BIKIRA YA BIBI HARUSI (09)

SEHEMU YA TISA
 .
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE : “hivi Stella, unaonaje tukilala Makambako tumpe kampani Monalisa, maana peke yake hapa ugenini anaweza kupata matatizo” alisema Denis huku akimtazama Stella, pia kwa ujanja waka sikilizia Monalisa atauchukuliaje ule ushauri, Stella aka inua uso wake kumtazama Monalisa, macho yao yaka gongana, Monalisa akatabasamu, akionyesha kuwa wazo la Denis, lita kuwa zuri sana, kwani katika vitu vilivyo mchanganya hakiri, ni kulala makambako peke yake. ENDELEA……….
Kwa tabasamu lile Stella akajuwa kuwa Monalisa amesha kubaliana na wazo la Denis, “ok! itakuwa vizuri, lakini itakuwaje kuhusu hawa rafiki zako, au kesho tuta panda bus?” aliuliza Stella, pasipo kujuwa kuwa ule mpango ni wa wale rafiki zao, “kwa hilo wala usiwe na na wasi wasi, tutakuwa pamoja ili tuwape campan” alidakia yule kijana alie kaa seat ya mbele karibu na dereva, huku ana jichekesha chekesha,
dakika ishirini baadae vijana hawa watano, waliingia mjini Makambako, kisha mojakwa moja waka elekea Panama Hotel, hotel moja tulivu ya hadhi ya juu sana hapa Makambako, wakaulizia vyumba na kukuta vyumba hakuna maana vyote vilikuwa vimewekewa oda, waka zunguka kwenye bar hotel mbiuli tatu mambo yaka wa vile vile, hii ilitokana na wanafunzi wengi, pamoja na watu waliokuwa wanasubiria usafiri wa trein kuchukuwa vyumba, mala wakaelekezwa kwenye hitel moja ya hadhi ya chini, lakini hotel hiyo pia mpaka muda ule ilibakiwa na vyumba viwli tu!, vyenye vitanda vidogo, hawwa kuvipenda, wakaelekezwa kwenye guest moja, iliyo ambata na bar pembeni kidogo ya mji, pembezoni mwa barabara iendayo Mbeya, hapo walikuta kuna vyumba kama vinne vilivyo bakia, wao wakachukuwa vyumba vitatu tena vyenye vitanda vikubwa na vizuri,
Wale vijana wawili wakiwa wame chukuwa cumba kimoja, namba tisa, kilicho tazamana na chumba na kumi na nane, alicho chukuwa Monalisa, Denis na Stella walichukuwa chumba namba tatu, wakikiacha chumba namba kumi na saba, ambacho ni kimoja ya chumba ambavyo avikuwa na wateja mpaka muda ule,
Monalisa baada ya kuweka mabegi yake chumbani, akapata wazo la kwenda kupiga simu nyumbani kwao, awajulishe kuwa amesha anza safari, na saa yupo Makambako, alichukuwa kile kibegi chake kidogo cha mgongoni, na kutokanacho nje ya chumba chake, alafu akaelekea kwenye mlango wa chumba namba tatu, akiitaji msaada wa kusindikizwa na Stella wakatafute sehemu ya kupigia simu, kwa malipo, Monalisa alitembea kwenye korido la guest house hii, huku akitazama namba, zilizo andikwa kwenye milango, mpaka alipo ifikia namba tatu, aka simama na kutaka kupiga hodi, “we unaharaka gani bwana wakati tuna lala wote mpaka asubuhi?” ilikuwa sauti ya Stella toka ndani ya chumba, baadae ni baadae bwana, ebu tufanye mala moja alafu tukaoge” Mona lisa aliweza kumsikia Denis akiongea kwa sauti ya kubembeleza, hapo akajuwa kuwa nini kina taka kufanyike mle chumbani, lakini akatulia kusubiri jibu atakalo litoa Stella, “na wewe uking’ang’ania kitu, haya basi tufanye haraka” hilo ndilo jibu la Stella lililo ambatana na michakacho ya uvuawaji wanguo, na mikwa luzo ya zip, Monalisa akahisi mwili ukimsisimka, maana nikama aliona kinachofanyika mle ndani.
Taratibu Monalisa akatoka eneo lile na kuelekea upande wa bar, ambako ndiko kuna mlango alio ingilia wakati ana kuja mahali hapa, pale bar kulikuwa na watu wengi sana, wakiendelea kupata vyakula na vinywaji, na kama ilivyo kawaida walevi nao wakaanza kumtazama kwa macho ya tamaha, huku wengine wakimfanyia masihara ya kumwita, lakini yeye akaongeza mwendo ili akatize mahali pale haraka, nikweli alifanikiwa, alikatiza mahali pale na kutokea nje kabisa ya bar, ambako sasa rangi ya dunia ilisha anza kubadirika, na kuwa nyeusi, maana juwa lilisha anza kuzama,
Akiwa hajuwi aelekee wapi, Monalisa alisimama na kutazama kushoto na kulia, akaliona duka moja la kawaida upande wa kulia, yani upande wakwenda kati kati ya mji wa makambako, akalifwata lile duka ambalo alimkuta kijana mmoja, ndie muuzaji, baada ya kunmsalimia aka mwulizia sehemu ambayo anaweza kupiga simu, “ni kule karibu na stendi, kuna sehemu wanaita muungano, wanapiga simu kwa hela” alielekeza yule kijana na hapo hapo Monalisa akaanza kufwata ulekeo wa stendi, wakati huo huo sijuwi nini kilimtuma ageuke nyuma, maana ile anageuka tu!, akaliona gari moja jeusi aina ya mercedis benzi toka Mbeya, likisimama kwenye ile bar aliyo toka yeye, lakini hakulijari akatazama mbele na kuendelea na safari yake, **
Baada ya lile gari dogo kusimama na Edgar kushuka huku aipewa mizigo yake, akawashukuru sana wazazi wa Salma, na Salma mwenyewe, kwa msaada waliompatia, kisha nao wakaagana na kuondoka zao, kisha Edgar aka beba mizigo yake na kuingia kwenye ile bar yenye Guest house, ambayo aliiona tokea akiwa kwenye gari, na kuomba shushwe hapo iliapate sehemu ya kulala mpaka keshon atapo chukuwa usafiri wa kuelekea Songea,
Edgar alipitia mlango wa mdogo wa uwani na kuingia ndani ya jengo hili la hotel, kisha akaelekea mapokezi, ambako aliomba kupatiwa chumba cha kulala, akapewa chumba namba kumi na saba, kijana huyu aliingia ndani ya chumba chake alicho kodisha, na kujilaza kitandani, huku hadithi yake na Monalisa iki anza kujifuta kichwani mwake, ***
Mtutuma baada ya kumshusha Lukas, na kuanza safari yake, akufika mbali akajikuta akisimamishwa na polisi, wenye bunduki mikononi, zilizo elekezwa kwenye gari lake, hapo mtutuma aliingiiwa na uoga mkubwa sana, na kujikuta akitetemeka kwa uoga alionao, maana hakuwai kuonyeshewa bunduki kama hivyo, aka simamisha gari pembeni ya bara bara, huku akijiuliza maswali mengi sana, akawaona polisi walioshika bunduki wakianza kulisogelea gari lake, huku wamelielekezea mitutu ya bunduki, “hallow charl oscal detal tume lipata gari aina ya Dutsun lililo tajwa” mtutu ma alimwona polisi mmoja akiongea naredio ya mkononi, yani redio call, “vipi mtuhumiwa yupo ndani ya gari, roja?” ilihoji sauti toka kwenye redio, “Charle, mpaka sasa naona kuna mtu mmoja ambae ni dereva, na sijajuwa kama ndie mtuhumiwa, majibu zaidi utayapata baadae over” baada ya kuongea hivyo yule polisi, akalisogelea gari na kufungua mlango, huku polisi wengine wakiendelea kulinyeshea mitutu lile gari la mtutuma,
Mtutuma aliwaona polisi wakifungua milango yagari na kumwamlisha atoke nje, nae akatoka nje yagari, akaambiwa apige magoti na kuweka mikono kichwani, akafanya hivyo bila ubishi, japo alikuwa anatetemeka sana, na kujiuliza maswali mengi kichwani mwake, Mtutuma akawaona polisi wakilikagua lile gari, “afande hakuna mtu mwingine ndani yagari” polisi mmoja alimwambia yule polisi alie shika redio call, ambae baada ya kupewa jibu lile, aka mgeukia mtutuma “hallow ebu taja majina yako” alisema yule askari kwa rafuzi ya kikulya, “naitwa Said mtutuma said” alijitambulisha bwana Mtutuma, “unauakika kuwa jina ulilotaja ni lakwako?” aliuliza yule askari polisi huku akimkazia macho ya hasira bwana Mtutuma, “ndio hilo ndilo jina langu, na ninafahamika kwa watu wengi sana, sababu ni fundi wa magari” alijibu mtutuma, akihisi kuwa yeye siyo mlengwa wa ile road bloack, “ok! umetokea Songea siyo…” kabla ajamaliza swali lake, wakaliona gari aina ya land rover 110, la jeshi la polisi, lililo sheheni polisi sita nyuma yake na wawli mbele, likija kwa speed kali sana na kusimama kwa bleack kali baada ya kuwafikia, na wale polisi wa nyuma ya gari wakiruka haraka toka kwenye gari, ata kabla gari halija simama vizuri, na kuwai pale walipokuwepo polisi wwengine, wakifwatiwa na Sajent Kibabu, ambae alishuka na bunduki yake mkononi, kama wale wengine, “yupo wapi Lukas Benjamin?” aliuliza Sajent Idd Kibabu, akimtazama yule polisi alie shikilia redio call, “afande ndio tumelikamata sasa hivi hili gari, na tume mkuta huyu bwana Mtutuma Said peke yake, na tulikuwa tuna endelea mkuhoji” alisema yule polisi.
Hapo Ghafla sajent Kibabu aka inua bunduki yake aina ya SMG, akigeuza kwenye kitako, na kutwanga nayo mgongoni, “sema huyo jambazi mwenzio umemwacha wapi we mshenzi” Mtutuma alihisimaumiivu kamali mgongoni, na ndipo alipojuwa kuwa ane tafutwa ni yule jamaa alie mshusha hapo nyuma kidogo, na ukweli hakuwa na haja ya kuficha, maana akijifanya mbishi ata umia bule bule, akaeleza kila kitu, mpaka mpango wa Lukas, kutafuta nyumba ya kulala wageni, ili kesho aelekee dar, Mtutuma alikili kuwa alimbeba mtu huyu pasipo kujuwa kuwa ni mwalifu, baada ya hapo yule askari aka toa report kwa OCD , ambae aliagiza mtutuma apelekwe kituoni, akaandikishwe maelezo.
Sajent Kibabu aka toa picha ya Lukas na kuwaonyesha wale polisi, akiwaelekeza kuwa amevalia jinsi la blue na tisht jekundu, asakwe mala moja huku polisi wengine asa wale wenyeji, waka zuwie magari yanayoelekea dar es salaam, baada ya hapo Kibabu na askari wake, walisongea kwenye chocho moja, kisha akaanza kuwapa mkakati mpya wakazi, “mpaka hapa Lukas anaonekana kuwa mjanja zaidi yetu, hivyo atuwezi kumpata tukiwa na uniform (yani sale za polisi) hivyo vaeni nguo za kiraia”
walitumia dakika tano kubadiri nguo, na kuvaa nguo za kiraia, kisha wakaziweka bunduki zao kwenye gari, yani sub machine gun, na kupewa pisto zenye viwamba sauti, “kumbukeni kuwa, hakuna kuacha ushaidi nyuma, lengo ni moja tu, kuuwa na kuchukuwa video tape” alisistiza sajent Kibabu, kisha aka watawanyisha askari wake kwa makuundi ya wawili wawili huku, yeye mwenyewe akibakia kwenye gari na dereva wake, wakizunguka mji mzima,**
Joseph Kisona alipokelewa na watoto ake wawili, yani mapacha, wakike na wakiume, aliowakuta wanacheza mbele ya nyumba yake, na wakati huo huo akajitokeza mwana dada mrembo sana, chotara wa kiaharabu, “hivi wewe kwanini unapenda kuniweka roho juu?” alisema doctor Elizabeth huku akiachia tabasamu mwanana, “hahahaha, punguza wasi wasi, siunajuwa siwezi kutafuta mwanamke mwingine” alisema Joseph Kisona huku anatabasamu, “nitajuwaje wakati unakuwa peke yako?” alisema kwa utani doctor Elizabeth, huku akimsogelea mume wake alie wanyanyua watoto wake wote wawili, wale wenye watoto mapacha, au walio zaa dabo dabo wanapata picha aliwabebaje, kisha aka mtandika busu la shavuni, wawili hawa kila siku nikama penzi lao lilianza upya, kwa jinsi lilivyo shamili, “ata kama nakuwa pekeyangu, lakini funguo ya chupi si umebakinayo” alisema Joseph na hapo mke wake akaachia kicheko cha mwaka, mala wakasikia simu ina ita toka ndani, doctor Elizabeth aka kimbilia ndani, akifwatiwa na mume wake, aliekuja taratibu, “hallow nyumbani kwa Mr Kisona hapa mke wake dr Elizabeth naongea” alijitambulisha doctor Elizabeth, lakini akaoneka kustuka kidogo, huku anamtazama mumewake alie kuwa ameingia na kusimama kati kati ya sebule, “ok! ok! ebu subiri uongee nae” alisema doctor Elizabeth, akimtazama mumewake, ambae aliwashisha watoto haraka na kusogelea, ilipo kuwa simu, “ata simuelewi anaongea haraka haraka sana” alisema Elizabeth huku akimpatia mume wake mkono wa simu, “hallow Kisona hapa na….” kabla ata ajamaliza kujitambulisha bwana kisona, akasikia upande wapili ukidakia, “mzee mimi naitwa Lukas,” ilikuwa sauti ya chini kidogo, kama ya kunong’ona, iliyo tawaliwa na wasi wasi, kabla Kisona haja uliza jambo Lukas akaendelea, “ndio yule ulie nifwata bombambili, afande mimi siyo jambazi ila polis wanataka kuniuwa kufuta ushaidi sababu wao ndio walio wauwa wenzao” alisema Lukas hapo Kisona aka mtuliza, kidogo, “sikia Lukas, viipi una ushaidi wowote?” aliuliza kisona, na Lukas akajibu, “ndio ninao mkanda wa video” alisema Lukas na hapo Kisona akatabasamu, “hupo wapi sasa?” aliuliza kisona, “nipo makambako mnjini, na polisi wamesha gundua kuwa nipo MAKAMBAKO” hapo Kisona akashikwa na butwaa, lakini haraka aka mkumbuka mtu mmoja ambae ni rafiki wa mke wake, yupo pale Makambako, “sikia Lukas, ebu ulizia duka la dawa la linaitwa SHINE, utamkuta dada mmoja aiaitwa Rehema atakupa ifadhi wakati tuna panga tufanye nini” alisema Kisona, na kukata simu, kisha akaanza kubonyeza namba za Rehema Haule, rafiki wa mke wake, ili kumweleza ujio wa Luas kwaajili ya kupewa msaada.****
wakati maongezi hayo yakiisha, kumbe basi hatua kama thalasini toka hapo, binti Monalisa alikuwa amesimama akimkodolea macho dada mmoja alie kuwa ame kaa, kwkenye upenu wa nyumba moja hivi nan doo moja ya lita kumi, yenye vitumbua viwili jyy yake, ikiwa ni halama kuwa ndani yake kuna vitumbua vingine, na vinauzwa, “sijuwi ni kanunue au ninunue wakati wa kurudi?” alijiuliza Monalisa……. itaendelea…….. endela kufwatilia mkasa huu hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata