
TOBO LA PANYA (87)

SEHEMU YA THEMANINI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SITA: “nyie wapumbavu acheni kupiga ovyo risas…..” Nyondo akupata nafasi ya kumaliza kile alichokuwa anakiongea, maana ulitokea mlipuko mkubwa ulioenda sambamba na vipande vya mwili wa gari kutupwa hewani, na na baadhi ya vipande vya moto vina shukia kwenye magari mengine, ambayo pia yanaanza kushika moto. ….ENDELEA…..
Vijana wanatawanyika kukimbia moto, ambao ulikuwa umesambaa eneo lile na kwenye magari mengine, tayari wamesitisha mapigo, hakuna aliekumbuka kama kuna adui wa hatari alie kuwa eneo ili.
Naaaaaaam!, huu ndio ulikuwa wakati mgumu, kwa wapiganaji wa Nyondo, maana wakati wanatawanyika ovyo, ili kuukwepa mlipuko, mala ghafla wakasikia milipuko mi nne mfululizo ya risasi, huku watu wanne wakianguka wakiwa tayariwamesha aga dunia.
ile wanashtuka na kutafuta maficho, tayari milipuko mingine miwili, ilisha sikika, na watu wawili wakianguka bila uhai, “shambuliaaaaa” inasikika sauti ya Kichondo, toka kwenye moja ya vungu ya gari.
Hapo sasa, ilisikika milipuko mingi ya mfululizo, iliyopigwa toka upande ule ambao, milipuko ya mwanzo ilitokea, na kufanya hali iwe kama ilivyokuwa kabla ya mlipuko, yani upande wa kulia wa eneo lile la maegesho, huku jamaa wakianza kujitoa kwenye maficho, kwa kuamini adui yao atakuwa amejificha, kutokana nashambulizi lao.
Lakini aikusaidia kitu, wakati mashambulizi aya yaliyo dumu kwa sekunde therasini yakiendelea, risasi zikielekezwa upande wa kulia, ndipo ghafla kasikia milipuko ya risasi, ikitokea pembeni yao.
Wote wanashtuka na kugundua kuwa, wanashambuliwa upande, ile wanageuka kwaajili ya kujibu mashambulizi, tayari mshambuliaji alikuwa karibu yao zaidi, anakuja kwa kasi ya ajabu, na SMG mkononi mwake, iliyokuwa inatema risasi kama mvua.
Alipo wakaribia akaruka kwenye ubavu wagari, akikanyaga kwanguvu, na kuruka juu, akipishana na risasi kazaa toka kwa vijana wa Nyondo, ambao nao wanakutana na risasi za toka juu.
Wakati wao wanaanguka, huku adui yao alikuwa anashuka chini, kwa kasi ya ajabu, usawa wa kijana mmoja wa Nyondo, akitangliza goti, linaloenda kukita usoni mwa jamaa huyo, ambae anatupwa pembeni aklijipamiza kwenye ubavu wa gari.
Anapo jaribu kuinuka anakutana na risasi ya kichwa, wakati wale wengine wanageuka ilikumshambulia, tayari alikuwa amesha toweka, lakini kama waliopangawa, wakapiga risasi oyo upande ule, bila kujari kuwa wenzao wengi walikuwa upande ule.
Hakika risasi zinapenya kwenye mbavu za gari, na kwenda kuwa tandika wenzao waliokuwa wamejificha, “mnatuuwa nyieeeee” zilisikika kelele, zenye kuomba msaada.
Lakini risasi azikukoma, mpaka risasi zilipowaishia wawili awa, na tayari walikuwa wamesha wadondosha wenzao kadhaa, ile wanaangaika kubadiri mikebe ya risasi zao, ghafla wakashangaa kuna mtu anapita toka nyuma yao, na fumba na kufumbua, waliopo jirani, waliona vichwa vina dondoka toka kwenye viwili wili vya jamaa wale, huku mtu alie valia jacket jeusi, na silaha mgongoni, akirukia kwenye gari la karibu, na kuangukia upande wa pili.
“anakuja upande huo” ilisikika sauti ya mmoja kati wale walio mwona, huku wengine wakiongea kwa vitendo, maana waliinua bunduki zao, na kuelekeza kwenye lile gari, wakiamini kuwa risasi zitapenya na kumpata adui yao upande wapili wa gari.
Sijuwi ilikuwaje, lakini mpaka ayo yanaanza kufanyika, tayari kijana Hance au Panya, vile wanavyo mwita SA-26, alikuwa anamalizikia kwenye gari tatu, nakuzunguka upande wa nyuma ya washambuliaji, njiani akiokota SMG, model 81, toka kwa marehemu mmoja, opamoja na mikebe miwili iliyojaa risasi.
Hance anajibanza kidogo na kuutoa mkebe wa risasi kwenye risasi, anautupa chini na kuweka mwingine uliojaa risasi, kisha anakoki na kujiibua toka kwenye maficho kwa taadhari, kicha anaenelekeza silaha yake kwa watu wanao shambulia, anaachia risasi kadhaa akiwalenga maadui zake, milipo kadhaa watu kadhaa wanaanguka, kisha anarudi mafichoni, huku maadui zake wakitawanyika na kujificha.
Kama kawaida ya vita ya sokwe, Hance anachomoka toka mafichoni, na kuanza kukimbia, kuelekea upande wa kushoto wa eneo ili, kwa lengo la kuwazungukia maadui zake.
Lakini basi, ile kijana Hance au SA-26 anaibuka kwenye ubavu wa gari moja lenye contena, anajikuta uso kwa uso na vijana sita wa Nyondo, mmoja wao akiwa na MMG mkononi.
Kama amejikwaa, Hance anajiangusha chini, na kubilingika kuingia kwenye vungu ya gari, lenye kontena, redio ya mawasiliano, ikiwa inaning’inia kwenye ukosi wa jacket lake.
Nyuma yake milipuko ya risasi ikisikika kwa fujo, na kugonga aridhini sentimeta chache toka mle alipokuwa anapita, nae anafanikiwa kutokea upande wapili, na kurukia juu ya kontena, wakati huo vinasikika vishindo vya jamaa wa Nyondo, wakija upande ule.
Hance akiwa juu ya kontena, anaamua kutokea upande wa nyuma wa lile gari, hivyo anakimbia kwa hatua za haraka, mpaka anapofikia ukingo wa kontena, anashika ukingo na kuruka kwenda chini, huku anajigeuza kwa haraka.
Lakini ile anafika chini, tayari kuna watu wengine wanne, walikuwa wamesha msogelea, nao wanainua silaha zao, tayari Hance alisha juwa la kufanya, maana kabla ata risasi ya kwanza aija chomoka, toka kwenye silaha ya mwenye uharaka kuliko wenzie.
Tayari Hance alikuwa amesha ruka, na kudandia body la gari la pembeni, kisha akajitupa kama nyani, kurukia kontena, huku anapishana na risasi ya kwanza, zikifwatia nyingine kadhaa, ambazo zilikoma mala moja kutoka kwenye silaha zao, kwamaana tayari walisha ishiwa risasi.
Wakati huo Hance akiwa hewani mikono ikizama kwenye koti lake, na kuibuka na visu viwili vya kukunja, ile anatuwa chini katikati ya kundi la wale jamaa wanne, tayari wawili kati yao walikuwa wamesha shikilia shingo zao, na kuanguka chini kama viroba, huku damu zina mwagika toka kwenye majelaha makubwa shingoni mwao. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

