TOBO LA PANYA (73)

SEHEMU YA SABINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI: Mala Anastansia akasikia milio wa simu, “mh!, simbovu hii?” anajiuliza Anastansia, huku anajiandaa kuinuka, lakini wakati huo huo, anaona mlango wa bafuni unafunguliwa na anatokea kijana mpole, akiwa na bukta, huku anajifuta maji na tauro alilokuwa amelishika mkononi. . ….ENDELEA…..

“tayari” alisema kijana mpole Hance, huku anatembea kuelekea sehemu simu ilipo, huku mwana dada Nancy akimsindikiza kwa macho, akiutazama mwili shupavu wa kijana huyu, mwenye sura na utembeaji a upole.

Nancy anamwona kijana pole, akiifikia simu na kuinua mkonga, “hallow, nani?” anauliza Hance, kwa sauti tulivu, “sikia Panya, nimepishana magari manne, yanakuja huko, mawili ni ya TSA, nahisi wanakuja kwako” anasema Farida kwa sauti ya chini yenye tahadhari kubwa, ni wazi akutaka wazazi wa Hance wasikie lolote.

Hapo Hance anatulia kidogo, kama vile anawaza jambo, kisha anatikisa kichwa cha kukataa, yani kushoto na kulia, “sizani kama wanaweza kulifikia, tobo la Panya” anasema Hance kwa sauti ya chini yenye uzani mkubwa waupole.

“hapana Hance, utakiwi kudharau kiasi hicho, mpaka wanakuja hapo inamaana wamesha pata taarifa nyingi, juu yako” alisikika Farida kwa sauti ya chini, Hance anatikisa tena kichwa.

“usihofu Farida, wanaweza kumjuwa Panya, lakini awawezi kumfikia” alisema Hance kwa sauti ile ile ya upole, “kwahiyo uitaji msaada wangu?” anauliza Farida, kwa sauti ya mshangao.

Unaitaji kupumzika, kesho nitaitaji msaada wako” alisema Hance kabla ya kurudisha mkonga wa simu sehemu yake, kisha akatazama kitandani, anamwona mwanamke mrembo kupitiliza akiwa amegeukia upande wake, anamtazama kwa macho yenye udadisi.

Hance mtazama kwa sekunde kadhaa mrembo huyu, ambae kiukweli siyo tu sura, ila ata umbo lake ni zaidi ya hatari kwa lile amlisho la kuto kutamani mali ya mtu mwingine, maana ulalaji wake ulikuwa ni ule wanusu chali a

Anastansia nae anaona utazamaji wa kijana huyu, ambae kiukweli siyo tu kuto kumfahamu jina, ila hapo mwanzo hawakuwa na ukaribu wakukaa chumba kimoja na mna hii.

“mh!, hii ni hatari, inaitaji moyo kushinda” alijisemea Hance, huku anatembea taratibu kuelekea kwenye friji moja dogo lililopo pembeni ya kochi, upande wa kitandani.

“mbona umenitazama hivyo, alafu unaanza kuongea peke yako?” anauliza Anastansia, huku anamtazama kijana mpole ambae anaendelea kutembea kuelekea kwenye friji, “ninakazi ya kufanya, pengine naweza kukujibu nikiimaliza” alisema kijana mpole, ambae safari yake inaishia mbele ya friji ilo dogo.

Anastansia akiwa bado anashangaa jibu la kijana mpole, anamwona akilifungua lile friji, kwa mtindo wa freezer, yani friji lilifunguka mlango wa juu, japo mwonekano wake, ni ule wa kufunguka kawaida, inamshangaza kidogo Anastansia, ambae toka anazaliwa tayari friji lilikuwepo nyumbani kwao.

Anastansia anatoa macho kwa shahuku ya umbea, kuona mle ndani kitatoka nini, anashangaa kuona upande wa ndani wa kifuniko kile cha friji, kuna kioo cheusi mfano wa TV za kisasa, mbele kukiwa na kibao cha elufi mshanyiko na namba.

Kioo kinatoa mwanga wa blue, na mwisho unageuka mweupe, sambamba na vipande vidogo vya picha tofauti tofauti, zilizo ambatana na majina ya kila kipicha, kikielekeza matumizi yake.

Ni kweli Anastansia nyumbani anacomputer, kifaa adimu sana, kuwa nacho mtu binafsi, kwa wakati huo wa miaka ya 99 na 2000, na kifaa iki kinafanana kiasi cha coputer, lakini kivipi kwenye friji.

“he!, kumbu hii ni computer” anasema Anastansia huku anainuka toka kitandani, akiwa amejifunua lile shuka alilofunikwa na Hance, pasipo kujari tumbo na kiuno vilivyoonekana kidogo, kutokana na tishert kupanda juu kidogo.

Anamsogelea Hance, huku akiachilia makalio yanatikisika ndani truck, na kuonyesha wazi kabisa kuwa hakuwa amevaa nguo yoyote ya ndani, “unazani nivyema kuangalia ninacho kiangalia?” aliuliza Hance kwa sauti ya upole, huku anafungua kipicha kimoja, kilicho andikwa camera.

“mh! ata kama unataka kutazama video za x, mimi nimesha vuka miaka 18” anasema Anastansia, huku ana cheka kwa aibu, “zaidi ya x” alijibu kwa kifupi Hance, huku kipicha kinafunguka na kioo kina badirika rangi can kuwa cheusi.

Anastansia anatazama vizuri, kuangalia kinachofwata, lakini anagundua kuwa ile aikuwa rangi nyeusi kama nyeusi, ila ni giza, maana katika mwanga afifu, tuna weza kuona watu kadhaa walio walia nguo nyeusi bullet proof na silaha zao mikononi, wakinyatia kwa tahadhari, kukatiza kwenye vichaka virefu.

“wapuuzi” anasema Hance, huku anabofya kitufe kwenye ubao wa elufi, na inadakia video nyingine, hapo wanaonekana tena watu kama wale, fofauti ni kwamba, awa walikuwa kwenye barabara, nao wanatembea kwa tahadhari kusogelea upande mpiga picha wao alipokuwepo.

“kwahiyo hii video inatisha hen?” anauliza Anastansia, huku anakaa kwenye kiegemeo cha kochi, “sina hakika, ila nahisi mwisho wake wakufurahisha” alisema Hance kwa sauti ya upole, huku anabofya tena kitufe kingine, na picha zote mbili zikajaa kwenye kioo, zikipeana nafasi, kila moja upande wake.

Baada ya hapo Hance anatoka na kuelekea upande wajikoni, “sasa mbona umeweka picha ya vita, alafu unaondoka?” anauliza Anastansia, huku anakaa viyema, “nina jambo la kufanya” anajibu Hance, ambae anapofika jikoni, anafungua moja kati ya makabati, na kutoa visu vya mkunjo wa nusu mwezi, kule #Mbogo_Land wanaita chikwa kwa, nikisu kilicho wai kutumiwa na mtu hatari sana, Jenssen Victor Yasson, au Captain Chui Mchafu.

“mh!, sasa mbona steling aonekani” anauliza Anastansia, ambae bado amekodolea machop TV, “steling yupo ndani anajindaa” anajibu Hance, huku anatembea kueleka upande wa bafu.

“he! watu wenyewe wanakimbia” anasikika Anastansia akiongea kwa mshangao, hapo Hance anakimbilia haraka kwenye kioo cha TV, anawaona wale jamaa ambao aliwatambua kuwa ni TSA, wakianza kuondoka eneo la tukio, kwa haraka na tahadhari, huku wakisisitizana kufanya haraka. . ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata