BINTI MDUNGUAJI (08)

EHEMU YA NANE

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA : waliongea wale vijana wakianza kuondoka eneo lile kuelekea ofisini ambako walitoka masaa manne yaliyopita wakienda kwenye chai, ndipo yule dada mama n’tilie alipo achia tabasamu dogo, huku nayeye akiondoka zake na kuvuka barabara kuelekea upande wa pili, huku moyoni mwake akiwaza tabia yake ya kuchukia wanaume wanaodai kuwa wanampenda, na siku zote yeye aliamini kuwa mwanaume anae mwambia anampenda ndie adui yake wakwanza, endelea …….
Alipovuka barabara, yule dada akanyoosha moja kwa moja, aiingia ndani ya mitaa ya Manzese akiipita bar moja kubwa sana ya Jambo pub, iliyopo mita chache kabisa toka barabarani, akaingia mtaa wapili, na safari yake iaishaia kwenye bar moja yenye guest house, yenye hadhi ya kawaida, inayoitwa Mapambano, akaingia ndani upande wa vyumba, “hoo! dada umerudi, vipi mambo?” alipokelewa kwa shangwe na muhudumu wa vyumba, “safi dada yangu, za tangu jana?” alijibu dada mama ntilie, huku aki mtazama kwa tabasamu yule dada mhudumu, ambae alimpokea siku iliyopita, yani jana jioni, alipo ingia hapa na kuchukua chumba “za tangu jana poa kabisa, sema kuna yule jamaa uliekuwa anakusemesha jana usiku, ukamchunia amenipa ujumbe wako”aliongea yule dada muhudumu wa vyumba “mh! kwani ananifahamu? We! hachana naye” alijibu yule dada mama n’tilie na kuanza kuondoka, kuelekea kwenye chumba chake, “sikia we!dada usipoteze bahati yako, yule mkaka anafedha nyingi, hacha ufala utakufa nanjaa mjini hapa” hapo dada mama n’tilie akasimama nakugeuka nyuma, akarudi alipo yule dada mhudumu “nazani atawewe una itaji hizo fedha, nivyema ukampatia anachoitaji, ili akupatie hizo fedha, wewe mweye shida nazo” aliongea mama ntilie kwa sauti ya chini, akimalizia kwa tabasamu laini, na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake, akimwacha yule dada amekunja sura kwa ghazab, akiona kabisa kuwa yule mschana ambae kwamanekano ni mrembo na mzuri wa haja, lakini ni fukara sana, kwa nguo alizo vaa, baada ya kuingia kule chumbani dada mama ntilie, alifunga mlango kwa ufunguo, akaanza kuivua ile kanga yake aliyo jifunga kiunoni, akifwatia lile gauni refu, ambalo siku izi wanaita dela, akabaki na kikaptula kifupi cha jinsi na tishet la rangi nyeusi, ambacho kilikuwa kimemkaa vyema na kutokana na mahips yake na makalio yake makubwa kiasi, akafungua mkanda alio valia kile kikaptula, akiruhusu bastora yenye kiwamba sauti (silence baler) na kisu kikiwa kwenye kifuko chake, alivyo vining’niza kiunoni kwa msaada wa mkanda mgumu wa ngozi, kuweza kutoka na kuweka pembeni, akamalizia kuvua nguo zilizobaki akimalizia ile ndogo kabisa ya ndani, kisha akaingia bafuni akaoga, alipomaliza, akajiweka sawa akavalia gauni lake jingine linalofana na lile la mwanzo, ndani akitanguliza nguo ka mazile alizo vaa mwazo, kikaptula cha jinsi na tishert, akiwa amenig’iniza bastora na kisu, kwenye kaptura ya jinsi ikifichwa na gauni refu, akatoka na kufunga mlango wake kwa nje, kisha akaenda upande wa bar ambapo panauzwa chakula, wakati anakula alikuwa akiangalia tv iliyopo mahari pale, akiwa na watu wengi wakipata chakula pi, na wengine wakinywa pombe, kuna habari ilikuwa ikitangazwa kwenye TV, ni kuhusu mauwaji ya mchungaji mmoja maharufu sana, wakanisa moja la kilokole, lilopo buguruni, mama ntilie alipomaliza kula akainuka na kuanza kurudi ndani, akiwa anaelekea ndani upande wa vyumba, akisindikizwa na macho ya wanaume wakwale, mama ntilie alipo tazama kwenye kona moja pale sehemu ya kupata vinywaji na chakula, alimwona yule mhudumu wa vyumba akiwa na kijana mmoja, alimkumbuka mala moja kuwa, ni yule ambae jana yake alikuwa akimtaka kimapenzi, lakini leo kulikuwa kuna utofauti kdogo, tofauti ni kwamba aliwaona wakiongea huku wakimtazama, na yule mhudumu akionyesha kutahaluki na kusisitiza jambo, yule dada mama n’tilie alitabasamu, kwani alikuwa amesha hisi jambo flani, na kuelekea chumbani kwake, akiwa amehisi kuwa kile kikao si’salama kwake, ***
Huyu dada anaitwa Jackline Michael Nyati, binti mrembo hatari wa mzee Michael Nyati na mke wake Anitha, miaka mingi iliyopita, baadaya Jackline kutimiza miaka mitano Michael alianza kumtengenezea mazingira yakupenda ngumi na sarakasi mwanae mdogo wakike Jackline, ikiwa pamoja na mazoezi ya pumzi na viungo, na kupita kwenye sehemu zenye vikwazo, adi anafikisha miaka kumi akiwa darasa la nne, alikuwa na uwezomkubwa sana wa kupigana, katika shule aliyo kuwa anasoma, akuna mwanafunzi aliweza kumpiga, awe wakike au wakiume, ni kuanzia mwanafunzi wa darasa la kwanza, Jackline mpaka darasa la saba, mpaka anamaliza darasa la saba, baba yake alisha wai kuitwa mala nyingi sana shuleni, akienda kujibu mashitaka ya kupiga wenzake, Jackline aliyafanya hayo akiwa ni mschana, mwenye sura nzuri na ya upole, pia mwili wake ulikuwa wakuvutia, katika kumbu kumbu chache, akiwa kidato cha pili shule ya wanawake songea, kuna siku walienda kushiriki michezo baina ya shule zote za songea mjini, siku hiyo, ilikuwa ina cheza shule ya songea wavulana na ruvuma sekondali, baada ya michezo kumalizika, binti huyu alishika njia ya kuelekea kwao, kumbuka Michael Nyati alijenga nje kidogo ya mji, hivyo ilimlazimu Jackline kutembea kamwendo kidogo kabla ya kufika nyumbani akivuka vichaka na mapori, pasipo kujuwa ili wala lile, jackline alichapa mwendo, kumbe kuna wanafunzi wa shule ya Songea wavulana wa kidato cha nne, walitangulia nakujificha, wakiwa na uakika kuwa Jackline lazima atapita tu! vijana hawa ni Festo, Kadoda na Majaliwa, vijana hawa walikuwa ni wakolofi sana, na walikuwa wanafahamika kwa ukolofi wao, kesinyingi zilisha fika adi polisi, lakini wazazi wao walinde na kuwatoa vijana wao kuwa kesi za wanfunzi zitafikaje polisi, nawakati mwingine kutokana na uwezo wakifedha na madalaka ya wazazi wao polisi walikataa ata kwenda kuwakamata, maana hawakuchelea kupiga simu kwa staff offcer au RPC kulaumu kukamwatwa kwa watoto wao, nale vijana hawa watukutu walikuwa wamepania kumbaka binti huyu, licha ya kusikia kuwa ni hatari, kwenye mapigano lakini wali amini wao watatu ndio bala zaidi kuliko mwanamke mmoja, waliamini wangefanikiwa walichokusudia, kweli bwana dakika chache wali mwona bint akija kwamwendo wa speed japo alikuwa anatembea, lakini alitembea kwa nguvu sana, ndipo walipo jitokeza barabarani, wawili mbele mmoja nyuma, kumbuka sehemu hiyo ina umbali wa kama km tatu toka mtaani na km moja kufika kwao wakina Jackline, “sasa kwahiyali yako, tuingie porini tumalizane, vinginevyo utajuta kuwa mzuri hivyo” aliongea Kadoda ambae alionekana ni mkorofi kuliko wote, kitu cha kushangaza binti huyu hakuonyesha wasiwasi wowote zaidi alitabasamu na kuwauliza, “hivi nyie, mkisema mkimbie, mtakimbilia wapi hapa?” Wote wakashangaa wakatazama pande zote, wakizani labda kuna mtu mwingine eneo lile ambaye anampa kiburi binti huyu, awakuona ta dalili ya mtu, kwa pupa kisha wakarudisha macho kwa Jackline, “poleni sana, mtakacho kipata leo ladhima kesho mnitafute tena” hapo walishuhudia tabasamu la hajabu ambalo hakuna ata mmoja wao, aliewai kuliona, kiukweli usingeweza kutambua kama huyu binti alikuwa anatabasamu au amekasirika, itaendela………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!