
BIKIRA YA BIBI HARUSI (88) MWISHO

SEHEMU YA THEMANINI NA NANE (MWISHO)
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA (87) pasipo kuongea neno lolote, wote wakarudisha macho kwa Monalisa, ambae ndie mwenye jibu la mwisho, ambae alikuwa ameshikwa mkono wa kushoto na Erasto alie piga goti moja, huku mkono wake wakushoto umeshikilia kikasha cha pete, Moalisa akainua uso wake kumtazama Edgar, akamwona ana mtazama, Monalisa akarudisha macho yake kwenye pete, huku anaachia tabasamu la furaha……. ENDELEA…….
Akika eneo zima la mbele ya Serena Hotel, wakimtazama Monalisa alivyokuwa anaitazama ile pete kweny mkono wa Erasto, huku akionyesha tabasamu la furaha kwakuiona ile pete, ambayo ilibidi aveshe toka jumamosi iliyopita, Monalisa aka tazama kule waliko simama baba na mama yake, akamwona baba yake akiwa katika hali ya mshangao, tofauti na mama yake ambae akuonyesha mshangao wala furaha, Monalisa akamwona baba Erasto pembeni ya wazazi wake, akionyesha uso wa furaha, hapo Monalisa akamtazama mama Rasto ammbae alikuwa karibu yake kabisa, nae alikuwa anamtazama kwa macho ya furaha, hapo Moanalisa aka mtazama mama Edgar aliyekuwa hatua moja nyuma yake, akamwona anatabasamu lakini tabsamu ambaloakuna ambae aliweza kulitafthiri, kama ni la furaha au udhuni, kumbuka wakati huo Erasto alikuwa bado ame piga goti moja, ameushikilia mkono wa kushoto wa Monalisa.***
Wakati huo ndani ya Chumba namba kumi na sita, dada mhudumu alipoingia ndani ya chumba hiho moja kwa mooja akaifwatameza na ambayo juu yake ilioneka wallet ya Erasto ikiwa pale juu, akaichukuwa na kuifungua haraka haraka, akikutana na noti kadhaa za fedha, akazichukuwa haraka na kuirudisha ile pochi mezani, kisha aka weka fedha kwenye mkoba wake na kutaka kutoka, nje ya chumba kile, lakini akasita kidogo, na kulitazama begi kubwa la Erasto, akalifwata na kulifungiua zip ya pembeni, ana kuzamisha mkono, akaibuka na vikopo vya mafuta na pafume, aka weka kwenye mkoba wake, alafu sakafungua zip ya kati, akapekua pekua, bila mafanikio, ile anataka kuunga akaiona bahasha ya kati, akaifungua na kuchungulia ndani yake, alicho kiona humo, ni maburungutu ya fedha, akujiuliza mala mbili, aka ibeba bahsha kama ilivyo, na kuiweka kwenye mkoba wake, kisha aka funga begi kama alivyo likuta, na kutoka nje haraka, akifunga mlango kama alivyo ukuta.***
Watuwote walikuwa kimya katika eneo la mbele ya kibaraza cha serena hotel, binti Salma Mohamed akiwa meza moja na wazazi wake, alishuhudia Monalisa mshana ambae kule chuoni alikuwa na sifa kubwa ya kutopenda mazowea na wanaume, akiwa anakaibia kuveshwa pete na mtu alie sewa kuwa ni mchumba wake,kijana mlevi, mwenye tamaha ya ngono, huku akitazamwa nahumati wawatu, sijuwi kwanini akupenda kile kitu kitokee, maana roho ilimuuma sana Salma, sababu alijuwa kuwa Erasto nikijana ambae hakuwa na sifa ya kuw na mschana mrembo anae jiheshimu kama Monalisa, Salma alizidi kuumia roho, baada yakuona Monalisa ametulia anaitazama ile pete uku akiwa ameachia tabasamu mwanana.
Lakini wakati watu wana endelea kutazama tukio lile, wakamwona Monalisa ana uondoa mkono wake kwenye mikono wa Erasto, ambae akajiandaa kufungua kikashacha pete yadhahabu, lakini kabla aja kifungua, ghala Monalisaaka kikwapua kile kikasha, na kuanzaku kimbilia kule alikokuwa Edgar, kila mtu akashangaa, ile Earsto ana gutuka na kuinuka ili amfwate Monalisa, akadakwa na askari wawili, kati ya wale wanne walinzi walioteuliwa kuwalinda Edgar, ambao wali mfyetua na kumbwaga chini wakimkandamiza pale pale chini, huku Erasto akishindwa kujipapatua toka kwenye mikono imara, ya askari wavita, alibakia ana mtazama Monalisa, ambae alienda mpaka alipo simama Edgar, aliekuwa anamshangaa, “si ulisema aukipata pete unanivesha” alisema Monalisa huku anakifungua kikasha cha pete, “hii hapa niveshe sasa” kwa wanae mfahamu Monalisa, walizidi kushnagaa, maana upole na heshima ya Monalisa, ingekuwa vigumu sana kufanya vile mbele za watu, lakini wa wanao wafahamu wotewawili, tena toka utotoni, wasinge shangaa, kwajinsi kipindi kile walivyo kuwa, maana mmoja wao likuwa tayari kufanya lolote, ili mwenzake awe na furaha,
Hali ya mzizimo ni kama ilizidi mala mbili, kila mmoja alitulia macho kwa Edgar na Monalisa, wakisubiri kuona Edgar atafanya nini, wakamwona Edgar ana tazama pale alipo kuwa Erasto ambae alikuwa amelazwa chinihuku ame kandamizwa, akizuiliwa asimwate Monalisa, Erasto alionekana akiwa amekodo macho ya huruma na mshangao, akimtazama Edgar, nikama anamwomba akatae kile anacho kitaka Monalisa, hapo Edgar akamtazama, mama yake ambae tabasamu lake lilionekana wazi usoni mwake, na yeye akatabasamu, huku ana geuza shingo yake, kutazama upande, alipo kuwa mama yake Monalisa, watu wote waka geuza shingo zao kumtazama mama Monalisa, ikionyesha wazi kuwa Edgar aliogopa kurudia makosa aliyo ytafanya miaka zaidi ya kumi iliyo pita, mama Monalisa pasipo kuonyesha tabasamu, au chuki, akatikisa kichwa juju chini, hapo Monalisa akaachia tabasamu huku anaushika mkono wa Edgar na kuiweka ile pete kwenye mkono wa Edgar, “nivalishe sasa, mimi si mchumba wako, ulisema unanipenda” alisema Monalisa ambae baada ya kuwa ameshampatia pete Edgar, na sasa aliunyooshamkono wake wa kushoto kwa Edgar, tayari kuveshwa pete.
Edgar akapiga goti Moja, kama alivyo fanya Erasto mwanzo, kisha akaukamata ule mkono wa Monalisa, na kuanza kumvesha pete kwenye chanda, “we! mama Mona, kwanini unaluhusu hili litokee, wakati unajuwa Erasto na Monalisa niwachumba?” aliuliza mama Erasto kwa sauti ya juu, iliyojaa mshangao, huku anamfwata mama Monalisa, wakati huo Edgar anamalizia kumvesha Monalisa pete, na watu wotewakapiga makofi, ikionyesha kuwa watu karibia wote walitamani tukio hili litokee, “mama Mona unajifanya uni sikii?, inamaana ile mipango yote tuliyo i[anga, ndio unaishia kumwacha Mona aveshwe pete na huyu mtoto mhuni” aliendeea kupayuka mama Erasto, kihasi kwamba watu wote mahali pale waka mshangaa, mama Monalisa akuonyesha kumjali, ndio kwanza aka piga hatua na kuwasogelea wakina Edgar na Monalisa, ambao walikumbatia na baada ya kumaliza kuveshana pete, hapo mama Erasto aka mgeukia mzee Anderson, ili amwulize swali ambalo mke wake akulijibu, lakini kabla aja mwuliza akamwona nayeye ana elekea kule aliko elekea mke wake.
Mama Monalisa alimsogelea mwanae na kutanua mikono ili kumkumbatia, Monalisa nae akamkumbatia mama yake, “samahani mama imenibidi kufanya hivi, nampenda sana Edgar” alisema Monalisa akiwa amekumbatiana na mama yake, “mwanangu huyu ndiyo mume wako wakweli, hili lilonekana toka utotoni, lilichelwa kwa makusidi, japo mimi nimmoja wapo kati ya watu tulio liichelewesha” alisema mama Monalisa huku sauti yake ikikaribia kutoa kakilio kafuraha, “mama Mona usi mfanyie hivi mwanagu, unazani ata jisikiaje ame kaa muda wote ana msubiria mwenzie, alafu leo achukuliwe na huyu mtoto alie kosa adabu” alisema mama Erasto akionekana kuwa amechukia sana, watu wote walikuwa wametulia wana mtazama mama Erasto ambae sasa aikuwa ana msogelea mama Monalisa pale alipo kuwa amekumbatiana na Monalisa, mama Monalisa aka aachiana na mwanae kisha aka mshika mkono Edgar, huku anamtazama mama Erasto, ikonyesha kuna jambo anataka kuweleza, watu wote waka tegamasikio akiwepo CDF, na wanadhimu wake, “mama Erasto, nazani kuna kitu unaitaji kufahamu kuwa, kila mzazi mwenye binti yake, anapenda kuona mwanae akipatamume sahihi, na huyu ndie mume sahihi kwa Monalisa, Edgar alionyesha upendo kwa Mona, ata kabla awajajuwa maana ya upendo wenyewe” aliongea mama Monalisa kwa sauti tulivu, huku akimtazama mama Erasto, ambae akulizika na majibu ya rafiki yake huyu, “leo ndio unajifanya kusahau kuwa huyu mtoto ndie alie sababisha tukahama mahenge, kwahuuni wake?, leo unajifanya umesahahu tulivyo kesha tukitoa machozi kwaajili ya huyu muhuni kumteka binti yako?” ilikuwa sauti kali ambayo sasa iliambatana na kilio, toka kwa mama Erasto, “nazani uliwa shahidi jinsi Edgar alivyo mlinda Mona, toka utoto wao, Eddy alikuwa tayari kuatarisha maisha yake kwaajili ya kumlinda binti yangu, ni hakiri ya kuazima iliyo nifanya nishindwe kutofautisha, michezo ya utoto, na upendo wakweli alionao Eddy kwa Monalisa” alisema mama Monalisa, huku watu wakiendelea kuwasikiliza, pasipo kujali kuwa wanasafari ya Dar es salaam, “inamaa mama Mona ume sahau urafiki wetu, umesahau urafiki wa familiazetu, leo hii mama Mona umesahau kuwa mwanangu ame jitolea kuacha shuguli zake, kuja kumfwata mchumba wake, alafu……” hapo hapo mama Monalisa, akamkatiza mama Erasto, wakati huo wana Misago alikuwa ametulia akimtazama mkewake anayo jitaidi kuokoa jahazi, “mama Erasto, mwanao akuja huku kwaajili ya Mona, ata wewe na mume wako mnafahamu kuwa mwanao amekuja huku kwaajili starehe zake, kama kweli angekuwa anampenda binti yetu, asinge weza kupata hamu ya kulala na mwanamke siku zote hizi, wakati mwenzie yupo, kwenye matatizo” hapo watu wotewaka tazamana, kwa mshangao, huku Erasto akitficha uso wake, mama yake alitazama chini kwa aibu, huku baba yake, akigeuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea ndani ya jengo la hotel, “lakini mama Mona hilo lilikuwa ni la kukaa chini na kuona tunafanyaje, siyokwa kitendo huiki mnacho tufanyia” sasa mama Erasto aliongea kwa sauti ya chini n yaupole, nakabla jibu alijatolewa, akasikia Erasto, “nataka pete yangu, niachieni bwana minataka pete yangu” liongea Erasto, huku akijipapatua toka kwenye mikono ya wale askari, ambao walizidi kumzuwia, “ebu wachieni kwanza, alisema kamanda wa jeshi la polisi, yani IGP, nna waleaskari wa jeshi la ulinzi wakamwachia Erasto ambae alikurupuka kumfwata Monalisa, alie kuwa karibu na Edgar na mama yake, “ebu subiri kwanza we kijana” alisema IGP, akimweleza Erasto ambae alikuwa amesha mfikia Monalisa, kwaajili ya kumvua pete yake, Erasto akatulia na kumtazama IGP, “pete hiyo iruhusiwi kuvuliwa na mtu mwingine, ni yeye mwenyewe lie mvesha, tena siku atakjayo mvesha pete ya ndoa, ebu niambie hiyo pete ume nunua bei gani?” aliuliza IGP, “hiyo ni gram mbili, nime nunua shilingi elfu 40” alisema Erasto kwa sauti ya jadhba, “ok! mimi natoa elfu kumi, kuchangia hiyo pete, kama kuna mwingine anayo aongeze” alisema IGP, huku anazama mfukoni na kutoa noti za elfu moja moja kumi, kipindi hicho thamani yake, ilikuwa kubwa sana, ungefananisha na laki moja kwa sasa, “umeniwai bwana IGP, kwashujaa wetu, naongeza Elfu kumi” alisema CDF, huku na yeye akifanya kama alivyo fanya IGP, aikuchukuwa at dkika, ikatimia elfu 40, maana kuna waliotoa elfu tano, wengine elfu mbili mbili, mpaka ikatimia Elfu alobaini, akakabidhiwa Erasto, ambae alizipokea, na kuondoka zake mahali pale akielelekea ndani yajengo la hotel, huku mama yake alie jawa na aibu, akimfwata mbio mbio.
Muda wote dada mhudumu ambae alisha uficha mkoba wake, wenye maela aliyo ya kwiba kwa Erasto, alikuwa amejichanganya na watu, akitazama jinsi mambo yalivyokuwa yanaenda, na sasa watu walikuwa wanaelekea kwenye meza zilizo andaliwa kwaajili ya vya kula, ambapo sasa waalikwa waliongezeka, wakiwepo mama na baba Monalisa, pia familia ya mzee Mohamed,**
Mzee isago baada ya kufika chumbani kwake alikusanya kila kilicho muusu yeye na mke wake kisiha akabeba begi lao kubwa na kutoka nalo nje, akikutana na mke wake anapanda ngazi, kuelekea kule anakotoka yeye, “akuna la kusubiri hapa tuwai magari yanayotoka dar” alisisitiza baba Erasto, kisha yeye na mke wake wakageuka nakurudi chini, moja kwa moja mpaka chumbani, kwa Eras5to ambae walimkuta anaangua kilio, kwa kuibiwa fedha zake zote, “ujinga wako wakuamini kila mtu, ebu twende bwana” alisem baba Erasto, akimsimanga mwanae, ambae hakuwa na lakufanya, zaidi ya kuchukuwa begi lake na kujiunga na wazazi wake, ambao walitokea mlango wa uani na kuelekea stend, hukuwakishushiana lawama, kila mmoja akimlahumu mwenzie, kuwa ndie alie sababisha majanga yale, kule stend awakuchelewa kupata usafiri wa kuelekea Songea, huku njia nzima wakihapakuto kuwa na ukaribu tena na familia ya Anderson,**
Tayari taharifa za kusakwa kwa Basso na mari zilizo ibiwa NMC, zilisha fika, na Basso ambae akuwa na habari kuwa mambo yamesha aribika, kwa upande wakina Kingarame, alikamtwa kulaini kabisa, akiwa kwenye ghara la silaha, huku akipewa mateso makali sana, ili aseme ziliko iadhiwa mali za wananchi, japo alinza kwa kukaza lakini kibano kilipo zidi akataja nyumba ya Kingarame iliyopo mahenge, na polisi wakaeekea huko kuchukuwa mari zile za thamani kubwa, ***
“akika ukichilia tukio la kusaidia kupatikana ushaidi, na kuwashinda awa majambazi, awavijana mekuwa na historia ya kushangaza sana” alisema CDF, wakati wanaendelea kupata chakula, “wanastahili zawadi kubwa sana awa vijana” aliongezea IGP, “atuwezi kutoa zawadi mapema, kabla atuja sikia maamuzi ya rais, ila kwa sasa nahaidi kuwa, nikifika dar es salaam nitawatumia fedha, kaajili ya harusi yao, nitafurahi sana wakifunga ndoa” hiyo ilikuwa ahadi ya CDF, IGP nae akaaidi kuongezea fedha katika harusi yao, pia makanda awa walimsifu sana mze Mohamed na familia yao, kwa kuonyesha moyo wa kizalendo na kibinadamu,
Kwa upande wa mama Monalisa, liomba msamaha kwa mama Edgar, akisema kuwa yote yaliyo tokea kati yao, mshawishi mkubwa likuwa ni mama Erasto, mama Edgar akuwa na kinyongo, alisamehe mala moja, wakashikana mikono,, huku mama Monalisa akisisitiza kwasasa waangalie maisha ya watoto wao yanakuwaje. ***
Naam masaa machache baadae, walishamaliza kula na kunywa kidogo, kisha IGP na CDF wakapanda kwenye helicopter zao, kurudi dar es salaam, hukubriged kamanda akiondoka na wakina mama Edgar na mama Monalisa, kwa hellcopter Monalisa alikataa, kwa madai atasafari gari moja na mchumba wake Edgar, ambao walipanda kwenye land lover mia na kumi lililo endeshwa na mzee Mbogo, huku Koplo katembo na askari wawili, wakiingia kwenye Nissan la mzee Anderson, safari ikaanza kuelekea songea, baada ya kufika songea Monalisa, akutaka kwenda kwao, nikama alihamia kwa kina Edgar, huku mizigo yo ikiletwa toka makambako, na siku tatu baadae waliitwa ikulu, kuonana na raisi, wakiwa na wazazi wao, ambae aliwatangaza kama ashujaa, kaika taifa, na aliwazadia shilingi laki nne, kila mmoja, akiwataka kufikilia kama wanaitaji kujiunga na jeshi au chombo chochote cha ulinzi nchini.
Siku saba mbele wakiwa wamerudi songea na kujadiliana, waka rudishamajibu yao kupitia brigedia haule, kuwa Edgar alikubari kujiunga na usalama wataifa, huku Monalisa akikataa kujiunga na jeshi lolote, hivyo akapewa ajira kwenye benk ya mwananchi, huku benk ya hadhina, ikiwa jengea nyumba kubwa, ya kuishi na fedha tathirim, laki tano kama wachumba, kwa kusaidia kuokoa mali za wananchi,
Upande wa baba Edgar yani mzee Mbogo, alizawadiwa fedha tathrim laki nne, kama wakina Edgar, pia akapewa kaziyamuda, kufundisha madereva wakijeshi, kuendesha magari katika mazingira magumu, ambapo angekuwa analipwa mshahara mnono kila mwezi,
Kisona na wenzake pamoja na kupandishwa vyeo, ngazi moja toka cheo cha hawali, pia wao pamoja na wakinaEdgar na mzee Mbogo, waliveshwa nishani za uzalendo, na ushujaa. akika ilikuwa ni faraja kubwa sana kwa wazazi wa Monalisa na mama Edgar, huku upande wa mzee Misago nafamilia yake, wakijilahumu kwa mambo waliyo yafanya.
Kwa kijana Earasto lilikuwa ni pigo kubwa sana, akika alijuta san kwa mambo aliyo kuwa anayafanya, akijiona kuwa ni shujaa, nasasa yaimfanya kuonekana kuwa ni mjing wamwisho kabisa, kijana huyu sasa alikuwa anajifungia ndani, akiona aibu kwa mambo yaliyo mtokea, ata siku ya harusi ya Edgar na Monalisa, ndio ilikuwa kama mwanzo wa kudhohofika kmwili na hakiri, kihasi cha kuonekana kama chizi, story hii ni kwa heshima ya babu yetu marehemu mzee Mbogo, akika tuliishi naekama rafiki sikuzote akisisitiza kujiendeleza katika vipaji vya Sanaa na muziki, ambapo kwa sasa tuna kamilisha studio ya muziki, kama alivyo tuagiza, ansateni sana wadau, kwa kufawtilia kisa hiki cha BIKIRA YA BIBI HARUSI
MWISHO

