SEASON 4: TOBO LA PANYA (71)

SEHEMU YA SABINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI: “Kichondo nakuja sasa hivi, naenda chooni mala moja” alisema Nyondo, huku anainuka toka kwenye kiti, lakini Kichondo anakiona kitu flani kinadondoka toka usawa wa mapaja ya boss wake. . ….ENDELEA…….

“samahani boss, sijuwi umeangusha nini?” alisema kichoondo, huku anainama, kwaajili ya kuokota kipande cha karatasi, kilicho kunjwa vyema kabisa, “ni la kwako ili?” anauliza Kichondo, huku anakujua lile karatasi.

Tino Nyondo, anatazama lile karatasi, ambalo lilikuwa na mandishi mengi, yaliyoandikwa kwa karamu ya wino, “sina kumbu kumbu, ebu kwanza nikione” alisema Nyondo uku anachukuwa karatasi toka mkononi mwa Kichondo, na kulitazama vizuri.

“kwako bwana Tino Nyondo, ushauri toka kwa mtu anae kutakia mema, kabla ujaendelea kumfwata huyo kijana, kuwa tayari kwa mambo ya fuatayo, ikiwepo na vifo vya vijana wako wengi zaidi, pili hasara kubwa ya mali zako, tatu pengine ni kifo chako wewe mwenyewe, sina uhakika na familia yako, engine akaionea huruma” inamfanya Nyondo atabasamu kidogo.

Ujumbe ule aukuishia hapo, “kwakifupi ni kwamba, unapambana na mtu hatari sana” hapo ndipo ulipoishia ujumbe ule, ambao ulimfanya Nyondo amtazame Kichondo, “hivi nani ameleta huu upuuzi?” aliuliza Nyondo, kwa sauti ya chini, lakini iliyojaa hasira.

“boss nashindwa kuelewa……., hooo nimekumbuka boss, atakuwa ni yule mwanamke mtu mzima” alisema Kichondo, kwa sauti ya ung’amuzi, “pumbavu, yani yule mwanamke anatufanya sisi wajinga” alisema Nyondo, kwa sauti ile ile ya chini, yenye hasira mbaya, safari hii akiwa anaanza kutembea kuelekea kwenye geti la kutokuea nje.

Kichondo nae anamfwata boss wake, ambapo wanatembea kwa mwendo wa haraka, huku wanatazama mbele, pengine wanaweza kumwona yule mama, ambae awakumwona mpaka walipo fika kwenye lango la kutokea nje.

Wanavuka geti, na walinzi wawili wanawafwata, watu wengi pale nje wanawatazama kwa macho ya udadisi, wana watazama watu hao wambao wanaenda kusimama mita achache upande wa kushoto, yani nje ya uzio.

Nyondo na Kichondo wanatazama kushoto na kulia, pasipo kuona kitu, “sijuwi amesimama wapi huyu mwanamke” anasema Nyondo huku anamgeukia mlinzi mmoja.

“yule mama mtu mzima alie toka sasa hivi, ameenda wapi?” anauliza Nyondo, kwa sauti ya chini yenye hasira, mlinzi anaonekana kukosa kumbu kumbu ya mwanake huyo, lakini bahati nzuri, mlinzi wa pili anaanakumbuka.

“aliondoka na gari, lilikuwa paleee” anasema yule mlinzi, na hapo Nyondo anaachia msonyo mkali sana, mnapaswa kuwa makini muda wote, kosa jingine nakata kichwa cha mtu” alisema Nyondo kwa sauti ya chini, kisha akaanza kutembea kurudi ndani ya geti.

“ndiyo boss tutakuwa makini boss” walisikika wale walinzi, huku wanamtazama Nyondo, alie ongozana na Kichondo, kuingia ndani ya geti.****

Yaaaaaaap!, tupo mashariki mwa mji wa Songea, ndani ya BMW jeusi, ambalo sasa linaendeshwa na mwanadada Farida, ambae wenzake wanamtambua kama SA-54, ambae sasa anaikamata barabara kuu iendayo mikoa ya kusini, yani Lindi na Mtwara.

Farida anaendesha gari, huku anakichwani mwake anawaza ili na lile, ni kuhusu hatima yake, je atamaliza salama jukumu ili, kabla ya kuingia kwenye mikono ya TSA, maana anaitaji maelezo ya kueleweka, ili kuepuka kifo, je maelezo gani yatamsaidia, ukichukulia anamsaidia mtu anae tafutwa na TSA, ili auwawe.

Wakati Farida anaendelea kuendesha gari, huku anawaza ili na lile, mala anayaona magari mawili aina ya Toyota land cruiser, yasiyo na namba yoyote, yakija upande wake, kwa mwendo wa kasi, ata alipotazama vyema, akuweza kuona mtu aliepo ndani ya gari, kamaana vioo vyagari vilikuwa ni vya giza.

“mh!, TSA, watakuwa wanaenda kwa Panya, inamaana wamesha juwa anapoishi” anawaza Farida, ambae alikuwa amejipatia jibu moja kwa moja, hapana natakiwa kuwai nyumbani kwa baba yake Panya, nikampigie simu, nimjulishe juu ya jambo ili” alisema Farida huku anakanyaga mafuta kuelekea upande wa mjini, sasa alikuwa anapita nyumba za makazi ya viongozi wa chama tawara cha kisiasa.

Lakini alipo kuwa anakatiza maeneo ya njia panda ya Songea boys, akashtuka magari mengine mawili aina ya land rover defender, yakija mbele yake katika mwendo mkali kupita kiasi, akakanyaga brake za haraka.

Hapo aliyaluhusu magari yale yapite kwa kasi ya zimamoto, yakieleka upande ule ule aliotokea yeye, safari hii, Farida anapata bahati ya kuona namba za gari, na kuwaona watu waliokuwepo ndani ya gari, huku mitutu ya bunduki ikiwa inachungulia, maana vioo vilikuwa chini.

“leo ni kashehe, lazima niwai nikamjulishe Panya, kisha nirudi kumsaidia” alisema Farida huku anakanyaga tena mafuta kwa nguvu kuondoa gari kuelekea mabatini.***

Naaaaaam!, huko seed farm nako, kwenye shimo la Panya, mwanadada Anastansia, ambae alisha maliza kula muda mrefu ulio pita, tayari alikuwa amesha safisha sahani alizo tumia kwa chakula, japo kuna kitu kilimtisha sana Nancy.

Ni kwamba, ndani ya chumba kile kilicho kamilika, kila kona kulikuwa na silaha, yani kwenye badhi ya mabati ya jikoni, baadhi ya friji na kwenye draw za kitanda, tena alikuwa anaamini kuwa, pengine kuna baadhi ajaziona.

Sasa mwana dada huyu mrembo, mwenye sura na umbo la kuvutia, ambae baada ya ukaguzi wa mle ndani, akakutana na simu na kuamua kupiga kwa mama yake, lakini alikuta simu ni mbovu, japo ilimshangaza sana, kwa kuwa kijana mpole alitoka kuitumia muda mfupi uliopita.

Sasa alikuwa amejilaza kwenye kitanda, amevalia tishert nyepesi na suruali ya truck suit, iliyo mkaa vyema, na kuonyesha umbo zuri za mwana dada huyu, alie jaliwa mapaja ya wastani makalio ya kuvutia. . ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata