: BIKIRA YA BIBI HARUSI (54)

SEHEMU YA HAMSINI NA NNE (54)

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU 53): “inamaana tuamini nini, hawa majambzi wwalikuwa wengi au …….?” alishindwa kumalizia swali RPC Ruvuma, siyo hilitu mna maswali mengi ya kujiuliza, maana gari mpaka liungue moto, lazima risasi nyingi zilipigwa kwenye tank, je wakati huo polisi walikuwa wapi, wakati Edgar ameacha kuwashambulia na kulimiminia risasi gari?” endelea………
kwa swali hili nikama makamanda walipgwa na butwaa flani, ambalo liliwafanya watulie kwa nukta chache, kabla ya OC FFU, toka Ruvuma ajajibu, “lakini azikuitajika risasi 30, kulipua gari, pengoine ni moja tu ilitosha kufanya hivyo” kwajibu hilo, Kisona Ambae akuweza kuwaeleza moja kwa moja juu ya tuhuma zake kwa SSP Kingarame, aliona kuwa kazi bado hipo ngumu sana mbele yake, “akika nawaambie, kama hamta mjuwa nani yupo nyuma ya hili, mtaendelea kupoteza askari wengi sana” alisema Kisona kiisha aka waaga wale makamanda na kuondoka zake, akiwaacha wale makamanda wa jeshi la polisi, wakimsindikiza kwa macho, mpaka alipo potelea nje ya hema.
Ndipo RPC Iringa aka watazama wenzake, “jamani tukkubari tukatae, mane no ya huyu jamaa, yana maana kubwa sana, mnaonaje tukienda kwenye eneo la tukio tukajionee na sisi wenyewe?” alishauri kamanda huyu polisi mkoa wa Iringa, na wenzake waka muunga mkono, na kutoka nje ya hema lao, wakielekea kwenye magari yao, wakimwona kisona akiwa na askari wake wame zunguka kwenye bonet la gari lao, wakiitazama ramani yao, na kuonyeshana bahadhi ya sehemu.
“siombei iwe kweli, kuwa hili swala lina usisha wenzetu, maana ni aibu kubwa kwa jeshi la polisi” aliwaza kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, sawa na mawazo ya RPC Ruvuma, “na kama kuna polisi wanausika, maana yake ni kutoka Songea, na Kibabu ni mmoja wapo” mpaka hapo RPC Ruvuma alisha hisi kuwa aibu yenye utata inakuja upande wake, na pengine kumwingiza matatani, kwa kuto kuwa ma umakini juu ya mwenendo wa askari wake, “kama ni hivyo huyu kijana anausikaje” aliwaza RPC Ruvuma, akimaanisha Edgar anausikaje, maana akama sanjet Kibabu ni muhusika, na Edgar ni mwenzake, basi awasinge msakama Edgar, na kusababisha jambo hili kuwa kubwa kihasi hiki.
Wakati RPC Ruvuma anawaza hayo, RPC Iringa nae alikuwa anawaza yakwake, “kama ni kweli huyu Kisona anachosema, basi tunaingia mashaka ni muda siyo mrefu” akika hapo mdau wa story za @LIBRA STAR SEVEN, unapata ukweli kuwa, siyo kwamba awakumwelewa Kisona, ila walijifanya kuto kuelewa, hili wajaribu kuikwepa aibu hii,
Pasipo kujuwa kuwa Kisona, huku nyuma yao, alikuwa anazidi kuipitia ramani kwa umakini mkubwa sana, akitazama eneo ambalo inasemekana edgar alionekana mala ya mwisho, na upande alio elekea,”mnaiona hii njia, inaelekea kwenye kiwanda cha kukaushia majani ya chai, kwahiyo basi wakijitaidi sana wana weza kupafikia hapa, pana kilomita hishirini na moja” alisema Kisona, kwasauti ya chini kidogo, akutaka polisi waliopo eneo lile wasikie chochote, “na kama watafanikiwa kufika hapa basi itakuwa ni usiku mkubwa sana, hivyo wata lala hapa, na wakilala hapa kuna hatari inaweza kutokea, awa raia wa hapa kiwandani, wanaweza kuwa chongea kwa polisi, huvyo tuna takiwa kuitafuta njia hii ili tuwai hapa, tuka wachukue vijana wetu, na kuwakisrisha ushaidi utakao watia watu mbaloni, na kumwacha huru huyu kijana wetu” alisema Kisona na kuikunja ramani, kisha wakaingia kwkenye gari, safari ikaanza kurudi barabara kuu, kule waliko elekea makamanda wakuu,**
mzee Mohamed na familia yake walifanikiwa kufika njombe, mida yua saa nane kasoro, na kuelekea moja kwa moja kwenye kituo cha polisi wilaya, ya Njombe, wakwaomba kuonana na RPC Iringa lakini waambiwa hayupo, wakaomba kuonana na OCD, mwenyewe, wakaambiwa kuwa alikuwa busy na pilika za operation Kifo mkononi, labda mida ya usiku, ambayo ndio uwa wanarudi toka huko porini, wanafamilia hawa wakajadiliana kwa dakika kadhaa, na kufikia maamuzi ya kuwasubiri, “sababu 5tumeamua kusaidia, basitusubiri mpaka huo usiku, ikibidi tulale hapa hapa Njombe tuondoke kesho asubuhi, hivyo wakatafuta sehemu nzuri ya kupumzika, mwisho wakaipata Serena hotel sehemu ambayo kiukweli kwa hapa Njombe, kipindi hicho, ndio ilikuwa hotel pekee yenye hadhi ya kupumzika mtu mwenye fedha zake, wakati wazee awa wakichukuwa chumba namba 28, ghorofa ya pili, Salma alichukuliwa chumba namaba kumi na nane, jilani na chumba namba kumi saba, katika jengo hili la chini kabisa. ***
Saa nane na nusu, Kingarame na askari wake watano walisimamisha gari lao kwenye kimwinuko flani, katia njia moja ya nzuri ya magari, ikiwa ni kilomita kama kumi na na tano kutoka barabara kuu, iendayo Makambako, “awa washenzi lazima watakuwa wanakuja huku, ebu tujaribu kusonga mbele, inaonyesha kuwa, ni kama kuna mji mdogo, au Kiwanda” alisema Kingarame, ambae aliona nyaya za umeme na simu ya kampuni ya mawasiliano ya serikari, Hokololo akaondoa gari, kusonga mbele, huku askari watano nyuma yake wakiwa makini na SMG zao mikononi, wakijigawa katika utazamaji, wakati gari linatembea, wakazidi kusonga mbele.
Nusu saa baadae waliingia kwenye kiwanda kimoja cha kukausha majani ya chai, sehemu ambayo ilikuwa na majengo machache ya kulala wafanya kazi, na mawili makubwa sana huku moja likiwa linafuka moshi, na jingine likiwa lime fungwa kwa mageti makubwa, likionyesha kuwa ni ghara la kuifazia majani yachai yaliyo kaushwa.
Baada ya kusimamisha gari lao, mlinzi mmoja akawasogelea, na kuwasalimia, “habari zakazi maafande” ilichukuwa kama dakika nzima kabla Kingarame aja ongea neno, “wewe ninani hapa?” aliuliza SSP Kingarame, kwa sauti flani ya kibabe, “ni mlinzi , mimi ni mlinziwa hapa” alijibu yule mlinzi ambae aliona fika kuwa, jamaa hawa awakuwa wanaitaji mazowea na mtu, “vipi kuna watu flani umewaona hapa kijana wakiume na wakike, wame beba vibegi mgongoni?” aliuliza Kingarane, akimkazia mcho yule jamaa alie jitambulisha kuwa mlinzi, “hapana, sija mwona mtu yoyote zaidi yenu, labda kama ni wafanya kazi wa hapa kiwandani” hapo Kingarame, alitulia kidogo, kama anawaza jambo, kisha akamtazama yule jamaa, “vipi hapa mnama wasiliano hapa?” aliuliza Kingarame, “ndio kunasimu sehemu tatu, kwenye kibanda changu, ofisi ya mkuu wa kiwanda, na kwenye jengo la wafanyakazi” alijibu kwa kufafanua yule mlinzi, “ok! kunajambo nanata unisaidie” alisema Kingarame kisha akanza kumpatia maelezo yule jamaa, alipo maliza akampa anamba za simu za hotelini, akimweleza kuwa atakapo ipiga aulizie Kingarame, “kumbuka jina hilo, yani usi sahau, na wala usifanye makosa, juu ya hilo” alisema Kingarame huku akiichanganya vitisho na ahadi ya zawadi endapo ata fanikiwa kuwaona watu hao na kutoa taharifa “ila ukikosea utailipia, na usimwambie mtu yoyote juu ya hili” alimaliza Kingarame na kuondoka zao, akimwacha yule kijana mlinzi anawasindikiza kwa macho, ***
Makamnda wa polisi ndio walikuwa wanza kufika eneo la tukio, yani pale kwenye gari lililokuwa linaungua, huku viazi na miili ya wafanya biashara ikiungulia ndani, ya gari lile, wakasimamisha magari yao pembeni kabisa na lile gari lililo kuwa linaungua, na kushuka toka kwenyemagari hayo, na kuanza kukagua maeneo yale kama walivyo elekezwa na kisona, nikweli waliona damu nyingi zikiwa sehemu mbali mbali nje ya gari, ikionyesha wazi wafanya biashara waliuwawa nje yagari, na wakati huo huo, gari la wakina Kisona lilikuwa lina kaingia maeneo yale, na kusimama, Kisha wakashuka na kuwasogelea makamanda wa polisi, “naona mna kagua kidogo” alisema Kisona, ambae makamanda awa walimwona kama mzimu hivi, “hivi awajamaliza tu huo uchunguzi wa eneo la zoezi?” alijiuliza RPC Iringa, juwa fika kuwa uwepowa mtu huyu maeneo haya, ni chanzo cha kugundulika kwa mchezo mchafu ulio chezwa na wenzao, “ndiyo bwana tumeona, lakini ngoja tuchunguze ni damu za wakina nani, maana kuna askari wetu wengi sana wamepigwa risasi, alisema RPC Iringa, na wakati huo huo waka waona vijana wawili wenye mbwa sita, wakija mbio mbio.
Vijana hao walio onekana kuwa na jambo flani muhimu la kuwaambia polisi wale, waka liwasogeleea polisi waliokuwa wana endelea kulipekua eneo lile, na kuwaeleza, “mafande kuna mtu amekufa kuleeee, karibu na barabara” alisema mmoja wa wale vijana, “sehemu gani?” aliuliza OCFFU wa Ruvuma, na wale vijana walitoa maelezo vizuri, na kuwa vijana wenzao wapo eneo la tukio, wao wametumwa kuja huku, kutoa taharifa, sababu waliyaona magari ya polisi yakija na kutokea huku porini,***
Mida hii ndani ya Serena Hotel, mambo yallikuwa ni amsha amsha, kama kawaida ya marafiki awa na familia zao, yani mzee Anderson na mke wake na dereva wao ongeza Misago mke wwake na kijana wao Erasto, walikuwa kwenye meza yao ambayo toka wame kuja hapa Njombe, nikama walikodi, maana kila siku na kila wakati, walikuwa wana ikalia wao.
ilatofauti na siku zilizopita leo mama Mona akuwaananakunywa sana, na hii ni kutokana na kunywa sana sikuzilizopita, tena leo alitumia mvinyo mwekundu kutoka Dodoma, na siyo pombe kali kama jana na juzi, hukuwenza ke wote wlikunywa pombe kali, .
Kwaupande wa Anderson, alikuwa anaendelea kuchapa pombe, huku akimfwatilia Erasto, ambe kama wazazi wake, alisha lewa sana, akionekana mala kwamala kumwita dada mhudumu na kumwagiza vinywaji, lakini kama ungekuwa makini lazima ungeona hishala walizo onyeshana, baada ya muda kidogo, yule mhudumu akapotea kidogo, na bada ya dakika kumi akaonekana akiwa amevaa nguo za kiraia, yani suruali yeusi, tishet jeupe na jacket zito, akasimama mlangoni na kumkonyeza Erasto, kwa umakini wa hali ya juu, ishara ile zaidi ya Erasto mwenyewe, ni baba mkwe wake mtarajiwa tu ndie alie ona, Kwaumakini wakilevi Erasto akamwonyesha ishara ya kuwa, atulie kama dakika chache, amalize kinywaji,
Wakati hayo yanaendelea ghafla mzee Ansderson akajishika tumbo, “hooo! mama Mona tume linaniuma” wote waka mtazama mzee Anderson, “nini tena baba Mona” nikama watu watatu wali mwuliza kwa pamoja, akiwepo mke wake, bwana Misago na mke wa Misago, “sijuwi naona tumbo limenishika ghafla” alisema Anderson huku anajaribu kuinuka, na kuyumba kidogo, mke wake akamdaka, “ebu nikupeleke chumbani” alisema mke wa Anderson na kuanza kumkokota mume wake kuelekea ndani ya jengo kubwa la hotel, huku mke wake akiingiwa na wasi wasi mkubwa juu ya afya ya mumewake.
Lakini hali ilibadilika baada ya kufika ghorofa ya pili, akashangaa kumwona mume wake, akijitoa kwenye mikono yake, huku anatabasamu, mke wake akashngaa, itaendelea………… hapahapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata