
SEHEMU YA SABINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MOJA: Sasa alikuwa amejilaza kwenye kitanda, amevalia tishert nyepesi na suruali ya truck suit, iliyo mkaa vyema, na kuonyesha umbo zuri za mwana dada huyu, alie jaliwa mapaja ya wastani makalio ya kuvutia. . ….ENDELEA…..
Alikuwa amelalia tumbo, mguu mmoja ameukunja, na kufanya makalio yake, yaonekane vyema, huku truck ikishindwa kuficha kiuno na kufanya mfeji wa makalio kuonekana kwamba, ni kwamba akivaa kabisa nguo ya ndani.
Anastansia pale kitandani, akuwa amelala usingizi, ukweli alikuwa macho anawaza moja na mbili, asa kuhusu mwisho wake, na usalama wake na kijana mpole, ambae sura yake na roho yake, ni vitu viwili tofauti.
Ukweli katika maisha yake yote, leo ameshuhudia mauwaji ya kikatili sana, kilicho saidia nikwamba, walio uwawa ni watu waliotaka kumtendea unyama, “kosa yule kaka, sijuwi ingekuwaje, maana wale watu wanawauwa ata polisi wenyewe” anawaza Anastansia, ambae anajiona kama yupo sehemu salama.
Anastansia anajiinua kidogo, sura yake nzuri iliyolegea kwa uchovu, inaonekana, yeye anapeleka macho kwenye saa ya ukutani, “saa sita nanusu, anajisemea Anastansia, huku analala kama alivyo lala mwanzo.
“lakini wale watu ni wakatili sana, sijuwi kama atarudi salama” anawaza Anastansia, akianza kuingia wasi wasi na huruma juu ya kijana wetu, “lakini anajuwa kupigana, lazima ata washinda tu” anajisemea Anastansia, ambae anakumbuka jambo.
“polisi pia wanamtafuta, sijuwi nae atapigana nao” aliwaza Anastansia, huku anajisgeuza na kulala nusu ubavu, akitazama ukutani, huku miguu yote ikiwa kifudi fudi, mmoja ameukunja, na kuzidi kuleta mwonekano wa utamanishi.
Wakati anawaza hayo, mala Anastansia anashtuka shuka likiangukia mwili mwake, usawa wakiuno, anashtuka na kugeuka, akimtazama alie mfunika, “usipende kuacha vitu muhimu vikiwa nje” ilikuwa ni sauti ya upole, toka kwa kijana mpole, aliealuiwa amesimama mita chache toka kitandani.
Anastansia anaganda akiwa ametoa macho ya mshangao, akimtazama kijana mpole alie jawa na damu kwenye koti na tishet lake, bila kusahau mikono yake.
Kijana mpole anaanza kutoa silaha, moja baada ya nyingine kwenye koti, ikiwa bastora za kirusia, na visu kadhaa, akiviweka sehemu alizo toa wakati ule anaodoka, yani kwenye makabati na friji.
Kisha akavua jacket le nyewe nakufwatia na tishert, na kuacha kifua chake, kilicho jengeka kimazoezi, kikiwa wazi, na kumfanya Anastansia akimtazame kwa macho ya mshangao, sasa yakibadirika na kuanza kuwa ya kustaajabu.
Anastansia ambae mpaka sasa ajasema kitu, anamtazama kijana huyu, alie chafuka kwadamu, ambae anavua suruali yake, na kubakia na bukta ndogo, mfano wa boxer, kisha anachukuwa nguo zote na kuingia bafuni, ambako kuna mashinde ya kufulia na kukausha nguo.
Na wakati huo ndio ambao Anastansia anakumbuka jambo, “hivi huyu mtu atalala wapi?” anajiuliza Anastansia, huku anatazama kile kitanda, “lakini kikubwa, tunalala wawili bila kugusana” alisema Anastansia huku anasogeza mto pembeni, upane wa ukutani, akifwatia yeye mwenye.
“hapo panamtosha” alisema Anastansia kwa sauti ya chini, huku anapapasa sehemu kubwa aliyo iacha, “lakini anaimaini akito tokea kitu” anasjisemea tena Anastansia kwa sauti yenye kujipa matumaini ya usalama wa kitumbua chake.****
Naaaaaam!, bado tupo seed farm, magari mawili aina ya Toyota land cruiser, yanasimama mbele ya nyumba ya mzee Haule, ambapo anaonekana mzee Haule mwenyewe.
Mzee Haule, akiwa amesimama mbele ya nyumba yake upande wa barabarani, alikuwa ame kamata bunduki ndogo aina ya pisto 92, toka Israel, huku valia nguo nyeusi, kwa maana ya suruali nyeusi na suetas jeusi, akimalizia na kofia ya sueta nayo nyeusi, pamoja vest ya kuzuwia risasi, yenye mikebe mitatu ya risasi za pistol.
Milango ya magari inafunguliwa, wanashuka wanaume sita, waliovalia kama mzee Haule, wakiwa na silaha aina ya SMG ya model 81, zao la SMG ya 57, PKM ya mwaka 48, hii ikitokea china, walizo zishika mikononi mwao, huku vifuani mwao wakiwa wamevalia vesti za kuzuwia risasasi, zenye mifuko iliyo jaa mikebe ya risasi.
“haraka sana hatuna muda wakupoteza” anasema mze Haule, huku anasogea barabarani zaidi, sehemu yenye uwazi, mbele ya gari la mbele ambalo lilikuwa bado limewasha taa.
Wanaume sita wanamsoglea mzee Haule, bwana Mahundi akiongoza, mzee Haule anahukota fimbo ndefu toka chini, kisha anaanza kuchora ardhini, “hii ni barabara hii tuliyo simama, hapa mwisho wa mtaa, huku mbele kuna mapori na vichaka vya wastani” anaeleza mzee Haule, akitumia mchoro anao uchora,.
“Huku nyuma kuna njia ndogo ya waenda kwa miguu, eneo ili la mbele, lina miti minne mmoja ni mkubwa, pembeni ya kichuguu kuna kibanda cha udongo, ambacho anaishi SA-26” alieleza mzee Haule huku SA wenzake wakimsikiliza kwa umakini.
“huku mbele kuna bonde la mtu luhuhila, likifwatia na mwinuka wenye makazi ya familia zaidi ya mia nne, kwahuyo ukiinua silaha yako nyunzi alobaini na tano, itaenda umbali wa mita elfu moja, yani kijiji cha luhuhila, na kuuwa familia za watu wasio na hatia” alisema mzee Haule, akisisitiza jambo, kumbuka hakuna kizuwizi cha milima wala miti mikubwa mingine ambayo inaweza kuzuwia risasi” alisema mzee Haule.
“AS wa gari la kwanza wata shukia hapa na kutembea kwa miguu, wakiwa wametangulia, na mala watakapo karibia na kutujulisha, SA wa gari la pili, wataenda na gari kwa haraka na kuingilia upande wa mbele, kisha kwa umakini mkubwa tuna vamia, na kumkamata SA-26, ambae atakuwa ajajiandaa kwa mapambano” alisema mzee Haule, akimaliza kwa kutoa mpango wa kuondoka.
“ikitokea tunaitaji kuondoka, ikiwa kwa kuzidiwa au baada ya kufanikiwa, makutano ni hapa, kwenye njia panda ya kuelekea msamala, kumbukeni, SA-26, hayupo peke yake” alisema mzee Haule kabla ya kuluhusu watu waondoke, huku yeye na bwana Mahundi wakibakia nyuma, na kutembea taratibu kwa miguu, kuelekea kule ambako kijana Hance anaishi.**
Anastansia akiwa bado kitandani, amesahau kuhusu mkasa wote wa toka jioni ya leo, anawaza namna atakavyo upitisha usiku waleo, akiwa kitanda kimoja, na huyu na kijana huyu muuwaji, asie mfahamu ata jina lake.
Mala Anastansia akasikia milio wa simu, “mh!, simbovu hii?” anajiuliza Anastansia, huku anajiandaa kuinuka, lakini wakati huo huo, anaona mlango wa bafuni unafunguliwa na anatokea kijana mpole, akiwa na bukta, huku anajifuta maji na tauro alilokuwa amelishika mkononi. . ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU