BIKIRA YA BIBI HARUSI (11)

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI : “alikuwepo pale, yule mscana alie ondoka na Lukas, yule dada anaweza kutuambia yule binti yupo wapi” alisema yule askari na hapo hapo, Kibabu akasema, bebeni huu uchafu pelekeni hospital, mimi Charles Mike, mtatukuta mitaa hii hapa” alisema Kibabukisha wakaondoka wakiwaacha wale polisi wawili wanaupakiza mwili wa Lukas kwenye gari, wao wakaelekea kwa dada muuza vitumbua. ENDELEA………
Wakati huo huo huku Songea, bwana kisona, alikuwa chumbani kwake anajindaa, kwa safari, maanayake tayari alisha wasiliana na mkuu wake wa kazi, yani brigedia Fransis Haule, na kumweleza jinsi mambo yalivyo, na kwamba mpango wake ni kwenda Makambako haraka iwezekanavyo, aka kutane na Lukas, kwaajili ya kupata ushaidi wa tukio la NMC, na pia kuokoa maisha ya kijana huyu raia mwema, pasipo kujuwa kuwa, kijana huyu kwa sasa tayari alishapoteza maisha, tayari Kisona aliisha luhusiwa kwenda makambako, nae aka wajulisha askari wanne na dereva mmoja, ambae aliambiwa aandae gari kwaajili ya safari, bwana kisona aliendelea kuandaa vifaa ambavyo aliviitaji safarini, kwaajili ya kazi ya huko, ambayo aliipanga kuifanya kimya kimya, huku pembeni yake mke wake doctor Elizabeth Leonard akimsaidia,
“baba baba, simu aita (inaita) ilisikika sauti ya Doto, yani mtoto wao, alie ingia chumbani ghafla, hapo bwana Kisona akajuwa kuwa kunasimu ina ita sebuleni, hivyo aka toka mbio kwenda kuisikiliza, maana kila simu ilikuwa muhimu kwake, “hallow canal Kisona hapa, nani mwenzangu?” alisema Kisona mala tu baada ya kupokea simu, “shemeji ni mimi Rehema” ulisikika upande wapili wa simu, ilikuwa ni sauti iliyo jaa unyonge mkubwa sana, “ndio shemeji niambie vipi kunatatizo?” aliuliza Kisona kwa shahuku, maana hakutegemea kupigiwa simu mapema namna hii, toka kwa rehema, “shemeji sikujuwa kama kazi hii ni yahatari namna hii” alisema tena Rehema kwa sauti iliyojaa unyonge mkubwa sana, “imekuwaje shemeji, wame fanyaje hao washenzi?” aliuliza Kisona kwa shahuku, huku hakiri yake ikimtuma kuwa tayari kuna jambo limetokea, “yani hawa jamaa ni wakatili sana” alisema Rehema, na kumsimulia bwana kisona jinsi ilivyo kuwa, kabla haja kutana na Lukas, na jinsi alivyo uwawa” lakini inaonekana hawaja kipata wanachokitafuta, maana niliwasikia wakisema kuwa, hana kitu” ukweli jambo ili lilimchanganya hakiri bwana kisona, na kumfanya agande kwa dakika kadhaa, akiwa na mkonga wasimu mkononi mwake, japo simu ilisha katwa, ata mke wake alipo mkuta, aka juwa kuwa kunajambo alija kaa sawa,
“kwamala ya kwanza na shindwa kumsaidia mtu anaeitaji msaada wangu” alisema bwana kisona na kuanza kupiga simu kwa brigedia na kumpa taalifa ya kusitisha safari yake, ****
“yule mschana ulie kuwa umesimama nae hapa, na baadae akaondoka na yule jambazi unamfahamu?” aliuliza sajent Kibabu, akiwa amemkazia macho yule dada muuza vitumbua, ni baada ya kusogea nae pembeni na kujitambulisha kwake, kuwa wao ni polisi, na kumwonyesha vitamburisho, “hapana simfahamu, hapa alikujakununua vitumbua tu!” alijibu yule dada kwa sauti iliyo changamka kidogo akijuwa kuwa anahojiwa na wana usalama, “kwa hiyo uwezi kujuwa anatokea mtaa gani kwamba ujawao kumwonaga sehemu?” aliuliza Mike, kwa sauti flani ya kushawishi, “yule siyo mwenyeji wahapa, yule ana safari kuelekea songea” alilopoka yule mwana dada muuza vitumbua, pasipo kujuwa kuwa ana muuza mwenzie, kwa watu wabaya, “ok! kwahiyo inawezekana kuwa amefikia kwandugu zake eti” aliuliza Mike, ambae alionekana mjanja katika kuteka hakiri za mtu, “amefikia kwenye guest house ilekuleee kwenye lile bango lenye taa, tena kama ameelekea huko basi mkiwai mtamkuta kabla haja fika….” hapo kabla haja maliza kuongea dada muuza vitumbua, tayari wakina Kibabu na watu wake walishatoka mbio kuelekea kule waliko onyeshwa, **
Edgar wakati huo alikuwa ndani ya chumba chake namba kumi na saba, akiwa amejiegesha kitandani, nikama alikuwa anawaza jambo flani, ilimjia picha ya gari lililo wafwata wakina Monalisa pale chuo, akawakumbuka wale jamaa wawili waliokuwa wamekaa seat zambele, hapo ilimjia hisia kuwa mmoja wapo kati ya wale, wawili atakuwa ana jilia kitumbua cha Monalisa, “upuuzi kwani demu yupo peke yake, atakama yupo na dume si yeye bwana” alijisemea Edgar huku anainuka toka kitandani na kulifwata begi lake dogo, kisha akachukuwa kiasi flani cha fedha nyingine akizirudisha kwenye begi lile dogo la mgongoni, aka funga na kutoka nje, akielekea upande wa bar, tayari kwenda kupata chakula cha jioni, maana toka alipo kuwa amekunywa chai na vitumbua, asubuhi, hakuwa amepata chakula kingine, na njaa ilisha anza kumchambanda,
Akiwa bado amevaa kama alivyokuwa wakati anatokea Mbeya, yani jinsi nyeusi tishert nyeusi na raba, Edgar alitembea taratibu huku akihisi baridi ikiingia mwili mwake, aka ghaili kuelekea kule bar na kurudi chumbani kwake, akacukue jacket, lakini ile anageuka tu!, mala akaona mlango wa jilani kidogo na wakwake yani upande wapili, ukifunguliwa, na wakatokea vijana wawili, wakionyeshana kitu mkononi, “sikia we bwege, hii unaiweka kidogo sana, yani ukiizidisha tu, tuta mbeba, sababu ata uchapa usingizi mzito pale pale” alisema mmoja wao, huku wakija anakotokea yeye, maana yake walikuwa wanapishana kwenye korido, “inamaana hapa ni tonye dogo tu! kwenye soda, tunakula mzigo mpaka basi?” aliuliza yule mwingine huku akikiinua kijichupa kidogo sana alicho kishika mkononi, nakukitazama kama vile anataka kutazama kilicho kuwepo ndani, “hiyo nikama nisu kaputi, yani kesho sisi tunafika iringa yeye ndio anaamka” alisema yule msemaji wakwanza, mpaka hapo Edgar akajuwa kuwa, hawa vijana kuna mchezo mchafu wanataka kumfanyia mtu flani, “washenzi hawa miaka hii ya kufanya ujinga kama huu?” aliwaza Edgar huku ana tazama mlango wa chumba walicho tokea wale vijana, kilikuwa ni chumba namba tisa, sijuwi angefanyaje kama ange juwa kuwa ni Monalisa ndie anae pangiwa kufanyiwa jambo hilo,
Edgar ali rudi chumbani kwake na alitoa Jacket lake la blue, toka kwenye begi lake kubwa la mgongoni, kisha akatoka nakuelekea kule bar, pasip kujuwa kuwa, wakati anatoa jacket kwenye begi, alidondosha kitambulisho cha chuo, ambacho leo mchana ndio kilikuwa mwisho wa matumizi yake, “tonye moja tu kwenye soda, tunakula mzigo mpaka basi” Edga alikumbuka swali la yule kijana mmoja, akajikuta anacheka kidogo, akizarau hakiri ya wale vijana, ambao Edgar aliwaona tena, dakika cache mbele, ni baada ya kuingia ndani ya ukumbi wa bar, ambao upo ndani kwa ndani, nazani kwaajili ya baridi, unazani aliwaonaje onaje, ni wakati anakatiza katiza kwenye meza, za watu mbali mbali walio jaa mle ndani, wengi wao wakiwa wawili wawili, wakike na wakiume, wakionyesha kuanza kulewa, maana palichangamaka kwa kelele za watu na music, ambao uliwananyua bahadhi yao, ambao waliamua kucheza, ambapo muda huo ulikuwa unasikika wimbo wa yondo sister, unaoitwa basoo, sasa basi wakati anakatiza meza moja hivi ili aifwate iliyo kuwa tupu, ndipo alipostuka akisalimiwa, “mambo vipi Edgar?” Edgar akastuka na kutazama alie msalimia, “hooo! poa tu Denis, kumbe na nyie mmefikia hapa?” alisema Edgar, huku ana zungusha macho yake, kutazama watu waliokuwepo pale mezani, mmoja baada ya mwingine, akitarajia kumwona Monalisa, lakini licha ya kumwona Stella, lakini hakumwona Monalisa, zikamjia hisia kuwa alikuwa chumbani anapewa mambo, “ndio tumefikia hapa, kesho tunahamsha, vipi ume mwona Monalisa?” aliuliza Denis, huku akimtazama Edgar, ambae alikuwa anawatazama wale vijana wawili, waliokuwa wana kunywa bia, tofauti na wakina Denis, waliokunywa soda, ni vijana wale ambao muda mfupi uliopita, aliwasikia wakipanga kumlewesha mtu flani, “Monalisa si mlikuwa nae nyie, kwani mliachana?” aliuliza Edgar, ambae sasa moyo wake ulipoa kidogo, na wivu uka pungua, “yeye aliingia chumbani kwake, lakini tume jaribu kugonga mlango wake tumeshangaa hakuna mtu” alijibu Deins, “atakuwa ameenda kununua kitu flani au kupiga simu kwao” alijibu Edgar, kisha akawaaga na kwenda kukaa kwenye meza, aliyoiona hipo wazi, na kuagiza soda na chipsi kwa mishikaki minne, kisha akasubiri kuletewa kama alivyo agiza.
“yani sisi tunafika iringa yeye ndio anaamka” wakati Edgar anasubiri vitu alivyo agiza, ilimjia hiyo kauri ya wale jamaa, waliokaa na Denis na Stella, “mh! Monalisa” alisema Edgar kwa mstuko, huku akiinua shingo yake na kutazama huku na huku, mle ndani ya bar, kama vile anamtafuta mtu flani, “awa jamaa wanataka kumfanyia vitu vibaya Monalisa” nikama Edgar alikuwa ameng’amua jambo, na anaitaji kumsaidia Monalisa, “sasa yupo wapi huyu mwanamke?” alijiuliza Edgar, huku akiendelea kutazama tazama mle ndani ya bar,
Mala ghafla akamwona Monalisa anaingia mle ndani ya bar, akitokea nje, akiwa amevaa kama livyo mwona wakati anaondoka kule chuoni, hapo Edgar akashangaa kidogo, ni mshangaon ulio ambatana na mstuko, maana mwonekano wa Monalisa ulikuwa tofauti kidogo, Edgar aka watazama wakina Denis, akawaona wapo busy wana endelea na vinywaji, tena mhudumu alikuwa ana waletea masaani yaliyo jaa chips, hapa makambako chips ni nyingi sana, tena kwa bei poa kabisa, Edgar aka mtazama tena Monalisa, akamwona anatembea haraka haraka sana, kuelekea upande wa vyumbani, akiwa ameshika viatu vyake mkononi wa kushoto na wakulia ameshika kijifuko kidogo cha kaki, wakati Edgar akitafari namna ya kumwokoa Monalisa, mwanamke alie vunja urafikinae miaka mingi iliyopita, mala akawaona watu watatu wakiingia mle ndani ya bar, nao wakitokea nje ya ile bar, na kusimama kati kati ya ukumbi akianza kuangalia huku na huku, kama vile walikuwa wanamtafuta mtu flani, Edgar akawaona wakitazama kule upande wa vyumbani, ambako alionekana Monalisa akipotele kwenye korido, hapo wakaonyeshana kwa vidolea, wakionyesha upande ule alikopotelea Monalisa, kisha mmoja wao akawaambia waende kule, kisha yeye akatoka nje ya bar, “huyu demu mjinga sana, yeye anajijuwa ni mzuri, alafu ana jifanya kuja kulala kwenye ma guest, ona sasa midume inavyo mfukuzia, watambaka huyu” alisema Edgar, huku anainuka na kuelekea kule upande wa vyumbani, akizania anaenda kumwokoa Monalisa toka kwa wanaume wenye uchu, wa ngono, pasipo kujuwa huo ndio mwanzo wa matatizo, kumbuka comment na like yako ni muhimu sana, kufanikisha hili, maana tunaitaji ushauri na maoni toka kwako mdau, ……. usikose sehemu ya kumi nambili hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata