BIKIRA YA BIBI HARUSI (76)

SEHEMU YA SABINI NA SITA (76)

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO (75) Kingarame akajuwa akimteka askari, anaweza kumzidi mahalifa na kumgeuka, hivyo aka ona kimbilio lake ni mama Monalisa, hapo kngarame aka mshika mkono mama Monalisa na kumfutia kwake akimkaba kabari moja matata, huku akimwekea bastola kichwani, “wekeni silaha zenu chini haraka vinginevyo nita mfyetua huyu mwanamke” endelea……….
Hakika makamanda na askari wa polisi, walishangaa sana, na hapo wakathibitisha kuwa kweli SSP Kingarame alikuwa ni mwalifu, hapo mitutu yote ika mwelekea Kingarame, “nasema wekezi silaha zenu chini, la sivyo na ondoa roho ya huyu mwanamke” alisistizza Kingarame ambae sasa alikuwa ana mburuza mama Monalisa ambae alikuwa ame toa macho ya huruma, yanayo omba msaada, huku akitetemeka kwa uoga, maana akuwai kuelekezewa bastola namna hile, “tafadhari mwachie mke wangu” alisema baba Monalisa, kwa sauti ya kuomboleza, lakini ndio kwanza Kingarame aliendele kumvuta mama Monalisa kielekea nae upande wa mapokezi, “shusheni silaha chini” alisema Kisona,kwa sauti ya juu, askari wotewa jeshi la wananchi na polisi waka shusha silaha chini, wakatihuo Kingarame, alikuwa anakatiza karibu na Mike, akamkata jicho la chuki na hasira, “nawew, kaa tayari, nikirudi naanza na wewe” alisema Kisona kwa sauti iliyo jaa chuki, kisha aka endelea kumkokota mama Monalisa kutokanae nje, “aande wewepekee unaweza kumsaidia mke wangu” alisema baba Monalisa huku akimtazama Kisona kwa macho ya huruma, “kingarame weka silaha chini, tunaweza kujuwa namna ya kukusaidia” alisema RPC Ruvuma, kwa sauti ya kubembeleza, na kujaribu kushawishi, lakiniilikuwa kamakumpigia mbuzi gitaa, ndio kwanza Kingarame alizidi kurudi nyuma akimkokota mama Monalisa alie mwekea mtutu wa bastola kichwani kwake, huku skari nao wakisoea kushuhudia anacho kifanya boss wao.
Wakati huo huo, Kisona akausogelea mlango wa chumba namba kumi na saba,akisindikizwa na askari wake wa jeshi la ulinzi “Edgar na Monalisa, kanal Kisona hapa, kuanzia sasa mpo salama mnaweza kutoka nje” alisema Kisona na hapo kikapita kimya kidogo, “Edgar unanisikia…” aliongea tena kisona lakini safari hii kajibiwa, “nipo hapa, baba yangu yupo wapi?” ilisikika sauti ya Edgar, huku akiibuka toka mlangoni, bunduki yake mkononi, nyuma akionekana monalisa ameshika pindo ya shati la Edgar, ikionyesha Edgar, alisha chungulia na kuona kuwa kweli aliekuwa anaongea ni Kisona, nawalikuwa wanafahamiana toka zamani, “baba yako…” ata kisona hakumalizia, mzee Mbogo alikuja mbio mbio, akakumbatiana na mwanae, kwashangwe, wakikaa kwa dakika kadhaa, bila kusema neno lolote, mpaka walipo achiana, mzee Mbogo akanyoosha mkono kwa Monalisa, ili mkumpa hongera ya kupona, katika seke seke hili la kifo mkononi, lakini Monalisa akuupokea mkono hule, zaidi alimkumbatia mzee huyu, “asante sana baba, kwa kumzaa Eddy, bila yeye ninge kuwa nimesh kufa” alisema Monalisa, akiwa amemkumbatia baba Edgar, akika ilikuwani furaha kati kati ya vita,
Walipo achiana, baba Edgar akaweka mikono juu ya vichwa vya kina Edgar na Monalisa, “siamini kama mumeweza kujilinda, akika ni furaha kwetu” alisema mzee Mbogo, huku watu kadhaa wakishuhudia tukio hili, wakiwepo Kisona na askari wake wajeshi la ulinzi, huku na wakina mzee Misago na Anderson, pamoja na polisi wakiwa wamesha toka nje yajengo la Hotel,
Huku watu waliokuwa vyumba vya jilani, nao walianza kuchungulia kupitia milango yao, kati yao walikuwa ni Salma na Erasto, ambe alimwona Monalisa akiwa jilani kabisa ya mtu ambae, alitokea kumchukia sana, toka utotoni, salma nae alijikuta kitabasamu, na kutoka chumbani kenda kuwasalimia wenzie alio soma nao, ambao walishangaa uwepo wake mahali pale, wakati huo mzee Mohamd na mke wke walish sogea toka gholofani, Kisona akitoa ufafanuzi uwepo wa wakina salma mahali pale, “mwanangu mama yako ametekwa na yule Kingarame, kumbe ni jambazi” alisema baba Mona ambae alikuja moja kwa moja nakumkumbatia mwanae, kabla ajaanza kumkagua usoni na mikononi, kuakikisha kama mwanae hajaumia sehemu yoyote, “nimesikia baba, nazani wakina Edgar wataenda kumwokoa” alisema Monalisa ambae sasa alikaribia kutooa kilio cha furaha, kilicho changanyika na majonzi ya kutekwa kwa mama yake, huku akionyesha kumwamini sana Edgar, kuwa ndie wakwenda kumwokoa mama yake, kitendo kilicho mfanya Kisona atabasamu kidogo, “ok! mbogo, ili ni goal moja bado mpra unaendelea, twende tuka mfwate mama wa huyu binti” alisema Kisona, huku akiwatazama askari wake na kuwaonyesha ishara ya kuondoka, “wnne wabakie kwaajili ya usalama wa hao mashaidi” alisema Kisona na hapo hapo Monalisaalifungua kibegi chake, na kutoa video tape, “wewe si ndio kisona, chuku hii, waanze kukufwata wewe” alisema Monalisa huku anamkabidhi Kisona video tape ndogo, akaipokea huku anatabasamu, “akika mna stahili zawadi na pongezi nyingi sana” alisema Kisona huku anatabasamu, huku anaanzakuondoka, kuelekea nje akiongozana na mzee mbogo na askari kadhaa, Edgar nae akaliunga, akiwa na SMG yake mkononi na magazine tatu za akiba, “afadhari aondoke ni mveshe pete mchumba wangu” yalikuwa mawazo ya kijinga sana ya Erasto, ambae aliona kila kitu akiwa kwenye mlango wa chumba chake, akakimbilia mezani kwenda kuchukuwa pete yake, ile anarudi akamwonaMonalisa na baba yake wakiwa wanakimbilia kule wanakokimbilia wakina Edgar, “Edgar nivyema unge pumzika kwa sasa” alisema Kisona huku wakipisha nabahadhi ya polisi, waliokuwa wanarudi ndani ya jengo la hotel, kwaajili ya kuchukuwa silaha za wenzao waliopoteza maisha, kwenye chumba namba kumi na saba, “hapana mzee Kisona, wacha twende wote, nina hasira sana na huyu mtu” alisema Edgar, na Kisona aka mtazama mzee Mbogo, ambe aliitikia kwa kutikisa kichwa juu chini akionyesha anakubaliana na Edgar, “ok! lakini kuwa makini zaidi, sababu hatujuwi wapo wangapi, ambao hatuja watambua” alisema Kisona huku akigeuka kutazama nje sehemu ambayo kunamaegesho ya magari,
Wakati huo tayari Kingarame alishaingia kwenye gari, huku ame mkaba mama Monalisa, akiwakuta Kibabu na Hokololo, ambae aliondoa gari mala moja, na kukamata uelekeo wa barabara kuu, poliai wenzake waki kodoa macho kumshangaa, wasi weze kuwashambulia kwakuwa walikuwa bado wanamshikilia mama Monalisa, na hilo ndilo lilikuwa kusudio la wakina Kingarame, maana walijuwa kuondoka na mama Monalisa kuta wasaidia wasi shambuliewe na mtu yoyote, “afande mbona tuna waachawanaondoka?” aliuliza OC CID, WA Iringa huku akimsogelea RPC wake, “kwani we uoni kama wapo nayule mwanamke, ebu tuingie kwenye gari haraka sana, tuakikishe awatupotei, alisema RPC Iringa waki shuhudia Toyota land cruzer alilopanda Kingarame, liki kata kona na kuchukuwa uelekeo wa songea, na wao wakaingia kwenye magari yao na askari wao, walio kuwa na silaha, kisha akaondoka kwa mwendo ambao wao waliuita mwendo wakasi, huku wakina Kisona wakiwatazama, makamanda na askari wao wakiondoka kwenye msafara wao wamagari sita, huku bpolisi wengine wakibakia mahali hapa.
Sasa tatizo likawa kama ifwatavyo, kati ya askari polisi walio ingia kwenye magari ya makamanda wa polisi, walikuwepo askari kumi na mbili walio shirikiana na Kingarame katika matukio mbali mbali, na ndio alio kuwa nao jana usiku, mpaka mida hii alipo kujanao hapa hotelini, kiukweli jambo hili makamnda awa hawa kuliwaza kabisa, lakini kuna mtu alie liona swala hili.
“Ok! Katembo askari waingie kwenye gari letu, na hili la makambko liwarudishe hao mashaidi makambako, akikisheni usalama wao” alisema kisona ambae akuonyesha uharaka wa kuwawai wakina Kingarame, “kijana naomba ukamwokoe mke wangu, polisi wale siwaamini kabisa” lisema mzee Anderson, akionyesha kuchanganyikiwa, usijali mzee we kuwa na amani, mkeo tuna rudi nae” alisema kwa sauti tulivu kabisa Kisona, wakati huo ana washuhudia askari wake aliotoka nao Songea, pamoja na Edgra, wote wakiwa na SNG zao mikononi, wakiingia kwenye gari lao, aina ya land rover mia na kumi, “lakini naona kama mnachelewa sana, sidhani kama mtawakuta” alisema baba Monalisa, nikama alianza kukata tamaa, na matendo ya taratibu ya Kisona, mbae sasa hakujibu kitu, alikuw anamshangaa Monalisa ambae alikuwa anaingia kwenye gari, hili la kijeshi, “we! binti, unaenda wapi?” aliuliza Kisona kwa mshangao, “naenda nanyie” alijibu Monalisa, akimalizia kuingia kwenye gari na kukaa kwenye set ya kati kati pembeni ya Katembo na Edgar, huku wale askari wanne, wakiwa wamekaa seat ya nyuma kabisa, yani zile zilizo tazamana, “hapana binti, ebu baki na baba yako, huko siyo salama kwako” alisema Kisona kwa sauti ya kawaida tu!, lakini ilionyesha aikuwa na utani, “mimi sitaki kuwa mbali na Edgar, alafu unataka hao mapolisi waniuwe” alisema Monalisa akionyesha, kutokuwa na dalili ya kuto kushuka, toka garini, “ok! umesha zowea risasi” inaonyesha Kisona aliona itawapotezea muda, aliongea hayo uku anaingia kwenye gari na kufunga mlango, kisha aka mtazama mzee Mbogo, “naufahamu mwendo wako, ndio maana sikuwa na wasi wasi, kama watatuhacha mbali” alisema kisona ambae alikuwa na hakili mala mbili,
ya kwanza ni kwamba, Kisona alijuwa kuwa nivigumu kwa wakina kingarame kufwata barabara moja kwa moja, lazima kuna sehemu wata chukuwa maficho, sehemu ili wenzao wapitilize, na wao watokeze na kutafuta uelekeo mwingine, nandipo wao watakapo kutana nao, na pili ni kwamba wao wangeondoka mapema lazima wakina Kingarame wangejuwa wanafwtiliwa na wakinani, na kuwexza kuwakimbia, lakini kwa sasa, watawaona wenzao tu! wanawafukuza, hivyo wataongeza mwendo wakiwakimbia polisi wenzao, lakini kwa mwendo wa baba Edgar, lazima watawapita polisi wanyuma, na kuwafukuzia wakina Kingarame, ambao watazania kuwa tayari wamesha wakimbia wenzao,**
Erasto likurupuka toka chumbani, akiwa na kikasha ha pete mkononi, na kukuta wazazi wake pmoja na mzee Anderson wakiwa waanajadiliana cha kufanya, lakini mwisho mzee Anderson alifikia uamuzi mgumu, akamtazama Dereva wake, ingia kwenye gari tuwafwate” alisema baba Monalisa, ambae akuona sababu ya kubakia hapa hotelini, wakati mke wake na mwanae hawapo, hapo mzee Anderson na dereva wake akaingia kwenye gari, akifwatiwa na rafiki yake Misago, na mke wake, ambao waliona kuwa kuonyesha ushirikiano ndio njia pekee ya wao kufuta makosa yao, yaliyo sabaishwa na Erasto ambae hakuwa anajuwa kuwa, alicho kifanya jana usiku, kilionwa na wakwe zake watarajiwa,”namimi naenda” alisema Erasto huku akiingia kwenye gari na kufunga mlango, hapo hapo kila mmoja akaziba pua yake, kwa harufu ya mikojo yapombe, mbayo kijana huyu alitopka kujikojolea wakati wa milindimo ya risasi, nazani leo fupi, ni sababu ya matatizo ya umeme, ila kesho ni kutwa mala mbili, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata