TOBO LA PANYA (70)

SEHEMU YA SABINI

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TISA: “siku za nyuma nimegundua mambo mengi, na kuyafanikisha, inakuwaje huyu mtoto mdogo, SA-26, ambae anauwa maeneo ya huku huku nyumbani….” anajisemaa mzee Haule, ambae anasita ghafla, huku anatazama upande wake wa kulia, yani nje ya barabara, ambako anaona picha flani iliyo jirudia kichwani mwake, baada ya kuiona msaa kadhaa yaliyopita. . ….ENDELEA …….

“Toyota hiace la mdogo wake Nyondo” anajisemea mzee Haule kwa sauti ya kunong’ona, “mschana mrembo” anasema tena mzee Haule, kwa sauti ya kunong’ona.

“mdogo wake Nyondo ameuwawa madizini” aliendelea kuwaza mzee Haule, huku akivuta ile picha aliyo aiona eneo lile, kwamba mschana mrembo kama yule kutokea seed farm, na kijana kama yule ambae mwonekano wake, nikama shamba boy.

“mpole, mtaratibu, uwezi kumzania” alisema mzee Haule, kwa sauti ile ile ya kunong’ona, “yes! yes! ni yule kijana mlinda shamba” alisema mzee Haule kwa sauti ya juu ya yenye furaha” huku anakanyaga mafuta kwanguvu, na gari linaongeza mwendo.

Familia nzima inatoa macho kwa mchangao, na kabla awajauliza, tayari mzee Haule alisha kanyaga klutch na kutupia gia namba nne, kisha akaachia clutch na kukanyaga pedeli ya mafuta, na gari linazidi kuongeza mwendo.

“we mzee, mbona atukuelewi” alisema mama Eric kwa sauti yenye mshangao, “ni yule kijana mlinda shamba” alisema mzee Haule huku anakanyaga tena klutch na kutupia gia namba tano, kicha akaongeza mafuta, “baba tumesha fika, mbona unakanyaga….” Eric akupewa nafasi ya kumaliza sentensi yake, mzee Haule alikanyaga clutch, na kukata kona kushoto.

Abilia wote, wanalala upande wa kulia, kisha wakaa sawa, mzee Haule anaokanyaga mafuta, kwanguvu, “baba mbona ujalewa sana” anasema Vestina, kwa sauti ya tahamaki.

“nawai kupiga simu, ni yule kijana mshenzi mlinda shamba” alisema mzee Haule, huku akiendesha gari kwa speed, na kufukia mashimo, kama yupo kwenye mashindano.

Ndani ya gari wote kimya, wanasikiliza sauti ya engine, na kushuhudia jinsi mzee Haule anavyo lala na kona, za mtaa, kukwepa nyumba za watu, na miti ya pembezoni mwa barabara.

Sekunde chache baadae, tayari mzee Haule alikuwa amesha simamisha gari nje ya nyumba yake, na kushuka haraka, akiliacha gari lina unguruma, akakimbilia ndani ya nyuma, akiicha familia yake ndani ya gari wanamtazama kwa mshangao.

“mh! Eric usije ukaingia kwenye iyo kazi, vinginevyo utakuwa kichaa” alisema mama Eric huku wote wametulia kwenye seat zao, “kwani baba anafanya kazi gani?” anauliza Vestina, “mh!, mimwenyewe sijuwi” alijibu mama Eric, huku anachukuwa chupa ya wine, na kufungua mlango wa gari kwa maana ya kushuka toka kwenye gari.

“Eric zima gari, kama na wewe umelewa mwambie huyo mwenzio azime” alisema mama Eric, huku anatembea kuelekea ndani, “he!, mimi najuliwa wapi” alisema Eva huku anashuka toka kwenye gari akifwatiwa na Vestina, kisha nao wanaelekea ndani ya nyumba wakimwacha Eric ndani ya gari.

Sekunde chache walitumia kuufikia mlango wa kuingilia ndani, kiasi cha kuanza kusikia sauti ya mzee Haule akiongea na simu, “bila kuchelewa Mahundi, yani haraka sana, vijana waje mtaani kwangu wakiwa na silaha za maana, silaha ambazo wanaamini, SA-26 awezi kuzikwepa” hayo ni baadhi ya maneno ya mze Haule, kabla ajakata simu.****

Naaaaaam!, kule Mateka uhindini, nyumbani kwa bwana Tino Nyondo, palikuwa pana zidi kuongezeka watu, na kubadirisha taswila, toka msibani kuwa kama sherehe.

Idadi kubwa ya watu waliokuwepo eneo lile, hakika walikuwa wanafurahi kwa kifo cha kijana Lukas, huku wengine wakionyesha furaha yao wazi wazi, sina hakika kama Tino Nyondo, angewaona angeweza kuwapa nafasi ya kujieleza.

“jamaa aliwai kumkosa kosa mama na gari lake, alafu akaanza kumtukana mama, dah! iliniuma sana, hapo ninge mjibu au kupigana nae, kaka yake lazima amengekuja kuuwa familia nzima” alisema kijana mmoja, kati ya wale walio jaa nje ya uzio.

“achana na hiyo, juzi wamemuuwa mfanyakazi wao, kina demu wa jamaa, alimkataa Lukas, walimkatakata vipande, kama jambazi alie waibia” alisikika mwingine, akisimulia habari iliyo watia unyonge wasikilizaji.

Tuachane na huku nje, twende ndani ya uzio, ambako tunawaona wakina Rose na Hidaya, bado wamekaa kwenye kundi la wanawake wenzao, ambao kwa idadi kubwa ni wafanyakazi wa bwana Nyondo, iwe kule ofisi, au hapa nyumbani.

Maongezi yalikuwa ya chini chini, huku kiwango kikubwa cha maongezi kikiwa ni juu ya mambo ambayo Lukas alikuwa anayafanya kwa watu, japo hakukuwa na jambo jema ata moja.

“weeee!, kuna mambo atuwezi ata kusimulia, kama alivyo mfanyiaga yule dada wa mapokezi pale ofisini, alikuwa mnene hivi” alisikika mwanamke mmoja akiongea kwa sauti ya chini.

“ndiyooo!, namkumbuka Fauster, aliachaga kazi ghafla” alisema mwingine akionyesha kuwa na shahuku ya kusikiliza ile hadithi, “ndiyo huyo huyo, tena Lukas ndiyo alisababisha Fauster aache kazi” alisema yule wa mwanzo, huku wenzake wakitega sikio kusikiliza, simulizi ile ya moja ya matukio ya marehemu lukas.

“siku hiyo Fauster alikuwa anatoka chooni, pale pale ofisini, sindio akakutana na Lukas, nae anatoka chooni, mbona alimvutia chooni, na kuanza kufanya, alimwambia ole wake upige kelele” alisimulia yule mwanamke, na mwenzie akadakia.

“bora Fauster, ilikuwaje kwa Semeni, yeye sialijifanya kumkataa Lukas, sasa unaambiwa waimchukuwa kwanguvu, wakampeleka chumbani kwa Lukas, kisha Lukas na wakina Kubaga, wakambaka weeee mpaka subuhi” alisema mwanamke mwingine.

Tuachane na hadithi za Lukas, ambazo zilikuwa zinaendelea kusimuliwa na wanawake wale, hadithi ambazo wanaushuda nazo, sisi tuna sogea upande wa wanaume, kule ambako, amekaa bwana Nyondo na mlinzi wake Kichondo, akiwa amesima nyuma yake.

“Kichondo nakuja sasa hivi, naenda chooni mala moja” alisema Nyondo, huku anainuka toka kwenye kiti, lakini Kichondo anakiona kitu flani kinadondoka toka usawa wa mapaja ya boss wake. . ….
MWISHO SEASON THREE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata