
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: “huyu mbona ananitazama sana, au anataka kunikumbushia mambo yake ya zamani?” aliwaza Monalisa, huku nayeye anamtazama Edgar macho yao yakakutana, wote katabasam, nikama Monalisa alihisi kitu kwenye tabasamu la Edgar, “sijuwi ajuwi kuwa mimi nimchumba wa Erasto?” aliwaza Monalisa akihisi kuwa, pengine inaweza kuwa tatizo, endapo Edgar atagundua hilo, endelea………
“nazani unaitaji kupumzika sasa” alisema Edgar, huku akiyaondoa macho yake kwa Monalisa, ambae alishusha pumzi na kutabasamu, “kweli Eddy yani nimechoka mwenzio” alisema Monalisa, huku Edgar akitazama huku na huku, akitafuta sehemu nzuri ya kupumzika, sehemu ilikuwa na miti midogo midogo, ya hasiri, na vichaka vyenye nyasi kavu, huku Monalisa akimtazama kijana huyu ambae aliwai kuwa rafiki yake mkubwa sana, hapo zamani, baada ya kukutazama kidogo, Edgar akavutiwa na mti mmoja mrefu kihasi, juu ya mwinuko mdogo, ulio zungukwa na vichaka vifupi, pasipo kujuwa kuwa, mita kama mia mbili mbele yao kulikuwa na barabara. iendayo vijiji vya Kihengu, mpaka mbuga kubwa inayo unganisha na mkoa wa Ruvuma, ikitokea mstu wa serous, mpaka vijiji vya Chitanda,****
kolomita tano nyuma yao, yani toka walipo wakina Edgar, walionekana askari polisi kumi walio ongozwa na PC Khassim, wakija upande huu waliopo wakina Edgar kwa mwendo wa taatibu ulio ashiria uchovu flani, ni kutokana namazingira magumu waliyo fanyia kazi.
Askari hao walisonga mbele taratibu, wakifwata alama za miguu na nyasi zilizo lala, huku wakiwa wamegawana mawazo na sababu za kumsaka Edgar, wakati wale wa kutoka Makambako, walikuwa na nia ya kulipiza kisasi kwa kupoteza askari wao wawili, pasipo kujuwa kuwa, askari wenzao kutoka songea, walikuwa wanawaza, kuipata tape ya video kisha kwenda kupata mgao wao wafedha, ambazo waliamini kuwa, zitakuwa fedha nyingi sana.
Upande wapili Sajent Idd Kibabu alikuwa amekaa seat ya mbele ya gari ili la polisi, lililokuwa alinatembea taratibu kwenye barabara hii ya vumbi, iliyo katiza kati kati ya mapori, huku polisi wengine wakionekana nyuma ya gari hilo, ambalo sasa lilisha uacha msitu wa miti yambao, na kuingia kwenye masitu wa hasiri, huku sajenti Kibabu na askari wake, wakikodoa macho kwenye mstu ule, wakitazama tazama, kutafuta mawindo yao, huku wakigawana mawazo na malengo yao, kama wale wa kule polini wanao tembea kwa miguu, “kazi iishe tukagawane vyetu” alisema Kibabu, akimwambia dereva Kado,***
Wakati huo huo Koplo Mapombeka alie kuwa ofisi za kituo kikuu, akikabidhiwa silaha na risasi, pamoja na askari wengine sita, bahadhi ya silaha alizo zipata, ni pamoja na midium machine gun, SMG, UZI GUN, na RPG, pamoja na mabomu mengi ya silaha hiyo ya RPG, bila kusahau mabox mengi ya Risasi, pamoja na vyakula kwaajili ya askari waliopo kule porini.
Hayo yalifanyika baada ya Koplo mapombeka, kutoa taarifa ya vifo vya askari wawili, ambao ilielezwa kuwwa wame uwawa katika mapambano na jambazi Edgar, lililo mteka binti Monalisa, taarifa hiyo ilipokelewa na mkuu wakituo hicho kikubwa, ambae alizituma wilayani, kwa OCD, huku OCD nae akiendeleza kutuma taarifa hizo, kwa kufwata mnyololo wa amri, wenyewe wanaita chain of command,**
Kanal Kisona alistushwa kidogo na ujumbe wa Rehema, aliopewa na mke wake, hivyo akaamua kumpigia simu Rehema mwenyewe, wakati huo ilikuwa saa saba na robo za mchana, “habaei za mida hii shemeji” alisalimia Kisona baada ya Rehema kupokea simu, “sijuwi niseme nzuri au niseme mbaya, maana kuna jambabo limetokea nahisi linausiana na yule mtu alie uwawa jana” alisema Rehema, na kuma mshawasha Kisona, “henhee! ebu nieleze vizuri, kwanini unahisi hivyo?” aliuliza Kisona kwa shahuku, na Rehema akaanza kumsimulia, kuanzia alipo waona wakina Edgar na Monalisa wakija dukani kwake, na kununua dawa za vidonda, pia akaeleza kuwa baada ya muda mfupi toka wameondoka wakina Edgar walio ulizia nyumba ya kulala wageni, wakaja watu wawili walio jitambulisha kuwa ni polisi, na kuwaulizia wakina Edgar, wakidai kuwa Edgar amemteka Monalisa,
“lakini kilicho ni stua ni maongezi ya vijana hawa, baada ya kuwabeba kwenye gari langu, walisungumza kuwa tunaweza kuuwawa, kama yule jamaa, alafu wakasema tena, kuwa huyu mvulana ambae amebandikwa kwenye matangazo, ndie anae tafutwa kama yule marehemu, na yule wakike, ndie kitu wanacho kitafuta” alisema Rehema, “kwahiyo shemeji unataka kuniambia kuwa, ume washushia porini?” aliuliza Kisona kwa sauti ya lawama, “ndiyo shemeji, maana sikuwa na uwezo wakurudi nao mjini, lazima tunge kamatwa, maana wanatafutwa sana hapa makambako, pia sikuweza kuwafikisha makambako, maana mafuta kwenye gari yalikuwa machache” alisema Rehema, ambae aalionekana kujijutia kwa kuto kujuwa mapema, kuwa swala lile, lina mausiano na tukio la jana, la kijana Lukas, “lakini unauakika sehemu uliyo waacha ni salama, watakuwa, hawaja patwa na lolote baya?” aliuliza Kisona, kwa sauti yenye mcheche, “sijajuwa kama wamesha vuka Njombe, kama wame vuka, watakuwa salama” alisema Rehema, na hapo Kisona aliona nivyema kuwa subira kidogo, maana akujuwa vijana hawa kwa sasa watakuwa wapi, lakini hakuwa tayari kuwapoteza kama ilivyokuwa kwa kiajana Lukas,
hapo Kisona akaonelea kabla ya kuelekea nyumbani kwake aende tena kwa brigedia Frasins Haule,alamweleze juu ya hili swala jipya la uwezekano wa vijana hawa wawili kuingizwa kwenye mkasa huu,**
Taharifa za vifo vya askari wawili zilitembea, na kusambazwa kwa kufwa utaratibu mpaka zika mfikia SSP Manase Kingarame, alieuwa anajiandaa kwenda kuongea kwenye Redio ya taifa tawi la hapa mkoani, ambayo wanaitumia sana kutolea taharifa kwa wananchi, taharifa hii siyo kwamba ili mstua peke yake bwana Kingarame, iliwastua pia RPC na jopo zima la wakuu wavitengo wa polisi mkoa wa Ruvuma, uamuzi wa kwanza wa wakuu hao ni kwamba, habari, ya vifo vya askari wawili, isitangazwe kwanza mpaka watakapo kaa na kujadiri,
Na bwana Kingarame akafanya kama ilivyo agizwa, aka elekea kwenye studio za redio ya taifa tawi la songea, kwaajili ya kutangaza kutafutwa kwa jambazi mwingine, alie mteka binti Monalisa Anderson, na baada ya hapo, wawaite wazazi wa Monalisa, kwa mahojiano zaidi, pengine kuna lolote, linaweza kusaidia katika uchunguzi,**
Taharifa za kutekwa kwa Monalisa Anderson, mtoto wa tajili mkubwa mkoani Ruvuma, ziliustua mji mzima wa songea, asa kutokana na matukio mengi ya ujambazi yaliyo usisha mkoa huu, ambao kiukweli aunaga matukio mengi ya namna hii, huku watu wanao mfahamu mtekaji, wakishangazwa na taharifa hii, japo wenye hakiri fupi waliunganisha na matukio ya wivu wa mapenzi.
Shughuri za sherehe zilisitishwa, na familia mbili zika ungana na kuelekea kituo cha polisi, wakiwepo mama na baba Monalisa, mama na baba Erasto na Erasto mwenyewe. “huyu mtoto mshenzi sana, atakuwa amesikia kuwa mwenzie anaolewa na Erasto” alipayuka mzee Anderson akiwa katika chumba cha mahojiano ndani ya jengo la polisi mkoa, akika bwana Anderson alikuwa amjawa na jazba “inamaana kijana huyu alikuwa na mausiano na mwanao?” aliuliza mmoja wa askari, akati ya wawili waliokuwa wana mhoji baba Mona, “aikuwa hivyo kiukweli, ila alikuwa anamsumbua binti yetu toka akiwa mdogo” wale polisi waliandika kila alicho jibu mzee Anderson,
na ukweli majibu ya wote watano yalifanana, maana waliusisha na wivu wa mapenzi, tena Erasto alienda mbali zaidi na kusema “lengo lake anikomoe, anajuwa kuwa Monalisa ni bikira, lazima anataka kumbaka” wakati mwingine polisi walicheka, alakini awakuacha kuandika kila jibu lililo tolewa,
wazazi na wakwe wa bibi harusi mtarajiwa, waliruhusiwa kuondoka, waki aidiwa kuwa watajulishwa kila kitu kinachoendelea, na wao wakaondoka zao wakiwaacha wakuu wapolisi, wakiingia ndani ya chumba cha mikutano, na kuanzisha mjadala, huku mjadala ukiwa mkali sana, maana nikwamba, mtekaji na mtekwaji inaonyesha kuwa, wanafahamiana, na wote ni wenyeji wa songea, na kesi hii inausishwa na mapenzi, lakini wao kama polisi wanajuwa kuwa, kijana Edgar alikuwa anashirikiana na jambazi Lukas, “jamani, kunammoja anaweza kunifafanulia kidogo” alisema RPC, ambae alionekana kuzidi kuchanganyikiwa, juu ya swala hili.
Hapo Kingarame ambae aliona dariri za kustukiwa, kwa mchezo mchafu anao ucheza, akasimama haraka ili kuweka sawa, “afande hapo kuna jambao ambalo tunatakiwa tulifahamu, ni kwamba huyu jambazi alimteka Monalisa kama kinga ya kuto kushambuliwa na polisi, wakati anawakimbia” alisema Kingarame, itaendelea……. wadau siyo kusudio kuchelewesha story, nahisi modem ina tatizo, maana kila siku natumia masaa manne adi matano kui connect ndio ikubari, ila tatizo linafanyiwa kazi, endelea kufwatilia mkasa huu Hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU