SEASON 1: BIKIRA YA BIBI HARUSI (01)

SEHEMU YA KWANZA

Mdau baada ya kimya kidogo, na wakati tunaweka mambo sawa, nimeona nikuletee kisa hiki cha kubuni, kisicho usiana na mtu yoyote wala tukio lolote, kilitokea miaka mingi iliyo pita, mwaka 1997, lakini leo nimeona nikusimulie mdau wangu, maana kwa mala ya kwanza niliposimuliwa, kilinisisimua sana, hivyo siyo mbaya mdau ukafwatilia mpaka mwisho, ili na wewe usome mkasa huu wa kusisimua na kuburudisha,

Ilikuwa juma mosi saa nane mchana nje kidogo ya mji wa songea, pembezoni mwa mtaa wa Luhuwiko, mita chache toka uwanja wa ndege, ndani ya jumba moja kubwa la fahari, lililo zungukwa na naukuta mkubwa sana, kwaajili ya ulinzi wa watu ma mari zilizomo ndani yake, ilisikika sauti kubwa sana ya music, ikipiga nyimbo za hasiri, kama vile ‘kamwali cheketu’, na ule wa ‘tiuka lepa’, ikiashilia kuwa kunashughuli flani au sherehe inaendea mahali pale, maana ukiachilia music huo wa nyimbo za hasiri, ulio mbatana na nderemo na vifijo za watu wachache walioanza kujisogeza eneo hili, pia nyumbani hapa kwa mzee Anderson, ambae ni mmoja wa majiri wakubwa hapa mkoani, palionekana kuwa namaandalizi moto moto, na pilika nyingi sana, na bahadhi ya magari ya kifahari yalionekna yakiingia pale nyumbani, na kushusha watu wenye nyazifa zao walio kuwa wamealikwa, kwenye hafla hiyo, ambayo ilisha fahamika sana hapa mjini, na watu kutamani kushuhudia siku hii ya kuveshwa pete mschana mrembo Monalisa, mtoto wa pekee wa tajiri Anderson, ambae leo hii anatarajiwa kuingia akitokea mkoani Mbeya, alikokuwa ana maliza masomo yake, ya degree ya usimamizi wa fedha, yani uhasibu, akitarajiwa kuwa mchumba wa kijana mtanashati Erasto Richard Misago, ambae pia ni mtoto wa tajiri mkubwa hapa mkoani, na mtoto wa Rafiki mkubwa wa mzee Anderson,

Wakati maandalizi yanaendelea, huku akisubiriwa mschana mrembo, mwenye sifa kibao za kuwa mke wamtu, Monalisa, mala anaonekana kijana mmoja anakuja mbio mbio pale nyumbani, akiwa na kiredio kidogo, na fimbo ndefu mkononi, alionekana wazi ni mtunzaji wa mifugo, alie onyeshakuwa anajambo muhimu sana la kustua, maana alikuja mbio na kupita kwenye geti kubwa la kuingilia kwenye nyumba ile ya kifahari, huku akinusulika kusukumwa na gari lililo kuwa linaingia kwa bwana Anderson, kuleta vinywaji, vitakavyo tumika kwenye sherehe, inayotarajiwa kuanza jioni, mala Monalisa, atakapoingia kutokea Mbeya, “jamani zimeni music! zimeni music!” alipaza sauti kijana huyu, huku akiendelea kukimbilia ndani ya nyumba hii, kubwa yakifahali akipigana vikumbo na watu waliokuwa wameshaanza kulewa, mapema kabla ya bibi harusi mtarajiwa kuingia nyumbani akitokea Mbeya, wapo walio msikia lakini hwakumjari, na wapo walio msikia na kumjari, “jamani zimeni mziki! wekeni upande wa redio” alizidi kupaza sauti yule kijana, ambae siyo mgeni kwa wenyeji wapale kwa bwana Anderson, ni mtunzaji wa mifungo ya mzee huyu tajiri, anaitwa Side, wengi wanapenda kumwita Zakayo, kutokana na ufupi wake, bwana Anderson ambae alikuwa amekaa na bahadhi ya wageni wake wakiendelea na vinywaji ni mmoja kati ya watu waliostushwa na ujio wa Zakayo, akainuka haraka, toka kwenye kochi, akamfwata Side Zakayo, alie onekana kupagawishwa na jambo flani, akiwaacha wageni wake wakimtazama kijana yule kwa mshangao, “wewe ebu tulia kwanza, unatatizo gani?” bwana Anderson, alimdaka mfanya kazi wake huyu, mwenye kiredio mkoni ambacho japo kilikuwa kinaonge, lakini akikusikika vizuri, kutokana na sauti kubwa ya mziki, na wakati huo huo mle ndani kwa bwana Anderson, simu ya mezani ya kampuni ya simu ya serikali, ikaanza kuita, aikuwa hajabu sana maana toka asubuhi yaleo, simu zilikuwa zinapigwa sana, kwaajili ya taflija hii ya binti yake, “mzee sikia! sikia! wana mtangaza dada Mona” alisema Zakayo kwa sauti iliyo tawaliwa na na pumzi nzito, zilizotokana na mbio alizokimbia toka mashambani anakotunzia mifugo, huku akijaribu kuisogeza redio sikioni kwa boss wake, bwana Anderson, kumsikilizisha taharif ambayo Zakayo aliiona kuwa ya kustusha, baada ya kusikiliza kidogo kilicho kuwa kina ongelewa kwenye redio, baba Monalisa alionekana kustuka kidogo, na kusogeza zaidi sikio lake kwenye redio, “polisi wanaendelea kumsaka mtekaji huyo anae fahamika kwa jina la Edgar Eric mbogo, alie mteka mschana Monalisa Anderson, na yeyote mwenye tahalifa za kulisaidia jeshi la polisi, pige simu namba ……..” mpaka hapo mzee Anderson akuwai kumalizia kusikiliza taarifa hiyo, alijihisi kizungu zungu, na miguu ikikosa nguvu, akawai na kwenda na kijikalisha kwenye kochi ambalo lipo karibu na ile simu ya mezani, huku wageni wake wakimtazama kwa mshangao, wakijiuliza ni taharifa gani imepatikana kwenye redio, “baba Mona usikii simu kama inaita?” alisema mke wa mzee Anderson, aliekuwa anatokea upande wajikoni, huku ana ifwata simu na kuipokea, pasipo kujuwa kilicho msibu mume wake, “hallo mama Mona hapa naongea, nani mwenzangu?” alisema mke wa bwana Anderson, malatu baada ya kuweka mkonga wa simu sikioni, kisha akatulia kusikiliza upnde wapili, “ndio baba yangu, kwani kuna tatizo lolote huko polisi?” alisikika akiuliza mama Monaisa, yani mke wa bwana Anderson, huku watu waliokuwepo pale sebuleni waki mtazama kwa tahadhari, wakiofia kumkuta kilicho mkuta mume wake, ambapo mama huyu, akusikika akiongea tena, zaidi ya kuonekana akibadirika sura kila dakika, akionekana kuwa anapokea taharifa ya kustua, na mwisho akaishia kuangua kilio kikubwa, kilicho mstua kila mmoja mle ndani, na muziki ukazimwa mala moja.

Ilikuwa ni tahalifa toka kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ruvuma, SSP Kamanda Kingarame, ni tahalifa mbaya, yakuwajulisha kuwa, binti yao wapekee Monalisa, ametekwa nyala na mtu alie fahamika kwa jina la Edgar Mbogo, janausiku huko Makambako, Edgar nikijana wanae mfahamu, kijana alie onyesha dalili mbaya toka zamani, kipindi anasoma na binti yao darasa la sita, kijana ambae alisabaisha wahame toka mtaa wa mahenge, na kuamia huku Luhuwiko, miaka kama kumi iliyo pita, “akika kijana huyu safari hii, atajuta kkuni fahamu” alisema mzee Anderson, kwa sauti iliyo jawa na hasira kali sana, mchanganyiko wa chuki na ghadhab, huku akijiinua toka kwenye kochi na kuufwata funguo ya gari lake Toyota crester, safari ya kuelekea mjini, kwa lengo la kuonana na mkuu wapolisi mkoa.

Taalifa hiyo ilizagaa kwa kasi ya hajabu, mji mzima wa Songea, kuwa yule binti mrembo mtoto wa tajiri Anderson ametekwa nyala, ikionganishwa na matukio ya uarifu yaliyo jitokeza siku mbili zilizopita, walionekana watu wakiwa ekaa kwa vikundi wakijadiri tukio hili ambalo kwa kifupi lili wastu a watu wengi sana, kwa waliokuwa wana mfahamu Monalisa waliuzunika zaidi, maana binti huyu, ukiachilia uzuri na upole wake, ulio ambatana na tabia njema, pia walio mjuwa undani walifahamu kuwa akuwai kuwa na mwanaume yeyote katika mausihano, na walijuwa kuwa kutkana na uzuri wake wa sura na mwili, mtekaji asinge mwacha salama,

Naam! kati ya watu walio changanyikiwa na tahalifa hiyo, ni kijana Erasto Richard Misago, mchumba mtarajiwa wa Monalisa, pamoja na familia yake, yani mama yake na baba yake Richard Misago, maana ukiachilia anamfahamu mtekaji kuwa ni kijana Edgar Mbogo, kama ilivyo tangazwa, na ukiachilia kujuwa kuwa Edgar alisha wai kumfukuzia Monalisa na yeye kumzidi kete, sasa leo amemteka nayala, na akiwa bado bikira, Erasto alijuwa kuwa mchumba wake mtarajiwa yupo hatarini kupoteza bikira yake, na yeye kuto timiza ndoto zake za toka utotoni.

Ukiachilia familia ya bwana Misago, pia tahalifa hizo, ziliwafikia wazazi wa Edgar, yaan kamanda mstaafu wa jeshi la ulinzi, na mke wake, wakiwa mitaa ya stendi kuu ya mkoa, wakimsubiri kijanawao huyo, ambae alikuwa anakuja songea, akitokea Mbeya, aliko kuwa amemaliza masomo yake ya bishara na usimamizi wa fedha, kilicho wachanganya baba na mama Edgar, ni kitendo cha kijana wao kujiusisha na utekaji wa binti Monalisa, kwakitu ambacho wao walihisi moja kwa moja ni shinikizo la kimapenzi, waliwaza hivyo kama walivyo waza wazazi wa Monalisa na kijana Erasto, ni kutokana na matukio ya miaka yanyuma, yaliyo sababisha mzee Anderson ahame mtaa, akiambatana na rafiki yake bwana Misago. “mh! baba Edgar, mbona moyo wangu unakataa kuwa Edgar amefanya tukio hilo” alisema mama Edgar akimtazama mume wake alie kuwa amekaa mbele ya usukani, wa gari lao land rover mia moja na tisa,

ukiachilia watu walio stushwa na tukio hili, Ila kuna mtu mmoja, tukio hili alilichukulia kama kituko cha kuchekesha, huyu anaitwa Joseph Kisona, mkuu wakitengo cha upelelezi wa siri, katika jeshi la ulinzi, ambae alipandishwa cheo mwaka mmoja uliopita baada ya kuonyesha juhudi katika kazi, (soma KIFO MKONONI, UTANI WABIBI), nakupewa cheo cha Kanali, “koplo Katembo umeisikia hiyo?” aliuliza Kisona, aliekuwa ana tabasamu, huku akimtazama askari mwenye cheo cha koplo, aliekuwa pembeni yake mle ndani ya ofisi, “nimeamini maneno yako afande” alijibu Koplo Katembo, “kwahiyo atuna namna zaidi ya kuingia kazini moja kwamoja” alisema Joseph Kisona, huku anainuka na kutoka ofisini kwake akielekea kwenye ofisi ya mkbwa wake, brigedia General, Francis Haule. maana kuna matukio yalimchanganya bwana kisona, ambae aliamua kulivalia njuga swala hili, ****

Ebu tuanze, Sikutatu zilizo pita, nje ya mji wa songea, katika kitongoji cha Luhuwiko, pembezoni mwa barabara kuu iendayo magharibi mwa mkoa huo, yani wilaya ya Mbinga na Nyasa, bila kusahau mji mdogo wa Pelamiho, ilikuwa siku ya alkhamis, saa sita usiku, ni usiku ulio ambatana na giza nene pasipo mwezi wala nyota, baridi lilikuwa linapuliza kisawa sawa, nazani wakazi wa nyanda zajuu na kusini mwatanzania, wana ijuwa baridi ya ukanda huo, kuanzia mwezi huu watano, usiku huu akukuonekana magari wala pikipiki, ikikatiza katika bara bara hiyo, zaidi ilisikika minyongo ya pedor (peda) za baiskeli, zikilalamika, kwa kulazimishwa kunyongwa kwa nguvu, ilimpanda baiskeli hiyo afanikiwe kumaliza kilima kilicho mkabiri, akiwa ame beba mkoba wake mkubwa mngongoni, huku kifuani kwake ame ning’iniza camera kubwa, mpandaji wa baiskeli hiyo alijitaiadi kunyonga pendor za baiskeli, ambazo zilimchemsha na kumfanya asisikie baridi, ambayo wengi iliwasababishia mida hii wawe wamejifungia ndani, maana ata sehemu za starehe nyingi za mji huu, uwa ni zandani, tena ni kipindi ambacho watu wengi uwa wana tumia kutengeneza watoto, maana kipindi hiki, wanandoa walio gombana uwa wanamaliza tofauti zao automatical, yani taka usitake uta mkumbatia mwenzio muda wakulala, lakini kijana huyu alionekana akiwa njiani, anaelekea mjini,

Huyu alikuwa ni kijana Lukas Benjamin, wengi wana mwita mpiga picha, alijitaidi kupiga pedor akiendelea kuupunguza mlima huu, akikatiza kwenye pori kubwa, lilitenganisha Luhuko kitongoji na eneo la serikali, kwa umbali wa kilomita kama tano hivi, sasa kijana Lukas Benjamini, alionekana kuwa ana zidiwa na kilima hicho, maana alipofikia katikati ya kilima hicho, akaanza kupunguza speed ya kukanyaka pedor, na mwisho akashuka kabisa kwenye baiskeli, na kuanza kuikokota, akikatiza kwenye msitu huu ambao, ulikuwa umepakana na majengo makubwa sana ya ifadhi (Bohari) ya serikali, ikiwepo maghara ya vyakula ya mkoa, NMC, national milling cooperation, na pia kulikuwa na jengo kubwa na imara linalotumika kama benk ya adhina, bank ambayo utumika kwa kuifandi lasilimari vitu, na fedha, yani mfano wake ni kwamba, mtu angeweza kuifadhi, vitu vyote vya thamani ambavyo, ni hatari kuifadhi nyumbani, kwa kuofia kuvamiwa, na majambazi, Benk hiyo ulindwa na polisi watano, walio makini sana, wakati mwingine ata wananchi wanao katiza eneo hili usiku, ata kijana Lukas alijijutia sana kuchelewa kukatiza eneo hili usiku huu, japo ilimlazimu kwenda Luhuwiko, alikokuwa ameitwa na familia ya bwana Anderson, ambae alimweleza kuwa, ata mwitaji jumamosi saa mbili usiku, ambapo kutakuwa na taflija ya binti yake wapekee, Monalisa Anderson, ya kuvalishwa pete na mchumba wake, Erasto Richard, binti huyo alikuwa anatarajiwa kuingia songea siku ya jumamosi mchana, akitokea Mbeya jumamosi, alikokuwa anasoma chuo cha usimamizi wa fedha, yani siku mbili mbele toka leo, baada kumaliza degree yake ya uhasibu, ambapo siku yatatu jumamosi, angeingia nyumbani mida ya saa nane mchana na kukuta maandalizi yamesha kamilika, tayari kuvalishwa pete, hivyo wazazi wake, waliamua kumkodi Lukas kuchukuwa picha za kawaida na za video, za tukio hili ambalo uwa lakipekee sana kwa watu wengi, maana ni kumbu kumbu muhimu katika maisha.

Ilikuwa bahati kubwa sana kwa bwana Lukas, kwenda kufanya kazi kwenye sherehe ya watoto wa matajiri wawili, wakubwa mkoani ruvuma, tena sherehe hii (part) ya kuvalishwa pete binti Monalisa, ilitarajiwa kuwa kubwa sana, japo sheehe kama hizi za uchumba zilikuwa adimu sana kwa kipindi hicho, zaidi ungesikia harusi, aua kipaimara, na pengine ubatizo kwa watu wenye uwezo, ua sherehe za majamanda, wwenyewe wanaita chama kiuyaye, lakini matajiri awa wawili marafiki, waliamua kufanya hivyo kutokana na fedha walizo kuwa nazo, na pia kutokana na kuwa watoto wao ndio wapekee katika familia zao, Lukasi alifuahia sana sababu ingesaidia, kupata wateja wengi sana, maana angekuwa amejiongezea umaharufu, na siyo kwamba kijana huyu alikuwa ana fahamika kwa matajiri hawa, ila leo jioni alisikia habari ya kuitwa na mzee Anderson, ata yeye alishangaa, maana ukiachilia umaarufu wa wazee awa bwana Anderson na bwana Richard, pia binti yao Monalisa, alikuwa maalufu sana hapa songea mjini, umaarufu ambao alianza kuupata toka alikuwa mdogo, anasoma chekechea, shule ya msingi sekondari O lever, mpaka A lever, kutokana na umakini wake na juhudi zake ki taharuma, ukiachilia tahaluma, pia binti huyu Monalisa alijulikana kwa uzuri wake, uzuri ambao ume wafanya wazazi wake watumie ghalama nyingi sana kumlinda mtoto wao, asishawishike kuingia katika mausiano ya kimapenzi, maana toka akiwa mdogo, kuna baadhi ya rafiki na majirani, walidiliki kutania kuwa “lazima atakuwa mkwe wangu” wengine “dah!, huyu mtoto atasumbua sana watu”

Ebu tuyahache hayo mdau, tumtazame kijana Lukas, ambae alitembae huku akisikiliza sauti za madege ya ajabu toka kwenye pori la msitu huu wa Luhuwiko, ambao alitumia kama dakika ishilini, kuumaliza mlima na msitu, na sasa alikuwa amesha yakaribia majengo ya hifadhi ya mari za wanachi na serikali, japo akuwa ametokea wenye mwanga yani usawa wa majengo yale, lakini alweza kuwaona askari polisi watatu waliokuwa wana linda eneo lile wakiwa na bundukizao aina ya SMG, yaani sub machne gun, mikonini mwao, akuwa na sababu ya kijiuliza wengine wapo wapi, sababu yeye alikuwa anendelea na safari yake, lakini wakati ana jiandaa kupanda baiskeli yake, ghafla akasikia “we! kijana, ebu simama” ilikuwa nisauti kavu ya kikamnda iliyo tokea karibu yake, yani pembeni ya jengo moja lilipo karibu yeke, kwenye kiambaza chenye giza nene, na yeye akasitisha zoezi la upandaji wa baiskeli, na kusimama hapo hapo, Lukas akiwa anatetemeka kwa uoga, japo akuwa anakosa lolote, huku anatazama upande ambao sauti ilitokea, akamwona askari ana kuja usawa wake, huku akiwa na bunduki kama wenzake, “mambo vipi dogo” alisalimia yule askari, kwa sauti ya kawaida, yani isiyo ya ukorofi wala uogomvi, akiwa atua chahe toka alipo simama Lukas, “safi braza” aliitikia kwa heshima bwana Lukas, japo kwa mtazamo huyu kijana alie mwita dogo, kimtazamo ni kama mdogo wake watatu, “unatoka wapi usiku huu?” aliuliza yule askari huku akimsogelea na kumtazama kwa umakini,

Lukas akamwelezea vizuri yule askari, kule alikotokea kwa bwana Anderson, na zumuni la kwenda kwa tajiri huyo, ambae anafahamika sana pale mkoani, ata yule askari alimwelewa mala moja, “ok! kumbe wewe ni mpiga picha, dah! afadhari, alisema yule polisi, huku ana ikagua kwa kuitazama ile camela ya bwana Lukas, iliyokuwa ina ning’inia shingoni mwake, “kuna picha za pasort naitaji unipige na nguo za kiraia, sijuwi nita kuate” aliuliza yule askari akionyesha kupata ufumbuzi wa tatizo lake, “we niambie tu, lini na mimi nikufwate wapi, kasoro jumamosi tu! nita kuwa kwa mzee Anderson” alisema Lukas, na yule askari akaonekana kutulia kidogo, akama kuna kitu anawaza, lakini kabla hajajibu, mala wakaliona gari moja likija kwa speed na kukata kona kuingia pale NMC, na sasa waliweza kuiona vizuri gari lile la polisi, aina ya Landa rover, one ten, lililo beba askari saba nyuma yake, lilisimama mbele ya jengo la hadhina na wale askari saba wa polisi, wakashuka haraka toka kwenye gari, hapo wale akari watatu wakajikusanya pamoja, karibu na lile gari, ambalo lilisha simama pasipo milango ya mbele kufunguliwa, hivyo akushuka mtu, zaidi ya wale askari walio kuwa nyuma yagari, “mbona mapema sana” aliongea yule askari aliekuwa na Lukas, kwa sauti ya mshangao, kisha akamtazama Lukas, “ebu nisubiri kwanza, naona afisa wa zamu amekuja kutembelea kituo” alisema yule askari kisha akaanza kutembea kuelekea kule walikokuwa wenzake, na hapo hapo Lukas akamwona askari mmoja mwingine akitokea nyuma ya jengo la uhifadhi wa hadhina, sekunde kumi na tano zilitosha, kwa wao kujikusanya mbele ya jengo lile la hadhina,

Lukasi akiwa mtulivu pasipo wasi wasi wowote, akaendelea kusimama pale pembeni ya bara bara, huku ana tazama kule walipo wale askari, ambao sasa walikuwa wamesha simama vyema kwa mstali mmoja, nikama walikuwa wanapewa amri na askari mwenzo mmoja, yani kati ya wale waliokuja na hili gari, nao wakaonekana kufwata amri iliyo kuwa inatolewa, akiwa ajuwi ili wala lile, bwana LUKAS, aliwaona wale askari walio shuka kwenye gari wakiwa nyooshea bunduki wenzao, hapo Japo Lukas akuwa anajuwa mambo ya kijeshi, lakini alianza kuhisi kuwa kulikuwa na tatizo, ni kweli aka shangaa kuona wale askari waliokuwa wamejipanga mstari wakikoki silaha zao na kuwaelekezea wale walio kuja na gari, ukweli ilikuwa kama tukio flani la kuigiza hivi, maana Lukas akuwai kushuhudia masiahara kama haya, nikweli nikama masihara, maana baada ya wale askari walio kuja na gari, kuonyeshewa bunduki na wenzao, lakini wao walicheka kwa dharau, huku wakisema maneno ambayo yeye Lukas kuyasiki, hapo Rukas akaona sehemu hii siyo ya kukaa kibwege, maana kama kweli ule ulikuwa ni ugovi wa kweli kweli, basi ata yeye akionekana lazima ange uwawa, aka sogeza baskel yake pale kwenye ukuta wenye giza, wa jengo ambalo alimkuta yule askari, ambae sasa yeye na wenza ke walionekana wakitoa vimikebe vya risasi toka kwenye bunduki zao na kutazama risasi zao, ambapo wanaonekana kushangaa sana, inaonyesha wale askari walinzi, walitegeshewa risasi za bandia, pasipo wao kujuwa, Lukas baada ya kuegesha baiskeli yake, akataka kuondoka eneo lile na kujificha kwenye kichaka, kilicho jiunga na msitu, lakini aka kumbuka jambo moja, nalo ni kutazama tukio lile, kama kuta kuwa na laziada, achukue picha ambazo zinge msaidia kuuza kwenye vyombo vya habari, ambavyo vinge mlipa ela nyingi sana, na kujipatia umaarufu miongoni mwa wapiga picha,

Lukas aka ivua camela yake shingoni na kuiweka, kwenye begi, kisha akata video camera tayari kwa kazi, aka zunguka upande wapili wa jengo, ambako aliamini kuwa anaweza kupata video nzuri, nikweli sasa aliweza kuwaona wale askari wa tano wakiwaamrishwa wapige magoti, nao wakaanza kutii amri ile, wkati huo Lukas alikuwa tayari ame iwasha camera yake, na kuanza kuchukua tukio lile, maana yake ata matukio yale sasa, alikuwa ana yatazamia kwenye camera ya video, wakati anaendelea kutazama tukio lile ambalo lilizidi kumtia mashaka kila sekunde iliyopita, mala akamwona yule askari aliekuwa ana ongea nae muda mfupi uliopita, kijaribu kuchomoka mbio toka pale chini alipokuwa napiga magoti, lakini bahati aikuwa upande wake, maana ililindima milio ya risasi tatu za SMG, na yule askari alirushwa na kutupwa mbele kule aliko kuwa na akimbilia, hapo Lukas akajuwa kuwa swala hili halikuwa na chembe ya mambo ya kijeshi, wala utani, ila huu ni uvamizi wa watu ambao wamejifanya kuvaa mavazi ya polisi, yani hivyo ndivyo alivyo amini Lukasa, hivyo akaona kuwa ule mkanda anao record ni chanzo kizuri cha kuwakamata majambazi hawa, Lukas aliendelea kuchukuwa tukio pasipo kujuwa kuwa anajiingiza kwenye matatizo, na ukichukulia mahali hapa palikuwa mbali na makazi ya wananchi, itaendelea 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata