BIKIRA YA BIBI HARUSI (16)

SEHEMU YA KUMI NA SITA
 .
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: taalifa hiyo ili mfanya sajent Idd Kibabu atabasamu kwa ushindi, “kifo chao kimewasidia washenzi hawa” alisema Kibabu, wakati huo wakiwa ndani ya gari lenye askari kibao, linalo fwatiwa na gari jingine, lililokuwa linakusanya askari wanao usika kwenye msako kila lilipo wakuta, huku wakiwa na bunduki zao mikononi, ENDELEA……….
Kwa wenyeji wa mji wa Makambako, walio kuwa wana ishi maeneo ya barabarani na wale walio kuwa wanapita njia kuelekea mjini, walishuudia magari mawili ya polisi, yakiwa speed kali sana kuelekea upande wa Njombe, huku taa kubwa za mbele za magari hayo zikiwa zime washwa, magari yote ya kiraia yalikaa pepembeni kupisha magari hayo ya porisi yaliyo beba askari polisi wenye bunduki mikononi mwao, kuna baadhi ya raia walishangilia na kupiga mbinja, (miruzi) kwa hamasa, wakizani kuwa polisi wapo katika kazi zao za kawaida. kumbe wanaenda kuwaangamiza vijana waisio na hatia.**
Ilisha timia saa mbili asubuhi, siku hiyo hiyo ya jumamosi, mji wa songea, mida ambayo kanali Joseph Kisona, alikuwa aanashuka kwenye gari lake la kazini, nje ya jengo kubwa la polisi mkoa wa Ruvuma, akimwacha dereva wake ndani ya gari, akitafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari hilo, yeye aliingia ndani ya jengo hilo, akiwa amevalia nguo zake za kazi, aina ya combat, wengi wana penda kuziita, nguo za mabaka mabaka, huku mabegani mwake akining’iniza vyeo vyake vilivyo mtambulisha kuwa ni kanali wa jeshi la ulinzi.
Bwana kisona alionekana akitembea kwa haraka sana, yani nusu kukimbia, akipandisha ngazi kuelekea ghorofa ya pili, ya jengo lile lenye ofisi nyingi za wakuu wa polisi mkoa, huku njiani akipishana na polisi walio msalimia kwa kumpigia salut, nae alizipokea huku akizidi kupandisha ngazi, mpaka alipozimaliza nakuelekea moja kwamoja kwenye mlango ulio andikwa, RCO, aka kutana na mapokezi ndogo, ambayo ndani yake kulikuwa na binti mmoja mdogo mdogo, alie valia kiraia, ambae alisimama molamoja na kumsalimia bwana Kisona, “shikamoo afande” bwana kisona aliitikia na kuomba kuonana na mkuu wa upelelezi, ambae kitengo chake ndicho kilicho kuwa kina simamia uchunguzi wa tukio la NMC,.
Yule askari wakike yani WP, akaingia ofisi ya ndani kabisa, ambako akukaa sana akarudi na kumweleza Kisona kuwa anaweza kuingia, kwenda kumwona ASP Manase Kingarame, hapo bwana Kisona akaingia ofisini kwa bwana Kingarame, “hoooo! kanali Kisona, karibu sana, nazani utakuwa una lolote la kunijulisha, au vijana wame ingia tena eneo la jeshi?” alisema bwana Kingarame kwasauti ya uchangamfu mkubwa sana, uchangamfu ambao ulikuwa unatafsiri mbaya kwa bwana kisona, ambae toka ameamka leo akuwa na chembe ya tabasamu, “asante sana bwana Kingarame, nimekuja kukupa hongera kwa vijana wako kuweza kumwangamiza kijana Lukas” alisema Josseph Kisona, huku ana kaa kwenye kiti mbele ya meza ya bwana Kingarame, ambae alistuka kidogo, lakini alijitaidi kuzuwia mstuko wake, usionekane wazi wazi, mbele ya Joseph Kisona, “asante bwana Kisona, ni majukumu yetu kuakikisha tuna zuwia uarifu, au kuwa thibiti waarifu kama hawa” alisema bwana Kingarame kwa sauti flani iliyo onyesha mashaka mashaka kwa ujio wa bwana Kisona, maana alimwona akimtazama kwa umakini sana, mtazamo ambao hakuwai kutazamwa akiwa katika cheo hiki alicho nacho.
“bwana Kisona nazani kuna kilicho kuleta asubuhi hii, unaweza kuniambia nijuwe kama nina weza kukusaidia, ili niendelee na mambo mengine” alisema bwana Kingarame ambae kwa umri, ilifaa kuwa baba mdogo kwa bwana kisona alie pata cheo akiwa kijana mdogo sana, “nikwelii kuna kitu kime nileta, lakini inaweza kukusaidia wewe, au taifa kwa ujumla, nasiyo mimi ninae tekeleza wajibu wangu” alisema bwana kisona kwa sauti tulivu, huku akimkazia macho bwana Kingarame, ambae nikama akuip0enda ile kauri ya Kisona, maana aliiona nikama ina mkejeri, “ok! bwana mdogo naomba unisaidie, japo sikumbuki kama niliomba msaada kwako” lilikuwa jibu la kejeri la SSP Kingarame, ambae alisha hisi kuwa Kisona anatilia mashaka juu ya swala la Lukas, ila alicho juwa ni kwamba kijana huyu awezi kupata ushaidi, “napenda kujituma kabla sija tumwa” alisema Kisona akiwa anamtazama Kingarame kwamacho makavu, ambayo hayakuwa na dalili ya utani ata kidogo, Kingarame aka tulia kumsikiliza.
“kwanza kabisa, inabidi uwe makini na askari unao watumia katika operation hii, maana naimani wame muuwa mtu ambae hakuwa na silaha yoyote” alisema Kisona, akiendelea kumtazama bwana Kingarame, ambae muda wote alikuwa anakwepesha macho yake yasikutane na macho ya Kisona, “lakini yule nijambazi na mkuu alisha sema ikibidi kuuwawa, auwawe, maana alisha fanya uarifu mkubwa sana” alisema Kingarame, kwa kujiamini, kana kwamba vijana wake wapo sahihi, “kumbuka kesi yoyote usibitishwa mahakani, vinginevyo apambane na polisi, tena awe na silaha” alisema bwana kisona, “ata kujaribu kulikimbia jeshi la polisi pia anaweza kuuwawa” alisema Kingarame kwa ukali kidogo, “anaweza kufanya hivyo kwa kuokoa maisha yake pia” alisema Kisona kwa sauti ile ile tulivu, iliyo mkela Kingarame, “kwahiyo kama jambazi linaokoa maisha yake, aachiwe aondoke?” alisema Kingarame kwa ukali, kama mawanzo, yani ilikuwa kama malumbano hivi, “lakini siyo kila anae kuwa eneo la tukio ni jambazi” alisema Kisona alie onyesha kuwa mwenye uchungu na Lukas, “kama angekuwa raia mwema, angejisalimisha polisi” alisema Kingarame kwa sauti ile ile ya ukari ambayo sasa ilionyesha kiburi ndani yake, Kisona akatabasamu kidogo, “unazani kwa nini akujisalimisha polisi, au vijana wako walijuwaje kama yupo kule chandamali?” aliuliza Kisona huku tabasamu la kejeri likionekana usoni mwake, “dah! ingekuwa vizuri tunge mwuliza bwana Lukas, lakini bahati mbaya, kwasasa ni marehemu” jibu la Kingarame lilikuwa mwiba kwa Kisona, ambae alichomwa ndani kwa ndani, akijizuwia kuonyesha wazi wazi kuumizwa na kauri ile, wapiganaji wanasema, usimwonyeshe adui yako maumivu yako, bdala yake Kisona alicheka kidogo, kicheko ambacho tafsiri yake aikuwa wazi, kama ni cha uchungu au cha dharau, “nikweli bahati mbaya kwa maisha yake, maana ingependeza sana kama angebahatika kuona mwisho wakazi aliyo ianzisha” kauri hii ilimstua Kingarame, ambae alistuka wazi wazi na kumtaza Kisona, ambae alikuwa anainuka toka kwenyekiti, akionyesha anajiandaa kuondoka, “kanal inaonyesha unataka kulipaka matope jeshi la polisi, maana kauri zako sizielewi” alisema Kingarame na yeye akisimama, kama alivyo simama Kisona, ambae alicheka sana kwa maneno ya Kingarame, “silipaki tope jeshi la polisi, ila nataka kulisafisha, maana kuna watu wana taka kulipaka tope” alisema Kisona, kwa sauti kavu isiyo na chembe ya kupoa poa, labda yupo kwenye ofisi ya watu, “kwa hiyo kijana unataka kuniambia ni kosa kumuuwa yule jambazi alie uwa polisi wanne, na kuiba mali za wananchi?” ilikuwa sauti iliyo shiba ghab, toka kwa Kingarame, “unazani Kijana mmoja, anaweza kuwasogelea polisi wenye SMG, na kuwakusanya sehemu moja, kisha kuwamiminia Risasi?” aliuliza Kisona, kwka sauti tulivu kama kawaida yake, “unajuwaje kama alikuwa peke yake?, pengine alikuwa na wenzie” aliuliza Kingarame, kwa sauti ile ile ya juu, yenye jazba, lakini Kisona alitabasamu kidogo, kisha akatazama chini, kama vile anawaza kitu flani, baada ya sekunde kadhaa akainua kichwa na kumtazama Kingarame, “hupo sahihi hakuwa mtu mmoja, walikuwa watu wengi wenye silaha, nizaidi ya huyu Lukas, alie kuwa ameshika kamera ya video, na kuchukuwa uushaidi uliomsababishia kifo” alisema Kisona, kwa sauti tulivu nikama alikuwa ana ongea na rafiki yake.
Hiyo ilikuwa kauri ya mwisho ya bwana Kisona, ambayo nikama ilimziba mdomo bwana Kisona, maana alikaa kimya kabisa, akimtazama Kisona ambae simama akitazama chini kwa sekunde kadhaa, kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni, pasipo kuaga, akafungua mlango na kuondoka zake, akimwaacha bwana Kingarame, akiwa amesimama mbele ya meza, anamsindiza kwa, mpaka alipomwona mepotelea nje ya ofisi, hapo ndipo bwana Kingarame aka jikarisha kwenye kiti chake, kwanguvu kama vile mtu alie choka sana, kisha akagonga ngumi mezani kwanguvu sana, “pumbavu sana huyu bwana mdogo, inabidi nimzibiti mala moja” alijikuta akisema kwanguvu bwana Kingarame, ama King kama anavyo itwa na vijana wake anao shirikiana nao kwenye maovu.**
tukiwa bado Songea, pande za Luhuwiko, gari aina ya Suzuki Maruti, lilipita kwa speed kwenye njia ya vumbi ya mtaa wa uzinguni, (sikuizi silisikii jina hilo, zamani lilitumika kwenye mitaa tulivu yenye watu wenye uwezo,) na kutimua hilo vumbi ambalo kwa huku songea ni kawaida sana kuwa na vumbi la namna hii, ila kilicho washangaza watu ni hii speed, maana licha ya kumfahamu vyema kijana anae endesha gari ili, kuwa ni mkorofi na wenye fujo sana, lakini leo iliwashangaza, ukweli akukuwa na dereva alie wai kuendesha gari kwa speed kama hii, katika njia mbovu kama hii.
Erasto aliekuwa anaendesha gari hilo aina ya Suzuki Maruti, alipita nyumbani kwa kina Monalisa, mchumba wake, anae tarajia kumvesha pete jioni ya leo, akaona pilika pilika ndio zinaanza, watu walikuwa wana tengeneza mahema kwaajili ya watu kutumia kwenye sherehe itakayofanyika jioni, kijana huyu ambae bado ile ndoto iliyo mwamsha asubuhi yaleo, pale mwembeni guest house. aliendesha gari kwa speed huku njiani akikosa kosa kuugonga bata na kuku wa watu, na alipofika kwao na kusimamisha gari alishuka hara na kuingia ndani, akishindwa kumsalimia baba yake alie kuwa sebuleni ana sikiliza habari toka magazetini, ambazo bahadhi yake zilikuwa ni zile za kuuwawa kwa kijana Lukas, mzee Richard Misago aliduwaa na kumsindikiza mwanae kwa macho mpaka alipo potelea chumbani, hapo mzee huyu alitulia kidogo, akijiuliza kilicho msibu mwanae, ambae leo alikuwa anatarajia kumvesha pete ya uchumba, “au anatatizo na mchumba wake?’ alijiuliza baba Erasto, lakini ilikuwa sawa na kuuliza kiziwi, maana akukuwa na mtu wa kumjibu, hivyo aka inuka na kwenda chumbani kwa mwanae, ambae alimkuta amejilaza kindani, mikono kisogoni, akionyesha kukosa amani kabisa, “Erasto vipi unatatizo lolote” aliuliza baba Erasto, huku na yeye akianza kuingiwa na wasi wasi, hapo Erasto akaanza kusimulia kilichomsibu.
“hahahahaha!” alicheka sana mzee Misago baada ya kiajana wake kumaliza kusimulia jinsi ndoto yake ilivyo mchanganya, “we! mpuuzi kweli, sasa ndoto ndio inakufanya uwe hivyo, ebu nenda kaoge upumzishe hakiri, usije uka tuaibisha baadae” alisema mzee Misago na kutoka nje ya chumba akipishana na mke wake, ambae alikuwa anakuja mbio mbio chumbani kwa Erasto, “huyu mtoto yupo salama kweli, maana nimemwona anaendesha gari utasema la kubeba wagonjwa” aliuliza mama Erasto, kwasauti yenyeshauku na wasi wasi mwingi, na baba Erasto akaanza kwa kuheka, kabla ajaanza kumsimulia mkasa wa mwaane. ***
Wakati songea yana endelea hayo, kati kati ya mji wa Makambako na Njombe, katika bara bara kuu, iendayo Njombe na Ruvuma, mwanzoni mwa msitu wa miti, iliyopangwa kwaajili ya kuvuna mbao, yalionekana magari mawili ya polisi yakichapa mwendo kisawasawa, yakielekea upande wa Njombe, huku gari la mbele likiongozwa na sajent Idd Kibabu, ambae wakubw wake wakazi wana mwmamini katika utendaji wake, uwa ashindwa kwenye jukumu lake la kazi analopewa, “maliza speed Kado, tuwai kabla hawajapata gari” alisistiza sajent Kibabu akimwambia dereva wake Kadu kadu, ambae aliongeza speed akifwata maelekezo ya afande wake.
Lakini wakiwa katika mwendo mkali, ghafla Kibabu akawaona vijana wawili, yani wakike na wakiume wakiwa pembezoni mwa barabara, ambao waliwapita kwa speed, na wakati huo huo, akasikia sauti toka nyuma ya gari, “afande walepale tunawapitaaaa” ilikuwa sauti ya Charles, aliekuwa nyuma ya gari lile, pamoja na wenzake,
Gari lilionekana likisota kwanguvu, na kuyumba, ni baada ya Kadu kadu kukanyaga bleack za ghafla, zilizo sababisha na lile gari la nyuma yao pia likakmate bleack kama hizo , likisota pia nusu ya kuligonga lile gari la mbele, na baada ya kusota kidogo, magari yale yakafanikiwa kusimama, yakiwa yame waacha wale vijana umbali wa mita mia mbili, na kuanza kurudi nyuma, kwa speed kuwafwata wale vijana, wawili ambao sasa walikuwa, nikama wame shikwa na bumbuwazi, “wapigeni Risasi” alipaza sauti sajent Kibabu ambae alikuwa amegeuza shingo yake kutazama nyuma, akitumia kioo cha gari kilichopo nyuma ya kichwa cha gari hili, na kuweza kuona vijanawake wakiinua silaha zao na kuzikoki, kisha wakaanza fyetua risasi, kuelekea kwa wale vijana waliobeba vibegi vyao mgongoni, yule koplo ambae alikuwa na askari wa hapa hapa Makambako, aliekuwa anaitwa John Mapombeka, alishangazwa kidogo, na kitendo kile, huku askari wake waliokuwa nyuma ya gari, nao walianza kushambulia kwanguvu.
pah! pah! pah! ilisikika milindimo ya risasi, kutoka kwenye SMG za wanausalama wa raia, lakini sekunde chache zilizo pita tayari Edgar niakama alishajuwa kitakacho fwata, maana alisha mkumba Monalisa, na kuanguka nae, kwenye mtaro wa pembeni ya barabara, mraro ambao nikama ulisha sahaulika, na alimashauri zote za Njombe na Makambako, maana ulikuwa na nyasi ndefu pembeni yake, lakini polisi waliendelea kumimina risasi eneo lile walilo angukia wakina Edgar, magari yote mawili yalisimama na wale askari wakiwa wameacha kushammbulia waka shuka kwenye gari na kukimbilia pale waliopo angukia wakina Edgar, wakitegemea kukuta watu walio toboka toboka, kama machujio,
askari polisi walipofika mahali pale, wote wakashangaa, wakishindwa kuamini macho yao, maana mahali pale palikuwa peupe, hapa kuwa namtu yoyote, lakini waliona alama flani flani za nyasi zilizo lala, kuelekea upande ule walio toka, hapo wote wakatazama upande ule, ile wanainua macho yao waka waona Edgar na Monalisa, wakiwa umbali wamita kama hamsini toka walipo wao, na sasa haraka haraka, walikuwa wana toka kwenye mtaro wa barabara, na kuingia porini kwenye msitu wa shamba la miti yambao, “mnashangaa nini shambulieni”alisema Kibabu na wale askari wakaanza kushambulia kwa fujo, lakini ilikuwa kazi bule, maana tayari wawili hawa walisha zama kwenye msitu wa miti ya mbao, “achene kushambulia acheni kushambulia” alipiga kelele koplo John Mapombeka, yule walie jiunganae huku huku Makambako, askari wakaacha kushambulia, “koplo kwanini nunawazuwia kushambulia?” aliuliza sajent Kibabu, kwasauti ya ukali, na kabla koplo John ajajibu, sasjent Kibabu aka ongeza swali jingine, au kunaviongozi wangapi hapa?” Kibabu alionyesha kukasilishwa sana, “samahani afande, lakini yule kijana mtekaji, yupo na huyo binti, wanaweza kumshambulia na yeye” aliisema Mapombeka, ambae yeye na askari wake, awakujuwa kinacho endelea, hapo sajent Kibabu aka mkazia macho ya ukari koplo Mapombeka, kisha aka mwambia, “fwata maelekezo koplo” alisema Kibabu kisha akageuka na kuwatazama askari wote waliokuwa wanawatazama, “ingia ndani ya pori, akikiisheni msako mkari unafanyika, kibari cha kupiga risasi kimetolewa” alisema Kibabu na hapo askarai polisi wakavamia pori kwa fujo, itaendelea…… hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata