
TOBO LA PANYA (64)

SEHEMU YA SITINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TATU: “sidhani kama umemaliza kushangaa bwana RPC, njoo ujionee kazi ya mtu ambae mnajifanya hamumjuwi, wakati anashirikiana na polisi, kuja kuuwa vijana wangu” alisema Nyondo kwa sauti yenye machungu na hasira. ….ENDELEA
RPC na jopo lake wanatembea kwa haraka kuufwata mlango wa lile jengo mfano wa ghara, na walipo ufikia waliingia ndani na kutazama vyema kwa msaada wa taa za umeme, zilizo tundikwa juu dali.
Naaaaaam!, wanacho jionea makamanda awa wajeshi la polisi, kinawafanya wapeleke nyuso zao pembeni, kukwepa kuona tena, kile walicho kiona mwanzo, maana hali yam le ndani aikuweza kutazamika mala mbili.
“unaweza kutueleza nini kimetokea, na huyo mtu unae msema ni ninani?” aliuliza RPC, huku anatoka nje yeye pamoja nawenzake, wakimkuta Tino Nyondo anawatazama kwa macho ya hasira.
“nani wakujibu swali ilo RPC, ni mimi nilie vamiwa na huyo Panya, alie ongozana na polisi wenu, au nyie mlie mtuma huyu muuwaji alie muuwa mdogo wangu, aje avamie hapa kwangu” alisema Nyondo, huku anawatazama viongozi wale wa jeshi la polisi, ungesema anaongea na watoto wadogo, au yeye ni kiongozi wa ngazi za juu wa jeshi ilo.
RPC na wenzake wanatazama kwa mshangao, “lakini wewe ndie ulie mteka Insp Aisha, nilikuona miongo mwao” alisema ASP Ayoub Mzee, ambae nikama alikosa uvumilivu wa zarau za bwana Nyondo.
Nyondo anamtazama RPC, huku ameachia mshangao wa hasira, “RPC, unamsikia huyu paka anachoongea, imaana mnataka kunigeuzia kibao kuwa mimi nime mteka huyo mwanamke, na kumtuma mtu alie muuwaji wa mdogo wangu aje awauwe walinzi wangu” aliuliza Nyondo kwa sauti ya juu, yenye ukali ambao, uliwashtua viongozi wale wajeshi la polisi.
Lakini aikuwa shinda kwa ASP Ayoub Mzee, ambae alisha choshwa na ukatili wa bwana Nyondo, “acha kuwa msanii mzee Nyondo…..” alisema Ayoub Mzee, ambae alishindwa kuendelea kuongea, baada ya RPC kumkanyaga mguu, akimzuwia kuendelea kubishana na mtu huyu hatari.
“kijana endelea kujifanya mwongeaji, sikuhakikishii kuliona jua la kesho, vinginevyo niletee yule kijana hapa akiwa mzima” alisema bwana Tino Nyondo, huku anaondoka zake, akiwaacha wakina RPC wakikuna vichwa vyao kwa sinto fahamu ya kauri ya bwana Nyondo, ambae kiukweli adhabu yake ndogo, ni kuuwa kwa risasi, vinginevyo ni kukata kwa msumeno nyororo, wakukatia miti.
Achana na wakina RPC, shida ilikuwa kwa ASP Ayoub Mzee, ambae kiukweli alijuwa yeye na familia yake wapo hatarini, “afande mme msikia huyu, anaweza kuuwa familia yangu” alisema ASP Ayoub Mzee, huku nae anaanza kutembea kuelekea upande wa mbele ya nyumba, yani kule walikotokea.
“haraka hakikisha unaamishia familia yako, inaingia ndania ya jengo la makao makuu, alafu chukuwa kikundi mumsake yule kijana haraka sana” alisema RPC huku nae pamoja na wengine wakimelekea ulekeo ule ule, alio elekea ASP Ayoub Mzee.
“vipi kama huyo muuwaji amemteka Insp Aisha” aliuliza staff officer, huku wanaendelea kutembea, wakikatiza kwenye mabanda ya mbwa waliokuwa wanapiga kelele za hasira, kama wafanyavyo mbwa wengine wakali.
“sidhani kama amemteka, ila nachoona ni kwamba, yule kijana amemwokoa Aisha toka kwa adui yake” alisema RPC, huku nao wakiendelea kuitembea, kuelekea upande wa mbele wa jengo, ASP Ayoub Mzee akiwa mita kadhaa mbele yake.
“tena Aisha, ndiyo atatusaidia kumpata yule kijana, alie tulitea mtafaluku” alisema tena RPC, kidogo staff officer anakunja uso kwa mashaka, “mh! kivipi afande, uoni kama ni hatari kwa askari wetu, maana inaonekana yule kijana ni hatari sana, na anauwezo mkubwa sana wakupigana, ameuwa watu wote hao bila kutumia risasi” alisema staff officer, akionyesha mashaka yake, juu ya uamuzi wa RPC.
“wala usiwe na wasi wasi, awezi kunuuwa Insp Aisha, nawajuwa wanawake, mpaka sasa wamesha jenga urafiki” alisema RPC, akionekana kuamini anacho kifikilia, “labda kama watatumia busara na dipromasia, kufanikisha zoezi ilo” alisema staff officer , akionyesha kuanza kuamini ule mpango.****
Naaaaaaaam!, nje ya kituo cha polisi, makao makuu ya jeshi ilo, wanaonekana askari wakiwa wamesimama nje ya gari aina ya landrover defender, wanaongea ili na lile, wengi wakijadiliana kuhusu, matukio ya leo jioni.
Kuanzia kifo cha kijana Lukas, vijana wa Nyondo, na sasa mtu mmoja asie julikana, katika maeneo yanayofanana, kwamaana maeneo ya chuo cha ualimu, na uongozi wa jamii.
Wakati polisi awa wanaendelea na hadithi zao, mala wakaliona gari dogo aina ya mercidise benzi jeusi, likija na kusimama karibu na mlango wa kuingilia ndani ya jengo la makao makuu.
Kisha wanashuka awatatu, walio valia suit nyeusi, na viatu vyeusi, ambao wanaelekea moja kwa moja ndani, na kusimama mapokezi, “sisi ni mawakara wa usalama wa taifa na kazi za siri, tunamwitaji mtu alie kutwa eneo la tukio kwnye chuo cha ualimu” alisema mmoja wao, huku anaonyesha kitambulisho chake.
Hapo wale polisi wawili, walio kuwepo pale mapokezi, wanatazamana, kidogo kama vile wanaongea kimoyo moyo, kisha askari wakiume mwenye cheo cha koplo anainuka toka kwenye kiti.
“nifwateni tafadhari” anasema yule polisi, huku anaongoza kwenye kolido la sakafu ya chini ya jengo ili, lenye sakafu nne za ghorofa, nao wanaanza kumfwata polisi yule.
Safari ni ndefu kidogo, ambayo inavuka vyumba kadhaa, kabla ya kuishia kwenye mlango mmoja mzito wa chuma, wenye kidirisha kidogo sana, tena lipo kwa juu, na limezibwa kwa kioo kizito. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

