TOBO LA PANYA (74)

SEHEMU YA SABINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TATU: “he! watu wenyewe wanakimbia” anasikika Anastansia akiongea kwa mshangao, hapo Hance anakimbilia haraka kwenye kioo cha TV, anawaona wale jamaa ambao aliwatambua kuwa ni TSA, wakianza kuondoka eneo la tukio, kwa haraka na tahadhari, huku wakisisitizana kufanya haraka. . ….ENDELEA…..

“nini kimetokea?” anauliza Hance kwa sauti ya wazi kabisa, huku anakodolea macho kioo cha computer yake, ambayo sasa anaona magari mawili aina ya land rover defender yakisimama nje ya nyumba yake, kisha wanashuka vijana kadha toka kwenye magari yale, wakiwa na silaha mikononi mwao.

Hance anatazama kioo kile chenye kuonyesha video, ambayo inawaonyesha watu wale wakisogelea banda dogo la udongo, huku wakipeana ishara za kuvamia kushambulia,.

“andikeni hamna bahati” alisema Hance, huku anaachia tabasamu pana, tabasamu ambalo, Anastansia analikumbuka kuwa aliliona wakati ule, kule midizini, kabla Hance ajaanza kuwashambulia wakina Lukas.

Kengere ya tahadhari inagonga kichwani mwa Nancy, ambae anamtazama Hance, kwa macho ya mshangao na uoga, “kuna nini kaka?” anauliza Anastansia kwa sauti yenye mshangao.

“kuna paka anakuja kwenye shimo la Panya, zima hiyo computer, kisha pamda kitandani, lala usingizi” alisema Hance, kwa sauti yake tulivu ya taratibu, huku anaanza kutembea, kueleka upande wa chooni.

Anastansia anatazama kioo cha computer, na kutazama vizuri ile video, ambapo anaweza kuona vyema, vijana zaidi ya sita wakiwa na silaha z-ao, wamezunguka kibanda cha udongo, ambacho anakitambua mala moja.

“kumbe yeye ndie steling” anajisemea Anastansia, kwa mshangao, huku anageuka na kumtazama kijana mpole, ambae sasa alikuwa anatokomea chooni, huku amevalia bukta pekee, visu viwili vikiwa mkononi mwake.

Anastansia anarudisha macho kwenye kioo cha cha computer, anaendelea kutazama watu wale, wakikoki bunduki zao, na kuelekeza kwenye kile kibanda cha udongo, kilichopo mbele yao, “sijuwi ameenda kufanya nini huko chooni, kwani akumaliza kuoga?” anajiuliza Anastansia, ambae alisha pewa maagizo ya kuzima ile computer. ***

ILIKUWA HIVI.
Dakika chache zilizo pita, wakati vikundi viwili vya TSA vinanyatia kusogelea kwenye banda, ambalo ni mlango wa shimo la Panya, wakitokea pande mbili tofauti, wakati kundi A likitokea mashariki, kupitia kwenye vichaka virefu na mafukutu ya miti mifupi mifupi.

Wakati huo kundi B linatokea kusini, kwenye njia nyeupe ambayo inauwezo wa kupitisha magari, bwana Haule na bwana Mahundi wakiwa upande wa kusini, nyuma zaidi, wakija taratibu kuelekea kaskazini, ambako shimo la Panya lipo.

Mala wakasikia ngurumo za magari toka nyuma yao, ata walipogeuka na kuona mianga ya taa za magari mawili yakija nyuma yao, umbali wa mita za idi ya mia moja, wakachepuka pembeni ya barabara na kusubiri magari yapite, ili waweze kuyatambua.

Magari yalipo katiza usawa wao, wote wanagundua kuwa, ayakuwa magari yao wala magari ya polisi, ila ni magari ambayo ayakuwa na namba za usajiri, na kwabahati mbaya, vioo vya madirisha vilikuwa wazi, hivo wakabahatika kuona vijana kadhaa waliopo ndani yamagari hayo, wakiwa wameshikilia bundu zao, maana mitutut ilionekana kichungulia.

Haraka sana kwa kutumia redio call zao, Haule na Mahundi wakawajulisha wenzao waliopo mbele, kuwa waondoke haraka eneo la tukio, kwamaana kuna uwezekano, wa kuwa, vijana wa Nyondo wamesha gundua makazi ya adui yao.

Muda mfupi sana baada ya TSA kuondona eneo la tukio, magari mawili aina ya land rover defender, yanasimama mita chache toka kwenye kibanda, cha udongo, kilicho jengwa pembeni kabisa ya kichunguu kikubwa, kilichozungukwa na shamba dogo lenye mazao machache, ikifwatia na vichaka virefu.

Licha ya TSA kuondoka eneo la tukio, lakini bado mzee Haule na bwana Mahundi, wana sogea mbele kidogo, upande wa kaskazini, kisha wanajibanza sehemu nzuri, kwenye kichaka chenye nyasi fupi pembezoni mwa barabara.

Kisga wanatoa viona mbali, yani darubini au binocular kama waingereza wanayo waita, alafu wanatumia darubini hizo, kutazama kasikazini zaidi, ambako kipo kile kibanda cha udongo, ambacho kina kaliwa na kijana mnyonge, ambae bwana Haule anaamini kuwa, ndie SA- 24.

Naaaaaaam, wawili awa, yani mzee Haule na bwana Mahundi, kwamsaada, darubini zenye muundo wa matumizi ya usiku, yani night version, wanaweza kuwaona vijana wale, wakielekeza bunduki zao za kivita, kwenye kile kibanda cha udongo.

Sekunde chache mbele, wanaona miali ya moto ikichomoka kwa kasi ya ajabu kwenye mitutu ya bunduki zao, kuelekea kwenye kibanda cha undogo, sambamba na milipuko ya risasi mfululizo.

Sekunde therasini za milipuko ya risasi, zinakoma na vijana wale wanaonekana wakitoa mikebe ya risasi kwenye bunduki zao, na kubadiri nyingine, ni wazi zilikuwa zimeishiwa risasi.

Lakini basi, wakati mzee Haule na bwana Mahundi wakiwa wanawatazama wale jamaa waliokuwa wanabadiri magazan za silaha zao, kwakutumia darubini zenye uwezo wakuona gizani, mala ghafla wanaona tukio la kushangaza, “mungu wangu, nini kile” anauliza mzee Haule huku anatoa darubin machoni mwake, na kumtazama Mahundi, ambae pia alikuwa amefanya vivyo hivyo. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata