani, nyumbani kwa Nyondo, watatulinda wakati tunaongea na Nyondo, tumwombe amwachie Insp Aisha, kwa iyari yake, ili kuepusha madhara kwa askari wetu, maana tuna weza kumwokoa mmoja lakini tukapoteza askari wengi” alisema RPC, ambae aliamua kumkomboa Insp Aisha, kabla makao makuu awajasikia lolote.***

Yhaaaap!, turudi Nyumbani Lodge, ambako bado mzee Haule na familia yake bado wanapata burudani ya vinywaji, na sasa Eric alikuwa anakunywa wine, kama ambavyo, wazazi wake walikuwa wanafanya.

“maongezi ya hapa na pale yaliyo beba maudhui ya utani, yaliyo ambatana na vicheko, yaliendelea na kutawara meza yao, nyuso zao zikionekana kuwa na furaha na uchangamfu, kuliko meza nyingine zote.

“hivi rafiki yenu Amina yupo jamani?” aliuliza mama Eric, wakati wanaendelea na maongezi, “yupo nilikutana nae juzi, wakati tunaenda saloon” alijibu Eva muzungu, “yani nikimbuka ule mkasa na yule mama yake wakambo, uwa nacheka sana” alisema mama Eric, na hapo wote wakacheka.

Wakati wapo kwenye kwenye kicheko, mara mzee Haule akahisi kuna mtu amempitia karibu, na kumgusa begani, “samahani mzee jifute uchafu mdomoni” ilisikika sauti ya kike, nyuma ya mzee Haule.

Wote wanageuka na kumtazama mwongeaji, wanamwona yule mhudumu wakike, alie mletea bili wakati ule, ambae sasa alikuwa anampatia kipande cha tishu mzee Haule, kikiwa kimekunjwa vizuri.

Mzee Haule anapokea mara moja, na kupitisha mdomoni, “inamaana yeye ndiyo anaona uchafu mdomoni mwako, kuliko mimi mkeo?” anauliza mama Eric kwa sauti iliyojaa wivu. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata