
BIKIRA YA BIBI HARUSI (30)

SEHEMU YA 30
ILIPOISHIA SEHEMU YA 29: “sikia Basso mambo yame kuwa magumu, nenda kwa bwana Wamboli Shilinde, mwambie aandae vijana wake wote kumi na saba, alafu nenda kwa yule mhindi tulie msaidia kwenye kesi ya pembe za ndovu, Rajani, akupe gari mbili za kuwasafirishia hao wakina Shilinde, waje huku, sasa hivi isiziidi saa limoja wawe wawmeondoka, uasiku waleo, lazima wawe huku, hii inshu ikivuka kesho tumeumbuka” yalikuwa maagizo mazito yakiharifu kwenye simu ya serikali,endelea……..
Kiukweli SSP Manase Kingarame, alichanganyikiw
a sana, akizingatia kuwa, mpaka sasa hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya, maana alitegemea kuwa, wakisha mpata kijana mpigapiicha Lukas, na kuichukuwa video tape, mambo yangekuwa yameisha, lakini sasa mambo yanazikdi kuwa makubwa, ikwa ni pamoja na kusababisha vifo vya askari polisi wengi, ambavyo yeye akuvijari sana, alicho fiiria ni kwamba makao makuu ya jeshi la polisi, wanaweza wakaitafi kufahamu zaidi, na jambo ambalo linge pelekea kufichuka kwa mpango wake wa wizi wa dhahacu na vutu vingine vya mathamani, kule NMC, “lazima huyu kisona apatikane na hawa washenzi wawili wauwawe, araka sana, vinginevyo ni hatari kwetu” alisema Kingarame, akiwa pembeni ya Hokololo, wakati wakiwa njiani wana enelekea porini,***
“vipi awa jamaa waliwakuta hospital?” aliuliza Kisona mala tu! baada ya kina baba Edgar kushuka kwenye gari, “afande atuja waona hao jamaa, maana tulibadiri uelekeao, baada ya kufika barabarani, tuliwapelekea Makambako base hospital” alisema Katembo huku anapiga saluti kwa cornel Kisona, ambae aliitikia kwa kupiga salut pia, “dah! sasa Katembo umeanza kunielewa, ulipataje wazo hilo?” aliuliza Kisona, kwa sauti yamshangao iliyo changanyika na furaha flani, Katembo aka mtazama mzee Mbogo, ambae alikuwa anacheka kichini chini, “nihuyu mzee ndie alie toa wazo hili” alisema Katemba, akiwa bado anamtazama mzee Mbogo, Kisona nae akamtazama mzee huyu, “ni moja ya hasara kubwa iliyopata serikali kumstaafisha mtu kama wewe” alisema Kisona akiwa ana maanisha kweli kweli,
Wakati huo wale askari Polisi wanne wa makambako, walikuwepo mahali pale wakiwasikiliza makamanda hawa wakijeshi, huku vichwani mwao wakitafakari maswali ya bwana Kisona, na majibu yao, ambayo nikama yalikuwa yanawafungua hakiri zao, “ok! kitu cha msingi tusichelewe, tuelekee kule tulikopanga kuanzia”alisema Kisona, na baada ya kuongea hayo yeye akawageukia wale askari polisi, akiwaacha askari wake wana ingia kwenye gari, “sasa wakubwa, ngoja sisi tuendelee na majukumu yetu” alisema kisona kwa maana ya kuwaaga, nao wakawatakia safari njema, nao wakaondoka zao, wakiwaacha wale askari wana anza kujadiriana juu ya maswali na majibu, wakati wanaongea na Kisona,
Itakosa raha kama nisipo kuletea maswali na majibu ya mahojiano, kati ya bwana Kisona na askari hawa wa makambako,***
Ilikuwa hivi baada ya Kisona kuwashuhudia wakina Kingarame wakiondoka kwa speed na gari lao, na kupotea zao, yeye aka wageukia wale askari ambao walikuwa wameregea kwa majonzi, “poleni sana makamanda wenzangu” alisena Kisona huku akilitazama lile gari lililo pigwa bomu, “ndio hivyo afande, huyu jambazi atakuwa anatumia dawa za kishirikina” alijibu mmoja wao, kwa sauti flani ya majonzi yenye machungu makubwa sana, jibu ambalo lilimfanya kisona aachie kicheko cha mwaka, kilicho washangaza wale askari, “kwanini unacheka? unazani aiwezekani?” aliuliza yule askari kwa sauti ya mshangao, huku wale wenzie, wakiachia tabasamu afifu lililo fifishwa na majonzi, “sina uakika kama inaweza kuwa kweli, labda nikuulize, kwani nini umesema hivyo?” alisema Kisona, huku akimaliza kucheka, “we fikilia afande, yani mtu huyu kila sehemu tunayo mfumania anatutoroka, na mbaya zaidi, yeye ndio anatumaliza, eebu ona, kuna mabomu ya RPG, kunamatundu ya risasi, unazani anauwezo gani mtu huyu?” aliuliza yule askari, kwa msisitizo, hapo Kisona aka jifanya kutazama tena lile gari, “inamaana mnafahamu kuwa huyu jambazi yupo peke yake?” aliuliza Kisona, wakati huo askari wake walikuwa wamezunguka lile eneo, wakifanya ulinzi, “ndio yupo mmoja tu! tumemwona kwamacho yetu,yani uwezi amani, nimtoto mdogo sana” alisema askari mwingine, hapo kisona alitulia kidogo, kisha aka mtazama yule muulizaji wakwanza, “umetazama vizuri hapa ukagundua zimetumika silaha ngapi?” aliuliza Kisona, hapo wale polisi wote wakatazama kwenye lile gari, nikama walikuwa wanatafuta jibu, alafu, polisi mmoja kati ya wale nne, yani kati ya wale wawili ambao awakuongea mwazo, akajibu, “hapa kama sikosi, zimetumika silaha mbili, mmg na RPG” hapo mdau kunakitu inabidi ukigundue, nikwamba jibu la huyu askari lilipatikana kwa msaada wa mazungumzo ya mwanzo kabisa, ya Kisona na Kingarame, “umekosea, zimetumika silaha za aina tatu” aliongwa Kisona huku ana tambea ataua kama tatu hivi pembeni kidogo, akainama na kuokota ganda la risasi, “hii ni risasi ya SMG, ndiyo iliyo wa uwa vijana watatu ukiondoa wale majeruhi, inamaana wauwaji walisogea mpaka hapa, na kuwashambulia ” hapo wale askari wakazamana kwa mshangao, maana nikweli waliyaona maganda mengine ya risasi, “labda nyie hamjuwi idadi ya askari walioenda mjini asubuhi?” aliuliza Kisona, na hapo walea askari wakaonekana kama wamekumbuka jambo flani, “nikweli jamani, afande Mapombeka aliondoka na watu watatu” aliongea mmoja wao, huku wote wakimtazama Kisona kwa mshangao, “sisi tume wakuta majeruhiwanne, na marehemu watatu” alisema Kisona, “hao wengine walichaguliwa kwa kazi maalumu, waliondoka na afande Kibabu” alisema mmoja wa askari hao, huku wote wakionekana kushangaa kidogo, hapo kisona hakuwapa nafasi ya kupumua, akawaliza tena, “huyo jambazi alikuwa na MMG au RPG?” awali ili lilijibiwa haraka sana, askari wote walitikisa vichwa vyao kushoto na kulia, wakikataa kuwa jambazi huyo alikuwa na silaha alizo zitaja bwana Kisona, “sasa mmg amezitoaa wapi?” aliuliza Kisona, hapo askari hawa wakatazamana, kisha wawili waka ongea kwapamoja, yani sauti zikagongana, “sijuwi” mmoja wao akaongezea, “labda kama amezipola za kwetu maana ata smg aliyo kuwa nayo ame ipola yakwetu” jibu hili lilikuwa kama kituko kwa Kisona, “kwahiyo amepola mmg rpg, mbele ya askari polisi saba, na kiisha kuwashambulia?” aliuliza Kisona, hakukuwa najibu,
Kisona alipoona askari wale hawana majibu, akauliza swali jingine, “hivi huyo jambazi mnamsaka kwa sababu gani, na alisha wai kufanya matukio gani?” hapo wale askari wakatazamana tena, kisha askari wakwanza akasema, “wanasema analikuwa anashirikiana na jambazi mmoja hivi alie uwawa juzi usiku” wapili akaongezea, pia kuna demu mmoja hivi ame mteka” hapo akadakia yule wakwanza, “lakini yule demu, aonyeshi kama amemtekwa, maana mpaka demu mwenyewe anatukimbia” Kisona alicheka kidogo, “kwahiyo unataka kusema kuwa, hamajuwi lolote juu ya hii operstion?” aliuliza Kisona huku akiwatazama mmoja baada ya mwingine, akawaona wana tazamana, nikama wanaulizana mwenyejibu nani, “ok! nazani majibu mtayapata kwawle watakao bahatika, maana maana hamjajuwa nani atabaki salama, mpaka mwisho wa jambo hili” lilikuwa kama fumbo flani toka kwa kisona.
mdau hayo ni bahadhi ya maswali na majibu toka kwa kisona, maswali ambayo askari hawa walianza kuya jadiri ili kupoata ufumbuzi wake, “ila inaonekana kunamchezo mchafu wanatuchezea hawa jamaa, wakutoka songea” alisema mmoja wa askari wale, “inawezekana ebu ona jinsi wanavyo tupeleka peleka” alidakia mwingine, huku watatu akiongeazea, “ebu ona walisema wanamtafuta yule jambazi, walie muuwa, sasa huyu dogo ametokea wapi?” kiukweli askari hawa ni kama walikuwa wamepata jibu flani, “jamani nikipata nafasi inabidi niongee na ocd, au OCSS” alisema mmoja wao, na wenzake wakamuunga mkono, ***
Edgar na Monalisa, walitembea taratibu sana, wakipita kwenye nyasi ndefu, na vichaka vya miba, wakishuka kwenye bonde moja la mto mdogo, iliwavukie upande wapili ambao walihisi kuwa, barabara itakuwepo, maana ndio upande ambako sauti ya gari ilitokea, “eddy bwana umenipitisha njia gani sasa” alisema Monalisa, kwa sauti ya kudeka, huku akiwa ameung’ang’ania mkonio wa Edgar, aliekuwa anaongoza njia, Edgar hakuwa na jibu, akabaki kimya, huku anaongoza kwa kuchagua sehemu zakipita.
Kila walipozidi kutembea na kusogelea bonde, ndivyo nyasi zilivyozidi kuwa ndefu, na kuwafikia kifuani, huku vichaka vyamiba vikipungua, “Eddy unakumbuka sikuile tulivyo lowa na mvua, ulinibebaga?” aliuliza Monalisa, likiwa kama swali la mtego, “kipindikile ukiwa mdogo?” aliuliza Edgar, “lione kwanza, kwani ukiwa mkubwa ubebwi?” aliuliza Monalisa lakini sasa kwa sauti yakuchukia kidogo, “we uliona wapi mmama kama wewe unabebwa?” aliuliza Edgar huku safari ikiendelea, “kwani we uonagi kwenye magzati, picha za bwana harusi wakiwabeba bibi harusi wao?” kwa swali hili la Monalisa, lilimfanya Edgar asimame kabisa, na kumtazama Monalisa huku anaachia tabasamu laini lililo mfanya Monalisa ashangae, “kumbe hapa tuna funga ndoa, basi panda mgongoni, kwa mume wako”alisema Edgar huku akiiweka vizuri SMG yake, na kuinama kidogo, lakini baadala yake akastukia kofi la mgongoni, “tabia mbaya hiyo” alisema Monalisa, na kumfanya Edgar acheke kidogo.
Safari ikaendelea, “kwani nilisema mimi, si wewe mwenyewe ndio umesema” alisema Edgar huku wakiendelea kutembea na sasa walikuwa wame bakiza mita kama ishirini kuvuka bonde lile, ambalo lilikuwa na na nyasi fupi, na ardhi ya unyevu unyevu, “hapa afadhari maana nilikuwa naogopa kule kwenye nyasi, na lile joka ulilo liuwa” alisema Monalisa huku anauachia mkono wa Edgar, lakini Edgar kabla hajajibu, ghafla akaonekana ana geuka nyuma, yani walikotoka, Monalisa nae akageuka na kutazama nyuma, wote wawili wakaona nyasi zikitikisika, umbali wa mita kama mia moja toka walipo kuwepo wao, huku mtikisiko huo mpana, ulikuwa una elekea kuja waliko wao, hapo awakuulizana tena, Edgar akaushika mkono wa Monalisa, na kuanza kukimbia, kuelekea kwenye bonde, ambalo mfano wake ni lile walilolima mpunga, na wakati huo huo wakaziona zile nyasi zikianza kutikisika kwa nguvu, ikiponyesha kuwa kuna watu na wameongeza speed, nawao wakaongeza speed, na kuingia kwenye yale majaruba ya mpunga, yenye nyasi fupi, na kujiona wakiingia kwenye maji yenye tope, huku wakizidi kuzama kila walipopiga hatua, wakizania kuwa watavuka.
Lakini bahati aikuwa upande wao, maana yale majaruba yalikuwa yana hasiri ya madimbwi ya maji, yaliyoota nyasi juu yake, ile hatua ya kwanza mpaka ya tano, wakibakiza hatua mbili wakajikuta maji na tobe vikiwa vime fika usawa wakiuno, wakinasa kwenye matope hayo na kushindwa kuendelea na safari, miguu yote ikinasa, Edgar akauachia mkono wa Monalisa, ambae alijuwa kuwa Edgar anamwacha, ilina yeye ajipapatue kivyake, “Eddy usiniache” alipiga kelele Monalisa, huku ana jaribu kuidaka nguo ya Edgar, ambayo ilimteleza kutokana na tope, na Edgar akuonekana kumjari, zaidi alionekana akianza kujitaidi kujitoa kwenye tope, mpaka akaweza “Eddy usiniache, peke yangu wataniua” alisema Monalisa, kwa sauti ya kukata tamaa, ambae bado alikuwa kwenye tope, akimtazama Edgar aliekuwa nje ya tope, akamwona ana geuka nakumtazama yeye, yani Monalisa, ambae alikuwa ameonyesha sura ya kukata tamaha, lakini alipo tazama kule kwenye nyasi tayari polisi walisha sogea karibu kabisa, na walibakiza mita kama kumi tu! kutokea za pale walipo kuwepo wao, ata nyasi ziliaza kusikika zikipiga kelele,
Monalisa akajuwa kuwa Edgar lazima amkimbie.itaendelea……. hapa hapa

