BIKIRA YA BIBI HARUSI (43)

SEHEMU YA 43

ILIPOISHIA SEHEMU YA 42: Walitulia kwa dakika kadhaa, pasipo kuona gari likipita, sasa ata ngurumo ya gari ilibadirika na kuwa kama lililo simama, “au wame tustukia nini, mbona awaji?” aliuliza Ngigo, ambae alisha wai kufanya kazi nyingi za hatari, “mh! wame tutega” alisema Ngigo huku anainuka na kuanza kumbia kuelekea mbele zaidi akifwatiwa na wenzake, akika yalikuwa ni machele ya hali ya juu. endelea……..
Lakini aikusaidia, mala akasikia pah! kugeuka akamwona kijana wake mmoja akirushwa juu na kutupwa chini kwa nguvu ya risasi ya SMG, na nyuma yake akimwona askari mmoja wa jeshi la ulinzi, ndie alie mtandika risasi, hapo Ngigo alishuhudia vijana wake wakitawanyika hovyo hovyo, wakijaribu kukimbia ilikujiokoa, lakini aikusaidia kitu, kumbe wanajeshi awa walisha wazunguka muda mrefu, mala akasikia tena Pah! mlipuko wa risasi ulio ondoka na mtu mtu mwingine tena, hapo bwana Ngigo aka juwa akuna ujanja, ni kukimbia kwa nguvu zake zote.
Lakini akupiga ata atua kumi, aka stuka akipigwa ngumi nzito kifuani, na kutupwa mita tano pembeni, na bunduki yake ikimtoka mikononi na kudondokea pembeni, Ngigo aka inua faster na kumtazama mshambuliaji wake, akamwona ni kijana mdogo sana, alie valia kombati na nyota zake begani, huko na ko akaendalea kusikia Pah! nikama wawindaji wanawinda nyumbu, kwa haraka haraka Ngogo, akajuwa huyu anaweza kummudu, aka kaa kibadach stance, na kujifyetua ngumi moja nzito, iliyo enda usawa wa kifua cha Kisona, lakini kama umeme, akashangaa kisona akinyimba pembeni kidogo, na kuikwepa ile ngumi, kisha kilicho fwata, aliuona mkono wa kushoto wa Kisona ukichomoka kamavile umefungiwa mashine, na kumtandika usoni, kiashi cha kumfanya Ngigo apoteze nuru ya macho yake, na kuanza kuona wingu la blue, lenye nyita za njano, kama vile aikutosha aka shuhudia mvua za ngumi ziki mshukia sehemu mbali mbali za usowake, mpaka alipoona wingu la blue likibadili langi na kuwa jeusi pasipo nyota, huku mwili ukikosa nguvu, akajibwaga chini bwaaa!
“Afande tumesha wamaliza wote” ilikuwa ni sauti ya Koplo Katembo, ni baada ya kuwa kuwamaliza wale vijana nane wa Ngigo, “ok! ebu njooni mumfunge kamba huyu mshenzi” alisema Kisona akiwa amesimama pembeni ya Ngigo alie kuwa amepoteza fahamu,
Dakika tano baadae tayari walisha isogeza, miili yote ya vijana wa Ngigo barabarani, wakiirudika pembeni ya barabara, kisha waka mpakiza Ngigo kwenye gari lao,huku bado amepoteza fahamu, wakiwa wame mfunga kamba za kueleweka, na pia waka chukuwa silaha za wale majambazi, “bado wale ma dereva, alisema Kisona huku akipanda juu ya gari, na darubini mkononi, na kuanza kutazama mbele, kule wanakoelekea.
baada ya kutazama kwa dakika kadhaa, Kisona akatabasamu kidogo, “mzee Mbogo, Endesha gari kwa mbio zako zote, mpaka tuwa kamate wale washenzi, maana wakisikia mlio wa gari tu! lazima wata itaji kukimbia” alisema Kisona huku ana shuka toka kwenye gari, ni bnaada ya kuyaona magari mawili ya wakina Ngigo, yakiwa mmbele yao umbali wa mita kama mia nane hivi, yakiyakitazama wanako elekea,
Wote wakaingia kwenye gari na mzee Mbogo akaondoa gari kwa speed, kuelekea kaskazini, kule walikokuwa wanaendelea, yani kuwafwata wale madereva wawili waliokuwa na yale magari.
Ile wana kata kona ya kwanza, wanaingia ya pili, mbele yao kama mita ishirini waka yaona magari mawilki mbele yao, yakiwa yame simama, na kutazama kule wanako elekea, huku vijana wawili wakigawana magari haraka, na kila mmoja akifungua mlango wa gari na kutoa SMG, wakionyesha kuwa walisha shtuka kuwa awa walikuwa ni maadui, hivyo walitaka kuwa shambulia, lakini kama umeme, tayari kisona alisha fungua mlango huku gari likiwa mwende wa kkasi na kujirusha nje ya gari akivilingika kama tairi, na bunduki yake mkononi, hapo ikafwata sauti ya milipuko mfululizo ya risasi, toka kwwenye bunduki ya kisona, mpaka mzee Mbogo ana simamisha gari, tayari wale vijana walikuwa wamesha nyofolewa roho zao, kilicho fwata ni kuchukuwa silaha zao na box risasi, waliyo yajaza kwenye magari yao, ni yale waliyo pewa na Kingarame jana usiku, kisha waka ingia kwenye gari, “twende zetu, atuna ishu nao washenzi hao, na hili litya kuwa fudisho kwa, yule mjinga” alisema Kisona, na mzee Mbogo aka kanyaga mafuta akipita pembeni ya yale magari, kama vile awa kufanya wao tukio lile. **
“huyu kijana ni mshenzi sana, yani kosa upumbavu wake, leo tunge kuwa tuna anza vikao vya harusi” alisema mama Erasto, kwa sauti ya kilevi, maana watu hawa toka wame fika hapa Serena Hotel ilikuwa ni pombe na wao wao na pombe, “yani ananichanganya sana huyu kijana, silipendi kabisa na ninazidi kumchukia” alisisitiza mama Monalisa, ambae pia alikuwa amelewa sana, “usiseme hivyo mke wangu, kila jambo utokea kwa maana yake” alisema baba Monalisa kwa sauti ya uchangamfu, japo wakilevi lakini ulikuwa tofauti kidogo, kila mmoja akamshangaa, “unamaana gani baba Mona?” aliuliza mama Monalisa, kwa mshangao sambamba na wenzake wote walimtazama mzee Anderson kwa mashangao, “mi mwenyewe sijuwi namaana gani, ila tusubiri tuone” alisema baba Monalisa, na wote wakaangua kicheko, wakihisi kuwa ni pombe ndiyo iliyo mzidi huyu mzee, anae jaribu kujiliwaza, kasolo Dereva wa bwana Anderson pekee ndie alie juwa boss wake ana maanisha nini.
“yani mi naombea huyu Edgar wampige risasi za miguu, anayojivunia kuchezea baisket” alisema Erasto kwa sauti ya kilevi levi, na baba yake akacheka kwanguvu, “alafu ana enda jela akaolewe” aliongeza mzee Misago huku ananedelea kucheka, “aende jela, anyongwe kabisa, yani akae na mwmanangu huko mapolini, alafu aende jela?” alisisitiza mama Mona, kwa sauti iliyo jaa hasira kali sana, huku wenzie wakimuunga mkono, kasolo baba Mona peke yake, “lakini sijuwi kwanini huyu kijana amefanya hivi, alikuwa rafiki mzuri sana wa Monalisa” alisema baba Monalisa, kwa sauti iliyo jaa uzuni kubwa sana, kiashi wenzie wakamshangaa, “hhhaaa! mna mwelewa huyu, hivi urafiki wa utoto, una ufgananisha na wa sasa?” aliuliza mzee Misago kwa mshangao, huku mama Monalisa aka dakia, “kwanza alimsaidia nini katika urafaiki wao?” hapo Mzee Anderson ali tulia kidogo kama ana jikumbusha jambo, alafu akainua kichwa chake, “mke wangu nazani ume sahau siku ile tulivyo itwa kama washaidi, kwa Mona, baada ya Edgar kuwa tandika wale watoto waliotaka kumzuru mtoto wetu” alisema baba Mona, na hapo mke wake nikama alikumbushwa kitu flani, “lakini ni kawaida tu kwa watoto kusaidiana , asa wakiwa wanakaa majirani” alijibu baba Erasto akisahahu kuwa sikuhiyo, mwanae Erasto ambae alikuwa na umri mkubwa kuliko Edgar, alishindwa kuwasaidia, “ila nikweli au sikuile ambayo walilowa na mvua, Edgar alimbeba Monalisa mpaka nyumbani” alisemamam Monalisa akionekana kuanza kunyongea, kitu ambacho baba Mona na wenzake walikiona, na baba Mona, aka juwa sababu ya mke wake kunyongea, akutaka kumsemesha neno, lakini aikusaidia, “najuwa Edgar alikuwa ana mjari sana mwanangu, lakini sijuwi kama atarudi salama huko aliko” akika ungemsikia huyu mama wakingoni, nauakika ungecheka, japo sauti yake ilikuwa ni yauzuni, “kurudi salama kivipi mke wangu?” aliuliza makusudi baba Mona, ambae alitamani mke wake aseme kama alivyo sema jana mchana, ili amrushe roho Erasto.
Lakini kabla mama Monalisa ajajibu swali la mume wake, wakamwona Erasto akiinuka ghafla, na kuelekea kwenye jengo kubwa la hotel, “mshenzi wewe, unataka kuni chokoza tu!” alisema mama Mona, huku akimpiga mume wake kikofi cha begani, wote wakacheka kidogo, pamoja na mzee Anderson mwenyewe, ambae macho yake yaliona uondokaji wa Erasto, akatazama kwenye meza ambayo alikuwa amejaa yule dada mhudumu, aka mwona anainuka na kueekea jengo kubwa la hotel, “nikuchokeze nini sasa, mama Mona, si useme tu!” alisema baba Monalisa, huku ana tazama grasi na chupa ya pombe ya Erasto, ilikuwa tupu, aka mtazama Dereva wake, macho yao yaka gongana inaonyesha kuwa, wote walihisi jambo moja, kwa wakati mmoja, waka watazama wazazi wa Erasto, yani rafiki yake bwana Misago na mke wake, aka waona wana nong’onezana jambo, “we haya tu! na mipombe yako unaona mazuri haya, mpaka mkwe ameondoka, kwajinsi anavyo jisikia uchungu, we unafurahia” alisema mama Monalisa ambae akuwa anajuwa kinacho endelea.
wakati huo huo mzee Misago akaaga, “jamani wacha nika punguze majini kidogo” inamaana alikuwa anaenda chooni, “ngoja ni chunge mzigo wangu” alisema mama Erasto na wote wakainuka kwa pamoja, “haya wapendanao, na watoto wetu waige mfano wenu” alisema mama Monalisa, huku wana wasindikiza kwa macho wazazi wale wawili wa Erasto, mzee Anderson aka mtazama tena dereva wake, maana wote wawili walisha juwa kuwa wana uelewa mchezo, na maana yake ulianza tokea jana mchana, “boss wa kuwa mpole, kila jambao utokea kwa maana yake, nazani ata wewe mwenyewe unajuwa” alisame dereva, huku na kuinua grass ya pombe kisha akaiweka mdomoni, na kugugumia pombe iliyomo ndani yake, “inamaana na wewe una muunga mkono huyu mlevi?” alisema mama Mona, huku akimtazama dereva, ambae alicheka kidogo, lakini baba Mona alidakia, “tatizo ujuwi busara za mlevi, ukilijuwa ndio utakapo juwa kuwa mume wako ana hakiri nyingi” alisema mzee Anderson, kwa sauti ambayo ilionyesha kuwa alibadirika na kuanza kuchukia, “ebu nisubirini na kuja” alisema mzee Anderson, huku ana inuka, “hapana boss subiri kwa nza warudi” alisema dereva, huku wakiwai kumzuwia boss wake, ambae akuwa mbishi, aka kaa tena, “ujawai kuni shauri vibaya” maneno haya, yali mshangaza mama Monalisa, japo alikuwa amelewa, “hivi we mzee umechanganyikiwa?” aliuliza kwa mshangao, “ujakosea ila wewe ndio uta changanyikiwa zaidi” alijibu baba Mona, kwa sauti ya kilevi, na kumfanya mke wake acheke, “nichanganyikiwe mala mbili, inamaana hakuelewa chochote. ***
Tukiachana na Serena Hotel, ebu turudi porini, wakanza kuingia kambini pale kwenye eneo la wakulima ambao leo walifaidika kwa uwepo wa polisi awa maana walipata mikate, na huduma ndogo ndogo, kama vile sukari chumvi na vyakula vingine, pia walisaidiwa ana vidawa vidogo vidogo vya kutuliza maumivu, alikuwa ni SSP Manase Kingarame, ambae aliingia pale saa kumi na mbili na robo, akikuta uaribifu wa wakina ngigo na kijana Edgar, maana alisimuliwa jinsi mapigano makali yalivyo tokea kule poini, na askari watatu kuuwawa, na wengine sita kujeruhiwa, akajifanya kusikitika sana na kumlahani Edgar, akidai kuwa ni jambazi sugu tena hatari sana, “yani afande lile wazo la kumleta akiwa hai, lita tugharimu sana, bola lifanyoike linalo wezekana, kama ikibidi kuuwawa auwawe tu, mpaka sasa amesha wamaliza askari wetu wanao karibia ishirini” alisema Kingarame kwa sauti ambayo ilionyesha kuwa ameuzunika sana, kwa tukio lile, lakini moyoni mwake aliwacheka viongozi wake, na kujitapa, “mimi ndio King, lazima niushinde huu mchezo” akika viongozi hawa, waliunga mkono juu ya maneno ya Kingarame, “wakuu wa vikundi wajulishwe, kuwa popote watakapoonekana, wauwawe, akuna cha Edgar, wala mjinga mwingine, maana hii imetosha sasa” alisema RPC Iringa, na wa Ruvuma nae akaongezea, “tena akikisheni analipia haya yote aliyo yafanya”
wakati mjadara huu unaendelea, yakaingia makundi mawili ya polisi, yaliyo ungana wakati wa umsaka Edgar, likiongozwa na ASP Msengi, ambae alisogea kwa wakubwa wake, akiwaacha askari wake wakijichanganya nawenzao, na kupeana story, “ebu tupeni habari zahuko mlifanikiwa kumshusha?” aliuliza Rpc Ruvuma, kwa shahuku ya kutaka kusikia kuwa “yupo hapo nje” lakini story ambayo aliitoa Msengi wote waka duwaha, inamaana mmezidiwa hakiri na huyo mtu mmoja?” aliuliza RPC Iringa, kwa mashangao, ulio changanyika na fadhaha, “ila afande kuna mambo ya hajabu tume yaona, na yame tushangaza sana” alisema Msengi, ambae askari wake alikuwa amewaacha pembeni, Kingarame aka mkata jicho ASP Msengi, lakini asifs huyu asie na kamishen akuliona jicho la afande wake, “nini tena ASP, hayo ndio mambo tunayo itaji ili kufanikiisha zoezi” alisema RPC Ruvuma, huku wote wakitega masikio kusikiliza kilicho mshangaa Msengi, “afande kwa jinsi nilivyo wasikia askari na mimi mwenywe nilivyo shuhudia, nikama wale majambazi wengine walikuwa wana taka kumshambulia huyu jambazi Edgar, inamaana nika awapo pamoja, pili yule binti, tunae sema ametekwa, inaonekana ni tofauti kabisa, maana anashirikiana bega kwa bega na Edgar, katika makabiliano na kutumbia, maana alikuwa na nafasi nzuri ya kumkimbia mtekaji, lakini cha hajabu ndio kwanza aliongoza kutu kimbia” hapo wote waka tazamana, kwa mshangao, “inamaana huyu binti anae itwa Monalisa Andderson, na yeye anashirikiana na jambazi?” aliuliza OCFFU kwa mshangao.
Hapo ukazuka mjadala wa maswali yaliyo kosa majibu, mpaka walipo liona gari la jeshi aina ya land rover mia na kumi, likisimama kwenye eneo lile la makao makuu ya oparetion Kifo mkononi, na wakashuka wanajeshi wa sita, wakiongozwa na kanal Kisona, dereva akibakia ndani ya gari, “awa jamaa bado wapo tu!” aliuliza Kingarame alie hisi kuwa ana jiuliza kimoyo moyo, kumbe alikuwa anauliza kwa ssauti, “tena tumeletewa ujumbe na CO wa makambako, kuwa wata kuwepo huku wakifanya uchunguzi wa eneo la zoezi” alisema OCFFU wa Iringa, huku waote wakiwatazama wale askari wa jeshi la ulinzi wa wananchi, japo giza lilianza kutanda, lakini walimwona Kisona akija upande, huku askari wake nao waki chukuwa silaha flani zaidi ya zile wazakwao, na kumfwata mkuu wao, huku wengine wakibebezana mabox ya risasi, “abari za jioni majemedari” alisalimia Kisona, baada ya kuwafikia wale makambanda wakuu wa polisi mikoa, “nzuri bwana Kisona, vipi unaitaji tukuifadhie hizi silaha?” aliuliza RPC Iringa, huku akiwatazama wale askari wa Kisona walio beba SMG na box za risasi, “mkulima abebewi jembe, hizi ni mari zako” alisema Kisona, kauri ambazo makamanda wale walichukulia kama utani, “ok! tuna shukuru bwana, lakini mkulima uwa anaenda shambani na jembe lake, sasa sijuwi kama unahaja ya kutuongezea majembe” alitania RPC Iringa, wakati huo Kingarame alikuwa ana tokwa kijasho chembamba, maana alipata hisia mbaya sana juu ya Kisona, na zile SMG kumi na moja, na yale mabox ya risasi,
“jamani tunaomba tuwa kabidhi hizi silaha na risasi, tume zikuta hapo nyuma kidogo, ni vyema mkienda kupaona sehemu ya tukio, pengine mkapata cha kusimulia” alisema Kisona, huku akielekeza sehemu ambayo aliwataka waende, wakajionee, pasipo kuwa fafanulia chochote, kisha akaingia kwenye gari na kuondoka zake, “twende makambako tuka mwache huyu kambini, tutaongea nae kesho” alisema Kisona, huku mzee Mbogo anaendesha gari, wakati huo Ngigo alikuwa amesha ziduka, lakini alikuwa amesha zibwa mdomo kwa kitambaa, akishindwa kupiga kelele, maana alitamani sana abakizwe pale kwa polisi, kuliko kuondoka na watu awa hatari,
Wakiwa wamepigwa na butwaha makamanda wapolisi, walilitazama gari la Kisona likitokomea porini, pande wa mjini, huku bwana Kingarame akiwa eme duwaha, jasho lina mtoka sehemu zasiri, “huyu mshenzi ataniaharibia kila kitu” ndio maneno yaliyo pita kichwani kwa Kingarame.
“OCD Njombe akatuandalie sehemu ya kulala mjini, ASP waambie askari bahadhi waingie kwenye magari, twende huko tuliko elekezwa” alisema RPC Iringa huku ana tetembea kuelekea kwenye gari lake, sambamba na wenzie walioingia kwenye magari yao,
Dakika tatu baadae msafara ukaondoka kuelekea mashariki, akiwemo bwana Kingarame, ambae sasa alikuwa ana hisi presha inapanda, presha inashuka, maana akujuwa kilicho watokea wakina Ngigo,….. mdau naomba tuishie hapa. leo nimetumia muda wangu mchache nilio upata ili usi kose kabisa, simulizi hii, itayo endelea hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata