TOBO LA PANYA (83)

SEHEMU YA THEMANINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI: Dakika chache baadae Hance anamaliza kuongea na simu, kisha anatembea kuelekea usawa wa eneo lenye kitanda, huku anavua tishert yake, Anastansia anaachia tabasamu, huku anamtazama Hance, ambae anaelekea bafuni. ….ENDELEA…..

“na mimi sija oga” anasema Anastansia, huku anajifunua shuka na kubakia kama alivyo zaliwa, kisha anamfwata Hance bafuni, kichwani mwake, akionbea kuwa, kitokee kile ambacho kilitokea jana usiku. ****

Naaaaaaam!, mchana wa siku ya jumamosi, ulipita kwa namna tofauti, kila mtu na kila upande ukiwa umepitisha mchana huo kwa namna yap eke yake, maana wakati Insp Aisha Amary, akiwa anawaza namna ya kumpata tena kijana mpole, ambae anaitaji awe mpenzi wake, na ikiwezekana awe mume wake.

Huku kijana huyu mpole mwenye uso wakinyonge na moyo wa kishujaa, akiwa anacheza na kufurahi na mpenzi wake mpya Anastansia, ndani ya jumba ili lililopo chini ya aridhi.

Japo wote walionekana kuwa katika wakati mzuri, lakini Anastansia ndie alieonekana kufurahi sana, kuliko Hance, ambae pia alionekana tofauti na kawaida yake, sasa alikuwa anafurahi na kucheka muda wote, huku wote wakiwa katika mavazi tata.

Yani Anastansia alikuwa amevaa bukta ya Hance, ambayo licha ya kuwa ndefu pale anapoivaa Hance mwenyewe, ila kwa Anastansia, ilionekana kama kitusi, maana kilipanda juu kidogo, huku kikishika mapaja na makalio manene ya mwanadada huyu.

Yeye Hance, alikuwa amevaa bukta fupi sana, ambayo ilishindwa kuficha vyema maumbile yake ya kiume, asa yanapo simama, kwa yamaa ya kimwili, maana kukaa na Anastansia akiwa hivi bila kupwiruka, icho nikipaji cha pekee sana, ambacho pengine anaweza kuwa nacho mwanaume mwenye tatizo la afya ya uzazi.

Wakati huo huo, bwana Haule yeye, aliutumia mchana huu akijaribu kufanya jambo la kuweza kumaliza swala la SA-26, huku maa gizo toka makao makuu ya TSA, yakisisitiza kijana apatikane, ili mambo mengine ya fwatie.

Bwana Augustino Nyondo, yeye alikuwa pale msibani, anasubiria taarifa ya kupatikana kwa muuwaji wa mdogo wake, huku anasisitiza kuhusu ratiba ya mazishi, kwamba mazishi yatafanyika mala tu, baada ya kupatika muuwaji.

Licha ya kwamba mwanzo baadhi ya watu walizania kuwa, ilikuwa ni kauri iliyotokana na hasira, lakini sasa walianza kuamini maneno ya bwana Tino Nyondo, kwamba amepania kumzika muuwaji pamoja na mdogo wake Lukas.

Sasa makanda wa kuu wa jeshi la polisi, wanaamua kuongeza nguvu kwenye doria, wakiamini kuwa vijana wa Nyondo, wanaweza kufanya fujo kubwa usiku waleo, maana akuwa kwao, kuwa bwana Tino Nyondo, licha ya kumiliki magari zaidi ya hamasini ya mizigo, pamoja na behewa yake, pia alikuwa anamiliki makundi kadhaa ya vijana, anao watumia katika shuughuri kharamu, za unyang’anyi wakutumia silaha, na uwindaji pasipo vibari.

Kwamaana hiyo, sasa bwana Tino Nyondo anenda kutumia watu na silaha zake, kumtafuta kijana huyo, ambae mpaka sasa siyo polisi, wala Tino Nyondo, alie mfahamu kijana huyu ni nani.****

Sasa ni saa nne za usiku, siyo polisi siyo Insp Aisha, wala Nyondo na vijana wake, hakuna alie mwona na kumpata muuwaji wa Lukas, hii ilizidi kumtia hasira bwana Nyondo, huku wengine wakianza kuamini kuwa muuwaji wa Tino Nyondo, aliondoka hapa mjini, na kwenda kujificha mbali, akimuofia Nyondo.

Lakini basi, mida hii ya saa nne, nyumbani kwa bwana Tino Nyondo, watu walikuwa wamejaa, zaidi ya jana, mpaka sasa palikuwa na watu wengi sana, wake kwa waume, vijana kwa wazee.

Lakini wakati huo huo, bwana Tino Nyondo, alikuwa upande wa nyuma ya nyumba yake, mbele ya kundi la wanaume zaidi ya hamsini, walio valia mavazi meusi, wenye silaha mbali mbali za kivita mikononi mwao, huku eneo lote likiwa lime zongwa nba wingu la moshi wa bangi.

“kesho saa saba mchana nataka nimzike Lukas, akiwa pamoja na huyu mshenzi, hivyo sitaki kusikia sababu yoyote ya kumkosa huyo Panya mmoja, mbele ya wanaume hamsini na saba” alisema Nyondo, ambae pembeni yake alikuwa amesimama Kichondo, wote wamevaa mavazi meusi, mze Nyondo akiwa amevaa suit yake nyeusi, ambayo ukimwona nayo ujuwe kunajambo zito.

“leo lazima damu imwagike boss, tunaaidi kumleta huyo Panya mbele yako, na afukiwe mzima kwenye kaburi atakalo zikiwa Lukas” alisema mmoja kati ya wanaume wale, ambae alikuwa mbele kabisa ya kundi lile, akimtazama mzee Nyondo.

Lakini basi, kabla ata kundi alijaanza kuingia kwenye magari, mala akatokea kijana mdogo wa kiume, “baba, baba kunamtu anataka kuongea na wewe, anasema ni muhimu sana, kwaajili ya kumpata mtu unae mtafuta” alisema kijana yule mdogo, ambae kwa ufafanuzi, ni mtoto wa bwana Nyondo. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata