
SEHEMU YA KUMI
.
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA : wakati maongezi hayo yakiisha, kumbe basi hatua kama thalasini toka hapo, binti Monalisa alikuwa amesimama akimkodolea macho dada mmoja alie kuwa ame kaa, kwkenye upenu wa nyumba moja hivi nan doo moja ya lita kumi, yenye vitumbua viwili juu yake, ikiwa ni halama kuwa ndani yake kuna vitumbua vingine, na vinauzwa, “sijuwi ni kanunue au ninunue wakati wa kurudi?” alijiuliza Monalisa, ambae jibu lake lilikuwa ni kwenda kwanza kupiga simu, kisha arudi kununua vitumbua alafu aelekee pale bar walipo fikia nawenzake,
Monalisa alitembea taratibu. akisogelea jengo moja dogo, lenye maduka matatu, mojwapo liliandikwa muungano communication, alipofika pale kwenye mlango wa kuingilia ndani ya jengo lile, chumba cha muungano, ile anataka kuingia tu! nusu apigwe kikumbo na mtu mmoja alie kuwa anatoka ndani ya chumba hicho, “samahani dada, samahani saba dada yangu” alisema yule mtu, alie nusulika kumkumba kikumbo, kwa sauti ya msisitizo wa kuomba msamaha, huku akikwepesha macho yao yaasi tazamane, “hakuna shida kaka yangu si auja nigonga?” alijibu Monalisa, huku akimtazama yule kaka usni, na bahati mbaya, kama siyo nzuri, macho yao yaka kutana, Monalisa akamwona yule kijana, ambae uso wake ulionekana kuwa na mashaka makubwa, akimtazama kwa namna flani ya mshangao wa kimya kimya, kabla ajamwona anageuka nakuanza kuondoka haraka, kwamwendo wa kuvuta mguu wa kushoto, akionyesha aukuwa sawa, huku kijana yule, akigeuka mala kwamala kumtazama, ukweli Monalisa alisha zowea kuona wavulana wanamkodolea macho, lakini kwa huyu ilikuwa mtazamo wa tofauti kidogo, hasa hali yake ya wasi wasi.
Monalisa alimsindikza kwa macho kijana yule, alie kuwa anaelekea kule alikotokea yeye, mpaka alipo potelea kwenye mitaa, “karibu dada” Monalisa alistuliwa na dada mpigisha simu wapale muungano, “asante” alisema Monalisa huku akitabasamu kidogo, na kuisogelea meza kubwa iliyopo mbele ya mwana dada mmoja mweusi sana, nazani kwaajili ya baridi, ambayo ata monalisa alisiha anza kuisikia, na kujilahumu kwa kulifungia koti lake kwenye begi kubwa, “ naitaji kupiga simu songea” alisema Monalisa huku akitoa kibegi chake mgongoni na kukifungua, “ok dakika moja mia mbili” alisema yule dada ambae alikuwa amevalia koti kubwa, ungesema kuwa anapanda mlima wa Kilimanjaro, “ok! aina tatizo” alisema Monalisa, huku anatoa kikaratasi chenye namba za simu na tsh elfu moja, akamkabidhi yule dada, “nipigie namba hii hapa” alisema Monalisa, na yule dada akamwelekeza sehemu ya kwenda kuongelea, “ingia kwenye kibanda kile cha kwanza” **
Kagiza ka saamoja moja, kalishaanza kutanda, mwanadada Rehema Haule wakati huo alikuwa ndani ya duka lake la dawa, ana fanya mahesabu ya kutwa nzima, ndipo aka sikia simu yake ya mezani inaita, akaipokea haraka akijuwa kuwa ni wateja wake wa siku zote, “hallow Rehema haule hapa naongea nani mwenzangu?” alisema Rehema mala tu baada ya kuinua mkonga wa simu na kuuweka sikioni, “habari za leo shemeji, unaongea na baba Prosper hapa toka songea” ulijibu upande wapili, “hooo shemeji habaari za huko jamani” alisalimia Rehema, na hapo ika fwata salamu ambazo azikuchukuwa muda mrefu sana, ikafwata nia na dhumuni, “shemeji tunaomba msaada mmoja, kuna mtu anakuja hapo, kwako, naomba umfiche ndani mwako sisi tunajiandaa kuja kumfwata” huyo alikuwa ni bwana Joseph Kisona, ambae alimwelezea kilakitu Rehema, juu ya bwana Lukas, na kwamba polisi tayari walikuwa wana msakama ndani ya mji wa makambako, rehema aka kubari kumpoke maana hakuwa na wasi wasi wowote, juu ya Kisona, alisha wai kupata habari zake katika utendaji kazi.
Hapo rehema aka toka nakwenda kusimama nje ya duka lake, akitazama pande zote kama ata mwona kijana anaekuja kwake, mala akawaona vijana wawili wakitokea upande wa mtaa wanyuma ya mtaa wao, maana duka lake lilikuwa hapo hapo nyumbani kwake, “unafanya nini hapo mbona kama kuna mtu unamsubiri” aliuliza mmoja wa wale vijana kwa sauti ya kibabe, kitu ambacho mwana dada huyu akukipenda, “nipo dukani kwangu au kunatatizo?” aliuliza Rehema mwanadada wa kingoni ambae yupo Makambako kusaka fedha, “ujamwona kijana mmoja amevaa tisheti jekundu na jinsi la blue, amefunga kipochi hapa kiunoni” swali hilo lilimstua sana Rehema, “hapana sija mwona, labda amepita wakati nipo dukani” alijibu Rehema huku ana watazama vizuri wale vijana, Rehema alipo angalia miguuni mwao, akagundua kuwa vijana hawa walikuwa wame valia viatu vya kijeshi, yani buti nyeusi, akagundua kuwa watu wale walikuwa ni polisi, “hoya mike, ebu tazama kulee” alisema mmoja wao, huku akionyeshea kiodole upande wa mbele, yani walikokuwa wanaelekea, Rehema nae aka tazama kule walipo onyesheana kidole wale jamaa.
Naam licha ya kuwa na giza flani jepesi, lakini umbali wa mita kama mia moja na hamsini hivi, Rehema aliweza kumwona kijana mmojo alie kuwa ana tembea haraka haraka, huku akivuta mguu wake wakushoto, lakini ghafla yule kijana alionekana kusimama ghafla na kuwakazia macho, hapo wale vijana wawili waka chomoka mbio, kumfwta yule kijana, ambae nae hakuzubaha, akachomoka mbio na kuufata uchochoro wa kati ya nyumba na nyumba, Rehama haku zubaha pasipo kufunga duka lake nae aka anza kuwa fwata wale vijana, lakini akuwa na mbio kama walle vijana walio itimu mafunzo ya kijeshi kwa miezi sita, hivyo wali zidi kumwachia hatua kila walivyo zidi kwenda mbele, ***
Nyumbani kwakina Monalisa, palionekana kuwa na shamla shamla za hapa na pale, maana mama Mona, alikuwa ame tandaza mazaga zaga kibao, juu ya meza, aliyo toka kuya nunua mjini, akimwonyesha mume wake, huku wakipanga mikakati ya sherehe ya kesho, ambayo walipanga kuifanya kesho, “hivi unajuwa kuwa yule mpiga picha wako ni jambazi” aliuliza mama mona, wakati wanaendelea kutazama mazaga zaga yale, “yani mpaka sasa sijamini kwa jinsi yule kijana alivyo mstaharabu, ila nimesha mpata mpigaa picha mwingine” alijibu baba Mona, na wakati ho huo wakasikia simu yao yam le ndani ikiita, mama mona alie kaa karibu na simu akaipokea, “mrs Anerson hapa naongea nani mwenzagu, huo ndio ulikuwa upokeaji wasimu kipindi hicho, “mimi Monalisa, shikamoo mama” ilikuwa sauti ya Monalisa, “hoooo! Mona jamani, mrahaba mwanangu, vipi mahaafari imeishaje?” aliitikia mama Monalisa, akionyesha mwenye furaha sana, “imeisha vizuri, nimemsh anza safari nipo Makambako, na lala hapa” alisema Monalisa, nahapo mama yake aka onyesha furaha zaidi, “hee! safi sana basi kesho mapema sana utaingia songea, vipi umesha mpigia maachumbawako kumjulisha” hapo mama Monalisa akaona ukimya kidogo, “hallow mona unanisikia?” aliuliza mama Mona baada ya kuona mwanae yupo kimya, “nakusikia mama, naona dakika zangu zime isha” alisema Monalisa, nakukata simu, “hallow! hallow! Mona” alisema mama Mona lakini akasikia tii! tiii! tiii! ikionyesha ukuwa simu imekatwa, akajaribu kupiga namba ile nayo ikaitakwa sekunde kadhaa, kisha aka pokea mwanake lakini sauti yake ilionyesha kuwa siyo Monalisa, “hallow muungano communication nikusaidie tafadhari” iilikuwa ni rafudhi ya watu wa njombe yani kama wabena hivi, au wapangwa, “samahani kuna bimti alikuwa amepiga simu hapo, naona ameishiwa dakika alizo lipia” kama ni huyu mschana mzuri , ametoka sasa hivi” ilijibu ile sauti, “ok! asante sana” alisema mama Monalisa, kisha akakatasimu, kwa kurudisha mkonga sehemu yake, kisha akamtazama mume wake, huku usowake ukiwa umenyongea, “Monalisa yupo makambako, anaonyesha kama anahofia sana ndoa yake na Erasto” alisema mama Mona, kwa sauti ya unyonge kidogo, “nazani hali kama hiyo, inamtokea kila mwanamke anae olewa kwa mtindo huu, wa kukabidhiwa mwanaume ambae hakuwa mpenzi wake mwanzo” alisema baba Mona, nakuanza kusisitiza maandalizi ya sherehe, ya kuveshana pete, itakayofanyika kesho hapo nyumbani kwao,***
Rehema akiwa ameacha atuwa kadhaa na wale vijana wawili aliowahisi kuwa ni polisi, aka jitaidi kukimbia, akiwafwata kwa kuingia kwenye chochoro ya upande wapili ambako aliwaona wakizidi kukumbia mbele, lakini sasa hakumwona yule kijana ambae alihiai kuwa ndie Lukas, sijuwi tuie ni umbea au nini Rehema aliendelea kuwa fwata wale vijana walio mwacha kwa umbali wa mita hamsini, mala akaliona gari la polisi likija mbele ya wale vijana, na kusimama, mbele yao na wale jamaa nao wakasimama, wakaonekana kuambizana kitu flani, Rehema akawasogelea akijifanya mpita njia,kuna umuifu wa kkwenda kuwa fwata wakina Makwinya, ili waongeze nguvu” alisema mmoja wa wale vijana akimwambia mwenzao aliekuwa kwenye gari, “ok! nyie piteni huku, na sisi tuna zungukia upande wa barabara, tuta kutana mbele” alisema mtu alie kaa ndani ya gari, upande wa abiria, ambae sisi yani mimi na wewe mdau, tuna mjuwa kuwa ni sajent Idd Kibabu, akionyesha pia kukubari wazo la wenzake, hapo haraka wale vijana wawili wakachomojka mbio na kuemdelea kukimbilia upande walio hisi Lukas amekimbilia**
Kumbe basi baada ya kutoka kwenye chumba cha kupigia simu, Monalisa alitembea taratibu akiwa ameshikilia shilingi mia saba mkono, zilizo bakia kama chenji ya kupigia simu, na kwenda kusimama mbele ya kibaradha cha nyumba ya dada muuza vitumbua, akayoa shilingi mia na kuchukuwa kitumbua kimoja, kilichokuwa kina uzwa shilingi hamsini, kipindi hicho, akakionja kidogo, kisha akatikisa kichwa juu na chini, akikubari kuwa kitumbua kile ni kitamu sana, “nifungie vitano” alisema Monalisa huku ana mpatia yule dada shilingi mia mbili, akimaanisha aongezee na ile shilingi hamsini, “kwani we dada unakaa wapi, mbona sikuonagi hapa?” aliuliza dada muuza vitu mbua, “mimi sika hapa makambako, na kaa songea, hapa nimefikia kwenye guest ile kuleeee” alisema monalisa akionyesha kidole kule kwenye ile guest house aliyo fikia, maana ilikuwa pembezoni mwa barabara yakwenda Mbeya, safu moja na nyumba hii aliyo kaa, dada muuza vitumbua, “kumbe ndio maana nilitaka kushangaa, maana sijawai kukuona hapa makambako” alisema yule dada na kumfanya Monalisa ashangae kidogo, “inamaana watu wote wa makambako unawajuwa?” aliuliza Monalisa, huku akimsaidia yule dada kuhesabu vitumbua kwamacho, “hapana lakini kwa jinsi ulivyo mzuri, lazima unge fahamika…..” ghafla wote wawili waka stuka na kutazama kwenye barabara moja ya vumbi inayotokea ndani ya mtaa, ambapo waliwaona watu wawili wakija mbio mbio, na kuwapita, vijana wale walikimbia na kwenda kusimama pembeni ya barabara ya lami, mala likatokea gari lapolisi na kusimama pembeni yao nikama waliongea jambo flani kisha vijana wale wakarudi tena walikotokea na lile gari la polisi likaendelea na safari, ***
Kati ya watu waliokuwa wana watazama wale vijana siyo Monalisa peke yake mmoja wapo alikuwa Lukas Benjamin, ambae alikuwa amejibanza kwenye chochoro moja, usawa wa nyumba ya mama muuza vitumbua, una juwa kwanini alijibanza hapo, ni sababu Lukas tok alipokutana na Monalisa pale muungano communication, alimtambua moja kwa moja, kuwa ni binti wa mzee Anderson, ambae kesho ilibidi akapigepicha kwenye sherehe yake ya kuveshwa pete, na mchumba wake, lakini hakutaka kuongea nae chochote, maana alijuwa kuwa asinge weza kumsaidia kwa lolote, zaidi ange mwingiza kwenye matatizo, sasa wakati ana mkaribia rehema kama alivyoelekezwa na bwana Kisona, aka mwona akiwa amesimamiswa na maaduii zake wakimwoji jambo flani, na ndipo walipo mwona na kuanza kumfukuza, sasa basi alipo karibia eneo hili, akamwona tena Monalisa akiwa ananunua vitumbua, lengo lake likawa ni kwamba, ajifiche kwanza wale polisi wapite, wakisha toweka yeye ampatie Monalisa kile kimkanda, apeleke kwa kamnda Kisona, maana sasa alihisi kuwa, ingekuwa vigumu kumfwatilia Monalisa, maana wasingeweza kuhisi chochote juu yake, ***
Mwingine alikuwa ni Rehema haule, ambae kwa msaada wa taa za majumbani, aliwaona wale polisi wakija na kumita kidogo, kisha wakasimama kwenye giza na kuanza kujadiliana waelekee wapi, na wakati huo huo akamwona yule kijana ane chechemea, ambae yeye alihisi kuwa, ndie bwana Lukas alie elekezwa na mume wa rafiki yake, yani bwana Kisona, akitokeza toka kwenye upenyo mmoja karibu na waliosimama waschana wawili, mmoja akinunua kitu flani toka kwa mwingine, wakati huo huo rehema aalipoangalia kule waliposimama wale polisi wawili, akawaona wakimtazama kijana yule, kisha nikama walio ambizana walichomoka mbi kuelekea alipo kuwepo kijana yule, ebu tusogee sehemu hiyo.
Akika kilikuwa kitu cham ghafla sana, maana wakati Monalisa anapokea kijifuko cha vitumbua, mala akamwona kijana mmoja alie mkumbuka malamoja, kuwa alikutana nae pale muungano, kwenye huduma ya simu, “samahani dada yangu, nakufahamu kuwa ni mtotoo wa mzee Anderson, naunaenda songea, naomba nikuagize kitu muhimu” alisema Lukas huku akihema kwa hofu kijana Lukas, na kumfanya Monalisa astuke kwa uoga, kisha akama vile alie kuwa anasita sita, Monalisa akaitikia kwa kichwa akionyesha kukubari, “naomba tusogee kidogo” alisema Lukas na kuongoza upande ule aliokuwa anaelekea Monalisa, yani upende ilipokuwepo hotel waliyo fikia wakina Monalisa na wenzake,
Pasipo kujuwa kama polisi wanakuja kwa speed kali sana, Lukas na Monalisa walitembea, mpaka walipo ufkia upenyo mwingine, ambao unatazamana na barabara kuu, iendayo mbeya, “sikia dada yangu kuna hiki kitu naomba ufike nacho songea, atakama sitapona lakini nataka watu waujuwe ukweli, mpelekee mtu moja anaitwa Kisona, ni askari wajeshi la ulinzi” alisema Lukas na kufungua pochi yake, iliyo ning’inia kiunoni mwake, na kutoa kijitape flani, akampatia Monalisa, nae akakipokea, huku ana tetemeka, “sikia dada usije ukamweleza mtu yoyote kuwa unayo hii tape, nawala usi mwamini polisi yoyote, mapaka una mkabidhi Kisona” alisema Lukas huku Monalisa akibakia ameduwaa, kama vile ajuwi kinacho endelea, maana alikuwa anaogopa sana kutokana na maneno ya Lukas, asa ile kauri ya ‘atakama sitapona’ mala wakati huo huo, ikasikika muungurumo wagari, na kukamata bleack za ghafla, aikuwa sili kwa Lukas kuwa lile gari ni la polisi, aka chungulia kidogo kuakikisha hisia zake, ndiipo alipo liona gari lile la polisi likiwa na askari wawili juu yake, huku wengine wawili wakija mbio mbio, upande alipo kuwa yeye na Monalisa, na kwahakili za haraka akajuwa kuwa alisha bainika tena, na akizubaha anaweza aka sababisha matatizo kwa binti huyu, sababu ana ijuwa vyema tabia ya polisi hawa, ya kumimina risasi ovyo, sasa fanyaje.
Hapo Lukas akageuka na kumtazama Monalisa aliekuwa ana tetemeka, asijuwe la kufanya, “kimbia haraka” alisema Lukas akimwonyesha ishala ya mkono Monalisa, lakini akamwona dada huyu akiwa ameganda pale pale, hapo Lukas akapata wazo flani, ambalo alihisi linawza kumsaidia Monalisa, asiingie kwenye matatizo, Lukas akajitokeza ghafla toka kwenye upenyo, ule ambao kwasasa ulikuwa na giza, kisha akaaza kukimbia kuvuka bara bara, ikiwa lengo lake ni kuwapeleka polisi mbali na Monalisa, hapo Monalisa aliweza kumwona kijana yule, akikimbia kwa kuchechemea huku akiungiwa na vijana wawili kisha watatu na kutimia watano, “mpige risasi asifike mbali” ilisikika sauti yamtu mmoja ambae alionekana kuwa nyuma kabisa ya wenzake wale wenzake, hapo Monalisa akawaona wale watu wanao mfukuza yule kijana wakijipapasa viunoni, na kutoa bastora, ambazo kwa sasa hazikuwa zime fungwa viwamba sauti, na kuzielekeza kwa Lukas, kisha ika sikika milipuko mfurulizo ya risasi, na vitu kama miali ya moto iki elekea kwa Lukas, na kumwingia mgongoni, na hapo Lukas kabla aja ikatiza barabara alionekana akirushwa juu na kutupwa chini, akidondoka kama mzigo flani, Monalisa akawaona wale jamaa wakimfwata na kumzunguka yule kijana ale kuwa amelala chini, alafu nikama walianza kumsachi,
Hapo nikama alie toka kwenye usingizi, Monalisa akakumbuka kuwa, kwa sasa amebeba kitu cha hatari, ambacho atakiwi kukikabidhi kwa watu wale, maana alijuwa kuwa siyo watu wema, kama nikupata wanacho kitaka, basi yule jamaa wasinge muuwa, hivyo ata yeye anaweza kuuwawa pia, Monalisa akaweka kile kijitape kwenye begi lake la mgongoni, na kiwa na mfuko wake wa vitumbua, akatoka pale upenyoni, na kuanza kutembea haraka, kuelekea upande wa hotelini, akihisi kuwa viatu vyake vyenye visigino virefu, viki mnyima uhuru wa kutembea haraka, akasimama na kufungua mkanda wa viatu vyake, kisha akavishika kwenye mkono wa kushoto, na mkono wa kulia aliushika mfuko wa vitumbua,**
Akiwa ajuwi kilichoendelea baada ya Lukas kuondoka na yule mschana pale kwa muuza vitumbua, Rehema alisogea na kuwafwata wale polisi walio mkimbilia Lukas, akawaona polisi wakiongezeka na kuanza mwandama kijana yule, na mwishoe waka mshambulia kwa risasi, sasa wannchi wa eneo hili walionekana kuanza kusogea eneo la tukio, “afande jamaa hana kitu, sijuwi ame peleka wapi?” alisema mmoja wa wale polisi waovu akiwa amshikilia kipochi alicho kinyofoa kiunoni kwa Lukas, ambae alikuwa amelala kwenye dimbwi la damu, ametulia ikionyesha wazi kuwa hakuwa na uhai, taharifa ile ilimstua sana sajenti Kibabu, “inawezekanaje, hapana lazima ipatikane” alipayuka sajent Idd Kibabu, “afande nimekumbuka kitu” alisema mmoja wa polisi, kati ya wale wawili waliokuwa wana mwandama Lukas toka mwanzo, huku ana tazama huku na kule, kama kunamtu anamatafuta, “kitu gani Charles?” aliuliza Kibabu kwa sauti ya chini, kisha yule polisi alie itwa Charles, aka sogea na kumnong’oneza jambo Kibabu, hapo wote wakaanza kutazama wau wawili watatu walio kuwepo eneo lile, na mwisho Charles akatazama kule kwenye kibaradha cha muuza vitumbua, akamwona yule dada muuzaji, akiwa nawenzie kadhaa, waliotoka kwaajili ya kushangaa tukio hili, “alikuwepo pale, yule mscana alie ondoka na Lukas, yule dada anaweza kutuambia yule binti yupo wapi” alisema yule askari na hapo hapo, Kibabu akasema, bebeni huu uchafu pelekeni hospital, mimi Charles Mike, mtatukuta mitaa hii hapa” alisema Kibabukisha wakaondoka wakiwaacha wale polisi wawili wanaupakiza mwili wa Lukas kwenye gari, wao wakaelekea kwa dada muuza vitumbua.. itaendelea …….. endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU