
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA (86)
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO (85) Mama Edgar alitumia dakika mbili kumaliza ngazi nakutoka nje, kisha akaanza kueleka kwenye maegesho ya magari maana alilionalile gari la jeshi likiwa limesimama eneo hili, huku polisi wakionekana wengi pale nje, lakini ghafla mama Edgar, ile kutazama kwenye gari vizuri, aka mwona mama Monalisa akishuka toka kwenye gari pamoja na Mume wake, huku askari mmoja wa jeshi la ulinzi akifungua mlango wa nyuma wagari, hapo mama Edgar akasimama na kutazama lile gari, akiona mlango wa nyuma ukifunguliwa na wakashuka wakinamama Erasto mume wake na kijana wao Erasto, mama Edgar akaishiwa pose, endelea……..
“Kumbe walishakuja huku” aliwaza mama Edgar huku anageuka na kurudi ndani, maana akuppenda kukutana na watu awa, ukiachilia kuwa Erasto alimkumba kikumbe pale dukani wakati anamsubiri mume wake, kwa sonara, pia akuwa na mausiano nao mazuri toka miaka iliyo pita, sababu ikiwa ni barua ya Edgar kwenda kwa Monalisa, lakini ile anageuka tu aka stuliwa, “samahani mama wewe ndie yule mgeni wa chmba namba tatu, ghorofa ya yatatu?” alikuwa ni dada mmoja hudumu wa upande wa vya kula, “ndio mimi” alijibu mama Edgar huku anageuka kuwatazama wakina mama Monalisa, kuakikisha kama watakuja huku au wataelekea wapi maana hakutaka kukutana nao, akawaona wana kuja upande ambao una viti pakionyesha kuwa nisehemu ya vinywaji na vyakula, japo leo apakuwa na watu wengi kama siku za nyuma, zaidi walionekana watu wachache wakiwepo polisi, na familia ya mzee Mohamed, “ndio ume kuja kula ni kuhudumie?, maana manager amesema, imeagizwa uhudumiwe kila kitu unacho itaji” alisema yule dada, ambae sasa alikuwa amesimama na mama Edgar, “hapana nitakula baadae kidogo” alisema mama Edgar, huku ana geuza tena shingo yake na kutazama kule waliko kuwa wanatokea wakina mama Monalisa, akwaona wakielekea kwenye meza mmoja na kukaa wote sita.
Mama Edgar kaanza kuelekea ndani ya jengo la hotel, ambako alikuwa ametoka huko muda mchache uliopita, akipishana na na dada mhudumu wa Erasto, alie kuwa anatoka mapokezi na kuelekea nje, wakati mama Edgar anapandisha gazi, dada mhudumu alikuwa anatoka nje, na kwenda kusimama kwenye kibaraza cha mbele ya jengo la Hotel, macho kwa mpenzi wake Erasto, alie kuwa amekaa na wazazi wake na wakwe zake, akaona kuwa bado awaja hudumiwa, akawasogelea, huku Moyo wakeukiwa umekosa amani kabisa, sababu alijuwa kuwa kuonekana kwa Monalisa, ndio kuondoka kwa mpenzi wake huyu, na ndio mwisho wa mapenzi yao, na yeye alikuwa anaitaji, mlevi huyu aendelee kuwepo mahali hapa, ili yeye endelee kujipatia fedha. “habari jamani, niwahudumie nini?” aliuliza dada mhudum, huku akimkazia macho Erasto, “kwanza kabisa tuitie mhudumu wa jikoni, alafu mimi niletee (hapo akataja pombe anayo kunywaga na mke wake) chupa mbili” alisema baba Monalisa kwa uchangamfu mkubwa, akiagiza chupa mbili za pombe kali, “mh! mzee uta amaliza kweli?” aliuliza kwa msangao dereva, sababu hiyomoja tu! uwa anakunywa na mke wake na wanaewa chakali, “nime agiza na yanjiani, si unajuwa leo tunaondoka” alisema baba Monalisa, na mke wake akamuunga mkono.
Kila mmoja akaagiza kinywaji chake, kasoro Erasto ambae aliinuka na kuelekea chumbani kwake, kwaajili ya kuoga, maana toka alipo jikojolea, wakati wa milindimo ya risasi akuwa ameoga, akiwaacha wenzake, wakiwa wanasubiria maagizo yao, yani vyakula na vinywaji, huku mama Monlisa akionekana kuwaza jambo flani,
Dakika chache baadae alikuja mhudumu wa inywaji, yani demu wa Erasto, akiwa na vinywaji walivyo agiza, aliiweka harakamezani, na kuondoka zake, akapotelea ndani yajengo la Hotel, ambalo leo lilitapakaliwa na askari polisi.
Erasto alienda moja kwa moja, mpaka kwenye mlango wa chumba namba kumi na sita, akasimama mlangoni na kutazama mlango wa chumba namba kumi na saba, zika mjia picha mbili, moja ndio chumba ambacho kilicho kuwa kina miminiwa risasi, “sijuwi kwanini awa kumuuwa huyu mshenzi, mpaka ssa Mona anang’ang’ani” aliwaza Erasto huku ana fungua mlango wa chumba chake, jambo la pili alilo liwazza Erasto nikwamba, “inamaana huyu mshenzi amelala na Mona mpaka asubuhi, na zile kelele ni wao?” hapo Erasto alijikuta akishikwa na uchungu wa rohoni, akiwa waza kuwa mchumba wake mtarajiwa pngine tayari amesha ondolewa bikira yake, “kwanini awakumuuwa huko huko porini?” alisema Erasto kwa sauti ya chini iliyo jaa chuki, pasipo kujuwa kuwa kuwa, uhai wa Edgar, ndio usalama wa Monalisa.
Erasto kabla ajavu nguo zake, ali ingiza mkono mfukoni, na kuitoa pete, ikiwa ndani ya kikasha chake, akitazama kwa sekunde kadhaa, “lazima nimveshe, atakama amsha gongwa,” aliwaza Erasto huku anaiweka mezani, kisha akatazama pale juu ya meza, na kuangalia kama vitu vyake bado vipo salama, maana wakati anaondoka akuweka vizuri, alikurupuka, ikiwa pamoja na pochi yake, (wallet) akaichukuwa na kuifungua, akaona fedha zake zipo salama. akatazama begi lake, nalo lipo salama, akukuwa na dalili ya kufunguliwa, maana ndani ya begi hilo kulikuwa na fedha nyingi kidogo.
Hapo Erasto akavua nguozake na kuingia bafuni, ambako ile anaanza kuoga tu! akasikia mlango wa chumba chake ukifunguliwa, na kabla ajauliza ninani alie ingia akasikia, “nilikumisi mpenzi wangu” ilikuwa sauti ya dada mhudumu, ambayo ilimstua sana Erasto, ambae alihisi kama nisauti ya zimwi, na akizingatia jana amesha msababishia masala kwa wakwe zake, “ume fwata nini huku?” aliuliza Erasto kwa sauti ya ghazab, ambayo ilimfanya yule dada mhudumu ashtuke akidogo, “kwani nivibaya mpenzi?” aliuliza dada mhudumu kwa mshangao, huku akisogelea mlango wa bafuni, ambako Erasto alikuwa anaoga, “kwani we ujuwi, jana wenzako wameshitukia mchezo” alisema Erasto huku anaendelea kuoga, hapo dada mhudumu alicheka kidogo, nikwamba alishajuwa udhaifu wa Erasto, “una wasi wasi gani na vile walivyo lewa watakuwa wamsha sahau kila kitu” alisema dada mhudumu, huku akianza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine, nikama Erasto aliamini maneno ya dada mhudumu, maana akuona dalili ya mama Mona kumchukia, “unajuwa inaweza kuwa kweli hen!…” alisema Erasto akistuka kumwona dada mhudumu akiingia bafuni uchi kama alivyo zaliwa, Erasto macho yakamtoka, ungesema ndio anamwona leo kwa mala yakwanza, “usijali mpenzi, nimekuja kusherehekea kupatikana kwa mke mwenzangu” alisema dada mhudumu huku ana mkumbatia Erasto, kwa lengo la kumchota hakiri, ili na yeye ajipatie mkate wake wakila siku, maana alijuwa fika Erasto hakuwa na mpenzi, sababu zile kelel za uchungu zilizo toka chumba namba kumi na saba, ziliashiria kuwa Monalisa tayari amesha ionja dudu, “umemwona hen” alisema Erasto kama mjinga flani huku akikumbatiana na dada mhudumu, “nime mwona mzuri huyo, yani ume juwa kuchagua, mpaka na mwonea wivu” alijibu dada mhudumu, na kumfanya Erasto azidi kuvimmba kichwa.***
Ndani ya msafara mambo yalikuwa mchangamano, kila moja alikuwa anazungumza la kwake, juu ya tukio lile, wakatimkuu wa majeshi na wanadhimu wake, wakijadiri na watu waliokuwa nao nadani ya gari, jinsi watu tisa walivyo saidiana kulimaliza, (yani Kisona, na askari wake watano, ongeza mzee mbogo, pia Edgar na Monalisa, “unajuwa tukisema silaha peke yake ni uongo, hapo zime tumika mbinu za hatari sana” alisema CDF, akiongea na walinzi wake mpambe na dereva wake, ambao walimuunga mkono, “alafu kijana nime mkubari sana, unajuwa kikawaida kuna askari nikisimama mbele yao, wanatetemeka, lakini yule utazani ni na yeye ni general, kwa jinsi anavyo jiamini” alisema CDF, mwenyewe, “ila safari hii nimeshuhudia kazi yak anal Kisona”.
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya karibu kila gari, kasolo gari la kisona, na mzee Mbogo, ambao walikuwapamoja na Koplo katembo na askari wawili, “mzee Mbogo, unaonaje mwonekanao wa Edgar na Monalisa, kina dalili ya kuanzisha mausiano?” swali hili la Kisona, lilipokelewa kwa vicheko, wato wa watano ndani yagari, waliangua kicheko, na kumshangaza Kisona, “Monalisa amekubari mbele ya CDF Kuwa ni mpenzi wa Edgar” alisema Koplo Katembo, “haa! ilikuwaje mpaka akamwambia hivyo?” aliuliza Kisona kwamshangao, Katembo akasimulia jinsi yale mahojiano yalivyonkuwa, na jinsi Edgar alivyo jibu kwa kujiamini, “kwanza kwa mambo aliyo yafanya ni askari tosha kabisa”
Wakati huo wakina Edgar na Monalisa walikuwa ndani ya land lover mia na kumi, wame zungukwana walinzi wao safari inaendelea, “hivi Eddy ukiambiwa univeshe pete utakubari?” aliuliza Monalisa kwa sauti ya chini, huku ana mtazama Edgar usoni, mategemeo yake wale askari wasisikie, Edgar akamtazama Monalisa usoni, huku anatabasamu, “bila atakuambiwa, nikipata pete siku yoyote nakuvesha” alijibu Edgar na Monalisa akaachia tabasamu languvu, ambalo lilimfanya azidi kuwa mzuri, kiasi cha kuwa kodolesha macho wanajeshi wawatu, waliokuwa nao ndani yagari.**
Mama Edgar akiwa chumbani pasipo kuhisi nja kwa kihoro, alicho kuwa nacho, mala akasikia muungurumo wa gari, ukipita kwa nje akachungulia haraka sana, akaliona gari la jeshi, aka shuka haraka sana kama alivyo fanya mwanzo, lakini ile kufika chini, aka waona watu walio shuka akuwa anawatambua ata kidogo, zaidi aliwaona wakienda mapokezi na kukutana na manager, ambe wali mpa magizo ya chakula cha mchana, kwamba kuna wageni muhimu wanakuja kula.
Mama Edgar pasipo kujuwa kuwa na yeye ni mmoja kati ya ageni hao, akaona aya muhusu, akaguka nakuzifwata ngazi za kuelekea ghrofani kwake, ile anagusa ngazi akaanza kusikia miguno ya mapenzi, mwna mke akilalama kwa utamu aliokuwa anapewa, akahana nayo na kuelekea juu**
Saa nane mchana, ndani ya bwalo la polisi, makamanda wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, pamoja na raia watatu, walikuwepo ndani ya bwalo hilo, la polisi, hapa wilayani Njombe, (kipindi hicho) Wote wakiwa wame yaelekeza macho kwa yao na masikio, kwa kanal Kisona, ambae alianza kueleza jinsi alivyo sikia milindimo ya risasi kwenye mlima wa chandamali, uliopo ndani ya kambi la lajeshi, na akaeleza jinsi alivyo fwatilia nyayo na alama za kijana Lukas, ambae alifanikiwa kumwona, lakini akufanikiwa kuongea nae, kutokana na polisi kumshambulia, (tusipoteze muda kwa kurudia yote aliyoeleza Kisona), ambae baada ya kumaliza kutoa maelezo yake, akafwatia kijana Edgar alie ambiwa asogee mbele, akaeleze jinsi mambo yalivyo tokea, ilibakiakidogo Monalisa amfwate Edgar pale mbele, lakini baba Edgar alie kuwa nao karibu aka mzuwia, “subiri hapa hapa”alisema baba Edgar huku akimdaka mkono Monalisa, ambae alimsikia na kumwelewa baba mkwe wake, Edgar nae akaeleza toka alipo mwona Monalisa anaondoka chuoni, na rafiki zake, na mpaka walipo kutana Makambako, Monalisa akifukuziwa na njeamba mbili, ambazo yeye kujuwa kuwa ni polisi.
Maelezo ya Edgar yalikuwa kama tulivyo soma kwenye mkasa huu, makamanda walikuwa wanamsikiliza huku wakiandika bahadhi ya maelezo ya kijana huyu, kama walivyo anya kwa Kisona, “ok! nazani Monalisa maelezo yake atayaandika kwenye karatasi kisha yatumwe kwa fax, zaidi ufwanywe utaratibu tuone ideo ambayo imeletakizaa zaa” aliongea CDF, na hapo ukafanywa utaratibu wa kuiweka ile tape kwenye video deck maalumu, kwaajili ya mikanda midogo kama hii, itumikayo kwenye camera, ikaonganishwa kwenye video screen ya nchi 42, iliyopo ndani ya bwalo lile, ikaanza kuonekana video ambayo, mwanzo ilitoa picha afifu, ambayo ilionyesha tukio moja la usiku, polisi wakiwa wana washambulia polisi wenzao, na mwishoni ana shuka Kingarame toka kwenye gari, na kuingia ndani ya Benk ya ifadhi ya mari z wananchi, ni baada ya polisi wake kuvunja geti, wanaonekana pia polisi wle wauwaji ambao kwa makamanda walitoka Ruvuma, wli watambua mmoja baada ya mwingine, nambaya zaidi kati yao ali bakia hai, ni Kingarame na Mike, ambae alinusulika kuuwawa na Kingarame mwenyewe, waliwaona wakitoa mabox ya chuma, na kuyapakiza kwenye gari, Kisha wakondoka zao, na ata walipo astuka kuwa kuna uwepo wa mtu mwingine mahali pale, ndipo video ilipo koma, “RPC kwahiyo walinzi walipewa risasi baridi” aliuliza IGP, kwa mshangao, “hiyo aina ubishi afande, sasa hivi naagiza mgawa risasi wa siku hiyo akamatwe, mala moja” alisema RPC Ruvuma, “afande siyo wa kutafutwa, mtoa risasi kwa sasa ni mmoja tu, PC Bosso” alisema OC FFU wa Ruvuma, “ok! IGP, kuna umuhimu wa kila mmoja wetu kupata nakala ya hii video tape, mimi namakamanda wangu tuna enda huko kilipo andaliwa chakula cha mchana, unaweza kuunga na sisi kam auto jali, kisha baada tuna rudi zetu dar, kuhusu awa raia wema walio shiriki kufichua uovu wa polisi wachache wasio na uzalendo, sina mengi ya kuongea, zaidi, nitajuwa baada ya kupeleka taarifa ikulu” alisema IGP na kufunga kikao kile, huku zikipigwa picha za kumbukumbu, kisha ukatoka wa msfara wa magari kumi kuelekea serena hotel, kwaajili ya chkula cha mchana, awakujuwa kuwa wanampeleka Monalisa akavalishwe pete….. mambo ni mengi muda mchache… tukutane kesho ili kujuwa kilichotokea Serena hotel, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU