
SEHEMU YA 28
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA 27: “waambieni wawe tayari wanakuja” alisema koplo Lusinde, kisha wakaondoa gari kwa speed kari sana, kuelekea mbele, wakikatiza sehemu ile ambayo ilikuwa na kona ya ghafla na mwinuko, huku yle askari alie pewa ujumbe akikimbilia kwenda kwa wale askari walio jiega kwa mashambaulizi, na kuwapa ujumbe kuwa, wawe tayari gari litakalo jitokeza ni la wale wanajeshi wanao wasubiri, hawakujuwa kuwa gari linalo kuja ni la polisi wenzao, tena lilikuwa lina waletea chakula, na sasa lilikuwa linakuja kwa speed kutokea barabara kuu, ENDELEA ……….
Wale askari watano walio, kuwa tayari kwa kushambulia, walipo pewa ujumba huo wakajiweka tayari, huku mitutu na macho yao yote kwenye kona, vidole vyao vikiwa kwenye vifyetulio, wakisubiri kuona gari likichomoza, kwenye kona hiyo, huku sajent Kibabu na wenzie wakiwatazama, kutoka pembeni kidogo, umbari wa mita kama mia mbili toka walipo.***
Dakika chache baada ya wakina Mapombeka kuondoka, kisona alie onekana kutulia kwa muda mrefu, akiwaza jambo,”afande tuwai kuondoka kuelekea huko porini” alishauri koplo Katembo, lakini Kisona akaonekana bado kushumbuliwa na jambo kichwani mwake, “moyo wangu unaangaika sana kuna jambo linataka kutokea” alisema kisona, hapo mzee Mbogo alimtazama Kisona kwa mshangao, “inamaana unamachale au?” aliuliza baba Edgar, kwa sauti flani ya utani, lakini Kisona akuonyesha utani akasema, “namlahumu sana alie nifundisha utambuzi” alisema Kisona, pasipo kuonyesha dalili za kuondoka mahali hapa. ***
Wakati wakina kibabu wana endelea kutazama, mala wakasikia muungurumo wa gari, ukitokea barabara kuu, wote waka tazama upande huo, huku akirini mwao wakijuwa kuwa litakuwa lile gari ambalo walikuwa wana lisubiri, yani gai la jeshi, kutokana na vumbi ambali gari hili likuwa lina timua, walishandindwa kulitambua kutoka mbali, ila gari lile lilipo fikia mita mia moja karibu yao, wakaliona gari la polisi aina ya land rover mia na kumi. hapo wote wakastuka, na kutazamana, “piga honi piga ho haraka” alisema kibabu wakati gari hilo likiwapita kwa speed kari sana, dereva akiwa karibu na mlango wa kuingilia kwa dereva, alifungua mlango na kuikandamiza sehemu ya kati kati ya msukano, na hapo ukasikika mlio mkari wa honi, ulio lia mfurulizo, ungesema ni kwamba ime nock.
Mlio huo wa honi uliwastua wakina Chaz na Dinno na wale wenzie watatu, ambao walijuwa kuwa ni ishala ya kujiandaa kushambulia, sababu tayari walisha sikia muungurumo wa gari, lililo kuwa lina kuja upande wao na wao wakajiweka sawa, na kuvuta pumzi kisha waka zibana, tayari macho yao kwenye vilengeo, wakiukadilia mwendo wa gari, kwa kupima muungurumo wake.
Nikweli wakina Mapombeka walikuwa wana anza kupandisha kipando kidogo chenye kona ya ghafla, ndipo walipo sikia honi kali ya mfululizo “umesikia hiyo?” aliuliza koplo Mapombeka, na hapo Dereva wake aka punguza mwendo kwa lengo la kusimama, lakini tayari alisha ikaribia kona hivyo akuwa na budi kuimaliza kwanza kona, ndipo wasimame, lakini akiwa katika mwendo mdogo, wakasikia mlipuko mkubwa sana, ukifwatia na kitu kama mvumo wa mruzi, kilicho ongezeka sauti kila nukta. kikiashiria kuwa kunakitu kinawafwata, aikutimia sekunde ya pili, tayari waka sikia kitu kizito kikigonga kwenye bonet (mbele usawa wa engine) ya gari lao, na kutokea mripuko mkubwa sana, ulio litupa gari lao, nje ya barabara, na kuangukia upande wa kulia wa barabara, huku ikifwatia mlipuko mwingine sambamba na milipuko midogo midogo, ya bunduki mbili, za aina ya medium machine gun, zilizo kohoa mfurulizo, na kutema risasi kuelekea kwenye lile gari ambalo sasa lilikuwa lime sha pinduka na kuwa miguu juu.
Lilikuwa tukio la dakika mbili, lililo wahacha midomo wazi wakina Kibabu, ambao waliwasha gari hara na kukimbilia kwenye eneo latukio, huku wakina Charles nao wakitoka mafichoni na kuelekea pale kwenye gari ambalo lilikuwa miguu juu, nyang’ang’a, alikutamanika kwa macho, wakanza kufika walikuwa ni wakina Kibabu ambao waliona uaribifu ule walio ufanya, huku wakionekana polisi wenzao wakiwa wametupwa pembeni ya gari, wakiwa awametulia na wengine wakijinyonga nyonga, “haaaa! kumbe wakina afande Mapombeka” alibwatuka askari mmoja ati ya wale watatu kutoka makambako walio shiriki mashambulizi yale, hapo vikafwatia vilio vya hali ya juu, toka kwa wale askari watatu, huku wakina Kibabu Charles na wale askari watano wakisogea pembeni na kuanza kujadiliana juu ya jambo hili lililo tokea mbele yao, wakiwaacha wale polisi wenzao wakiwa wana garagara chini wakiangua kilio,
“jamani nime waita hapa kwa inshi moj tu” alisema Kibabu baada ya kusogea pembeni, na wale askari wake kutka songea, ambao walikuwa wanafahamu mchongo mzima, huku ana chomoa bastora yake na kfunga kiwamba sauti, “tumesha aribu kazi, kinacho takiwa ni kufanya, ni kufuta ushaidi haraka sana, kisha tutangaze shambulizi la yule jambazi” alisema Kibabu huku akiwatazama wale askari watatu, waliokuwa wakiwalilia wenzao, qaliokuwa wana angaika pale chini, “nakweli afande maana huu ni msala” aliunga mkono Charles, huku wakiwatazama wale askari wenzao, “afande bado wazima tuwa peleke hospital” alipaza sauti askari mmoja kati ya wale watatu, ambao sasa walianza kuwapa huduma ya kwanza wenzao, hapo Kibabu akaonysha ishara kwa wale askari wenzie alio simama nao, ambao bila kuchelewa waka koki bundukizao na kuzielekeza kule waliko kuwepo wezao watatu.**
milipuko ya makombora na risasi za mmg zilisikika sehemu nyingi sana, ikiwa mpaka pale barabarani walipokuwepo wakina Kisona, “mme sikia hiyo, pandeni kwenye gari haraka” ilikuwa kauri ya kisona, iliyo wapandisha mala moja kwenye gari na mzee Mbogo akaendesha gari kwa speed kuelekea ulikotokea mlipuko, akika ailikuwa nispeed kali sana, kila ndani ya gari, alishikiria roho yake, na kusema kimoyo moyo, kuwa “endapo tukifika salama, atuta anguka tena na hili gari” ata kisona mwenyewe na fujo zake zote hakuwai kuona mtu anatembea na gari, kwa mwendo huo, “ile hadithi ya safari harusini, ya huyu mzee ilikuwa yakweli” aliwaza Kisona, huku land rover 110, likichanja mbuga vibaya sana, kusogelea eneo la tukio, ambapo dakika chache baadae walianza kuona moshi, na hapo hapo wakasikia pah! pah! pah!, “unajua nini hapo?” aliuliza Kisona baada ya milipuko ya risasi kukoma, mapambano yanaendelea wakati” alijibu Katembo, lakini Kisona akatikisa kichwa kukataa jibu lile, “hyo ni moping up, wana futa ushaidi.
Mvumo wagari la kina kisona uliwawafikia wakina Kibabu, na waliokuwa wamesha watandika risasi wale askari watatu, wakishindwa kuwa malizia wale majeruhi, “jamani gari la jeshi lenyewe ndio hilo linakuja, tukwepe ushaidi, hawa awana maisha awafiki popote” alisema Kibabu huku, wana kusanya silaha zilizotumika kwa shambulizi, anakimbilia kwenye gari akifwatiwa na wenzie, walio dandia gari huku linaanza kuondoka, “hawa washenzi sijuwi walikwamia wapi,
huku nako Kingarame alikuwa amesha sikia milipuko ile, akaamuru dreva wake kuwasha gari waelekee eneo latukio, na wakati wana ondoka waka kutana na land cruzer iliyoenda kulifwatilia gari la Kisona mjini, wakawaonyeshea ishara ya kugeuka, Kingarame alie kuwa na hamu ya kuushuudia mwili wa Kisona, akuwa na haja ya kusimama, alipishana nao wakina koplo Lusinde, ambao waligeuza gari malamoja na kuwafwata wakina Kingarame,
lakini kilicho washangazama baada ya kuanza kuona moshi ulio ashilia kuwa ni eneo la tukio, mbele yao wakaliona gari la kina Kibabu lina kuja mbio mbio, na kwa vile ilikuwa ghafla wakapishana na kwenda kusimama hatua chache mbele, na gari lanyuma lika simama, huku wakina Kibabu nao wakisimama, na kurudisha gari lao nyuma, mpaka usawa wa gari la Kingarame, kisha Kibabu akashuka na kusogea upande wa Kingarame, “afande imetokea bahati mbaya” alisema Kibabu kwa sauti ya chini kidogo, ili wale askari waliokaa nyuma, wasisikie, maana walikuwa ni wakutoka makambako, “kivipi Kiba?” aliuliza Kingarame, kwa saut ya chini iliyo jaa mshangao, na kibabu alkatumia kama dakika mbili hivi kusimulia kilichotokea, na kuitu walichoamua kikifanya, “umefanya vizuri sana, Kiba, maana unge waacha wange tuvua nguo, ebu tuwai tuka shughulikie hilo, ila tangaza jambo kwa askari wa nyuma, na wewe na wenzako ondokeni na hizo silaha, kufuta ushaidi” alisema Kingarame kwa sauti ya chini, “jamani kuweni makini, hapo mbele kuna mapigani yame tokea jambazi Edgar ameshambulia gari letu moja atujuwi kama wenzetu wapo salama” alisema kibabu kwa sauti ya juu, huku anaelekea kwenye gari lake, hapo askari wanne wenyeji wa makambako, waliokuwa kwenye gari la Kingarame walionekana wakianza kukoki bunduki zao, huku Hokololo akiondoa gari, kuelekea mbele akifwatiwa na gari la koplo Lusinde, huku gari la kiba Kibabu, likiondoka kuelekea upande wa mashariki, yani polini zaidi, saa Kibabu alikuwa na askari sita, ukitoa yeye na dereva wake. **
Huku nako tayari Kisona alisha fika eneo latukio, hali ilikuwa mbaya, waliwakuta wale polisi walio waacha barabarani wakiwa wamelala hawajiwezi wana tapa pata, huku bahadhi ya maeneo ya miili yao ikiwa na jelaha makubwa sana, “iliuwa yetu hii” alisema Kisona huku akitazama mazingira na eneo lile, huku askari watatu wakiwa wamekaa mkao wa kimapigano, kila mmoja akitazama upande wake, huku wale akari wawili yani koplo Katembo na mwenzie mmoja wakiwa beba majeruhi na kuwa sogeza barabarani, wakisaidiwa na mzee Mbogo, “inamaana wame pigana wenyewe kwa wenyewe?“ aliuliza baba Edgar, ndio maana yake, tena ikiweze kana wapakizeni kwenye gari muwakimbize hospital ni ushaidi mzuri sana huo,” alisema Kisona ambae alikuwa ana endelea kukagua kagua eneo lile, pamoja nagari lenyewe,
Sekunde cache mbele nik bwana Kisona aliona kitu flani, mita kadhaa, upande wa mashariki, aka geuka haraka, na kuanza kusaidia kuwa pakiza wakina Mapombeka kwenye gari, na walipo maliza akawasitiza haraka sana katembo na askari mmoja, waingie kwenye gari, waondoke haraka kuelekea Njombe, ambako kulikuwa na Hospital kubwa, na hapo wakaingia kwenye gari na kuondoka zao, huku Jisona akisistiza “endesha unavyoweza Mbogo, nakuaminia” dakika mbili baaadae waka yaona magari mawili yapolisi yanayo fanana yakiingia pale, kwenye eneo la tukio, huku Kingarame akionyesha mstuko wa wazi, **
kundi la polisi sita lililoongozwa na PC Khassim, na PC Mike, lilitembea kwa muda wa masaa matatu, pasipo kuona dalili ya kuwepo wakina Edgar na Monalisa mbele yao, mpaka wana tokea kwenye kijiji kimoja kidogo hawa kuwa wame waona vijana hao, wakachukua uamuzi wa kuanza kuuliza kwa wanachi wa kijijikile, kama wame waona vijana wawili, wakike na wakiume, lakini jibu likawa hapana, “Mike, naona tupumzike kidogo, alafu turudi tulipotoka” alishauri Khassim na Mike akaunga mkono na kuwatangazia askari wenzao, ambao walifurahia sana, maana walikuwa wamesha choka sana, hapo kila mmoja aka fungua kizigo cha nyama waliyo panga kupelekea familia nakuanza kula,
Wakati huo upande wapili, ndani ya msitu, kilomita tisa toka sehemu waliyo chepuka wakina Edgar, walikuwa wame kaa chini ya mti mmoja mdogo, wakionekana wana pumzika kidogo, kutokana na kutembea sana, wakiwa na miwa miwili mapera na nyamaya waliyo ifunga kwenye majani ya mgomba, na hapa ndipo waliposikia mlipuko wa kombora, kilomita kama nane hivi mbele yao kidogo, upande wa kulia yani upande wa barabara kuu, “yani utazni kwenye video, milio ya mabomu tu” alisema Mnalisa aliekuwa ame kaa pembeni ya Edgar, alie kuwa ana kata mua kwa kisu alicho kichukuwa kwa wale wawindaji haramu, “nazani umesha zowea sasa” alisema Edgar, na Monalisa akacheka kidogo, “sioni tena aibu,” Monalisa akajibu, lakini ilikuwa tofauti, “mh! kwani wewe una waza nini, siyo hizo aibu zako namaanisha milipuko ya mabomu n a risasi” hapo Edgar akastuka kikofi cha mgongoni, “lione kwanza” hapo kikapita kimya kidogo.
“Hivi Edgar nikikuuliza kitu uta nijibu vizuri?” aliuliza Monalisa akiwa anamtazama Edgar usoni, “kikiwa kizuri jiibu lake litakuwa zuri” alisema Edgar, hapo Monalisa akajichekesha kidogo, “hivi ile chupi uliyo ninunulia ulitaka niivae wakati wa kufanya nini” aliuliza Monalisa huku anacheka cheka, ata Edgar nae akacheka kidogo, “nilikupa kama zawadi, au wewe ulifikilia nini?” aliuliza Edgar, “mh! sawa, lakini sijuwi nilikuwa na waza nini, sikuzote nilikuwa nawaza unione nikiwa nimevaa” alisema Monalisa huku akicheka kidogo, ata Edgar alicheka kidogo, “Mona inamaana uwa unakumbukaga?” aliuliza Edgar jwa mshangao, “siyo ku kukumbuka tu! ata ile nguo nime itunza mapaka leo?” alisema Monalisa huku najichekesha, “mh! acha uongo wako” alisema Edgar na wakati huo huo, wakasikia sauti ya muungurumo wa gari, mita kadha mbele yao, itaendelea……..hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU