BIKIRA YA BIBI HARUSI (84)

SEHEMU YA THEMANINI NA NNE (84)

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TATU (83) maana mbele na nyuma yao walisha zungukwa, ndipo Polisi walipo pata wazo la ghafla, maananikama waliambizana wote wakatawanyika kila mmoja akielekea upande wake, kwa hili lili wachanganya askari wa jeshi la ulinzi, hapoKisona aliwaona askari wake wakiduwaha, huku polisi wakitokomea porini, Kisona aka mtazama Edgar, ambae alikuwa amesimama mita kama kumi natano upande wa magharibi, SMG mkononi, nyuma yake Monalisa amejibanza. ENDELEA……….
Kisona alipo mwona Edgar nae anamtazama, aka inua mkono wake wakushoto na kumwonyesha ishara ya vidole viwili vya kati, kwa kuvipeleka usoni kwake na kuwaonyeshea polisi wa waliokuwa wanakimbilia upande wa kulia, na kisha aka mtazama mzee mbogo, nae akamfanyia hivyo hivyo akimwonyeshea upande wa kushoto, kiisha aka akamtazama Katembo, nae aka mwonyeshea upande wa barabarani, na wale wengine akawaonyesha watazame pandezote, kisha yeye aka comoka mbio kumkimbilia Kingarame, ambae alikuwa anakimbilia upande wa kusini, yani kulia,
Hapo kilicho fwata ni haraka sana, kila mmoja akaa kwenye mkao ambao anaona ata weza kutumia vizuri silaha yake, wakati mzee Mbogo na atembo wali kuwa wamesimama, Edgar na waleaskari wengine walipiga goti, Monalisa nae alipiga goti nyuma ya Edgar, hapo zikaanza kusika ‘pah! pah!’ huku askari mmoja baada ya mwingine wakianguka chini, wakilia kwa machungu, ya risasi za miguu, walizo tandikwa, ikiwa ni moja kati ya maagizo ya Kisona, katika operation hii, maana ni sehemu ya makubaliano yake na RPC Iringa, kuwa watu awa, wasiuwawe ili wafikishwe kizimbani, lakini tayari mmoja alisha uwawa. ***
Ndani ya mji mdogo wa Njombe, ilionekana Helcopter ya jeshi a ulinzi, ikishuka taratibu kwenye kiwanja cha mpila wa miguu, kilichopo kwenye kambi ya polisi, ya wiliya hii ya Njombe kisha wakashuka makamanda watu wajeshi la ulinzi pamoja na mama mmoja mtu mzima, lie kuwa amevalia kinyumbani nyumbani, inaonyesha hakuwa amejiandaa na safari, maana alivalia gauni la kawaida na kujifunga vitenge viwili kimoja kikianzia kiunoni, na kikingine kifuani, uso wake ulionyesha tabasamu la flani lililo changanyika nakihoro, wote waliongozana na walinzi watatu, wenye silaha aina ya M-16.
Makamanda awa yani briged commander na wa nadhimu wake wawili, walipokelewa na mkuuwa kambi la makambako, mwenye cheo cha kanal, ambae alisha fika muda mrefu na askari wake, pia alikuwepo OCD, na OC CID, wa hapa Njombe, “hatuwezi kuondoka mpaka CDF aingie, yupo njiani anakuja” alisema brig Haule, baada ya kuwa amesha salimiwa kwa salut na mkuu wakambi la Makambako, ambae waliongozana mpaka pembezoni mwa uwanja, ulio zungukwa na askari na maafisa wa jeshi la ulinzi, na polisi wachache, walio onekana kuwa wapo tayari kwa mapambano.
“wakati tuna wasubiri wakuu, ebu nieleze kwa kifupi, jinsi hali ilivyo kuwa mpaka sasa ilivyo” alisema mzee Haule, na hapo CO wa kambi la Makambako, akisaidiana na OCD, walieleza jinsi kila mmoja alicho sikia na kushuhudia katika mapambano yah ii operation, inayojulikana kama KIFO MKONONI, maelezo ya CO yalikuwa mafupi tu alieleza jinsi alivyo mpokea Kisona nawatu wake, na misaada aliyo mpatia, pia alimweleza jinsi walivyo pokea majeluhi na kuwaifadhi kwenye hospital ya jeshi, pmoja yule jambazi lie kuwa mahabusu ya kijeshi, mpaka leolajili alipo kuja kumleta mgonjwa mwinginena kuomba msaada wa askari,
Kwa upande wa OCD, yeye alisimulia kuanzia alipopokea simu toka iringa akipewa maelekezo ya kuwa kuna askari wanakuja toka songea, wana fukuzia jambazi, na kwamba asichangae wakinya kazi ndani ya wilaya yake, na baada ya hapo akasikia tena wamesha muuwa jambazi, lakini imetokezea tukio jingine, kuwa kunajambazi mwingine amemteka mwanamke, na hivyo anatatfutwa, OCD aksimulia ujio wa RCO Kingarame, mpaka kuanza kwa mauwaji na kisha kuongezekakwa askari na makamanda wakuu wa mikoa, mpaka kufikia leo ilipo bainika kuwa Kingarame mwenyewe ndie jambazi,
Wqakati huo huo wakaanza kuona Helcopter Mbili zikiwa hewani, Moja ikiwa mbele, na nyingine ikiwa nyuma inaonekana kwa mbali, lakini ilikuwa inakuja kwaspeed kuliko ile ya mbele, “haoooo! wanakuja, ninacho cha kuanzia” alisema Briged commander wa brigade ya tano, huku ana geuka pande zote mbili kutazama jinsi askari walivyo jipanga, lizika na mpango walio kaa askari wote, yani polisi na wa jeshi la ulinzi.
Dakika mbili baadae tayari Helcopter ya polisi iligusa ardhi, pale pale kwenye uwanja wa mpira, nae akapokelewa na briged kamanda, wakati huo tayari Helcopter ya jeshi la ulinzi aina ya Holex gun ship callier, ikiwa ime ganda juu ya uwanja, ina subiri helicopter ya polisi, itulize panga lake la juu, ili na wao washuke, “leo kazi ime kuwa kubwa, dar es salaam yote imeamia njombe” aliwaza Haule.
Dakika cache baadae tayari makamnda wa jeshi la ulinzi nao walisha tuwa na kukutana na brigadier Haule, ambae aliwapa utangulizi wa opretion Kifo mkononi, kwa kifupi, na hapo majeshi yaka amuliwa yaondoke kuelekea upande wa kusini, yani barabara ya songea, kule kwenye mapambano. huku mama Edgar akipekwa Serena Hotel, ambako leo ulinzi ulikuwa mkali sana, kutokana na tukio la mchana asubuhi yaleo,
Baada ya kufik pale alikanbidhiwa funguo za chumba cha mzee Mbogo, yani zile za hakiba, nae akajiungia chumbani humo akingoja mume wake na mwanae warudi kutoka porini. **
“Yule ni baba Eddy anae endesha gari, awezi kusimama” alisema mama Erasto, kwa sauti iliyo jaa chuki kubwa sana, “kumbe niyeye ndie anae endesha gari?, atakwa dawa asinge simama” alisema Erasto, kwa sauti ya kuaminisha kuwa, mzee Mbogo ni mtu mwenye roho ya hivyo, “yani wanatuchukia sana wale, ndio maana Edgar amemteka Mona, ili kunivurugia mipango yangu ya kumvisha pete” alisema tena Erasto, kwa sauti iliyoonyesha chuki ya wazi kwa Edgar, “wala usiwe na wasi wasi Monalisa ni mchumbawako, tena leo unamvesha pete, pale pale Hotelini” alisema mama Erasto kwa kujiamini, wakati huo waka liona lile gari la jeshi likiwa lina kuja kutokea upande wa Njombe, “haooo! kumbe walikuwa awaendi mbali” alisema Erasto, huku Misago na familia yake wote wakilikodole macho lile gari, la jeshi ambalo lilikuja karibu yao na kukugeuza tena kutazama Njombe, kisha likasimama.
Safari hii, Misago na familia yake ndipo walipo pata nmafasi ya kuwaona waliokuwemo ndani ya gari, waka duwaha, “twendeni” alipanza sauti mama Monalisa, kwa sauti ya uchangamfu, “dada, umepona, yani hapa, nilikuwa na hofu, presha inapanda muda wote” alisema mama Erasto huku ana lisogelea gari ambapo Askari mmoja aliwafungulia mlango wa nyuma kabisa, na wao wakaingia, “we! acha tu, kumbe yule kijana mwanajeshi kama tunge msikiliza, tusinge wasigelea wale polisi majambazi” alisema mama Monalisa, huku dereva anaondoa gari, wakati huo arufu ya mkojo ikianza kusambaa mle ndani ya gari, “kwahiyo ume watoroka?” aliuliza mama Erasto kwa shahuku, muda wote baba Edgar, alikuwa akimya akitazama mbele, “nisingeweza uwatoroka atakidogo, atahivyo na washukuru sana wakina Edgar, wamenisaidia sana” alisema mama Monalisa, na kuwafanya wakina Erasto wastuke, “kwani Mona yupo wapi?” aliuliza Erasto aliuliza kwa sauti iliyo jaa shahuku, “yupo na Edgar, wanatakuja na gari langu” alijibu baba Monalisa, kwa sauti kavu na tulivu, huku akitazama mbele, “ haaaa! mme mwacha na Edgar?” aliuliza Erasto kwa sauti ya juu iliyo jaa mshangao na hamaki, kiasi cha waleaskari wawili kumshangaa sana Erasto, walikuwa wana mfahamu maana walisha mwona mala kadhaa pale Serena hotel.
“Kwani kuna tatizo, si amebaki na mchumba wake?” askari mmoja alijikuta ame lopoka, pasipo kujuwa kitu, Erasto na wazazi wake, wote wakazizima, kwa mshangao, “nani kakuambia Mona mchumba wa Edgar?” aliuliza mama Erasto kwa mshangao, yule askari akaonekana kushangaa kidogo, akamtazama mwenzie ambae pia alikuwa ameshangaa, wakatazamana, “wale nimarafiki tangu utotoni, Edgarmekuwa akimsaidia sana Monalisa, ata mama Eddy alisema kuwa watoto awa watakuja kuwa mke na mume” alisema mama Mona kwa sauti moja tulivu sana, iliyo vuta kumbukumbu ya zamani, nikama aligundua makosa yake, mama na baba Monalisa, walistuka kidogo, wakiona dalili ya mama Monalisa kuanza kulizik na ukaribu wa Monalisa, na Edgar, “lakini Edgar, akaja kuwa rafiki mbaya kwa Mona, alitaka kumfundisha uhuni, ndipo Monalisa na wazazi wake awakutaka tena familia yao iwasogelee, sindio mama?” alisema Erasto huku ana mgusa mama Mona begani, ili athibitishe maneno yake, “nandilo kosa tulilo lifanya, kuamini kuwa Edgar, anamfundisha Monalisa huuni” safari hii alijibu baba Monalisa, “yani huyu, asijifanye kumtongoza Mona, nita mpiga mbele ya wanajeshi anao jivunia” aliongea Erasto kama mjinga, hapo wale askari pamoja na wazazi wa Monalisa, na dereva wakacheka kidogo, kisha mama Mona akasema, “usije ukasababisha tupitilize hospital, atakacho kufanya, autokaa usahau” ***
Dakika tatu za milindimo ya risasi, zilikoma, tayari askari wote waliokuwa wanajaribu kukimbia walikuwa wamesha lala chini, wana ugulia maumivu ya risasi za miguu, kasoro SSP Kingarame ambae akuwepo eneo hili, siyo yeye peke yake, ata Kisona nae akuwepo mahali hapa, hilo alikuwastua wakina Edgar, ambao walisadiana na wakina Katembo, na baba yake, kuwaswaga wale askari polisi, walio saliti kihapo chao, na kushiri ujambazi, akiwepo Hokololo, ambao waliwapeleka upande wa barabarani wakiwa wamesha wanyang’anya silaha zote, muda wote Monalisa alikuwa nyuma ya Edgar, kiasi kwamba mama Edgar alijikuta akitabasamu.
Kingarame alikimbia kwa dakika kadhaa, akikatika vichaka vifupi na miti mirefu, akujari uchovu, wala kuchoka, akujari vijiti wala miba zilizo kuwa zina nasa kenye nguo zake, na kuivuta ngozi yake, akizidi kutokomea porini, pasipo kuona mtu yote anae mfwata, “shauri zao waache wauone moto, nini nalala mbele” alijisemea kimoyo moyo Kingarame, akijuwa kuwa tayari ameshafanikiwa kuwatoroka.
Kingarame baada ya kukimbia umbali alio uona ni mrefu, na milio ya risasi, aikusika tena masikioni mwake, akasimama na kugeuka nyuma, kutazama kama kuna mtu ana mfwata, akaona kuwa hakukuwa na dalili ya kufwatwa na mtu yoyote, hapo aka shika magoti na kuhema kwanguvu, akivuta nguvu ya kuendelea kukimbia, lakini ghafla akaona kitu kamakimvuri kikiwa mbele yake, ile anainua uso, yani kabla ajaona kilicho simama mbele yake, aka stuka ngumi nzito ikituwa usoni mwake, na kumfanya sikie maumivu makali, sambamba na giza zito lenye vyota za njano, itaendelea hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata