BIKIRA YA BIBI HARUSI (36)

SEHEMU YA 36

ILIPOISHIA SEHEMU YA 35: “hapana Mona, tayari kazi imeanza ebu tazama kule” alisema Edgar, huku ana mwinua Monalisa, toka kwenye miguu yake, na kumwonyesha upande wa magharibi, yani kule waliko tokea wao.
Wote kwa pamoja, wakiwa wanatazama upande huo, wa maghalibi, umbali wa mita kama elfu moja hivi, waliona mianga ya taa za magari mawili, yakija kwa kasi upande wao,endelea ………
hapo wakainuka haraka na kuanza kuchukuwa nguo zao kwenye ile miti waliyo iegesha ili zikauke, bahati nzuri zilikuwa zime kauka, pamoja na vibegi vyao na viatu, kisha Edgar aka mshika Monalisa, mkono huku Monalisa kanga iki mdondoka, wakazunguka nyuma ya nyumba, “aya vaa haraka tuondoke zetu, hapa tufai tena hapa,” alisema Edgar huku akimwachia mkono Monalisa, kisha kila mmoja akaanza kuvaa, pasipo kumwonea mwenzake aibu,
Edgar alikuwa wakwaza kumaliza kuvaa, akamsaidia Monalisa kumvalisha viatu huku yeye ana malizia kuvaa tisheti, dakika tano ziliwatosha, kumaliza kuvaa, “nisubiri” alisema Edgar aki kimbilia ndani ya kile kijumba, akimwacha Monalisa ana vaa begi lake la mgongoni, Edgar akukaa sana mle ndani katoka na jacket moja kubwa sana, tofauti na lile la kwao, aka mdaka mkono Monalisa, “twende zetu” alisema Edgar, huku ana tembea kuzama kichani, nyuma ya kile kijumba, na sasa walisha anza kusikia ngurumo za magari yale, **
Mida hii ya saa nne za usiku, bado watu walikuwa wengi sana bale kwenye ukumbi wa vinywaji na vyakula, Serena hotel, kwa upande wa wakina mzee Anderson walikuwa wamelewa sana, ila upande wa kisona, wale askari wanne walisha lewa, lakini kihasi, mzee Mbogo nae alikuwanywa kihasi akama wakina Kisona na Katembo, ambao bado walikuwa wanapanga vita yao, ya siku inayo fwata, mala wakasikia ngurumo ya gari, ikija pale Hotelini, na baada ya lile gari kusimama, zika pita sekunde chache, wakaonekana Kingarame na yule dereva wake, wana ingia Hotelini, na ndipo wakamwona mzee Anderson anainuka haraka na kumfwata Kingarame, ambae alisimama na kuanza maongezi na mzee Anderso, yani baba Monalisa.
Nikweli, safari hii Kingarame alikuwabari kuongea vizuri na baba Monalisa, ambae alimkimbilia mala tu baada ya kumwona akikatiza, “mzee usiwe na wasi wasi, hivi navyo kuambia, vijana wapo porini, wana msaka huyu jambazi, na uakika mpaka asubuhi atakuwa amesha patikana” alisema Kingarame, kwa sauti ya uchangamfu, “asante sana afande, lakini vipi, atakuwa salama kweli inti yangu?” aliuliza Anderson, kwa sauti yake iliyo jaa ulevi, “kwa hilo pia, usiwe na wasi wasi” alisema Kingarame, huku hokolplp akiwa amesimama pembeni yake, na bunduki yake begani, “nashukuru sana afande, akika nita kuandalia zawadi kubwa sana, ukimpata mwanangu” alisema mzee Anderson kwa sauti iliyo changamka kwa ulevi, “ondoa shaka bwana Anderson, ila ukipata taharifa yoyote, nijuliishe mala moja” alisisitiza Kingarame, kabla wawili awa awajaagana, na wakina Kingarame na Hokololo kuingia ndani, wakielekea mapokezi, “mpatie chumba huyu kijana, kwa siku moja” alisema Kingarame, akimweleza mhudumu wa pale mapokezi, kisha yeye akaondoka zake, akiacha Hokololo anapewa chumba anamba kumi na saba, jilani kabisa na chumba namba kumi na sita cha Erasto, ambae alikuwa ndani ya chumba hicho, ana pena dudu na mpenzi wake mpya, wakishushia na pombe, sijuwi alikuwa anajiliwaza juu ya mchumba wake. Hokololo alipita nje ya chumba namba kumi na sita, huku akisikia sauti za miguno iliyo ashilia kuwa, ndani kuna mtu ana ingiziwa dudu, lakini akuwa na la kufanya zaidi alitebea mpaka kwenye malango unaofwata, na kuingia ndani, akiwa amekodishiwa chumba hicho kwa siku moja tu!.
lakini huku nje kwenye meza ya mzee Anderson na wenzake, i kama walikuwa wame pokea taharifa njema, maana walifurahi sana, baada ya Anderson, kuwaeleza kuwa, Kingarame amesisitiza kuwa mtoto wao yupo salama, na wao wasiwe na wasi wasi, kwakuwa mpaka kesho asubuhi Monalisa atakuwa amepatika.
Kwa upande wa Kisona na kikundi chake, wao waliendelea kusoma mchezo, na mwisho waka shauriana wakapumzike, ili kesho, wajihimu kwenda porini, “maana mambo ya vikundi vikubwa, lazima wachelewe kuingia msituni, hivyo sisi inatupata tuwai” alisisitiza Kingarame,**
Ngigo na kikundi chake, waliokuwa wana jipa moyo, kwa tamaha za fedha walizo aidiwa na Kingarame, walisimamisha magari yao, mbele ya kibanda kimoja wapo, kati ya vingi vya wale wakulima wa viazi, “karibuni jamani, nao siku hizi tuna bahati ya wageni” alisema yule mzee mkaribishaji, ambae baada ya kuwaangalia vizuri wageni wa safari hii, alistuka kidogo, maana sura hizi azikuwa za kawaida, mzee yule aliwatazama wale wageni, ambao licha ya kuwa karibisha kwa uchangamfu, lakini wao awakuitikia kabisa,
Babu, alishuhusia sura za kazi, ukiachilia Ngigo, am,bae sura yake ilipambwa na midevu ambayo iliuzinguka mdomo wote na kujaa kwenye kidevu kama jumba la nyuki, pia kuna sura zilizo tisha zaidi, zikipambwa kwa makovu na mishono mbali mbali, “kuna vijana wawili, tuna watafuta wame kuja huku” aliuliza Ngigo, kwa sauti kavu, huku akimkazia macho babu.
“Unamaanisha wale wanafunzi wawili, waliopotea?” mama mmoja, baada ya kuona babu ame duwaha, “ndio hao hao! vipi mme waona?” aliuliza Ngigo, kwa uchangamfu, “ndio wapo kuleee, Karinga wapeleke” alisema tena yule mama, akionyesha kidole upande wa kijibu cha mwagoda, “hapana, atuitaji mtu” alisema Ngigo, kisha aka waonyeshea vijana wake ishara ya kuondoka kuizunguka ile nyumba, nao bila kuchelewa wakaanza kutawanyika, kila mmoja akipita upande wake, huku akiikoki bunduki yake, wakiwaacha wenyeji wao wakishangaa, “kuna usalama kweli” aliwaza yulle babu, kabla aja waambia watu wake waingie ndani.
vijana walio sogelea kibanda cha Mwagoda, walikuwa kumi wengine wanne walibakia kwenye magari, huku Ngigo mwenyewe akitembea nyuma kabisa ya kundi hili, akifwata njia ya kati kati, huku akiwa shuhudia vijana wake ambao wamesha fanya kazi nyingi za hatari, na kufanikiwa, waliokuwa wana tembea kwenye vichaka kwa tahadhari kubwa, wakikizunguka kibada cha Mwagoda, na walipo akikisha wamekizunguka vizuri, ndipo wawili kati yao, walipo usogelea mlango na kuusukuma, kwa nguvu, kisha wakazama ndani, huku wezao huku nje wakisikilizia milindimo ya risasi, lakini ikawa kimya, na sekunde chache baadaea wale vijana wakatoka, “hakuna mtu” alipayuka mmoja wao, mala tu baada ya kutoka nje, Ngigo aka kimbilia nje ya kibanda hiki, pale kwenye mto, na kuanza kukagua nyayo, “inaonekana walikuwa hapa sasa hivi” alisema Ngigo, kwa sauti ya butwaha, wakati huo huo kuna mmojaa wa vijana wa Ngigo, alitokea ubavuni mwakile kibanda akiwa na vipande vya kanga, nikama alisogea kuzitazama vizuri kwenye mwanga, kisha akazirushia kwenye moto, “ebu sambaeni huko polini haraka tuna weza kuwa kurupusha” alisema Ngigo, huku ana inama na kuchukuwa kuni yenye moto, kisha aka zama kichakani sambamba na vijana wake walio tawanyika eneo lote lile, na baada ya kuembea kama mita mia hivi aka chuchumaa na ma kuuweka ule ukuni, kwenye nyasi kavu, kisha akaanza kupuliza akisaidiwa na kijana wake mmoja.
Aikutumia ata dakika mbili, moto ukaanza kuwaka, na taratibu ukaanza kusambaa, kwenye zile nyasi kavu, “zungukeni kote, kuweni makini wasitoroke” alipaza sauti Ngigo, huku vijana wake wakizidi kusambaa, eneo lile ambali dakika nne mbele, lilikuwa ila onekana wazi, kabisa kutokana na mwanga wamoto ambao sasa, ulikuwa una sambaa kwa kasi sana,
Kumbe Edgar na Monalisa walikuwa mita kama mia mbili mbele, toka walipo kuwa vijana wa Ngigo, na moto wao, ambao uliwawezesha kuwaona vyema kabisa, “hawa siyo polisi” alisema Edgar alie kuwa amechuchumaa nyuma ya kichaka, sambamba na Monalisa, alie kuwa amechuchumaa nyuma ya Edgar, huku kifua chake kikimgusa Edgar mgongoni, na kama chuchu hizi kwa jinsi zilivyo simama, zingekuwa ni sindano, akika zinge mtoboa Edgar, sababu Monalisa alikuwa mmwegemea kabisa Edgar, kisi cha pumzi zake kumpuliza Edgar shingoni, na kumtekenya, “kama siyo polisi, watakuwa wakina nani?” aliuliza Mona lisa huku akivunja kibega, kwenye bega la Edgar, “watakuwa wamekodiwa, maana polisi uwa afugi ndevu kama vile” alisema Edgar huku ana geuza uso wake, na kumtazama Monalisa, “tuondoke kabla moto auja sogea” alishauri Edgar huku ana iweka silaha zake vizuri, na kumshika mkono Monalisa, kisha kwa tahadhari wakaondoka na kuzidi kuzama porini zaidi, wakiwaacha wakina Ngigo wakisambaa eneo lile kuwatafuta, na wakati huo huo ukasikika muungurumo mwingine wagari ukiingia mahali pale, alikuwa ni sajent Kibabu, na askari wake, waliokuja huku kwa lengo la kutafuta sehemu ya kupumzika,***
Saa sita usiku sehemu nyingi watu walikuwa wame lala, ata wakina mzee Anderson, nao walikuwa hoi vitandani kwaajili ya pombe walizo kunywa, bila kuwa sahau Erasto na mwanamke wake, ambao walikuwa hoi, kitandani uchi wa mnyama, wana koroma kama vile matrekta yana lima, ata bwana Kingarame alikuwa amelala pia, akiwa amesha pata matumaini ya kufanikisha zoezi lake, la kuwa pata wakina Monalisa, na kuupata ushaidi wa video tape.
Ila kuna watu ambao awakuweza kulala, usiku huu waleo mpaka siku ina pinduka na kuingia jumatatu, mmoja wao alikuwa ni mama Edgar, ambae muda wote, alikuwa anasali na kuitazama picha ya mwanae Edgar, akishindwa ata kula, maana chakula alikiona kama udongo, akikuwa na radha kabisa, huku mala kwa mala machozi yakimtilika machoni mwake,
Mingine ambae hakuwa amepata usingizi ni mama Kijacho, yani mke wa bwana Mapombeka, ambae alikuwa amekaa pembeni ya kitanda cha mume wake, ambae toka ameletwa hapa hospital ya jeshi, akiwa amepoteza fahamu, huku jeraha lake la kichwani na tumboni kupatiwa matibabu, haja fungua macho mpaka sasa, “mama kutokana na hali yako unaitaji kupumzika, shukuru mungu mmeo aliwaishwa hospital, akika atapona tu!” alisema doctor wa kijeshi, alie kuwa amepewa jukumu la kuakikisha kuwa wagonjwa wale wanakuwa salama,
mke wa bwana Mapombeka ndio mmoja kati ya watu waliopewa kibari cha kuwaona wagonjwa hawa.
Wengine ni makundi ya askari wa songea na Iringa, walio kusanywa kwaajili ya safari ya Njombe, huku wakuu wapolisi mikoa hiyo, nao wakijiandaa kuelekea huko, kufatia maagizo ya mkuu wapolisi tanzania.***
Sajent Idd Kibabu, alisogea porini ambako moto ulikuwa una waka, aka kutana na Ngigo, “tume wakosa kidogo sana” alisema Ngigo akimweleza Kibabu, ambapo alimsimulia jinsi walivyo elekezwa na wenyeji wao, “lakini awezi kuwa mbali, lazaima watakuwa maeneo haya haya, wana watazama tu!” alisema Kibabu, ambae aliwashauri kizidi kusambaa ili wawa tafute, na yeye aka elekea kwenye kijimba ambacho, aliambiwa ndimo walimo kuwepo wakina Edgar, akiwaacha wakina Ngogo wakijipanga na kuazama msituni zaidi kuwasaka wakina Edgar, na silaha zao mkononi.***
Edgar na Monalisa, baada ya kutembea mita kama mia uonse wa mashariki, waka kutana na mto, ambao ulikuwa una tililisha maji mengi sana, wakashindwa kuvuka, hivyo waka rudi upande wa kaskazini, wakiliacha lile eneo la mashambani umbali wa mita kama mia tano hivi, pembeni ya mto, wakisindikizwa na sauti za vyula na vidudu vya mtoni, mpaka alipo fika kwenye mti mmoja mkubwa sana, ambaulizungukwa na mawe makubwa sana ulio tawanya matawi yake na kufwanya kama kuku ane tanua mbawa kufunika vifaranga, “hapa ndio sehemu tutakayo pumzika usiku waleo” alisema Edgar, huku akizama chini ya mti hule, ambao ulitawaliwa na joto flani la kufurahisha, Monalisa nae aka fwatia, wote waka ingia ndani ya fukuto lile la mti, na kusimama kwa sekunde kadhaa, kisha Edgar aka mpatia Monalisa lile koti alilo liiba kwa Mwagoda, “haya lala hapo” alisema Edgar, lakini Monalisa alipokea Jacket, lakini akufanya chochote, “kaa nikulalie, mi siwezi kulala mwenyewe” alisema Monalisa kwa sauti ya kudeka, Edgar aka cheka ule mcheko wa mguno,, kisha aka enda kukaa pembeni ya jiwe moja kubwa, kisha akajigemeza kwenye jiwe hilo kubwa, alafu bila kuambiwa Monalisa akaja na kukaa pembeni yake kisha akalaza kichwa cheke, kwenye kifua che Edgar, ikawa kama nusu ame pakatwa, aiku chukuwa dakika tano, Monalisa akaanza kukoroma, huku akiizungusha mikono yake na kujikamatia mgongoni, kwa Edgar, maziwa ya Monalisa, ambae akuwa ame funga koti lake, yani zip ya koti lake, yaki mgusa Edgar maeneo ya tumboni, Monalisa akikikandamiza kifua chake kwa Edgar, huku nywele zake ndefu zikiwa kelo kwa Edgar, ambae alikuwa ana waza, na kuvuta kumbu kumbu ya matukio yote, yanayo ashiria mapenzi kati yao, “kumbe nilikuwa na mfikilia vibaya, Erasto ndio alie peleka ile barua kwa mama Mona”. **
Mida hii huko porini, Ngigo na vijana wake baada ya kuangaika kwa muda mrefu,pasipo mafanikio, wakaamua kupumzika kidogo, ili pakipambazuka, waendelee na kazi yao, ya kuwasaka wakina Edgar, “ila kumbukeni inabidi iwe mapema kabla wao hawajaamka, ndio tuna weza kuwapata kiulahisi” alisisitiza Ngigo, akiamini kuwa kazi ya kuwa pata wakina Edgar ni ndogo, kama kula kitumbua cha mlevi. ambae aliilaza timu yake pembeni ya mto, “kama inabidi kuvuka mto basi ni hapo asubuhi” alimaliza kwa kauri hiyo ***
Saa kumi na moja za alfajili ni, nusu saa toka magari manne ya polisi, aina ya land rover, mia na kumi, kuingia Njombe, yakitokea iringa, yakiwa yame beba askari nane kila gari, na kufanya jumla yao kuwa 32, ukiondoa madereva na wakuu mbali mbali walio ongozana na RPC, wote wakiwa na SMG zao pamoja na masanduku ya risasi na mabomu.
Mida hii ndiyo mida ambayo, magari matatu toka songea, nayo yaliingia, kama ilivyo kuwa kwa RPC wa Iringa, pia RPC wasongea, aliongozana na wanadhimu wake, yani OC Fild Force na OC CID, huku magari yao pamoja na madereva jumla kila moja lilibeaba askari tisa, na kuwa 27, nao wakiwa full kivita, kwa lugha ya vitani wanaita full battle.
Waliingia kituo cha polisi Njombe na kusimamisha magari yao, wakiwaona wenzao wakiwa wamejipanga mistali, wenyewe wanaita parade, “yani awa washenzi ni kwenda kuwafyekelea mbali, akuna kujari haki za bina damu” alisikika RPC iringa, wakati wale polisi kutoka songea wana jiunga na parade ile, ila kumbukeni kuwa adui zetu wana mashikilia mateka mmoja, na mbaya zaidi, ana silaha kubwa, ambazo wamesha zitumia kuwashambulia wenzetu” alisisitiza RPC iringa, “tuna enda kujiunga na wenzetu waliopo polini, lengoi ni kumpata mateka akiwa hai, na kuwaangamiza majambazi hao, ambao wamesha poteza askari wetu zaidi ya kumi” ilikuwa sauti iliyo jaa uchungu mwingi sana, aliongea mengi sana RPC, Iringa mwisho akisisitiza jambo moja kwa askari wake, “chamsingi kumbukkeni kuwa adui zetu wana mbinu nyingi za kimapigano, hivyo kumbuka kuwa mna tembea na vifo vyeno mikononi, ukizubaha, utang’ata pamba” aliongea RPC Iringa, pasipo kujuwa kuwa hao adui ni vijana wadogo, waliotoka zao chuo, kujiandalia maisha yao ya siku inayofwata, na wameingia kwenye mtego, kwa bahati mbaya, baada ya kuingia kwenye hanga za askari wasio na uadirifu. “ndio afande tuta tekeleza jukumu kadili ulivyo tuagiza” walijibu askari wale zaidi ya hamsini na sita maana kuna askari kama 30 ambao walikuwepo hapa kituoni toka jana usiku, ukiachilia wale waliotoka inga na songea, ambao kila mmoja kichwani kwao, akijaribu kuvuta picha ya hao majambazi wanao enda kuwasaka, huko polini, **
Kisona na askari wake mida hii walikuwa tayari kwa kuingia kazini, maana tayari waikuwa wamesha vaa guo zao za kazi, na silaha zao wakielekea kwenye gari, lakini Kisona aka ingia mapkezi na kuomba simu, kwa minajili ya kupiga kwa mwenzie, aliepo Makambako, sijuwi waliongea nini, maana alitumia dakika kama nne tu kuongea na mwenzie huyo, alafu aka toka nje kuungana na wenzie safari ikaanza, kuelekea polini, ambapo walipishana kama sekunde kumi tu na Kingaramealie enda kumgongea Hokololo, ili waondoke zao kuwai polini, maana ata wenzie walio toka Songea na Iringa, wali amini kuwa SSP Manase Kingarame, yupo porini na askari wake, wanaendeleza msako, hivyo hokololo alipita chumba namba kumi na sita, ambacho mida hii ilikuwa inasikika mikoromo ya kutisha, iliyo pokezana kwa zamu, ikionyesha watu wawili walio lala mle ndani walikuwa wame lewa sana jana usiku.
King na kijana wake Hokololo awakutumia muda mrefu sana, nao wakaanza safari kuwai porini, ili wakapate mnajibu sahihi, ya kazi waliyo iagiza. kwa bwana Ngigo, au madevu kama wengine wavyo penda kumwita kisiri siri, maana mwenye uwa apendi aitwe hivyo, na mandevu hao uya fuga makusudi, kutokana na jelaha la kisu alilo lipataga miaka sita iliyo pita,
Hokololo alichoma mafupa pasipo kujuwa kuwa, Kisona na wenzie wamesha katiza huko mda mfupi uliopita, “hawa jamaa wafike kule, wakute shughuri ime kwisha kabisa” alisema Kingarame wakati wana katiza pale kituoni, na kwa mbali wakiwaona askari wengi wakiwa wamejipanga mstari, “nikama nime liona kibaka la OC FFU” alisema Hokololo, akimaanisha kuwa ameliona gari moja la mkuu wa FFU, Rvuma, ambalo walizowea kuliita Kibaka, “itakuwa wamesha ingia, si unaona ata uwingi wao?” alisema Kingarame huku wakishuka mtelemko wa mto kibena, kwa speed kali.
Walitumia dakika kama kumi hivi kufika pale njia panda, ambayo sasa walisha ikalili sana, na kuwakuta wakina Lusinde wakiwa wametulia na doria yao, “vipi kunajipya huku?” aliuliza Kingarame ambae liicha ya kuvalia koti kubwa, lakini bado alikuwa anatetemeka baridi, sijuwi awa walio lala huku inakuwaje, “afande jipya ni kwamba nime liona gari la yule mjinga tulie mkosa kosa jana, limeelekea Makambako, zaidi ya hapo wakina Ngigo wamesha elekea huko mbele, pamoja na Kibabu, ila atujapata mrejesho” alisema Lusinde, kwa sauti iliyo zidiwa na baridi, “ok! nazani tuelekee huku mbele, tuka juwe kulichoendelea” alisema Kingarame kisha akaingia kwenye gari, sambamba na Lusinde aliie ingia kwenye gari lake, pamoja na askari wake, safari ikaanza magari yaki toka speed ya hajabu, ilikuwa ina karibia saa kumi na mbili kasoro.**
Mida hiyo ndiomida ambayo huko porini pembezoni ya mto, Ngigo na wenzie sio kwamba walilala, hapana, walikesha wakiugulia baridi, iliyo wachamanda usiku kucha, na sasa walikuwa kama wame mwagiwa maji, kwa umande ulio walowesha, Ngigo ebu ona ile mbona kama nyayo ya binadamu, tena ni ya usiku?” alisema mmoja kati ya vijana wa Ngigo, alie kuwa amesogea pembeni kujisaidia, yani kukojoa, “kweli bwanaaaa, tena Dah! wanaelekea huku juu, alisema Ngigo, huku ana jaribu kuzi fwatilia nyayo ziliko elekea, lakini macho yake hayakuweza kuona mbali, maana mwanga badpo ulikuwa afifu, hivyo wakaanza kutembea taratibu kufwata zile nyayo huku wakikagua kwa umakini, “tena ni watu wawili, na alama za viatu nikama nilizo ziona pale kwa wakulima” alisema Ngigo, yani bwana madevu, huku wanazidi kusonga mbele***
Hisia za Ngigo zilikuwa na ukweli, mita mia tano mbele, toka walipo wakina Ngigo, yani pembezoni mwa mto, chini ya mti mkubwa, uliojifunga, ndio kwanza Monalisa alikuwa na fumbuamacho, akiwa bado ame mwegemea Edgar, ambae muda wote alikuwa ana pambana na usingizi, usi mteke, huku Monalisa akihisi dudu ya kijana huyu rafiki yake wa zamani, ikiwa imesimama na kumguza maeneo ya kifuani kwake, sababu ndio alikuwa ame iegema, “naona ume amka” alisema Edgar huku akimtoa Monalisa toka kwake, “ndio mime amka lakini pole” alisema Minalisa huku akiuweka mkono wake kwenye dudu ya Edgar iliyo asimama, Edgar hakujibu kitu zaidialicheka kicheko cha mguno, hapo wote waka simama, Monbalisa akamsogelea Edgar, na kumku,mbatia, akizungusha mikono yake na kuishikia mgongoni, akimwacha Edgar anashangaa, alafu mwisho wake itokee nini?” aliuliza Edgar, ili unizowee, usiwqe unasimamisha simamisha” alisema Monalisa akiwa bado ame mng’ang’ania Edgar, ambae alicheka kidogo, akisha na yeye akaizungusha mikono yake kiuno ni kwa monalisa, “nikiambiae kitu?” aliuliza Edgar, Monalisa inua uso wake, “niambie tu! unazani nita kubishia” alijibu Monalisa, “akika sitozoweza kukuzowea ata siku moja” alisema Edgar kwa sauti mmoja nzito na yataratibu sana, “mh! ata kama nikiwa mke wako?” aliuliza Monalisa kwa sasuti ya mashaka, lakini kabla haja jibu, mala wakasikia kama kuna kijiti kime kanywagwa na kuvunjika maeneo ya karibu ya hapo walipo kuwepo, yani nje ya kichaka kile cha mti walio ingia chini yake, Edgar aka tega siko, kwa umakini, itaendelea……. hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata