
SEHEMU YA SITINI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TANO: Lakini kabla ajawafikia wale askari wenzake, akaona msururu wa magari yakiingia pale makao makuu ya jeshi la polisi, likiwepo gari la RPC, staff officer, RCO na gari lwenye polisi kadhaa likiwa nyuma kabisa, Insp Aisha anakumbuka kuwa, aliwaona wakina RPC kule msibani, nyumbani kwa mzee Nyondo. . ….ENDELEA
“wanavyo kuja, utazani wanakuja kukamata mwalifu” alisema Insp Aisha huku anasogea pembeni kupisha magari yale, yaliyo ingia kwa kasi ya ajabu, moja kwa moja, magari yale manne, yana enda kusimama mbele ya jengo kubwa la makao makuu ya jeshi la polisi.***
“naaaaaaaaaam!, turudi nyumbani lodge, ambako sasa baadhi ya watu walionekana wakiondoka mmoja baada ya mwingine, bwana Haule anatazama saa yake ya mkononi, ni saa tabi kasoro za usiku.
Anamtazama mke wake, mke wake, “nazani tunatakiwa kuelekea nyumbani, kesho tunasafari ya shambani” anasema mzee Haule, mke wake, yani mama Eric, anamtazama mume wake kwa jjicho lililolegea sijuwi kwa ulevi au kitu kingine, akitumia sekunde kadhaa, kama vile anatafuta neno la kumjibu mume wake.
“hivi baba Eric, kwani unazani sioni ulivyo busy, atahuko shambani akuendeki tena” alisema mama Eric, huku anaachia tabasamu lenye kulegeza macho.
Baba Eric anasogeza mdomo sikioni kwa mke wake, siyo hivyo mama Eric, nataka tuondoke, umeshaanza kulegeza macho” anasema mzee Haule kwa sauti ya kunong’ona.
Mama Eric anamtazama mume wake tena, safari hii tabasamu limetawara usoni mwake, kwa sekunde chache, tofauti na mwanzo, kabla ajasogeza mdomo sikioni kwa mume wake.
“sasa je, unazani mchezo, pombe yote imekimbilia chini” anasema mama Eric, huku anamalizia kwa kicheko, baba Eric yani bwana Haule akusubiri ata sekunde moja, akasogeza mdomo sikioni kwa mke wake.
“hiyo siyo shida, tatizo tupo mbele ya watoto” alisema mzee Haule, ambae kabla ile maliza kuongea tu, tayari kuna karatasi ilikuwa inawekwa mezani kwake, wote wanainua macho yao na kumtazama mtu alie weka karatasi mezani, tena mbele ya pale alipokaa mzee Haule.
Anaonekana mschana mhudumu, ambae mala kadhaa amekuja pale mezani na kuleta tishu, au bili za vinywaji, “samahani boss, sikupanga kuwavurugia” alisema yule mwanamke, alie valia sale za wahudumu, kisha akaondoka zake.
Mzee Haule anachukuwa kile kipande cha karatasi, na kukigeuza upande wapili, ambako anakutana na ujumbe “SA-24, amefanya mauwaji nyumbani kwa mmiliki wa TINO TRANS, ameuwa watu tano wenye silaha” ndivyo ujumbe ulivyosema.
“Nyondo atapoteza watu wake wote” anajisemea mzee Haule, huku akitulia kwa tafakari, “hivi, ni kwanini Nyondo anamsakama huyu Panya?” alijiuliza Haule, huku anajaribu kuongeza na kutoa, kugawanya na kuzidisha.
Mzee Haule anageuka yule mhudumu, ambae alikuwamita adhaa toka kwenye meza ya mzee Haule na familia yake, anamwonyesha ishala ya kumwita, na mhudumu anaanza kutembea kwa haraka kuifwata meza ya mzee Haule.
Yule mhdumu anamfikia mzee Haule, “nakusikiliza mheshimiwa” alisema mhudumu kwa sauti yenye nidhamu ya kihuduma za kijamii, huku anainama kidogo, kusogeza sikio lake mdomoni kwa mzee Haule.
Mzee Haule ana sogeza mdomo wake kwenye sikio la mhudumu, na kuanza kuongea kwa sauti ya chini, “piga simu kwa Mahundi, mwambie apeleke ujumbe kwa huyo bwana Nyondo, amwambie kuwa akae mbali na SA-24, vinginevyo atamaliza ukoo wake wote, na kuacha gumzo hapa mjini” alisema mzee Haule, kisha mhudumu akaondoka zake.
“aya mama Eric, tuondoke sasa, kama kuna mtu ajamalizakinywaji chake abebe” alisema mzee Haule, huku anasimama, na kumfanya kila mmojaachame mdomo kwa mshangao, lakini hawakuwa na lakufanya, zaidi ya kuinuka na vinywaji vyao mikononi, kisha wakaanza kuelekea kwenye gari.***
Naaaaaaaam!, muda unazidi kwenda, masaa yanasogea, sasa ilisha timia saa tano za usiku, mji ulikuwa unapoa huku nazizima kwa habari nyoingi za mauwaji, yaliyo tokea kwa usiku mmoja.
Sisi turudi mateka uhindini, nyumbani kwa bwana Augustino Nyondo, ambako, licha ya kuwa ni usiku, lakini watu walikuwa wanaendelea kuongezeka, sasa walionekana vijana kadhaa wenye miili iliyojengeka wakiangalia usalama getini na eneo la nje ya nyumba hii, hakika ungesema labda marehemu au mfiwa, alikuwa ni mtu wa watu.
Ila ukweli ni kwamba, watu awa walikuja hapa kwa wingi, wakiwa na kiu ya kujuwa nakufahamu kitacho tokea baada ya kifo cha Lukas, kijana ambae Nyondo alikuwa anampenda, na hakutaka chochote kibaya kimtokee, na alikuwa tayari kufanya chochote, pale anaposikia mdogo wake amechokozwa aua amekosa kile anacho kiitaji.
Watu walionekana wamejaa, nje na ndani ya uzio, wakigawika katika makundi yaliyo usisha hadhi na hali ya kiuchumi, bila kusahau jinsia, wakina baba wakikaa wenyewe, na wakinamama wakikaa wenyewe.
japo upande wanje, wapo wanawake walio changanyika na wanaume, asa wale waliotoka maeneo ya karibu, kama vile makambi, majengo, kimoro na mahenge.
Kiukweli tofauti na misiba mingine, hapa nyumbani kwa Nyondo hapakusikika kilo cha mtu ata kimoja, zaidi ya nyimbo za maombolezo, toka kwenye speeker kubwa za redio.
Kwenye kundi la waombolezaji, upande wa wanawake, tunamwona mwana dada Rose, akiwa amekaa pembeni ya kundi la wanawake wenzake, huku pembeni yake akiwa rafiki yake mpendwa Hidaya, huku wote wakiwa wamejitanda nguo vichwani mwao.
“Rose ebu tuondoke, unazani wakituona itakuwaje” alisema Hidaya kwa sauti ya kunong’ona, huku macho yake yakikosa utulivu, maana alikuwa anatazama huku na huku.
“unazani sasa hivi tutapata usafiri gani?” anauliza Rose kwa sauti ya chini, “ilakweli, sas ivi hakuna dala dala” anaunga mkono Hidaya, kwamba swala la kuondoka mida hii, lilikuwa gumu kwa upande wao. . ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU