BIKIRA YA BIBI HARUSI (83)

SEHEMU YA THEMANINI NA TATU (83)

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI (82) “Ingekuwa ametokea songea, ningesema yupo mpango mmoja na Kingarame” alisema RPC Ruvuma akiendelea kumlahumu mwenzie wa kutoka Iringa, ghafla wakasikia mlio wa risasi ukitokea nyuma ya msafara wao, RPC Ruvuma akageuka kutazama nyuma, alicho kiona kilimstua RPC Ruvuma, “aya ndio aliyo yataka huyu mpuuzi” alisema RPC Ruvuma, huku anashuhudia lile gari lanyuma kabisa. ENDELEA ……..
Liki poteza uelekeo na kuanza kuyumba yumba, kisha likaa sawa na kusimama, inamaana mmoja kati yawatu walio kaanyuma alipiga risasi hewani na Dereva kwa uoga akapoteza uelekeo, akijuwa kimeshanuka, ile anasimisha gari tayari askari wawili walisha ruka toka nyuma yagari, na kufungua milango yote miwili, ya mbele kisha waka wachomoa wale waliokuwa mbele, yani dereva na yule koplo, waka wanyang’anya silaha na kuwa sukumia pembeni, wakiwasindikiza kwa mateke, na ngumi nzito, alafu wakaingia kwenye gari na kugeuza gari, kisha waka kanyaga mafuta, kuanza kurudi waliko tokea, yani uelekeo wa Songea,
Hakika kilikuwa kitendo cha haraka sana, wakati huo tayari msafala wa magari ya mbele ya polisi ulisha simama, na kushuhudia kitendo kile, huku RPC Ruvuma alisha mwamrisha dereva wake ageuze gari kuwafwata, lakini kutokana na kuwa lilikuwa lina vuta gari lingine, ikawa vigumu kwao kugeuka haraka, na ndivyo ilivyokuwa kwa magari mengine pia, RPC Ruvuma akashuka toka kwenye gari na kumfwata RPC, Ruvuma ambae pia alikuwa anashuka toka kwenye gari lake, akiwa na SMG yake mkononi, kilicho mshangaza RPC Ruvuma, nikwamba RPC Iringa akuonyesha wasi wasi wowote, ndio kwanza alitabasamu, “afande kuna jambo la kulitabasamia kweli” aliuliza RPC Ruvuma kwa mshangao, wakati huo walishuhudia helcoptel ya jeshi ikikatiza hanga kwa speed ikielekea Njombe, “ilikuwa lazima haya yafanyike ilikuwapata wenzake” alisema RPC Iringa huku anaikoki silaha yake na kuiinua juu, kisha kwa mala ya kwanza toka aichukue ghrani, silaha hii, akafyatua risasi mbili hewani, kwa kupishanisha sekunde kma tano hivi, “afande unamaana gani kuwajuwa wenzake, haya sasa kama tumsha wajuwa siwamesha kimbia?” aliuliza RPC Ruvuma, kwa sauti ya mshangao, wakati huo makamnda wenzao walisha sogea, usiwe na wasiwasi kaka, waambie askari wafungue hayo magari yanayo vutwa turudi tuka chukue mizoga na watakao salia” alisema RPC Iringa kwa sauti ya kujiamini, “lakini afande kumbuka Kisona umesha mklofisha na amesha pita hapa….” kabla ajamalizia RCO wa Iringa, RPC Iringa akaachia kicheko kikali sana, “kumbe na mimi ni wiva katika kupanga game, inamaana amkufahamu kama nilikuwa na igiza?” mpaka hapo wote waka tazamana kwa mshangao, “tena kwataharifa yenu huko anakoelekea Kingarame, anajipeleka na Kifo chake mkononi, Kisona anamsubiri huko” hapo sasa mwenye kucheka alicheka na mwenye kumsikitikia Kingarame alimsikitikia.**
Milio hii ya risasi iliwafia wengi ata wana kijiji cha Kifanya ambacho kilikuwa nyuma kidogo ya pale, walipo kuwa polisi, wengine ni mzee Misago na familia yake, ambao wali kuwa wa tembea kidogo wakivizia magai toka songea ili wapande mapaka Njombe, awa kujuwa kuwa mida hii ya saa saba mchana magari uwa yamesha pita muda mrefu sana, hapo mpaka saa tisa na saa kumi ndio magari uwa yana pita kuelekea Njombe, “sijuwi akama watatoka salama, naommbea ata wafe kabla awaja msimulia mtoto wao, kilicho toke jana” alisema mama Erasto, na kuwa stua baba na mwanae Erasto, “he! mama kwanini unasema hivyo?” aliuliza Erasto kwa mshangao.
Wakati huo walikuwa wanatembea taratibu, huku pori na misitu ikiwa ime tanda pembeni ya barabara, “hivi we unazaniuliyo yafanya jana ni mambo madogo?” aliuliza mama Erasto kwa suti ya ukli kidogo, huku akisimama kw uchou na kumtazama mwanae, hapo Erasto aka vuta kumbu kumbu ya tukio la jana, pale mapokezi, “haaa! inamaana mlisikia?” aliuliza Erasto kwa mshangao, “siyo kusikia tumeona kabisaaaa” alisema baba Erasto, huku na yeye ana simama, na kujishika kiuno kwa uchovu, “mama weeee! inamaana na wakina mama Mona walisikia?” aliuliza Erasto huku akihisi miguu yake inakosa nguvu, safari hii akuna alie mjibu, kikapita kimya cha sekunde kadhaa, wote wakionekana wana tafakari jambo, “jamani mbona magari ayapiti?” alisema baba Erasto, na Erasto akadakia, “yani baba baada ya kuikilia utanisaidiaje, wewe unawaza gari?” nikama wazaziwake awakumjali sana, lakini baada ya sekunde kadhaa, mama yake akajibu, “usiwe na wasi wasi, kwanza walikuwa na mawazo ya Mona, pia walikuwa wameshalewa sana, awawezi wakakumbuka mambo ya jana” alijibu mama Erasto, pasipokufikili yeye amewezaje kukumbuka, jibu hili lilimpa moyo Erasto, maana uwa anamwamini sana mama yae, anapo mwambia jambo lazima lifanikiwe.
Wakati huo huo, wakasikia muungurumo wa gari, wote wakageuza shingo zao kutazama walikotokea, wakaliona gari aina ya land rover , mia na Kumi, rangi ya Kijani, “wote wakatabasamu “afadhari gari a wale wanajeshi hilooooo” alisema mzee Misago, huku wakijiandaa kulisimamisha litakapo sogea karibu,wanafamilia awakujuwa wakina nani walio kuwa ndani yagari. **
Walikuwa ni wakina mzee Anderson, mke wake na askari wawili, huku dereva wake akiendesha gari hili kwa speed kali, huo ndio ulikuwa mpango wa Kisona, kuwa changanya hakili wakina Kingarame, wajuwe kuwa wao wamesha tangulia, Monalisa kama kwaida yake akutaka, kuwa mbali na Edgar, sijuwikwajili ya usalama wake au mpenzi yao yaliyorudikwa kasi ya maana.
“mi menzenu simwelewi Mona, hivi bado yupo salama kweli?” aliuliza mama Monalisa, alie kaa kati kati ya awa wanjeshi wawili kwenye seat za kati kati za gari, “mama Mona umeshaanza kwani yeye Mona ajitambui” alisema baba Monalisa huku macho yakiwa mbele, kwenye barabara, kama vile anamsaidia dereva kuangalia sehemu zakupita, “atakama anajitambua, we siunajuwa Mona anavyo mpenda Edgar?” alisema mama Monalisa, kwa msisitizo, hapo baba Monlisa akacheka kidogo, “sasa kama anampenda?” aliuliza kwa namna ya kujizuwia kuendelea kucheka, “sijuwi kama ajajilegeza, na kutolewa bikr….” alishindwa kumalizia mama Monalisa, na kuwatazama wale askari aliokaa nao, kwa awamu, lakininikama walisha juwa alicho taka kuongea mama huyu, “si makubaliano yao, kwani angekuwa ame mbaka, wasinge kuwa pamoja vile” alisema baba Monalisa, na wakati huo mbele yao wakawaona wakina Misago wana wasimamisha, “wakina mama Erasto haoooo, wamekujaje huku?” aliuliza mama Monalisa kwa mshangao, maana akutegemea kuwaona hapa, akujibiwa zaidi mzee Anderson alisema “usisimame” na hapo dereva akaongeza mafuta, na kuwa pita ka awawajuwi, “we mzee mbona una roho ngumu hivyo?” aliuliza mama Mona kwa mshangao, mana akuamini kilicho fanywa na mume wake, “walisema wao tutakutana Njombe, sasa hapa siyo Njombe” lijibu baba Monalisa, ata wale wanajeshi walishangaa kwanini mzee huyu anasema hivyo, “hapana jamani siyo vizuri, unajuwa awa wame kuja huku kwaajili yetu?” alisema mama Mona kwa sauti ya kubembeleza, walisha tembea zaidi ya mita mia nane, toka waipo waacha wakina mzee Misago, na hapo baba Monalisa akamwambia dereva, ageuze gari wawarudie wakina mzee Misago.***
Kingarame alishukuru sana mizimu yake, asa baada ya kuona kuwa, polisi awakuwa na mpango wa kuwafukuzia, “sasa ni kuknyaga mafuta mpaka madaba tumwambie Bosso, aamishe mizigo pale nyumbani kwangu, tukakutane nae Matimila, maana hatuna ujanja zaidi ya kwenda kujificha msumbiji” hiyo ilikuwa ni sauti ya Kingarme, ambae alikua amekaa nyuma yagari na bahadhi ya askari wake, wapuuzi sana, walifanya kosa kumkorofisha yule mpumbavu” alisema tena Kingarame, akimanisha kuwa, RPC alifanya kosa kumkorofisha kanal Kisona, ambae mpaka mida hiyo alikuwa anajuwa kuwa alisha pita kuelekea mjini, “kama Hokololo ungekuwa aujapigwa risasi ya mguu, ungekamata gari” alisema tena Kingarame, huku gari likiwa limesha kiacha kijiji cha Kifanya, na sasa lilikuwa lina ingia kwenye pori la kuelekea lukumbulu,
Baada ya kutembea kwa kilomita nne mbele wakiwa wanapunguza mwendo, ilikuanza kona lukumbulu, wakatazama mita mia moja mbele yao, wote waka hisi miili iki wasisimka na matumbo yakijikologa, kama vile walikula chakula kilichoanza kuaribika, maana yaliungruma, kwa hofu iliyo wapata.
Kingarame akuamini macho yake, baada ya kuwaona askari wawili wa jeshi la jeshi la ulinzi, wakiwa wamesimama kati kati ya barabara, huku wame zinyoosha silaha zao, kuwa tazama wao, nikama ilivyo tabiliwa na kamanda Kisona, Dereva wa gari lililo wabeba wakina Kingarame alipoona hivyo ali kanyaga breck za ghafla, na kusababisha gari liyumbe nusu ya kujichota, huku likikosa mwelekeo na kuacha njia, likielekea upande wa kushoto wa barabar, kama unaende songea,
Mwisho wake ukiwa ni kuuvaa mtaro wa pembeni ya barabara, ambapo lilikita kwa nguvu na kukwamia hapo hapo,
Hapo akuna alie subiri wala kusikilizia maumivu, kila mmoja alie kuwa ndani yagari alijitoa kwenye gari, na kuingia porini, ata wale walio shambuliwa na risasi za miguu, awakuzubaha, walijikongoja nakuingia porini, “afande nisaidie, na mimi” alilalamika Hokololo lakini Kingarame akujari, wala kumsikiliza, maana alisihajuwa sasa ameingia kwenye angaza Kisona, ila kuna jambo Kingarame akulijuwa, kuwa tayari askari wa jeshi la ulinzi walikuwa wame gawanyika kwenye maicho pande zote mbili za barabara, ambao alikuwa ni yeye Kisona na mzee Mbogo, walikuwa upande wa kushoto mwa barabara, kule waliko kimbilia wakina Kingarame, pia upande wa kulia mwa barabara, walikuwepo koplo Katembo, Edgar na kama kawaida Monalisa akutaka kukaa mbali na Edgar.
Wale askari wawili wa barabarani walianza kukimbilia kule waliko kimbilia wakina Kingarame huku wakina Edgar nao wakihama, toka upande wa kulia wa barabara na kuamia upande wa kushoto, waliko kimbilia wakina Kingarame,
maskini kingarame baada ya kupiga hatua kadhaa, za mbio, ndani ya pori, huku askari wawili wakiwa mbele yake, na wengine wakijikongoja nyuma yake, aka stuka kumwona askari wake mmoja akidakwa na Kisona, alie ibuka ghafla na kumtandika kumi nzito ya Kifua, iliyo mtupa nyuma, hatua kadhaa, akitengana na SMG yake, huku yule wanyuma ya yule alie pigwa ngumi, yani mbele ya Kingarame, akiangaika kujiweka tayari, ili kumtandika Kisona, ambae alimuwai kwa kumrukia teke lla kifuani, (frayng kick) lililo mrusha yule askari alie angukia karibu na Kingarame, aliekuwa anakuja mbio mbio, huku silaha yake ikimtoka mkononi, huku Kinagarame akajikuta ana mpalamia askari wake na kujibwaga chini, kiliicho msaidia ni kwamba yule askariwa kwanza alikuwa ameinuka na kutaka kumshambulia Kisona, lakini bahati akuwa ya kwake, alikutana na teke la uso, lililo tuwa maeneo ya shavuni, na kabla ajapoa vizuri, akakutana na ngumi kadhaa za kifuani zilizo mrusha nyuma, hapo tayari Kingarame alijiinua na kugeuka akirudi aliko toka, kwa mbio za kuogopa mbwa, sababu kitumbo chake kilitangulia mbele, huku yule askari wa pili akiinuka na kuanza kuitafuta bunduki yake lakini kabla ajaipata aka stukia akizibuliwa teke la usoni, na wakati huo huo ikasikika ‘pah!’ Kisona akageuka kutazama nyuma yake, akamwona yule askari alie mshambulia mwanzo, akianguka chini huku amesha poteza maisha, kumbe alipigwa risasi na baba Edgar, ambae alimwona yule askari polisi akiokota silaha yake na kutaka kumshambulia Kisona, hapo Kisona aka mtandika ngumi nzito ya uso yule askari alie kuwa anatafuta silaha yake, nae akakata moto, (alizimia), tayari polisi waliisha badiri uelekeo na kurudi barabarani.
Lakini awakufika mbali, tayari walisha waona askari wengine wanakuja, wakiwa pamoja na Edgar na Monalisa, hapo ikawa mtafaluku, japo Polisi walikuwa wengi kidogo, lakini walijiona kuwa ni wachache sana, maana mbele na nyuma yao walisha zungukwa, ndipo Polisi walipo pata wazo la ghafla, maananikama waliambizana wote wakatawanyika kila mmoja akielekea upande wake, kwa hili lili wachanganya askari wa jeshi la ulinzi, hapoKisona aliwaona askari wake wakiduwaha, huku polisi wakitokomea porini, Kisona aka mtazama Edgar, ambae alikuwa amesimama mita kama kumi natano upande wa magharibi, SMG mkononi, nyuma yake Monalisa amejibanza, itaendelea hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata