TOBO LA PANYA (81)

SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI: Mzee Haule anamtazama Eric, “kanisubiri hapo pale, naitaji kuongea kidogo, na kijana mfugaji” alisema mzee Haule, na bila kuuliza Eric akatembea kurudi upande wa barabarani. ….ENDELEA…..

Wote wanamsindikiza kwa macho, mpaka anapo fika umbali wa mita kama kumi hivi, mzee Haule akamtazama Hance, “ok!, kijana nazani umeshangazwa na ujio wangu asubuhi hii” alisema mzee Haule, kwa sauti ya chini, yenye tadhari.

“bila shaka SA-7, leo ujaja na vijana wako” anasema Hance kwa sauti tulivu, huku anakwepesha macho yake kumtazama mzee Haule, ambae aliachia kicheko, “kweli wewe ni SA-26, ambae nimesikia habari zako” alisema mzee Haule huku anaendelea kucheka.

“unaitaji nini kwangu?” aliuliza Hance, kwa sauti tulivu ya upole, “ok! ni kweli kuna mambo mawili, naitaji toka kwako” anasema mzee Haule kwa sauti ya chini, na Hance akaitikia kwa kichwa, yani juu chini, kwamaana ya kukubari.

“kwanza kabisa, nazani unafahamu kuwa unatafutwa na TSA, na lengo ni kukuuwa kabisa” anasema mzee Haule, na Hance anaitikia kwa kichwa, kukubariana na mzee Haule.

“sasa kwanini uliamua kuondoka TSA, na kuweka maisha yako hatarini?” aliuliza mzee Haule, kwa saut makini ya upole, kama anaongea na kijana wake, “lakini niliondoka kwa kufwata utaratibu, sijuwi kwanini wananitafuta” alisema Hance, kwa sauti ile ile, tulivu ya upole.

“siunajuwa kuwa TSA awaachi wakara wao nyuma, nivyema kama ukitambua kuwa, SA uwa astaafu, unamambo mengi unayo ya fahamu, umepata mafuzo mengi sana, na mbaya zaidi , wewe unauwezo mkubwa sana, ambao unawatia hofu viongozi” alisema mzee Haule ambae akuishia hapo.

“isitoshe, wewe bado kijana mdogo sana, uoni kama lazima viongozi wapate hofu juu ya usalama wataifa, kwamba unaweza kushawishika na ukatumika vibaya kulihujumu taifa?” anasema mzee Haule kwa sauti ya chini, yenye msisitizo.

“mzee sishani kama vibaya, nilipoamua kushika njia nyangu ya maisha” alisema Hance kwa sauti ile ile tulivu, na kumfanya mzee Haule atabasamu kidogo, “lakini umechagua njia mbaya, na hatari kwa maisha yako” alisema mzee Haule kwa msisitizo.

“hivi mzee, utajisikia vipi endapo Eric atatumika kama mashine ya kuuwa watu, utajisikia vipi kila siku Eric arudi nyumbani amechafuka damu zawatu, awezi kuishi na mke maana ata waweka hatarini, awezi kufikilia watoto, maana watakuwa hatarini, toka kwa maadui wenye visasi, utajisikiaje mzee wanguu?” anauliza Hance, safari hii akimtazama mzee Haule, ambae alitoa macho akishindwa kujibu chochote.

“mzee wangu ongea na TSA, waambie na mimi nataka kuishi kama watu wengine, nataka kuishi kama watoto wao wanavyo ishi, nataka kuishi kama mtoto wako Eric, nitembee huru njiani, nicheze na watu wengine, niwe na mke nipate watoto nao wawe salama, nimechoka kuuwa watu, sitaki tena kumwaga damu zawatu, aijalishi ni watu wa aina gani” alisisitiza Hance, kwasauti iliyomaanisha anacho kiongea.

Mzee Haule anamtazama Eric, aliekuwa amesimama mita kadhaa, toka pale walipo kuwepo wao, kisha anamtazama Hance, kabla ajatazama chini na kushusha pumzi ndefu, “hupo sahihi Hance, nazani ata bwana Kingu, anajuta kukuingiza kwenye ili, ndiyo maana anakupa msaada kadiri awezavyo” alisema mzee Haule, kwasauti iliyopoa.

Kikapita kimya kifupi, nikama mzee Haule alikuwa anatafakari jambo, kisha akamtazama Hance, “kijana, najuwa unakiporo cha kumalizia, baada ya hapo utakuwa tayari kukabiliana na kitachofwata mbele yako” alisema mzee Haule, kwa sauti isyo na utani wala urafiki, kisha akageuka nakundoka kuelekea kule aliko elekea Eric.

“twende zetu nyumbani” alisema mzee Haule mala baada ya kumfia Eric, huku anaelekea uelekeo wa kule waliko tokea, yani nyumbani kwao, “kwahiyo mazoezi ndio yameishia hapa, bola ungeniacha nyumbani nilale, siunajuwa jana nilikunywa ile wine” anasema Eric kwa kulalamika, huku anamfwata baba yake.

“unataa nikimbie mpaka wapi, au unazani mimi ni kijana mwenzio, mimi ni mdingi kama madingi wengine” alisema mzee Haule, ambae sasa akukimbia tena kama mwanzo, ila walikuwa wanatembea kwa mwendo wa kawaida tu.

Hance anawasindikiza kwa macho, mpaka walipo toweka, kisha anatazama ile mizoga ya mbuzi, kabla ajatazama mizoga ya kuku, alafu anaachana na fagio na kuelekea ndani ya banda la udongo, ambako akai sana, anaibuka na sururu na chepeo, kisha anazama kichani, kule kule aliko elekea jana usiku, kwenda kufukia miili ya vijana wawili wa Nyondo.***

Yaaaaaaap!, mji mzima wa Songea ulikuwa umezizima, kwa matukio ya jana usiku, habari kuu ikiwa ni kifo cha kijana Lukas, mdogo wake Tino Nyondo, kila alie ulizakuhusu ratiba ya mazishi, aliambiwa Lukas atozikwa, mpaka apatikane mtu wa kuzikwa nae, ambae ni mtu alie muuwa Lukas, ambae mapaka sasa, hakuna aliekuwa anamfahamu kwa majina.

Kauri ile iliwafikia viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, nao licha ya kujuwa matendo maovu ya bwana Tino Nyondo, lakini waliamua kuacha mpaka asila zake zipungue, kwamaana waliamini kuwa itafikia wakati, bana Tino Nyondo, atapunguza hasira na kumzika mdogo wake, kisha baadae umtafuta adui yake kimya kimya.

Kitu ambacho kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma, yani mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa majeshi yani polisi mageraza na jeshi la ulinzi, ni kwamba, bwana Nyondo, mida hii aliagiza vijana wake wote anao watumia kwenye matendo ya kiarifu, waliokuwa sehemu mbali mbali, waje hapa Songea, kwaajili ya kwenda kuvamia kwenye tobo la Panya, ili kumsaka Panya huyo.

Habari za kifo cha Lukas, kwa wale waliochelewa kuzipata, wengi walizipokea kwa mtazamo tofauti, wakiaminikuwa utulivu utarejea pale mjini Songea, huku wachache wakiingiwa na hofu kubwa, kuwa mji unaingia kwenye vita kubwa, kwamba walio usika na wasio usika wataingia matatizoni.

Polisi wengi leo hii walikuwa wametanda mji mzima, wakizunguka huku na huku, kuangalia usalama waraia wake, japo ni kama walikuwa wanazuga tu, maana kwa fujo na usalama wa mji, wasingeweza kushambuliana na vikundi vya bwana Nyondo, endapo ingetakiwa kufanya hivyo, kwamaana risasi nyingi zingewashambulia raia wema.

Mke wa bwana Nyondo tayari alikuwa amesha ingia mjini Songea, akipokelewa na dada yake, yani yuleanaefanyia kazi kwa Tino Nyondo, aliangua kilio kikubwa sana, akimlahumu mume wake, kwa kushindwa kumlinda shemeji yake Lukas. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata