
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Monalisa alimtazama Edgar pale alipo lala fofo, akapata wazo la kumchungulia sehemu zake za siri, sijuwi wazo hilo lilikuja kivipi, basi taratibu Monalisa akaijinyayua na kuanza kufungua mkanda wa suruali ya Edgar, lakini kabla aja anza kufungua, ghafla akastuka kuona mlango wa chumba kile, unafunguliwa na wakaingia wale vijana wawili, waliotaka kumbaka kule kwekenye ile hotel, yani wale walio muuwa Lukas, safari hii wakiwa na mapanga mikononi mwao.endelea………..
Na sio bastora kama alivyo waona mwanzo, Monalisa akamwona mmoja wa wale watu, ambao aliambiwa kuwa ni polisi, akimsogelea pale alipo lala, na kuinua panga lake juu, kisha akalishusha kwanguvu, usawa wa kichwa chake, “mama na kufaaaaa!” alipiga kelele Monalisa, na hapo hapo aka stuka toka usingizini, akamtazama Edgar alie kuwa ana mtazama kwa mshangao, akiwa amekaa kitandani huku akijiegemeza kwenye ukuta, na akuwa amelala kama amaonalisa alivyo kuwa anaota, “kumbe ndoto,” alisema Monalisa kwa sauti iliyo jaa hofu kubwa, huku ana hema kwanguvu, ungesema alikuwa anafukuzwa, na jitu la kutisha au mnyama mkali, lakini Edgar akumsemesha kitu, zaidi alimtazama tu!.
Hapo Monalisa akajilaza tena pale pale pembeni ya Edgar, alipokuwa amelala mwanzo, na kujifunika tena shuka vizuri, huku Edgar akimtazama tu! pasipo kuonyesha dalili ya kulala, Edgar alimtazama Monalisa kwa dakika kazaa kanakwamba kuna kitu ana waza, Edgar alikuwa amerudisha mawazo yake miaka ya nyuma, kipindi wakiwa wadogo, wakicheza pamoja, kipindi ambacho Monalisa, akutaka Edgar acheze na mschana mwingine, na iwapo Edgar angefanya hivyo, basi Monalisa angezila kucheza nae kwa siku nzima,
Edgar alitabasamu kwa kumbukumbu hiyo, aliangalia jinsi mwili wa Monalisa alielala kiubavu ubavu, ulivyo jichora, kwenye shuka na kuonyesha kimsambwanda chake, kilicho inuka upande wa hips na kuchomoza kwa nyuma, kisha aka matazama usoni, ile sura yake yakitoto aikuwa imepotea, Edgar akatabasamu kidogo, “haaaa! ilikuwa zamani bwana” alijisemea kimoyo moyo Edgar, kisha aka geuza usiwake na kutazama mbele, kisha kushoto alafu kulia, alafu juu, yani nikama alikuwa anakagua kile chumba, alifanya hivyo mpaka alipo msikia Monalisa akianza kukoroma. *****
kati ya watu walio kosa usingizi mzuri usiku ule, mmoja wapo alikuwa mama Edgar, yani moyo klwake ulijawa na hali flani ya kukosa amani, japo akutaka kuamini kuwa mwanae Edgar alikuwa katika matatizo, lakini alihisi kuna jambo baya lina taka kutokea kwa mtu wake wakaribu, mala kwa mala mzee Mbogo alipostuka na kumtazama mke wake, alimkuta bado ajalala, na yeye ambae akuwa na wasi wasi wowote, alijuwa akimwongelesha mke wake usiku huu, ndio mwanzo wa kukesha, wakizungumzia juu ya hisia za mke wake, ambae akiwa katika hali kama hii, ujuwe kuna jambo lime tokea, au litatokea, kwa mtu wao wakaribu.
Mwingine alikuwa ni mama Monalisa, ambae alitamani, sherehe ya jkuveshana pete, ya vijana wao ipite haraka sana, maana akuelewa msimamo wa Monalisa, ambae toka mwanzo alipoambiwa juu ya kuolewa na Erasto, alionekana kuto kupendezewa, maana ata kukubari kwake, ulitumika ushawishi mkubwa sana wa mama yake na mama Erasto, ilifikia kipindi ata walinuniana na mama yake, ndipo Monalisa alipo kubari kuolewa, kwa shaliti moja la kuto kukubari, kushiriki tendo la ndoa, mpaka ndoa ipite, lakini leo mama Monalisa ameona wazi kuwa, mwanae bado ajalizika kuolewa na Erasto, mtoto wa rafki yake mkubwa, ambae walipania kufanya sherehe kubwa sana ya harusi, kwa vijhana wao hao, wakisaidiwa na waumezao walio panga mambo mengi sana kwa watoto wao, ikiwa ni pamoja na kuwafungulia bishara kubwa sana, itakayo wasaidia katika maisha yao, na kitu ambacho mama huyu kili mfanya akose usingizi zaidi, ni kwamba aliona wazi kuwa endapo Monalisa atakataa kuolewa na Erasto, atakosa ile heshima aliyo itafuta kwa miaka mingi sana, ya kwamba mwanae ataolewa akiwa na bikira yake, yani ajaguswa na mwanaume yoyote,
Wakati yeye anawaza hayo yote, huku mama Erasto nae, alikuwa anawaza yakwake, kwanza alikuwa ana waza jinsi mwanae Erasto, atakavyo bahatika kumpata mscha mzuri kama Monalisa, aliekuwa bikira, ukiachilia uzuri wa sura mwili na tabia za Monalisa, pia mama huyu, alionakuwa atakuwa ametimiza lengo lake, alilolipanga miaka zaidi ya kumi iliyopita, kipindi mama Edgar alipo jinadi kuwa Monalisa ni Mchumba wa Edgar, kitendo kile kilimuuma sana, maana aliona kuwa mama Edgar ni mbinafsi, na mwenye kumpendelea mwanae vitu vizuri, wakati yeye pia alikuwa na mtoto wa kiume, hapo ndipo alipo zamilia kuwa lazima mwanae Erasto aoane na Monalisa, na bahati nzuri kwake leo hii wanajiandaa kushuhudia watoto wao wakiveshana pete za uchumba hapo kesho, “Erasto ndieo ana stahili kuwa na mwanamke mzuri kama huyu” aliwaza mama Erasto, huku akijuwa wazi kuwa mwanae anae mwazia hayo, usiku huu akuwepo nyumbani, alikuwa kwenye nyumba za kulala wageni na wanawake wake anao wa badirisha kila siku, wakiwepo wafanyakazi wake wandani, kwakulijuwa hilo mama Erasto akacheka kidogo, “Mona atajiju mwenyewe, ndoa uvumilivu” alijisemea kwa sauti ya chini, huku anainuka na kuelekea chooni, ambako sekunde chache baadae ikasika sauti ya kumwagika kwa mkojo, ‘pwaaaaaaa’ “navile anvyo jifanya mpole na nzuri” aliendelea kuwaaza mama Erasto, ***
Mwiingine alie kosa usingizi ni bwana Kingarame, ambae licha ya kuwaza juu ya utajiri ambao upo mbele yake, pia alishangazwa jinsi, swala la kuupata uishaidi wa tape ya video, ulivyo kuwa mgumu, maana alitegemea ingekuwa lahisi kumpata Lukas, na kuupata ushaidi, lakini licha ya kumpata Lukas na na kumpoteza kwenye uso wa dunia, lakini bado kuna watu wame ingilia kati, “pumbavu kabisa, watakufa ikibidi” alisema bwana Manase Kingarame, ambae alikuwa amesha jilaza kwenye kitanda chake, toka nusu saa iliyopita, “na yeyote atake jiingiza lazima afe” aliendelea kuwaza mzee huyu, ambae serikali ilimwamini na kumpatia dhamana ya kuongoza kitengo nyeti kabisa kwenye jeshi la polisi,**
Monalisa na alimtazama Edgar akamwona akiwa amesimama ana vua nguo, yani suruali na kubakia na bukta, na yeye aka kodoa macho kutazama vizuri, asijuwe lengo la Edgar kuvua nguo Mbele yake, akamwona ana ana maliza kuvua suluali na kufwatia bukta ya ndani, hapo Monalisa akajuwa sasa anakaribia kuiona dudu ya Edgar, lakini akamwona kama anachelewa, sijuwi kwanini, Monalisa aka inuka na kumsogeolea Edgar pale aliposimama, na kutaka kumvua bukata yake, lakini Edgar aka mzuwia, “we si mchumba wamtu, unataka nini sasa?” aliongwea Edgar kwa hasira, iliyoonyesha kuchukizwa na kitendo cha Monalisa kuolewa na Erasto, laikini Monalisa alipotaka kujibu, akashindwa, sababu aliona kama sauti yake ina mezwa na kitu kama hewa flani, sijuwi ni hasira au uchungu, hapo akajaribu kumvua tena, lakini Edgar aka mzuwia na kutaka kumsukuma pembeni, Monalisa aka udaka mkono wa Edgar, na kumng’angania, hapo wakaanza kuvutana,
wakati wanaendelea kuvutana, mala mlango ukafunguliwa, wote wakaacha kuvutana na kutazama mlangongoni, Macho ya Monalisa yaka shuhudia kitu ambacho kilitaka kumdondosha kwa mstuko, kwanza kabisa alimwona mchumba wake Erasto, akiingia, mle chumbani, sijuwikwa nini maana hilo alikumtisha sana, kilicho mtisha ni wale aliongozana nao, walikuwa ni mama Erasto, na wale polisi wawili waliotaka kumbaka kule hotelini, ata Monalisa alipotaka kughhoji jambo flani kwa Erasto, ilishindikana, maana sauti yake ilimezwa na hewa, wakati huo huo Monalisa akamwona Erasto akiwa mejawa na hasira, akimrukia na kuanza kumkaba kooni, hapo akaanza kutapa tapa,
“we Mona! Mona!” hapo Monalisa akastuka toka usingizini, baada ya kuamshwa na Edgar, Monalisa alistuka huku anahema kwa nguvu, kisha akamtazama Edgar aliekuwa amepiga magoti pembeni yake, “unatatizo gani wewe, unajuwa mala yapili hii una weweseka ndotoni?” aliuliza Edgar ambae alikuwa amemwamsha Monalisa, baada ya kuona anaangaika ndotoni, “niliwaona tena wamekuja” alisema Monalisa, akionyesha kuwa, bado yupo kwenye hofu kubwa sana, Edgar alitabasamu, “wakina nani hao?” aliuliza Edgar, huku akimtazama Monalisa, aliekuwa amekaa juu ya kitanda, kwakujikunyata, “wale polisi wauwaji, naaa…. naaaa, Erasto na mama yake” alisema Monalisa kana kwamba akutaka kulitaja jina hilo mbele ya Edgar, ambae akuwa anajuwa mausiano mapya ya Monalisa na Erasto, Edgar akacheka kidogo, “nindoto tu! ebu jaribu kusali kabla ya kulala” alisema Edgar, kwasauti tulivu, “Edgar kama autojari naomba nilale hapo” alisema Monalisa huku akionyesha kwa mkono, kwenye mapaja ya Edgar, Edgar alitabasamu kidogo, huku anamtazama Monalisa, “kama itakusaidia sawa” alijibu Edgar, huku anakaa vizuri, hapo Monalisa aka jisogeza kwa Edgar na kujilaza, miguuni kwa Edgar, kwa mtindo wa kujikunyata, Edgar akavuta shuka na kumfunika, Monalisa aliinua usowake na kumtazama Edgar usini, macho yao yaka kutana, wote wakatabasamu, “asante Eddy” alisema Monalisa, kisha kika pita kimya kidogo, alafu Monalisa akaongea tena, “Edgar na kumbuka sikuile tuliyo nyeshewa na mvua, ulini kumbatia kama hivi, nilipo sikia baridi kali” hapo wote walicheka, kwa kumbukumbu hiyo tamu ya utotoni, siku waliyo nyeshewa na mvua wakiwa wanatoka shuleni, waliongea mengi sana mpaka Monalisa alipo pitiwa na usingizi mzito, na safari hii, akiota ndoto nzuri za kupendeza, zikiusisha matukio ya chuo na utotoni iliyompatia raha ya usingizi **
Saa tisa za usiku, ndani ya mji wa Makambako, ambao mida hii ulikuwa tulivu sana, hapa kuwa na mianjo ya watu, wala magari, giza lilikuwa lime tanda kweli kweli kweli, baridi ilichamanda vilivyo, ikiambatana na upepo ulio timua vumbi, lililo wakela wakina Sajent Kibabu na askari wake, ambao sasa walikuwa wamekutana, maeneo ya karibu na hoteli ambayo wakina Edgar walifikia mwanzo, huku pembeni yao magari mawili aina ya land rover mia na kumi, yakiwasubiri, “ni vigumu kumtafuta mtu alie tulia sehemu moja, ni sawa na kutafuta sindano gizani” alisema sajent Kibabu akiwa mbele ya askari wake, aliotoka nao songea, na wale walio ongezea nguvu, yani wa hapa hapa Makambako, “nikweli afande, japo makambako ni ndogo, lakini kunasehemu nyingi sana za kujificha” alisema askari mmoja mwenye cheo cha koplo, ni kati ya wale wenyeji, “hivi afande, itakuwaje endapo watakuwa wamesha hama mji, na kwenda Njombe, aliuliza Mike, huku wengine walio onekana kuchoka kisawa sawa, waki mtazama sajenti wao, “awawezi kukatiza Njombe, maana tayari tumesha peleka matangazo ya kumtafuta Edgar, yana bandikwa mji mzima” alisema Kibabu na yule koplo akadakia, “na awawezi kupata usafiri wa songea usiku huu, ni mpaka kesho asubuhi, na watu watakuwa wamesha soma matangazo” walipanga mikakati ya mingi ya kuwakamata wakina Edgar, “sasa hivi tunaenda kukaa stendi, tusubiri muda ambao abiria wataanza kupanda kwenye mabasi, ili tuwanase, awa washenzi” alisema Kibabu, ikifwatia na wale askari kuingia kwenye magari, tayari kuelekea stendi kuu ya mji wa Makambako, ****
Erasto Richard Misago, alionekana akitembea kwa mwendo wa haraka sana, kati kati ya mji wa Songea, hakujuwa alikuwa anaenda wapi kufanyanini, lakini alikuwa ni mwenye hofu kubwa sana, na mwenye kukosa amani, moyoni mwake, safari yake iliishia maji maji hotel, aka kumbuka kuwa alikuwa anakuja kumwona Happy mpenzi wake, nikama alijuwa sehemu ambayo Happy alikuwepo, maana Erasto kama bwana harusi mtarajiwa aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye chumba kimoja wapo, kati ya vingi vya hotel hii, ambavyo utumika kwa kulala wageni, p[asipo kuuliza akausukuma ule mlango na kuingia ndani,
Alicho kikuta ndani ya chumba hicho kili mstuasana Erasto, kwanza badala ya kumkuta Happy akama alivyotegemea, alimkuta Monalisa, akiwa amlala kitandani, licha ya kuwa alikuwa amejifunika shuka, lakini alionyesha wazi hakuwa na nguo atamoja mwilini mwake, tena akiwa na mwanaume, ambae sura ya mwanaume huyu nikama ilikuwa ina mpotea potea, na kushindwa kuitambua vizuri, “Monalisa” alipayuka Erasto na kukurupuka toka kitandani,
Kumbe Erasto alikuwa ndotoni, alitazama huku na huku akajikuta yupo chumbani, tena ni chumba mwebeni Guest House, “utachanganyikiwa mwaka huu, hapo bado uja mtoa bikira yake, ukionja je?” ilisikika sauti ya mwanamke, alie lala pembeni yake, Erasto akainua uso wake na kutazama pembeni, akamwona mpenzi wake mhudumu wa pale mwembeni bar, “afazali siyo kweli” alisema Erasto, kwa sauti iliyo ambatana na kuhema kwanguvu, “sijuwi kwanini nimeota ndoto mbaya kama hii?” alijiuliza Erasto kwa sauti kubwa sana na kumshangaza ata mpenzi kwake, ambae hakujuwa amjibu nini bwana wake huyu, ambae sekunde xhaxhe baadae akamwona akiinuka toka kitandani na kuanza kuvaa nguo zake haraka haraka, pasipo kupitidha maji mwilini mwake, labda kujiweka safi kwa kitendo alicho kifanya usiku kucha, tayari kulisha kucha, na muda ulisha timia saa moja na nusu, **
Mida ambayo Edgar na Nonalisa ndio walikuwa wanatoka pale guest house, wakiwa wamevaa kama jana, ila Monalisa alisha vaa viatu vya Edgar yani raba, “Edgar kwanini umeamua tuchelewe kutoka namna hii?” aliuliza Monalisa, wakati wana tembea kwenye korido, huku akimfwata Edgar alie ongoza kuelekea kwenye mlango wa kutokea nje, ya hii guest bubu, “unajuwa wale jamaa watakuwa wamekesha wakitutafuta, sasa watategea kuwa, lazima sisi tutaondoka mapema sana, kuelekea Songea, hivyo, lazima wameenda sehemu zote ambazo wanahisi wata tupata kilahisi” alisema Edgar huku anafungua mlango, na kuchungulia nje, kama vile anaangalia usalama wao, wakati huo bastola yake alikuwa ameisundika kwenye kiuno, akiibana na suluali yake ya jinsi, “sehemu kama zipi?” aliuliza Monalisa, ambae alisha pata uakika kuwa Edgar hakuwa na chuki na yeye, “kama stendi au kwenye vituo vidogo vya kupandia magari, alijibu Edgar ambae baada ya kuchungulia nje na kuona kupo salama, aka toka nje, akifwatiwa na Monalisa, ambae sasa alitembea vizuri, siyo kama jana usiku,
Walitembea atuwa chache kidogo baada tu ya kutoka pale guest, mala waka stushwa na sauti ya mtu toka nyuma yao, “wapendwa naona mme enjoy usiku wenu” wote waka stuka na kugeuka, ilikuwa sauti ya kike sauti ya mwana dada, ambae ata walipo mtazama awakuweza kumtambua kwa haraka, “umeni sahau Edgar, mimi si yule nile wauzia dawa usiku” alijitambulisha dada huyu ambae tuna pata kumbu kumbu kuwa ni Rehema haule, dada muuza duka la dawa, “ok! nime kukumbuka ilikuwa usiku” alisema Monalisa, lakini Edgar akatulia akimtazama huyu dada kwa umakini zaidi, maana alihisi hatari juu ya huyu mwanamke, “lakini sikukutajia jina langu” alisema Edgar, huku akimkazia macho yule dada, ambae alitabasamu kidogo, “Edgar bwana, unazani kukufahamu ni tatizo, ebu tazama kwenye ile nguzo ya umeme” alisema yule dada yani Rehema akionyeshakidole kwenye guzo moja ya umeme iliyo kuwa karibu yao, Edgar na Monalisa waka tazama ile nguzo, macho yao yakaona karatasi jeupe lenye picha ya Edgar, iliyo chapishwa kwa rangi nyeupe na nyeusi, “jambazi Edgar Eric Mbogo, anatafutwa na Polisi, kwa kosa la utekaji nyala, yoyte ataye muona, atoe taarifa kituo chochote cha polisi” Monalisa alisoma maneno yaliyo andikwa kwenye karatasi hilo, najuwa mnasingiziwa sababu jana niliwaona mkiwa pamoja, kwa taarifa yenu polisi ni wengi sana huko mjini, hamtaweza kupita huko, kuna gari lipo hapo nyuma twendeni niwatoe nje ya mji, ili mkatafute usafiri, na sijuwi mnaelekea wapi” alisema Rehema, na kuwafanya Edgar na Monalisa watazamane, nikama walikuwa wanaulizana jambo flani, kisha Monalisa aka itikia haraka kuwa wana itaji msaada wa Rehema,
Aikutumia muda mrefu tayari walikuwa ndani ya Toyota crester muundo wa zamani, wakiwa wamekaa seat ya nyuma, wakipita kwenye chochoro za mitaa, kuelekea nje ya mji, wa makambako, upande wakusini, “Mona tumeingia kwenye hatari kubwa sana, na inabidi tuwe makini sana” alisema Edgar, kwa sauti tulivu lakini hisiyo na uoga, “Edgar mwenzio naogopa nime waona wana muuwa yule mkaka” alisema Monalisa, aliekuwa anatetemeka kwa uoga, “utakiwi kuogopa, naimani ukinisikiliza ninavyosema, tutafika songea tukiwa salama, vinginevyo lazima watatukamata na kutuuwa” alisema Edgar, huku Rehema akifwatilia maongezi yao, maana hakuwa na wazo kuwa, mkasa huu wa kina Edgar unausiana na mkasa wa Lukas, “Edgar, naomba unisaidie kama zamani” alisema Monalisa ambae amani ilisha toweka moyoni mwake, wala usiwe na wasiu wasi, ila kumbuka kuwa mimi ni sawa na yul;e kijana walio muuwa, na wewe ndie kile wanacho kitafuta” nikama Rehema alie jitolea kuwasaidia vijana hawa wawili aliohisi kuwa ni wapenzi, alizidi kuvutiwa na maneno ya vijana hawa, lakini alishindwa kuhoji zaidi,
Sasa walikuwa wamesha fanikiwa kutoka nje ya mji, na kuingia barabara kuu iendayo Njombe na Songea, walitembea kwa mwendo wa kilometakama kumi natano, wakikipita kijiji cha utwango, na kuingia mstu unao tenganisha mji wa Makambako na Njombe, ndipo Rehema aka wa simamisha gari, “naona hapa pana watosha, nikisema nisogee mbele zaidi nitashindwa kurudi Makambako, mafuta yataisha” alisema Rehema hapo wakaachana, na Rehema akageuza kurudi Makambako, huku wakina Rehema wakimshukuru sana,
Edgar na Monalisa walisimama pembeni ya barabara, hali ya hewa ilikuwa ni baridi kali, asa misa hii ya asubuhi, wawili hao walio walianza kusubiri magari yaendayo Njombe, ukweli magari hayo yalikuwa machache sana, walijaribu kusimamisha kila lililopita, liwe binafsi au la abiria, lakini kitu cha hajabu magari hayo yalioonsha dakiki ya kusimama, kwa kuopunguza mwendo, lakini yaliongeza mwendo mala tu baada ya kuwasogelea karibu yao, lakini kwao ulikuwa kama mchezo flani, maana waliongea na kutaniana huku wakicheza kwa furaha, pale pembeni ya barabara “Edgar naomba koti, mwenzio najisikia baridi” alisema Monalisa huku akianza kumvua Edgar jacket, hawakujuwa kuwa kuwepo pale barabarani ni hatari kwao, sababu tangazo la kutafutwa kwao limezagaa sehemu nyiongi sana, ***
Mida hii mtutuma Said, alisha achiwa na kuendelea na safari yake ya mbeya, huku wakina Stella pia wakiondoka mapema sana kuelekea Iringa, pasipo kujuwa kinachoendelea juu ya Edgar na Monalisa,***
Mji wa makambako asa maeneo ya stendi kuu na maeneo ya karibu, palikuwa pame chafuka, maana polisi walikuwa wengi wamezagaa mjni wakiendesha msako mkali sana, kuanzia stendi kuu mpaka mitaani na maeneo ya barabara karibu na mjni, na sasa walikuwa wanatumia redio call, katika mawasiliano yausuyo opetaion hii,
Wakati wanaendelea kuwasaka abiria wanao ingia kwenye mabasi, yaendayo Njombe, mala sajent Kibabu akapata taarifa ya kuwa watu wanao tafutwa wameonekana mpakanikambako na Njombe, taalifa hiyo ili mfanya sajent Idd Kibabu atabasamu kwa ushindi, “kifo chao kimewasidia washenzi hawa” alisema Kibabu, wakati huo wakiwa ndani ya gari lenye askari kibao, linalo fwatiwa na gari jingine, lililokuwa linakusanya askari wanao usika kwenye msako kila lilipo wakuta, huku wakiwa na bunduki zao mikononi, itaendelea…………. hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU